UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka...

SMS katika server za mitandao ya simu zitakuwa ni mwongozo wa mwenendo mzima wa kesi na pia mazingira ya tukio.

Umri wa 17 na 18 unabarikiwa binti kuolewa na katika mazingira ya kutaka kubakwa yatachunguzwa, pia mahusiano yao kwa kina yatachunguzwa. Kama waliokuwa ni wapenzi au la kwa tendo la kujamiiana lazima liwe la hiari na la maandalizi.

Yawezekana jamaa alitaka ile kitu ghafla na bibie hakuwa tayari kwa hali ya kawaida akamsukuma na kwavile kanumba alitoka bafuni yawezekana ndala zake zilimletea mushkali akaangukia kichwa kwa nyuma.

Siyo vyema mkatoa majibu ambayo Lulu angetakiwa kuulizwa na kutoa majibu yake akiwa mahakamani, mwenye ukweli ni yeye. Huoni kashaanza kabla ye kesi kuhusu umri wake?
 
noted!but based on assumption

Kayla...You have done well but, life is made of assumptions.........................the safety line between reality and conjecture is really misty and foggy too............
 
Last edited by a moderator:

ngaranumbe........................mwenzetu unachapa lomoni wakati wenzio tunatafakari msimamo wa sheria.............tunapita njia mbili tofauti kabisa hatuwezi kukutana ...........LOL
 
Last edited by a moderator:
Na mara nyingine mahakama huwapata na hatia watu wasiohusika na makosa waliyoshitakiwa nayo.

Nyani Ngabu waema kweli wengi ya waliofungwa hawana hatia kulingana na sheria zetu ila hufungwa kwa kutojua sheria iko wapi nao........
 
Last edited by a moderator:
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Utata umri wa Lulu kusikilizwa Mei 28 [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Friday, 18 May 2012 22:39 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

James Magai
MAOMBI ya uchunguzi wa umri wa muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji, yamepangwa kusikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Mei 28, 2012.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Hata hivyo, umri wake halali umezua utata kiasijambo ambalo limewalazimu Mawakili wanaomtetea kuwasilisha maombi mahakamani wakiitaka mahakama ifanye uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo.

Maombi hayo yaliwasilishwa Mahakama Kuu na mmoja wa mawakili wake, Peter Kibatala, Mei 17.

Habari ambazo Mwananchi lilizipata jana kutoka mahakamani hapo na kuthibitishwa na Wakili Kibatala zinasema kuwa maombi hayo yamepangwa kuanza kusikilizwa Mei 28 na kwamba yamengiwa kusikilizwa na Jaji wa Dk Fauz Twaib.

Katika maombi namba 46 ya mwaka 2012, mawakili hao wanaomtetea msanii huyo wanaiomba Mahakama Kuu itoe uamuzi kama Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kuamua ufanyike uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo.
Jopo la mawakili hao maarufu linadai kuwa linaamini kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo kwa sasa ndio bado inayoshughulikia kesi hiyo, ina mamlaka ya kufanya au kuamuru ufanyike uchunguzi wa umri mshtakiwa huyo.

Lakini pia wanaiomba Mahakama Kuu kama itaridhika kuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo huo, basi Mahakama Kuu yenyewe ifanye uchunguzi huo.

Mawakili hao walifikia uamuzi wa kuwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu baada ya maombi ya Mahakama ya Kisutu kujiondoa katika kuyashughulikia.

Akifafanua juu ya maombi hayo Kibatala ambaye pia ni Makamu wa Raisi wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS) alisema kuwa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 kifungu cha 113 inaruhusu Mahakama kufanya uchunguzi wa umri wa mshtakiwa.

Wakili Kibatala alisema lengo la uchunguzi huo ni ili mahakama iweze kujiridhisha kama mshtakiwa ni mtoto au ni mtu mzima kwa lengo la kujipa angalizo juu ya maslahi ya mtoto.

"Baada ya uchunguzi huo mahakama ikijiridhisha kuwa ni mtoto basi mwenendo wa kesi hiyo utaendeshwa kwa maslahi ya mtoto kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria hiyo ya mtoto," alisema Wakili Kibatala.

Kwa mujibu wa Wakili Kibatala kifungu hich ambacho huelezea ulinzi wa maslahin ya mtoto katika uendeshaji wa kesi kwa watoto wanaokinzana na sheria.
Kabla ya kuwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu, mawakili hao mawakili hao waliwasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 7,2012 wakiiomba iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto wakidai kuwa bado ni mtoto.

Mawakili hao walidai mahakamani hapo kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na kwamba kwa maana hiyo yeye bado ni mtoto na kesi yake haipaswi kusikilizwa katika mahakama za kawaida kama mtu mzima.
Kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea msanii huyo wakili Kenedy Fungamtama alidai kuwa mteja wao ana umri wa miaka 17 na si 18 kama inavyotamkwa mahakamani.

Alidai kuwa hata cheti cha kuzaliwa walichokiwasilisha mahakamani kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa hivyo kuwa na umri wa miaka 17.

"Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inatafsiri kuwa mtoto ni yule aliyekuwa na umri chini ya miaka 18 hivyo katika suala la mteja wetu alipaswa kushtakiwa katika mahakama ya watoto," alidai Wakili Fungamtama.

Hata hivyo upande wa mashitaka kupitia kwa wakili Elizabeth Kaganda ulipinga maombi hayo na kudai kuwa bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo na hivyo kuomba wapewe muda zaidi.
Wakili Kaganda pia alidai kuwa hata jina linaloonekana katika cheti cha kuzaliwa cha mshtakiwa huyo linasomeka kama Diana Elizabeth wakati mshtakiwa huyo ametajwa mahakamani hapo kama Elizabeth Michael.

Akijibu hoja hiyo, wakili Fungamtama alikiri jina hilo kusomeka Diana Elizabeth na kusema kuwa ni jambo la kawaida hasa kwa wakristo kuwa na majina mawili

Katika uamuzi wake, Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo alisema kesi hiyo bado iko kwenye upelelezi na kwamba kulingana na jinsi ilivyo isingekuwa busara kuamua hoja yoyote.
Hivyo Hakimu Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo, aliutaka upande wa utetezi uwasilishe maombi hayo kupitia Mahakama Kuu.

Mbali na Kibatala na Fungamtama ambaye pia anaitetea Kampuni ya kufua umeme wa dharua ya Dowans dhidi ya Tanesco, mawakili wengine katika jopo hilo ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Joaquine De- Melo.

De-Melo ambaye amewahikuwa Rais TLS, pia ni mshindi wa wa tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania ya Martin Luther King. Jopo la mawakili hao wanaomtetea msanii huyo linahitimishwa na Fulgence Massawe kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)

Msanii huyo bado anaendelea kusota rumande kutokana na kesi inayomkabili kutokuwa na dhamana na kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Mei 21 mwaka huu.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Lulu akwama kupanda kizimbani [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 18 June 2012 20:54 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

James Magai
MSANII wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji jana amefikishwa mahakamani na kurejeshwa tena mahabusu bila kupandishwa kizimbani.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akituhumiwa kumuua aliyekuwa muigizaji nyota wa filamu Tanzania, Steven Kanumba.
Anadaiwa kutenda kosa hilo April 7, 2012 nyumbani kwa marehemu Kanumba.

Jana, mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake kutajwa, lakini hakupandishwa kizimbani na badala yake alirudishwa tena mahabusu katika gereza la Ukonga.
Hata hiyo, taarifa zilieleza kuwa mshtakiwa huyo hakuweza kupandishwa kizimbanbi jana licha ya kufikishwa mahakamani kutokana na Mahakama Kuu kuamuru mwenendo wa kesi hiyo katika mahakama hiyo usimame.

Juni 11 Mahakama Kuu iliagiza mwenendo wa kesi hiyo katika Mahakama ya Kisutu usimame, baada ya kuamua kufanya uchunguzi wa usahihi wa umri wa mshtakiwa huyo, kufuatia maombi ya mawakili wanaomtetea mshtakiwa huyo.

Umri wa mshtakiwa huyo umezua utata kama ni mtoto au ni mtu mzima, jambo ambalo liliwalazimu mawakili hao kuwasilisha maombi hayo ya uchunguzi wa umri wake Mahakaama Kuu, baada ya Mahakama ya Kisutu kuyaktaa ikisema kuwa haina uwezo wa kisheria kuyashughulikia.

Katika Maombi hayo namba 46 ya mwaka 2012 yaliyowasilishwa Mahakama Kuu Mei 15 na mmoja wa mawakili wake, Peter Kibatala walikuwa wakiiomba Mahakama Kuu itoe uamuzi kama Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kuamua ufanyike uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo.

Walidai kuwa wanaamini Mahakama ya Kisutu ambayo kwa sasa ndio bado inayoshughulikia kesi hiyo, ina mamlaka ya kufanya au kuamuru ufanyike uchunguzi wa umri mshtakiwa huyo.
Hata hivyo waliiomba Mahakama Kuu kama itaridhika kuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo huo, basi Mahakama Kuu yenyewe ifanye uchunguzi huo.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Rais amteua wakili wa Lulu kuwa Jaji
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Tuesday, 19 June 2012 21:30 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

Leon Bahati
RAIS Jakaya Kikwete amemwapisha kuwa Jaji wakili wa kujitegemea, Joaquine De-Mello ambaye alikuwa akimtetea msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) anayetuhumiwa kwa mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Wakili huyo, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania ya Martin Luther King ya mwaka 2012 na ambaye alikuwa pia alikuwa mmoja wa makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) ni miongoni mwa majaji 10 walioapishwa jana na Rais Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
De-Mello ni miongoni mwa mawakili wanne waliojitokeza Aprili mwaka huu kumtetea Lulu katika kesi hiyo ya mauaji inayomtuhumu kumuua usiku wa kuamkia Aprili 7, mwaka huu.

Mawakili wengine wanaomtetea Lulu ambaye umri wake umekuwa na utata ni Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Massawe.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Asante bwana Ruta ila hii kesi mmh..
[MENTION]
FirstLady1[/MENTION] kesi iko wazi kabisa umri ukiishwa kuthibitishwa alikuwa chini ya miaka 18 basi imekula kwa mwendazake.............
 
niliwaambia huyu kinda ataachiwa sasa kesha pewa mdhamana.........na mwanzo wa kufutiwa mashitaka yote dhidi yake...........
 
gfsonwin pitia hii mada uone ambavyo tumeburutana humu................naona unapenda mijadala ya sheria
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin pitia hii mada uone ambavyo tumeburutana humu................naona unapenda mijadala ya sheria

By House of Lord:
What is a disputing matter here perhaps this might be a foremost question to ask? I guese the problem here is to understand very well btn murder and manslaugher. According to section196 of the Penal Code states "Any person who, with malice aforethought, causes the death of another person by unlawful act or omission is guilty of murder" Now section 195 gives very well the meaning of the manslaughter "Any person who by an unlawful act or omisson causes the death of another person is guilty pf manslaughter" I t is clear that now one can make a distinction between the two. The only clear distinction one might find is that "malice aforethought" the word caries the latin maxim mens rea which means guilt intention or bad intention. It is from that explaination which puts our conflict mind that manslaughter has no any guilt intention but merely involuntarily act.
I am geting confusion if Isee that some people do contradict the two terms. It is clear from my mind that no prosecutor under Tanzanian law can institute a manslaughter case before the court of law but rather manslaughter case emanate from murder case, it is a lesser offence of murder of which it is under the descretion of the court and not the prosecutor.
It is under the court's descretion after satsfying under all reasonable doubts that the accused person had not killed the deceased with malice aforethought. Interfering this specific job of the court is acting under utra vires by the Director of Public Prosecutor DPP which is also an offence. However this job is normaly made during the judgement delivered by the court when the court will announce that....after cosidering all the evidences tabled before this court by both parties, the court is satisfied beyond all reasonable doubts that the accused person is not guilty of murder but he or she is found guilt of manslaughter.
Therefore under this case before us-Lulu's case it is reasonable to conclude that the DPP has interfered the court',s judicial procedure which is beyond his jurisdiction, he has acted utra vires..he has no mandate to act so but it is more judicial
Coming to last dispute whether manslaughter is bailable or not it is better to understand whether manslaughter can be instituted as a case of first insitance before the court of law? As I have mentioned early that manslaughter can not be instituted before the cort of law but develops from murder case and since murder is a non-bailable offence it is well clear that manslaughter carry the same character. Let us say more clear that manslaughter is not an offence persee but it is subsituted from murder which is not bailable offence. Therefore manslaughter is non-bailable offence....refer section 140 of Criminal Procedure Act.
 
Last edited by a moderator:

House of Lord what the DPP did is to vary the charge sheet..it is within his powers to do so............but the main problem is DPP has no iota of evidence on the matter even for a lesser charge of manslaughter.......
 

Unachokiongea wewe ni "pure theory", in pratice hicho unacho-criticize ndicho kinachofanyika,unadhani legislators walikuwa wajinga kuweka hizo offences zote mbili kwenye Penal Code, do you think Prosecutors hawana mamlaka ya kumcharge mtu na Manslaughter?, ni kweli Manslaughter ni lesser offence kwa Murder lakini theory yako inaaply pale tu am ambapo mtu alishtakiwakwa Murder lakini mwisho wa siku ikaonekana ushahidi uliotolewa unassuport Manslaughter zaidi kwa hiyo mahakama inaweza kumconvict kwa Manslaughter (suo mottu) ingawaje Charge ilikuwa ni ya Murder.

Kumfungulia mtu mashtaka ya Manslaughter inawezekana kabisa although mara nyingi huwa inakuja at the later stages maana kwa mara ya kwanza theory ya prosecutors huwa inapoint on Murder (rightly so because it is the capital offence) lakini baadae wakiona upelelezi wao umeshindwa kupata ushahidi wa kutosha kuprove dhamira ya kuua (malice aforethought or mens rea) lakini matendo mengine yote yanasupport Manslaughter basi huwa wanabadilisha mashtaka kutoka kwenye Murder kwenda Manslaughter (kumbuka tofauti pekee ya ingredients za offence hizi mbili ni presence/absence of malice aforethought).

Pia umeshawahi kusikia kitu kinaitwa "plea bargain"?.,kama bado fanya research kidogo utajua impact yake kwenye charges (simaanishi kuwa ndicho kilichofanyika kwenye kesi ya Lulu)-hiyo huwezi kuipata kwenye statutes although in practice inafanyika.

Kuhusu dhamana kwenye Manslaughter hiyo mbona ipo wazi sana,section 148 (5)(a)(i) inazuia bail kwenye Murder na sio Manslaughter,hizi ni offence mbili tofauti mkuu,unless mtu anyimwe dhamana kwa grounds nyingine (si unajua offence inaweza kuwa bailable lakini bado ukakosa dhamana?) soma section 148(5)(b-e) ya Criminal Procedure Act.

Halafu point of correction.,section 140 uliyorefer haizunguzii bail.
 
yote mawili yanawezekana lulu kuwa huru au kufungwa ni mazingira ndio yatakayo amua ,suala la umri lulu atatakiwa athibitishe mahakamani alizaliwa lini na cheti cha kuzaliwa kionyeshe hivyo ,suala la ripoti ya madaktari nalo hapa ni pazito hapa jamii inatakiwa ijue nin kilisababisha kifo cha kanumba ,suala kama alianguka je alipatwa na kifafa au kuna kitu kilisababisha akaanguka ,hoja bado ni mapema ninacho sisitiza ni kuwa yote mawili yanaweza kutokea ,jamii inachoangalia hasa ni madhara ya pande zote mbili akiachiwa jamii itampokeaje na familia ile ilotendwa itajisikiaje na akifungwa itakuwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…