UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka...

UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka...

1. Nikuongezee mwaka jana kama sijakosea alifanya bonge laparty la kufikisha miaka 18 na alishaojiwa na Ramaradi wa Clouds TV na Salama wa EATV kuhusu maisha yake na alisema kuwa tayari amefika miaka 18 na yuko huru sasa kusaini mikataba mbalimbali yeye mwenyewe kwakuwa sheria inamruhusu hana wakumkataza kwani ni mtu mzima anaelewa jema na baya, tena salama nakumbuka alimchomekea kuhusu kuwa na boyfrien akasema hana kwani she is just 18yrs so anasubiri kwanza aangalie upepo.

2. kama ni 17yrs alifuata nini usiku kwa Kanumba, haya kama ulipigiwa simu kuhusu kazi ya filamu huwa zinafanyika usiku wa zaidi ya saa 6????
ok ni masuala ya kikazi ilikuaje ukaingia chumbani kwake anapo lala na wakati unajua mazungumzo hufanyika sebuleni ama barazani ikiwa uko nyumbani kwa mtu ama Kanumba alimwambia kule chumbani ndio studio waende wakaongee..... narudia tena jana nilisema anayemshauri Lulu anamshauri vibaya kwani wanajifunga wenyewe, ushaidi wa picha hata video za uchafu w lulu zipo, picha za party ya miaka 18 na interview alizohojiwa zipo atatokea wapi??[/QUOTE]

Utata wa umri angalia hapa chini
[h=1]LULU akiongelea maisha yake baada ya MIAKA 18 ndani ya TAKE ONE link hii hapa LULU akiongelea maisha yake baada ya MIAKA 18 ndani ya TAKE ONE - YouTube[/h]

 
Advocate Ruta, umetulia sana. Mimi sio mwanasheria ila naona kuna ugumu wa kuthibitisha pasi shaka kuwa ni kweli lulu alimsukuma kanumba na kuanguka au alimpiga na kitu kizito. Maana waliomuona mwanzo wanadai alitoa povu, kwa uelewa wangu kama angeanguka kwa msukumo angetoa damu au maji na si povu. Lakini tusisahau ushahidi wa madaktari umembeba Lulu tayari. Na maswala ya umri kwa jamii zetu za kiafrika Lulu anaweza kusema mama aliniambia ninamiaka 17 lakini kwa ugumu wa maisha nilijifanya mkubwa ili nipate kazi. Majaji hawatoki mbinguni wanayajua mazingira ya bongo pamoja na njaa zetu.

Mpitagwa waona mbali sana...........usijali hao majaji kwa sababu nafasi zao zenyewe kuzipata ni ufisadi mtupu............sisi tutendelee kutafakari namna ya kurekebisha mfumo mzimwa wa mahakama..........muhimbili hawajatusaidia sana kwa sababu hawajatueleza zile anti hiv cocktail alizokuwa anameza mwendazake zinapochanganywa na jack Daniel na vile vinginevyo vina madhara gani katika mwil na status ya mwendazake ya hiv ilikuwa imefikia hatua gani waathirika wengi wa vvu wanaokunywa pombe na kutumia madawa tajwa huwa wana tabia ya kudondokadondoka na kutokwa mapovu mdomoni sasa sielewi mwendazake alikuwa katika hatua gani................mimi nina miaka 50 sina daktari na wala simhitaji daktari binafsi unapoona nchi masikini kama hii kijana wa miaka 28 ana daktari wake wapaswa kujiuliza alikuwa wa nini kama siyo kumsogezea cocktail bila ya kujulikakana kama naye yumo kwenye tiba endelevu........
 
Rutta,
Nakubaliana na wewe wakati fulani hakuna haja ya kumweka mtu ndani kama hujakamilisha uchunguzi. Yule RPC alisema tunafanya uchunguzi, lakini jumanne tutampeleka mahakamani. Unafanya uchunguzi lakini tayari una conclusion. Ndo mambo ya yule kiongozi wa Polisi aliyetumwa kuchunguza vurugu Songea............

Nakubaliana kabisa kesi kama hizi zinahitaji weledi mkubwa sana katika kuchunguza kuliko kukimbilia kuwa Lulu ndo ameua. Kuna maswali machache ya kujiuliza
  • Je ilimchukua muda gani mdogo wa SK kusikia kelele za vurugu hadi kuingia chumbani kwa Kanumba
  • Kwanini hakutoka mara moja wakati vurugu zinaendelea
  • Je Lulu aliondoka na usafiri gani toka hapo nyumbani
  • Dr wa SK alikuwa umbali gani toka eneo la tukio
  • Ilichukua muda gani kumuita Daktari wa Kanumba hadi kufika hapo?
  • Je unapomuona mtu unconscious kama vile hatua ya kwanza ni kumuita daktari au kumkimbiza hospitali
  • Je SK alikuwa na matatizo kama hayo kiasi kwamba mdogo aliona bora amuite DR wake kama anavyofanya-ga siku zote
  • Je SK alikuwa na maradhi/hali ya afya yoyote inayojulikana?
  • Je SK alikuwa anatumia dawa zozote - was he under medical prescription
  • Kwanini Dr aliamua kumpigia simu Lulu?
  • Nani alipiga simu kwa wasanii ambao walikuwepo kwenye msafara wa kupeleka maiti Muhimbili?
  • Katika hali ya kuchanginyikiwa vile inawezekana vipi mwanafamilia angeweza kupiga simu kwa wasanii
 
lulu-top.jpg

Elizabeth Michael Kimemeta

Mkakati wa Lulu kujitoa kenye makucha ya hii dola kandamizi sasa umeanza kuchipuka pale ambapo mshitakiwa wa hii kesi ya mauaji alipokerwa pale mahakamani alipokuwa akisomewa mashtaka tajwa dhidi yake na hata kunyosha kidole na kutoa sahihisho ya kuwa umri wake ni miaka 17 na wala siyo 18. Kwa kawaida kwenye kesi za mauaji mara ya kwanza husomwa katika mahakama ya hakimu mkaazi na mshitakiwa anayo haki ya kukaa kimya kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo lakini Lulu aliona aanze kuweka utetezi wake vyema hata katika hatua hiyo ya awali...............

Athari za kisheria za umri wa miaka 17
.

Umri huo unamweka Mwendazake -Steven Kanumba- ambaye ana umri wa miaka 28 katika khali mbaya ya kitabia na mwenendo kulingana na sheria ya makosa ya kijinai katika kujamiana pamoja na ya kuwa kwa vile yeye ni marehemu hawezi kushitakiwa nayo lakini yanapunguza makali ya Lulu kuwa na kesi tajwa ya kujibu.

Umri wa miaka 17 ni binti mtoto na wala siyo mtu mzima hivyo kuwa na mapenzi naye hata kama alipenda iwe hivyo unamgeuzia kibao mwendazake kuwa alikuwa anakusudia au alikuwa akimbaka Lulu na hivyo kuweka kesi ya mauaji kuwa na utetezi wa "self-defence" kwa maana ya kuwa Lulu alifanya yoyote yale yaliyo ndani ya uwezo wake kujitetea dhidi ya mwanaumme mtu mzima tena mwenye umri wa miaka 28 aliyekuwa anamkamia kumbaka.

Vilevile umri tajwa unamwondolea Lulu adhabu ya kifo endapo mahakama kuu itamtia hatiani kwenye makosa ya mauaji (very unlikely, though- uwezekano wa kumtia hatiani ni mdogo sana) na pia kumpa haki ya kuondolewa kwenye lupango ya watu wazima jambo ambalo polisi wetu wameendelea kukiuka haki zake kwa kumchanganya na lupango ya watu wazima. Utetezi wa kiawali wa Lulu unakuwa hauna mashiko pale Lulu atakapolalamikia ya kuwa polisi walimlazimisha kumshikilia kwenye lupango ya watu wazima na hivyo kumfanya aghafilike kiakili na hivyo kushindwa kutoa ushahidi sahihi na hivyo kuilazimu mahakama kuutupilia mbali ushahidi wa kiawali na hivyo kumruhusu autoe ushahidi mpya ambao ndiyo huu ninaouchambua na kuuwakilisha hivi sasa.

Lakini kubwa zaidi ni utetezi wa kimazingira ambao Lulu atautoa mahakamani wa ya kuwa yeye ni kinda wa chini ya miaka 18 na hivyo utamweka mwendazake katika mazingira ya kiubakaji au kukusudia kumbaka na hivyo utetezi wa self-defence kuwa na uzito wa kipekee.

Haya ni baadhi tu ya dondoo ambazo Lulu aweza kuzitumia katika kujinasua katika makucha tajwa:-


a) Mwendazake ndiye aliyemwita kuwa ana mazungumzo naye ya haraka usiku wa tukio juu ya tasnia ya filamu. Hivyo yeye Lulu hakuwa na makusudio ya kwenda kwa Kanumba kwa minajili ya kumwuuwa. Kumbuka DPP ni lazima athibitishe nia ya kuua ili mahakama imtie hatiani Lulu lakini kama ni kanumba ndiye aliyemwita mtuhumiwa nia ya Lulu kwenda kwa mwendazake kwa nia tajwa itaota mbawa kuwa isingewezakana kuwa vivyo kama DPP anavyodai.

b) Marafiki wa Lulu watathibitisha ya kuwa wao ndiyo waliokuwa wakimpigia simu na kutaka kujua alikuwa wapi na kwa nini amechelewa. Ushahidi huu wa kimazingira utazidi kubomoa hoja ya polisi ya kuwa Lulu alikwenda kwa mwendazake kwa nia ya kumtoa roho.

c) Lulu atathibitisha mahakamani ya kuwa kanumba siye mpenzi wake na kwa hivyo hoja ya DPP kuwa kulikuwa na ugomvi wa mapenzi kukosa mwelekeo.

d) Lulu atajenga hoja ya kuwa Kanumba alitaka kumbaka na yeye alitumia nguzu za mikono yake kujihami na kutokana na umri wa miaka 17 mahakama lazima ikubaliane naye ukizingatia mazingira yenyewe: Yawaje mtu mzima amkaribishe binti mdogo wa chini ya miaka 18 chumbani mwake kama lengo siyo kumbaka? Yawaje Kanumba akutwe hana nguo kwa maana ya kuwa yuko uchi wa mnyama na binti mdogo hivyo tena chumbani kwake? Kwa hiyo, hata kama lulu alitumia silaha iliyokuwemo chumbani kujilinda, mahakama itampa manufaa ya "benefit of doubt" na hivyo kuukubali utetezi wake. Lulu hakutumia silaha yoyote kulingana na ushahidi uliopo mikononi mwa DPP.

e) Lulu atadai kilichomwangusha Kanumba chini na kukosa fahamu hakina uhusiano na yeye bali ni matatizo yake ya kiafya na atatumia taarifa ya madaktari wa Muhimbili kuthibitisha ya kuwa kilichomtoa roho mwendazake ni mshtuko mkubwa katika ubongo wake (Brain concussion) ambao haukusababishwa na majeraha ya mwilini mwake ambayo hata hivyo hayapo. Mwendazake hakuwa na jeraha lolote kuonyesha lingeweza kumsababishia mshtuko tajwa.

f) Lulu atadai mahakamani ya kuwa hakuna ushahidi wowote ule wa kitaalamu ya kuwa marehemu alikufa kwa lolote jinginelo na inashangaza hata DPP kumfungulia kesi ya mauaji na hivyo kumbughudhi na kumdhaliliisha mbele ya jamii na hivyo kuiomba mahakama iangalie namna ya kumfidia dhidi ya kubambikiziwa kesi ambayo hata haipo au "malicious prosecution".

g) Lulu atarejea ushahidi wa ndugu wa marehemu aitwaye Seth ambaye alidai Lulu ana mazoea ya kwenda pale na ya kuwa hakuona kama kuna ubaya wowote kwa hiyo alimkaribisha na ya kuwa kaka yake ndiye aliyeanzisha zengwe pale aliposikia mlio wa simu ya Lulu na kuhisi ya kuwa Lulu alikuwa anapigiwa simu na mwanaumme mwingine. Hapa lengo litakuwa kuonyesha ya kuwa kama kuna ugomvi marehemu ndiye aliyeuanzisha kwa minajili ya kumbaka kwa kumzuia asiendelee na safari zake. Vile vile mdogo wa marehemu- Seth- aliona Lulu siyo mtu wa shari na ndiyo maana hakumzuia kuingia ndani kutokana na kuwa mtu wa amani na siyo wa hata kuweza kutishia maisha ya nduguye..........

kwa ushahidi huu na mwingineo mwingi, hakuna Jaji ambaye atakubali kuchafua heshima yake kwenye jamii na kuhalalisha mabinti wadogo wafanyiwe unyama hata kama unyama huo unafanywa na aliyekuwa akijiita mwenyewe "mcheza filamu nambari moja hapa nchini".

Hivyo basi mahakama itaamua Lulu hana kesi ya kujibu na mwendazake ndiye aliyejenga mazingira kwa yote yaliyomkuta na hapaswi kumtupia lawama mtoto mdogo aliyechini ya miaka 18.......

FUNDISHO KWETU SOTE


Aidha ni jukumu la watu wazima kuwa mfano wa malezi ya watoto wadogo badala ya wao kuwarubuni na kuwafunza namna ya kuyaharibu maisha ya watoto hao kupitia makosa ya jinai ya ubakaji kwa kuwarubuni na kuwapa ajira njaa za hapa na pale.............

Ruta hoja ya kupangua utata wa umri wa Lulu hapa;
LULU akiongelea maisha yake baada ya MIAKA 18 ndani ya TAKE ONE link hii hapa LULU akiongelea maisha yake baada ya MIAKA 18 ndani ya TAKE ONE - YouTube


 
Utata wa umri angalia hapa chini
LULU akiongelea maisha yake baada ya MIAKA 18 ndani ya TAKE ONE link hii hapa LULU akiongelea maisha yake baada ya MIAKA 18 ndani ya TAKE ONE - YouTube

huu ushahidi haukubaliki mahakamani - kwani ulitolewa kwa kiapo?-na usiome sheria ya sexual offences jinsi ilivyofafanua nama ya kukusanya uishahidi wa tuhuma za ubajkkaji.........................kauli ya binti mahakamani ni final kama hakuna birth certificate
 
mawazo mazuri lakini mwaka wa kuzaliwa hauwezi kuchakachuliwa na driving licence...............awe nayo au la..........kama anadai ana miaka 17 yabidi tukubali au tutoe ushahidi wa birth certificate inaymuumbua...........na hata kama ana miaka 18 bado utetezi wa kubakwa lazima uchunguzwe..............hata mtu mzima bado aweza kudai kabakwa......
Kwa kutumia cheti cha kuzaliwa tena bongo Kwa nini umri usichakachuliwe wakati hapo ulipo unaweza kwenda kwa wanaohusika na ukapata cheti cha kuzaliwa chenye taarifa ulizozitoa wewe?

Habari ya kubakwa imetokea wapi tena wakati mtuhumiwa kasema walikuwa na kutoelewana kwa sababu alipigiwa sm na kutokanayo nje ili apokee ndipo marehemu akahisi kuwa anaongea na mwanaume mwingine na mwenyewe amekiri kuwe alikuwa anaongea na mpenzi wake mwingine?

na alimaliza F4 akiwa na miaka 15?

Siungi mkono mahusiano ya kimapenzi na mabinti wadogo.
 
Mimi pia siyo Mwanasheria lkn nataka kuunga mkono hoja ya Allien kuwa utetezi wa Bwana Ruta hauna mashiko,anafikiria mambo kwa juujuu sana,anasahau kabisa kuwa technology siku hizi inaweza kurahisha mambo mengi tofauti na zamani...kwanza nikianza na suala la umri,nakumbuka mwaka jana tukielekea mwishoniX2 Lulu alifanya bonge la party ya birthday yake ya kufikisha miaka 18 na ndo hapo alipokuja na kauli mbiu ya kuwa yeye si "WATOTO SHOW" tena bali ni "WAKUBWA SHOW" sasa iweje leo hii arudie kwenye miaka 17 tena?!! nafahamu Wanasheria wake watakuwa wanamfunza namna atakavyoweza kuepuka mkono mkali wa sheria kwa kigezo cha kutofikisha umri wa ki'utu uzima lkn kama Washtaki watakuwa makini lazima watamtia hatiani tena kwa kosa lingine la kujaribu kudanganya umri hata kama watakuwa wametengeneza cheti kingine cha kuzaliwa kitakachokuwa kinamuonyesha ana miaka 17,trust me guys.
2. Suala la kukana kuwa Kanumba hakuwa Mpenzi wake halipo ksbb technolojia pia inaweza kulithibitisha hilo pasipo shaka yeyote kupitia mawasiliano waliyokuwa wakifanya siyo siku hiyo tu hata siku za nyuma, na katika hilo mawasiliano ya mtu na Mpenzi wake lazima yataonekana tofauti na yale ya mtu na Mbakaji wake, na si hivyo tu hata kitendo cha yeye kukiri kuwa Kanumba alikuwa ni Mpenzi wake na kisa cha ugomvi wao siku ile ni yeye kupokea simu ya Basha'ke mwingine siyo tu kinaondoa maswali katika hili bali pia kinaonyesha(kama alivyosema Bwn Allien) ni jinsi gani alivyokomaa katika tasnia ya ugawaji uroda usio na mpangilio.
3. Napenda kumkumbusha Bwana Ruta kuwa watakaotakiwa kuthibitisha kuwa Lulu alipigiwa simu na nani siyo marafiki zake ni Service provider(i.e Tigo,Voda etc) ambao mtandao wao ulitumika katika mawasiliano yale kwahiyo utetezi huu na wenyewe ni "0"
4. Tayari Madaktari wameshatoa report ya kiichosababisha kifo chake ambacho ni mtikisiko wa Ubongo kwa jina la kitaalamu inajulikana kama "brain concussion" na hii inaweza kusababishwa na mtu kijigonga kichwa sehemu ya nyuma,huwa haitokei tu mtu amekaa au amelala ubongo ukatikisika,wataalamu wanasema lazima kichwa kigonge sehemu fulani,sasa tukiunganisha na kukiri kwake kuwa walikuwa na ugomvi ndo tunapata taswira ya kuwa alimsukuma na kusababisha aliyekuwa Msanii wenu Nguli kuwa "Mwendazake"
Kwahiyo kwa mtazamo wangu mimi Dogo hawezi kukwepa mkono wa sheria,lazima atatiwa hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia ambalo definately litakuwa lina disqualify utetezi wa kuwa Kanumba ndiye alimpigia simu kumuita aende wakajadiliane vitu gani sijui.
I can bet kama sheria itaachwa ichukue mkondo wake Dogo haruki hata iweje.

Umesema wewe kuwa SI MWANASHERIA, mwisho kabisa una conclude kuwa: 'Dogo haruki hata iweje' So why do you bet, if you know that you are ignorant of the Law?
 
Sasa haka katoto kalienda kufanya nini chumbani kwa wakubwa usiku?Au kalikuwa kidnapped????

hata kama kalienda kwa hiari yake kubakwa bado kanalindwa na sheria ya sexual offences act............
 
Umesema wewe kuwa SI MWANASHERIA, mwisho kabisa una conclude kuwa: 'Dogo haruki hata iweje' So why do you bet, if you know that you are ignorant of the Law?

Okuberwa uko kwenye mstari kabisa....tatizo la wachangiaji wanaona DPP ni kama Mungu kwa hiyo kama kafungua jarida basi wanaona huo ndiyo the gospel truth...................wanafuatilia tu kam anyumbu a wavivu katiak kutafakari............
 
Kwa kutumia cheti cha kuzaliwa tena bongo Kwa nini umri usichakachuliwe wakati hapo ulipo unaweza kwenda kwa wanaohusika na ukapata cheti cha kuzaliwa chenye taarifa ulizozitoa wewe?

Habari ya kubakwa imetokea wapi tena wakati mtuhumiwa kasema walikuwa na kutoelewana kwa sababu alipigiwa sm na kutokanayo nje ili apokee ndipo marehemu akahisi kuwa anaongea na mwanaume mwingine na mwenyewe amekiri kuwe alikuwa anaongea na mpenzi wake mwingine?

na alimaliza F4 akiwa na miaka 15?

Siungi mkono mahusiano ya kimapenzi na mabinti wadogo.

utetezi wa mtuhumiwa mbele ya mahakama ya kuwa yeye ni mtoto usiupuuze hata chembe...................chini ya sheria ya sexual offences act mtoto kama huyo hana hatia kwa sababu hapaswi kujua au kufuata sheria ila wewe ambaye umezidi miaka 18 unapaswa kumwongoza kuwa umri bado hauruhusu usipofanya hivyo maji yanapomwagika ndipo utakapoonja joto la jiwe............
 
Sababu zinazofanya nisiamini yupo under 18-
!. Alishakiri mwenyewe kwenye interview kuwa ana miaka 18
2. Ana drive gari kwa maana hy ana driving license
3. Ame saini mikataba na kampuni za filamu
4. Ana bank account ambapo anatoa na kuweka pesa mwenyewe
5. Anaingia night club
6. Ninahisi anaweza akawa na passport
7. Katika mfumo wetu wa elimu mara nyingi wanaomaliza kidato cha nne miaka yao ina range kwenye 18
Mazingira kama hayo hapo juu yananifanya nipate wasiwasi na umri wake manake kuwa na kufanya vitu kama hivyo lazima uwe na miaka 18+

Mkuu hapa ruta atapotezea as if hajaona kwakuwa hana majibu...
 
Rutta,
Nakubaliana na wewe wakati fulani hakuna haja ya kumweka mtu ndani kama hujakamilisha uchunguzi. Yule RPC alisema tunafanya uchunguzi, lakini jumanne tutampeleka mahakamani. Unafanya uchunguzi lakini tayari una conclusion. Ndo mambo ya yule kiongozi wa Polisi aliyetumwa kuchunguza vurugu Songea............

Nakubaliana kabisa kesi kama hizi zinahitaji weledi mkubwa sana katika kuchunguza kuliko kukimbilia kuwa Lulu ndo ameua. Kuna maswali machache ya kujiuliza

  • Je ilimchukua muda gani mdogo wa SK kusikia kelele za vurugu hadi kuingia chumbani kwa Kanumba
  • Kwanini hakutoka mara moja wakati vurugu zinaendelea
  • Je Lulu aliondoka na usafiri gani toka hapo nyumbani
  • Dr wa SK alikuwa umbali gani toka eneo la tukio
  • Ilichukua muda gani kumuita Daktari wa Kanumba hadi kufika hapo?
  • Je unapomuona mtu unconscious kama vile hatua ya kwanza ni kumuita daktari au kumkimbiza hospitali
  • Je SK alikuwa na matatizo kama hayo kiasi kwamba mdogo aliona bora amuite DR wake kama anavyofanya-ga siku zote
  • Je SK alikuwa na maradhi/hali ya afya yoyote inayojulikana?
  • Je SK alikuwa anatumia dawa zozote - was he under medical prescription
  • Kwanini Dr aliamua kumpigia simu Lulu?
  • Nani alipiga simu kwa wasanii ambao walikuwepo kwenye msafara wa kupeleka maiti Muhimbili?
  • Katika hali ya kuchanginyikiwa vile inawezekana vipi mwanafamilia angeweza kupiga simu kwa wasanii

yaani sikutegemea kama nitakutana na michango mizito kama hii. Keep it up Kintiku...afya ya mwendazake ndipo kesi inakatikia ikichanganywa na matumizi ya pombe kali na huku akitumia madawa ya kupunguza makali ya vvu..........lakini huo nimjadala mpya nitaufugnua siku nyingine baadaya kupata takwimu fulani fulani ambazo ninazisubiria...........maswali ambayo unajuliza ndiyo any serious DPP angelijiuliza badala ya kupokea mshahara mkubwa na kutarajia malipo ya pensheni ya viongozi kwa utendaji bomu kama huu wa kufungua kesi ya mauaji kwa kifo kilichosababishwa na uzembe wa kuchanganya pombe kali na adawa ya cocktail za vvu..........muhimbili nao walipaswa kutoa tamko kuhusu hilibadala ya kuzungumzia hisia zao za nini kina sababisha "brain concussion"
 
Du! Mawakili wetu wa Bongo bwana, No wonder magereza yamejaa.
 
Mkuu hapa ruta atapotezea as if hajaona kwakuwa hana majibu...

hizo hoja za matendo ya mtoto yanhalalisha kubakwa hazikubaliki mahakamani. sheria inamtambua mtoto hajui afanyacho........usiende huko mtaani ukabaka mtoto halafu kesho ukasema mbona alikuwa anafanywa na wengi au kila siku yuko night club.................hakuna atayekusikiliza........
 
Du! Mawakili wetu wa Bongo bwana, No wonder magereza yamejaa.

magereza yanajaa kwa sababu ya mawakili au maovu yameongezeka au magereza ni chache na haziendani na mahitaji ya jamii.........??????????.......achana na majibu mepesi kwa maswali magumu.............
 
huu ushahidi haukubaliki mahakamani - kwani ulitolewa kwa kiapo?-na usiome sheria ya sexual offences jinsi ilivyofafanua nama ya kukusanya uishahidi wa tuhuma za ubajkkaji.........................kauli ya binti mahakamani ni final kama hakuna birth certificate

Mkuu mwazoni nilielewa hoja yako lakini kadri unavyozidi kuitetea unapotoka.......
Unataka kuniambia ni document ya birth certificate tu ndio inaweza kuthibitisha umri wa LULU?
Na kama haipo ni kauli yake tu mahakamani ndio inathibitisha umri wake?

What about kadi za kliniki, rekodi zake shuleni, vyeti vya ubatizo, driving license, passport nk
Unataka kutuaminisha ni LULU pekee anayetakiwa kuthibitisha umri wake kwa kutamka mahakami kama hakuna Birth cert?
Hivi LULU na mzazi wake ni nani anatakiwa kuthibitisha umri wa LULU mahakamani
 
Lukolo, Lukolo..........anza na hii mada tangia mwanzo.............ukifanya hivyo utagundua ya kuwa sheria zote tata za umri wa msichana zilirekebishwa na sheria ya sexual offences act cap 101........................umri wa msichana unaishia akifikisha miaka 18 na chini ya hapo ukimgusa hata kwa ridhaa yake umembaka.........

Acha kuinajisi tasnia ya sheria wewe... ni juzi tu nilikuwa kwenye mkutano wa wadau wa CHRAGG na pale tulikuwa na mawakili toka ofisi ya mwanansheria mkuu wa serekali pamoja na wizara ya katiba na sheria kuangalia Mambo ambayo Tanzania inatuhumiwa na UN kuwa yanakiuka sheria. Mojawapo lilikuwa kuendelea kuruhusu sheria ya ndoa kutambua ndoa ya under 18 with the consent of parents... Majibu ya serekali (ninayo hardcopy) ni Kuwa Swala hilo lijadiliwe kwanza na wadau kabla ya kutolewa maamuzi kwani ni sensitive na linagusa imani za kidini..... Leo hii wewe unayejiita mwanasheria unatudanganya kuwa SOSPA imefuta?? Kifungu gani?? Umeisoma yote??

Nakumbuka pia ulitolewa pia mfano wa issue ya binti wa miaka 15 aliyekuwa ameolewa huko mbagala if i am not mistaken, kwa shinikizo la wazazi akakimbilia TAMWA na ITV wakarusha taarifa yake siku moja kabla ya hicho kikao ambapo yule bwwana alipohojiwa na mtangazaji aliljibu kuwa "Kwani nimevunja sheria gani wakati sheria ya kidini na ya nchi inaniruhusu....Kama mwanataka wanirudishie mahari yangu millioni 2"...


Hoja hapa ni kuwa wewe ni nani hata ubishane na wizara inayohusika na sheria yenyewe inayotambua kuwa hiyo sheria kandamizi bado ni operatioal?? pamoja na UN?? KWA QUALIFICATIONS GANI ULIZO NAZO??KWANZA NAASSUME WANASHERIA WOTE MAKINI WAPO MAHAKAMANI SAA HIZI WALA HAWANA MUDA WA KUSHINDA HUMU JF KAMA WEWE MAANA USIKU NA MCHANA KUCHA upo JF... Acha uongo , acha kupotosha umma.

 
Mkuu Ganesh, hii dunia ya vijana naona huifahamu. Siku nyingine wala usiongelee kabisa.

Eti nini? Snoop Dogg hana kwenye Video? Hebu angalia huu wimbo wake na Wiz Khalifa ".... so what we get drunk, so what we smkoke weed (Bangi) .... We are young, wild and free"


Unamtetea Lulu kama vile ni dada yako. Mimi simfahamu huyu Lulu wala Stephen Kanumba,mara ya kwanza kuwasikia ni baada ya huu mkasa. Lakini how do you know kama huyo Lulu hana historia ya ujeuri? In my experience watu kama hawa[akina Lulu] wanaifahamu sheria,wanafahamu kwamba hawapaswi kufanya makosa kama haya,laini wanadhani sheria haziwahusu. Au labda maisha ya alcoholo na rugs wanayoishi hawa vijana matatizo haya. Utaona katika music video za bongo fleva meza zimepambwa vinywaji vikali,jambo ambalo huwezi kuliona katika music video ya Snoop Dogg.
Polisi wakimkamata mtu kwa mahojiano,halafu baada ya mahojiano wakiamua kumshikilia,baada ya kumshikilia wakiamua kumpeleka mahakamani,ujue there could be trouble for that one.
 
Last edited by a moderator:
Nahisi wana Jukwaa tuko nje ya mada, mbona tunajadili kubaka na umri? Kwani Lulu kashitakiwa kwa kosa la kubaka mahakamani.
Hata kama tunajadili uwezekano wa Lulu kujitetea kwa kigezo cha kujitetea ili asibakwe, mbona hakuna mazingira hayo kabisa katika tukio lile?????

Au kuna m2 amemsikia Lulu au mtu wa karibu wa Lulu akijiandaa kupeleka utetezi wa kutaka kubakwa.
Swali Kwani marehemu alikuwa akifanya mapenzi wakati kifo kinamkuta????????

Kubakwa = Penetration of the p*****s into female's v****#na + absence of female consent.

absence of Female Consent inaweza kupatikana through minor age defn.
What about Penetration????????

Je hayo yalitokea??????
 
mawazo mazuri lakini mwaka wa kuzaliwa hauwezi kuchakachuliwa na driving licence...............awe nayo au la..........kama anadai ana miaka 17 yabidi tukubali au tutoe ushahidi wa birth certificate inaymuumbua...........na hata kama ana miaka 18 bado utetezi wa kubakwa lazima uchunguzwe..............hata mtu mzima bado aweza kudai kabakwa......
Hoja zako ni za kulazimisha kbs. Naona unajipa psychological consolation. Subiri tu, muda si mrefu utaujua Ukweli.
 
Back
Top Bottom