Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
WAJA
Dawa ya kipwepwe nini,
Siyo maji na sabuni?
Basi jipu tumbueni,
Mnayemhofu nani?
Mtachopoteza nini?
Mkidai kwani shani!
Kuna nini utaani,
Hadi muogope nari?
Ona mwafanyiwa ndaro,
Muishipo kwa kihoro,
Mwafanana na nguchiro,
Wawawinda kama ndoaro!
Wameshawapiga ndonga,
Mwaambwa mambo yanoga!
Wanahofu kuwanonga,
Endelea kujivunga.
Mie nyama n'shafunga,
Nenda kutulia Vanga,
Nikitoka n'ende Manga,
Nimsabahi Mghanga.
Nimelonga nil'olonga,
Acha nisijebananga,
Sikuifichua kunga,
Nawaachia malenga.
Enyi mwakalia kumba,
Mwajidanganya ni nyumba!
Utapofika msiba,
Mi' sikio nitaziba.
Nawatakia salama,
Inshallah tendeni wema,
Ninawakabidhi noma,
Bora mfike salama.
Dawa ya kipwepwe nini,
Siyo maji na sabuni?
Basi jipu tumbueni,
Mnayemhofu nani?
Mtachopoteza nini?
Mkidai kwani shani!
Kuna nini utaani,
Hadi muogope nari?
Ona mwafanyiwa ndaro,
Muishipo kwa kihoro,
Mwafanana na nguchiro,
Wawawinda kama ndoaro!
Wameshawapiga ndonga,
Mwaambwa mambo yanoga!
Wanahofu kuwanonga,
Endelea kujivunga.
Mie nyama n'shafunga,
Nenda kutulia Vanga,
Nikitoka n'ende Manga,
Nimsabahi Mghanga.
Nimelonga nil'olonga,
Acha nisijebananga,
Sikuifichua kunga,
Nawaachia malenga.
Enyi mwakalia kumba,
Mwajidanganya ni nyumba!
Utapofika msiba,
Mi' sikio nitaziba.
Nawatakia salama,
Inshallah tendeni wema,
Ninawakabidhi noma,
Bora mfike salama.