UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka...

UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka...

Umri wa Lulu waibua mvutano kortini

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Umri wa Lulu waibua mvutano kortini [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 07 May 2012 22:04 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0digg

000000antluluuuu.jpg
Msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana, chini ya ulinzi mkali wa askari Magereza. Picha na Venance Nestory

Nora Damian
UMRI wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba jana ulizua utata katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya mawakili wanaomtetea kutaka kesi hiyo iondolewe mahakamani hapo ili akashtakiwe kwenye Mahakama ya Watoto.

Kesi hiyo ilitajwa jana huku mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Keneth Fungamtama, wakiwasilisha maombi kuhusu suala hilo la umri wa mteja wao wakitaka asishtakiwe mahakamani hapo kama ilivyo sasa. Fungamtama ambaye alikuwa akisaidiana na Mawakili Peter Kibatala na Fulgence Masawe, alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo ana umri wa miaka 17 hivyo, kesi yake ilipaswa kusikilizwa katika Mahakama ya Watoto. “Mshtakiwa ana umri wa miaka 17 na tuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa ambacho kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa,” alidai Fungamtama.

Fungamtama alisema Kifungu cha 4 cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 Kipengele namba 21, kinatamka wazi kuwa mtoto ni yule aliye na umri chini ya miaka 18. Wakili huyo aliendelea kunukuu vifungu mbalimbali vya Sheria ya Mtoto kama 98 (i) na 114 (ii), ambavyo alidai kuwa vyote vinawapa nguvu ya kuwasilisha maombi yao hayo ya kuihamisha kesi hiyo. “Hata katika suala la Mahakama, vifungu vyote vya sheria hii vimefafanua, hivyo tunawasilisha maombi yetu kwamba mteja wetu ana umri wa miaka 17 na shauri hili lingepaswa kusikilizwa Mahakama ya Watoto,” alidai.

Kwa upande wake, Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda aliomba wapewe muda zaidi kwa sababu bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo. “Kesi hii imekuja mahakamani hapa kama ya mauaji na upelelezi bado haujakamilika. Tunaposema haujakamilika, tunapeleleza kila kitu, likiwamo suala la umri,” alieleza Kaganda. Alisema hata jina linaloonekana katika cheti cha kuzaliwa kilichowasilishwa mahakamani hapo, linasomeka Diana Elizabeth wakati mshtakiwa ametajwa mahakamani hapo, kwa jina la Elizabeth Michael. “Tunaomba muda tuweze kuchunguza kuhusu umri wa mshtakiwa kwa sababu aliwaeleza polisi kwamba ana umri wa miaka 18 halafu mawakili wake wanakuja kueleza hapa mahakamani kwamba ana umri wa miaka 17,” alidai Kaganda. Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa kutokana na mvuto wa kesi hiyo katika jamii, wanaomba wapewe muda zaidi kufanya upelelezi ili kumtendea haki mshtakiwa huyo.

Kuhusu cheti hicho kusomeka Diana Elizabeth, Wakili Fungamtama alikiri na kudai kuwa ni jambo la kawaida hasa kwa Wakristo kuwa na majina mawili. Fungamtama alidai kuwa hawana pingamizi na maombi ya upande wa mashtaka kwamba wapewe muda zaidi wa kufuatilia cheti cha kuzaliwa cha mshtakiwa, ingawa alidai kuwa suala hilo halina ugumu. Akitoa uamuzi baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Mkazi Augustina Mbando alisema: “Mahakama imesikiliza maombi yaliyoletwa na Fungamtama na Kaganda na imeona kesi iliyopo hapa ni ya mauaji na jinsi kesi hii ilivyo, hatuwezi kufanya hoja yoyote hadi upelelezi utakapokamilika.”

“Kama defence (upande wa utetezi) wana maombi yoyote wanaweza kufanya hivyo kupitia Mahakama Kuu,”
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 21, mwaka huu itakapotajwa tena. Inadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican, Dar es Salaam msanii huyo wa kike, alimuua Kanumba. Jana Lulu alifikishwa mahakamani hapo saa 2:50 asubuhi akiwa peke yake kwenye gari linalobeba mahabusu, huku akisindikizwa na magari mengine mawili.

Alipoingia mahakamani alikuwa amezingirwa na askari Magereza na Polisi zaidi ya 10 na kuufanya umati mkubwa wa watu uliofurika mahakamani hapo kushindwa kumwona. Miongoni mwa watu waliofika mahakamani hapo jana ni baba mzazi wa msanii huyo, Michael Kimemeta na ndugu zake wengine kadhaa.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

acheni mambo yenu ya uongo,lulu mwenyewe tulimsikia akisema ana miaka 18 katika kipindi fulan tena kwa kingereza i am 18,na doc anazo,wewe ulieandika maelezo haya huna unchokijua
 
acheni mambo yenu ya uongo,lulu mwenyewe tulimsikia akisema ana miaka 18 katika kipindi fulan tena kwa kingereza i am 18,na doc anazo,wewe ulieandika maelezo haya huna unchokijua

big niga..........................mambo ya mahakamani wayajua weye............kauli haina mashiko kama kuna ushahidi wa maandishi.......wanasheria wa Lului wanacho cheti chake cha kuzaliwa kutoka hospitali ya Muhimbili na kufanya chochote kile ambacho Lulu kuongea kupotea maana.......................
 
Last edited by a moderator:
000000antluluuuu.jpg

Msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana, chini ya ulinzi mkali wa askari Magereza. Picha na Venance Nestory

Hizi kauli kuwa Lulu ana uja wepesi wa mwendazake naona umeanza kupata mashiko...............
 
The girl is innocent period. Kanumba alianza mahusiano na huyu mtoto akiwa bado ni minor hili limekaaje?? Ingawa si tiketi ya Lulu kufanya mauaji lakini hakuna ushahidi wa kutosha Lulu ndiye aliyesababisha kifo hicho. Lulu ana haki ya kupewa dhamana wakati upelelezi ukiendelea.
 
Pakawa..........hata polisi naona wameanza kukataa tamaa baada ya kuona cheti cha kuzaliwa cha kinda Lulu.....................game over....ila akitoka ajihadhari wapambe wa mwendazake wasije kumdhuru tu.........
 
Last edited by a moderator:
idont think so kuwa lulu ana makosa ,pia tanzania bado iko nyuma kiuchunguzi ,

wahida tuko wote hapo............................uko wapi leo mbona sikuoni kule MMU?
 
Last edited by a moderator:
leo ilikuwa bz day kwangu ndio nimefika home muda s mrefu nimefungua kuangalia wht goingon ktk jf
 
Mkuu

Huyu Dogo Janja atafungwa! Why?

1. Ameiaminisha Dunia Nzima kuwa ana miaka 18 including Kanumba

2. Dunia nzima itamshuhudia kuwa ni Mchafu

3. Live Video na Watangazaji wa TV watatoa ushahidi wa Mahojiano wa Ukware wake.

4. Picha zake za kimitego na ulevi zitadhihirisha uchafu wake (waliomuuzia pombe under 18 nao watafungwa?).

5. Dotnata ameshadhihirisha nia njema ya Kanumba kuwa alitaka Kumwoa na alikuwa na taarifa rasmi. Lulu alikubali na alisema tatulia lipotakiwa kufanya hivyo. Wamekuwa marafiki for 6 months na Kanumba hakutaka wawe in Spotlight mpaka atangaze Uchumba. Kuna wanaojua walikuwa wanapika na kupakua.

6. Mama yake atabomolewa mbali kwa malezi hafifu, rafiki zake watapondwa kuwa ni marafiki wabaya na wasiomshauri,

7. Sumu zake na SMS zake zimeshachunguzwa. Alikuwa na mpenzi mwingine kitu kinachoonyesha ukomavu katika tasnia ya Ngono (siyo Filamu) (Lulu atasema naye alikuwa anambaka?)

8. Lugha yake ya kejeli na mzaha itawatia hasira majaji maana hana staha, records zipo.

9. Alishawahi kupatikana na makosa mahakamani na kuhukumiwa kwa mwenendo mbaya na matusi

10. Jamii yenye hasira haimtaki ndo maana walivamia kituo cha polisi Oysterbay.

Mi si Mwanasheria, lakini Advocate Ruta una kazi ya ziada kama utetezi ni huo. hauna mashiko! Hana pa kutokea!

Mkuu umesema kweli.
Huu utoto wa Lilu unatoka wapi leo?
Lulu ni mkubwa mwenzetu, na dunia nzima inajua kwamba ni KAKAHABA
 
Hivi kama mkigombana wote wawili (yaani wapenzi wawili) na bahati mbaya mmoja akadondokea kitu na kufariki, bado unahesabiwa wewe uliyebaki ni muuaji? au imetokea bila kukusudia?
 
Hivi kama mkigombana wote wawili (yaani wapenzi wawili) na bahati mbaya mmoja akadondokea kitu na kufariki, bado unahesabiwa wewe uliyebaki ni muuaji? au imetokea bila kukusudia?

Inategemea na huyo mwenzako kadondokaje...

Ulimsukuma ndiyo akadondoka au alidondoka tu mwenyewe kwa kujikwaa kwenye kitu? Au alidondoka wakati wewe unamkimbiza?

Kuna mambo mengi ya kuzingatia katika kuamua. Kuhusu hii kesi ya Lulu mimi sidhani kama prosecution counsel wana ushahidi wa kutosha kumpata na hatia kwa murder one (ingawa mpaka sasa sijui hata anatuhumiwa kwa kosa gani hasa).
 
Mi huwa nasikia nchi zilizoendelea mpaka wachunguze kabisa wawe na uhakika ndo unapelekwa mahakamani, ila huku mahakamani kwanza uchunguzi baadae.
 
Mi huwa nasikia nchi zilizoendelea mpaka wachunguze kabisa wawe na uhakika ndo unapelekwa mahakamani, ila huku mahakamani kwanza uchunguzi baadae.
[MENTION]
Joyceline[/MENTION] haki za mtuhumiwa hapa kwetu zinachezew sana labda kwenye hii katib ampoya suala hilo litaangaliwa
 
Inategemea na huyo mwenzako kadondokaje...

Ulimsukuma ndiyo akadondoka au alidondoka tu mwenyewe kwa kujikwaa kwenye kitu? Au alidondoka wakati wewe unamkimbiza?

Kuna mambo mengi ya kuzingatia katika kuamua. Kuhusu hii kesi ya Lulu mimi sidhani kama prosecution counsel wana ushahidi wa kutosha kumpata na hatia kwa murder one (ingawa mpaka sasa sijui hata anatuhumiwa kwa kosa gani hasa).

Nyani Ngabu...........DPP anadai hiyo ni murder case lakini pia nanakiri hana ushahidi wa kuendelea na kesi bado anautafuta ushahdi......................yaani kafanya mahitimisho wakati hana ushahid....only in Tz huu uzembe unaruhusiwa kufanyika...........
 
Hahahahaaaa so much for the so-called "learned" brother/sister
 
Hivi kama mkigombana wote wawili (yaani wapenzi wawili) na bahati mbaya mmoja akadondokea kitu na kufariki, bado unahesabiwa wewe uliyebaki ni muuaji? au imetokea bila kukusudia?

BlackBerry hiyo ni manslaughter.............................haina ubishi lakini hapa kwetu wataiita murder kwa sababu hata ushahidi hawajui namna ya kuukusanya...........
 
Last edited by a moderator:
BlackBerry hiyo ni manslaughter.............................haina ubishi lakini hapa kwetu wataiita murder kwa sababu hata ushahidi hawajui namna ya kuukusanya...........

Lakini Ruta, hata kama mlikuwa mnagomba...kama mtu alianguka kwa kujikwaa mwenyewe halafu akajibamiza kichwa chake sakafuni na kufa, kwa nini iwe manslaughter?

Kwa nini charges zisiwe dismissed kabisa?
 
Back
Top Bottom