Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe unao huo ushahidi?? kwanini kupiga makelele huku huna information yeyote? unataka kutuaminisha wewe unayajua mazingira ya kesi kuliko DPP?? wewe ni mwanasheria au kilaza wa sheria?? Unadhani maisha ya mtu ni sawa na kuku wako unayeweza kumchinja anytime bila kuulizwa?? Watanzania bana... kila kitu wanajua kila kitu wana majibu na ndio maana hatuendelei kuanzia kwenye soka kila mmoja ni kocha na ana majibu hata kwenye upelelezi wa kesi??
hizi hoja nilijkwisha kuzijibu awali pitia tena maelezo yangu ya kuwajibu wachangiaji wengineo.......kifupi tu hakuna mahakama itakayohalalisha wachumba kuvunja sheria ya ubakaji.............leo ubake mtoto wa watu halafu utewtezi uwe nimemwoa au nitamwoa...............hiyo itakula kwako..............gusa watoto wa watu khalafu nenda na huu utetezi ndipo utajua mvua za mawe zimedondokea wapi...................huhitaji kuwa mwanasheria kufikiria tatizo lenu mnafikir shule inakupa vipaji.............shule yaweza kuviendeleza vipaji lakini Ni Mwenyezi Mungu ndiyo anayekupa vipaji na waweza kuviendeleza bila ya hata siku moja kukaa darasani........usikubali kuwa mtumwa wa kutafuniwa darasani jifunze kutafuna mwenyewe..........meno....brain/ubongo umepewa wa nini?
kosa la marehemu kushindwa kucontrol hasira zake
DPP utendaji wake ni maruerue tu wakati umefika wa kuangalia ni kwa nini wale walioshindwa darasani ndiyo tunawasukuma waende polisi na matokeo ndiyo haya haki zetu zinapindishwa kwa sababu DPP mwenyewe na wasaidizi wake ni vilaza............hawana uwezo wa kutafakari hata kidogo na nionavyo kuna watuhumiwa weggi wa kesi za mauaji wengi wako mahabusu ambapo hawastahili kuwa huko kwa kulingana na ushahidi uliopo........
Sijui hata kama unataarifa kuwa kwa sheria za bongo mtoto wa miaka 15 anaruhusiwa kuolewa kwa consent ya wazazi wake sasa sijui hiyo hoja ya ubakaji ulojishika nayojishika kwa kicheche kinachosingizia miaka 17 unasitoa wapi. Tumefuatilia mahojiano yake alipokuwa akiongea hadi mishipa inamtoka kuwa yeye tayari ana miaka 18 na akafanya party. Sijui kama umeona pia statementi aloitoa mama yake lulu ambayo ukimsikiliza kwa masikio mawili anakiri kufahamu mahusiano yaliyokuwepo.
magazeti yanaripoti walichosimuliwa.................Lulu ndiye mwenye taarifa sahihi. Mpira umekwisha...the gal is innocent. full stop........
Aisee!!!, nina wasiwasi na uelewa wako wa sheria na utendaji wa vyombo vya dola, DPP sio polisi ni raia mwema kama mimi na wewe tu, tofauti ni kuwa yeye amesomea sheria na kuteuliwa na Mh. Rais kuwa DPP.
Huyo Lulu alishaojiwa Clouds TV kwenye kipindi cha Take one. Alikuwa amefikisha umri wa miaka 18 na alikuwa amefanya birthday party,,, Na alikuwa anajipongeza kwa kufikisha umri huo... Alisema hii ndio fursa yake ya kuanza kufanya mambo makubwa zaidi maana umri ulikuwa kikwazo kwake... Sasa ishu ya umri hapo haina mshiko wala ukweli,... Umri wake upo wazi kwa kila mtanzania...
tabia yake haihalalishi abakwe...............kwa hiyo hoja zako Alien 1-9 zinapoteza mwelekeo. Hoja no. 10 ya kuwa mahakama itazingatia mob-justice....................sioni hata umuhimu wa kujibu kwa sababu that is the last thing the court wants to entertain....................pitia polepole hoja zangu utagundua Lulu has no case to answwer ila DPP anafanyakazi kwa mashinikizo ya mob-justice na wala siyo kwa kuongozwa na sheria au ushahidi alionao mikononi mwake..........
Muhimbili wamesema ni kifo cha kawaida....................haya yote wala hayana maana yoyote.........
zaidi ya asilimia 99 ya wateule wa Raisi hawana sifa na ndiyo maana nchi hii ni masikini pamojana kuwa na utajiri asilia kibao..............hata Nyerere mwenye alikiri kuwa tuna kila sababu ya kuendelea lakini kikwazo chetu ni uongozi mbovu..............as I have said be4 DPP huyu ni bomu na hata yule aliyemteua ana walakini...........
![]()
Elizabeth Michael Kimemeta
Mkakati wa Lulu kujitoa kenye makucha ya hii dola kandamizi sasa umeanza kuchipuka pale ambapo mshitakiwa wa hii kesi ya mauaji alipokerwa pale mahakamani alipokuwa akisomewa mashtaka tajwa dhidi yake na hata kunyosha kidole na kutoa sahihisho ya kuwa umri wake ni miaka 17 na wala siyo 18. Kwa kawaida kwenye kesi za mauaji mara ya kwanza husomwa katika mahakama ya hakimu mkaazi na mshitakiwa anayo haki ya kukaa kimya kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo lakini Lulu aliona aanze kuweka utetezi wake vyema hata katika hatua hiyo ya awali...............
Athari za kisheria za umri wa miaka 17.
Umri huo unamweka Mwendazake -Steven Kanumba- ambaye ana umri wa miaka 28 katika khali mbaya ya kitabia na mwenendo kulingana na sheria ya makosa ya kijinai katika kujamiana pamoja na ya kuwa kwa vile yeye ni marehemu hawezi kushitakiwa nayo lakini yanapunguza makali ya Lulu kuwa na kesi tajwa ya kujibu.
Umri wa miaka 17 ni binti mtoto na wala siyo mtu mzima hivyo kuwa na mapenzi naye hata kama alipenda iwe hivyo unamgeuzia kibao mwendazake kuwa alikuwa anakusudia au alikuwa akimbaka Lulu na hivyo kuweka kesi ya mauaji kuwa na utetezi wa "self-defence" kwa maana ya kuwa Lulu alifanya yoyote yale yaliyo ndani ya uwezo wake kujitetea dhidi ya mwanaumme mtu mzima tena mwenye umri wa miaka 28 aliyekuwa anamkamia kumbaka.
Vilevile umri tajwa unamwondolea Lulu adhabu ya kifo endapo mahakama kuu itamtia hatiani kwenye makosa ya mauaji (very unlikely, though- uwezekano wa kumtia hatiani ni mdogo sana) na pia kumpa haki ya kuondolewa kwenye lupango ya watu wazima jambo ambalo polisi wetu wameendelea kukiuka haki zake kwa kumchanganya na lupango ya watu wazima. Utetezi wa kiawali wa Lulu unakuwa hauna mashiko pale Lulu atakapolalamikia ya kuwa polisi walimlazimisha kumshikilia kwenye lupango ya watu wazima na hivyo kumfanya aghafilike kiakili na hivyo kushindwa kutoa ushahidi sahihi na hivyo kuilazimu mahakama kuutupilia mbali ushahidi wa kiawali na hivyo kumruhusu autoe ushahidi mpya ambao ndiyo huu ninaouchambua na kuuwakilisha hivi sasa.
Lakini kubwa zaidi ni utetezi wa kimazingira ambao Lulu atautoa mahakamani wa ya kuwa yeye ni kinda wa chini ya miaka 18 na hivyo utamweka mwendazake katika mazingira ya kiubakaji au kukusudia kumbaka na hivyo utetezi wa self-defence kuwa na uzito wa kipekee.
Haya ni baadhi tu ya dondoo ambazo Lulu aweza kuzitumia katika kujinasua katika makucha tajwa:-
a) Mwendazake ndiye aliyemwita kuwa ana mazungumzo naye ya haraka usiku wa tukio juu ya tasnia ya filamu. Hivyo yeye Lulu hakuwa na makusudio ya kwenda kwa Kanumba kwa minajili ya kumwuuwa. Kumbuka DPP ni lazima athibitishe nia ya kuua ili mahakama imtie hatiani Lulu lakini kama ni kanumba ndiye aliyemwita mtuhumiwa nia ya Lulu kwenda kwa mwendazake kwa nia tajwa itaota mbawa kuwa isingewezakana kuwa vivyo kama DPP anavyodai.
b) Marafiki wa Lulu watathibitisha ya kuwa wao ndiyo waliokuwa wakimpigia simu na kutaka kujua alikuwa wapi na kwa nini amechelewa. Ushahidi huu wa kimazingira utazidi kubomoa hoja ya polisi ya kuwa Lulu alikwenda kwa mwendazake kwa nia ya kumtoa roho.
c) Lulu atathibitisha mahakamani ya kuwa kanumba siye mpenzi wake na kwa hivyo hoja ya DPP kuwa kulikuwa na ugomvi wa mapenzi kukosa mwelekeo.
d) Lulu atajenga hoja ya kuwa Kanumba alitaka kumbaka na yeye alitumia nguzu za mikono yake kujihami na kutokana na umri wa miaka 17 mahakama lazima ikubaliane naye ukizingatia mazingira yenyewe: Yawaje mtu mzima amkaribishe binti mdogo wa chini ya miaka 18 chumbani mwake kama lengo siyo kumbaka? Yawaje Kanumba akutwe hana nguo kwa maana ya kuwa yuko uchi wa mnyama na binti mdogo hivyo tena chumbani kwake? Kwa hiyo, hata kama lulu alitumia silaha iliyokuwemo chumbani kujilinda, mahakama itampa manufaa ya "benefit of doubt" na hivyo kuukubali utetezi wake. Lulu hakutumia silaha yoyote kulingana na ushahidi uliopo mikononi mwa DPP.
e) Lulu atadai kilichomwangusha Kanumba chini na kukosa fahamu hakina uhusiano na yeye bali ni matatizo yake ya kiafya na atatumia taarifa ya madaktari wa Muhimbili kuthibitisha ya kuwa kilichomtoa roho mwendazake ni mshtuko mkubwa katika ubongo wake (Brain concussion) ambao haukusababishwa na majeraha ya mwilini mwake ambayo hata hivyo hayapo. Mwendazake hakuwa na jeraha lolote kuonyesha lingeweza kumsababishia mshtuko tajwa.
f) Lulu atadai mahakamani ya kuwa hakuna ushahidi wowote ule wa kitaalamu ya kuwa marehemu alikufa kwa lolote jinginelo na inashangaza hata DPP kumfungulia kesi ya mauaji na hivyo kumbughudhi na kumdhaliliisha mbele ya jamii na hivyo kuiomba mahakama iangalie namna ya kumfidia dhidi ya kubambikiziwa kesi ambayo hata haipo au "malicious prosecution".
g) Lulu atarejea ushahidi wa ndugu wa marehemu aitwaye Seth ambaye alidai Lulu ana mazoea ya kwenda pale na ya kuwa hakuona kama kuna ubaya wowote kwa hiyo alimkaribisha na ya kuwa kaka yake ndiye aliyeanzisha zengwe pale aliposikia mlio wa simu ya Lulu na kuhisi ya kuwa Lulu alikuwa anapigiwa simu na mwanaumme mwingine. Hapa lengo litakuwa kuonyesha ya kuwa kama kuna ugomvi marehemu ndiye aliyeuanzisha kwa minajili ya kumbaka kwa kumzuia asiendelee na safari zake. Vile vile mdogo wa marehemu- Seth- aliona Lulu siyo mtu wa shari na ndiyo maana hakumzuia kuingia ndani kutokana na kuwa mtu wa amani na siyo wa hata kuweza kutishia maisha ya nduguye..........
kwa ushahidi huu na mwingineo mwingi, hakuna Jaji ambaye atakubali kuchafua heshima yake kwenye jamii na kuhalalisha mabinti wadogo wafanyiwe unyama hata kama unyama huo unafanywa na aliyekuwa akijiita mwenyewe "mcheza filamu nambari moja hapa nchini".
Hivyo basi mahakama itaamua Lulu hana kesi ya kujibu na mwendazake ndiye aliyejenga mazingira kwa yote yaliyomkuta na hapaswi kumtupia lawama mtoto mdogo aliyechini ya miaka 18.......
FUNDISHO KWETU SOTE
Aidha ni jukumu la watu wazima kuwa mfano wa malezi ya watoto wadogo badala ya wao kuwarubuni na kuwafunza namna ya kuyaharibu maisha ya watoto hao kupitia makosa ya jinai ya ubakaji kwa kuwarubuni na kuwapa ajira njaa za hapa na pale.............
ninafahamu lakini akienda polisi kuwa umembaka kwa sababu ya umri mdogo imekula kwako chini ya sexual offence act..............
5. Dotnata ameshadhihirisha nia njema ya Kanumba kuwa alitaka Kumwoa na alikuwa na taarifa rasmi. Lulu alikubali na alisema tatulia lipotakiwa kufanya hivyo. Wamekuwa marafiki for 6 months na Kanumba hakutaka wawe in Spotlight mpaka atangaze Uchumba. Kuna wanaojua walikuwa wanapika na kupakua.
Pia kumbuka katika sheria ya Ndoa Binti under 18 anaweza kuolewa kwa ruksa ya Mzazi.
Mama Lulu na Mama Mlezi wa Wasanii walishabariki uchumba wao kiasi cha kula na kupakua.
Anayo kazi ya kuudhihirishia Mahakama kwa nini ghafla amekuwa 17 na si 18 kama alivyotamba katika media na walimwengu. nani anapooa au anapokuwa na GF anaulizia cheti cha kuzaliwa zaidi ya miaka.
Ushahidi wa Kimazingira tu utamweka pabaya. Imekula kwake japo tunamwonea huruma.