Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Theoretically yes lakin practically kwa nyakati zile nani ndani ya hicho chama angemkatalia Jiwe mwenye mamlaka ya kimungu ya kikatiba? Labda mpinzani lakin siyo mwanassm.
Unajua haya makosa ya dogo ukiiyaangalia kiuhaki kabisa si yake, na wala si ya mwendasake, bali ni ya katiba. kwa asilimia karibu 95 mateso ya watanzania, hasa wanayopewa na wanasiasa, yanatokana na katiba mbovu na dhaifu
 
Yeyr aligeuka kuwa Kama yule malaika wa Mungu mkuu ambaye alilewa madaraka akaanza kuyatumia vibaya. Kama alitumwa akakamata mtambo wa kuunda fedha banfia hilo Ni jema
Kosa lake ni kuamua kuiba baada ya kumkosa mtuhumiwa aliyeelekezwa kumkamata. Kakiri kosa, kasema aliyoyafanya ni mengi ya kutumwa na yake binafsi. Kwa kuwa alitumia madaraka vibaya acha sheria ikae mahala pake. Asubiri tu hukumu. Si salama kwake kumfanya hayati mtetezi wake. Akunbuke kuwa hakuna kinywa cha marehemu kinachofika mahakamani kufanya utetezi. Kwa watu wa kawaida tunasema anatania mahakama na wengine wa kutafsiri maneno Kama watu wa Mithali katika biblia tunamwita ni "Mfamaji"
Ajue tu kuwa Siku za mwizi ni arobaini.
 
 

Attachments

  • 2881413_333.mp4
    6.3 MB
Lakin walau kwa mara ya kwanza imethibitishwa na mtu wa karibu kabisa wa jiwe kuwa jiwe alikuwa katili na mtesaji wa wananchi na ndiye aliagiza wengi waumizwe
 
Watu wameshangaa kijana Ole Sabaya kuwataja baadhi ya viongozi wa juu kwamba walielewa/ kumtuma kile alichokifanya na sasa ameshtakiwa nacho.

Binafsi nimekumbuka nasaa za IGP Sirro kwamba Freeman Mbowe ni binadamu siyo malaika anaweza kukosa kwa namna yoyote ile.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Angekubali Naye ni binadamu na amaweza kukosea musa wote .Ningemuelewa
 
Kuna siku polisi watagoma..
 
Hujaeleweka vizuri,unajaribu kusema kama JPM alikuwa akimtuma Sabaya kufanya ujambazi na unyang'anyi wa kutumia silaha basi yawezekana na Mbowe alituma watu kufanya ugaidi??
 
Asante Mwenyezi MUNGU kwa kuliondosha lile dubwasha kutoka Chato.

Huwa sijui maana ya 'Allah akbar!', huwa nasikia tu wakosema hivyo, sasa kutokana na huo utetezi wa kipuuzi wa Sabaya acha nami leo niseme "ALLAH AKBAR! 📢".

Lakini pia nitasema...

1.PRAISE THE LORD!
2.BWANA MUNGU asifiwe!
3.Sebha Akujiwe!
4.Imana ishimwe!
 
Hayo maagizo yako wapi, achaneni na muhuni kapatikana
Mkuu maagizo au amri si inatolewa kwa maneno, kasheshe iliyopo hapa shahidi ametangulia mbele za haki....ndo maana jambo lililo la umuhimu mkubwa ni katiba mpya ili kusaidia kurekebisha kasoro kama hizi za kiutendaji zinazohusisha mamlaka na wajibu wa kiuongozi......kama rais anaona kabisa mhimili wake umejichimbia zaidi kwenda chini kuliko mahakama na bunge hapo kuna tatizo kubwa sana sana.......
 
nimependa definition ya neno integrity from Oxford dictionary, inasema hivi
integrity:
the quality of being honest and having strong moral principles.
"a gentleman of complete integrity.
Palipo ni furahisha zaidi ni hapa kwny similar words; honest, uprightness, brobity, rectitude, honour, moral, ethics, morality, righteousness, truthfulness, fairness, decency. sincerity, trustworthiness.
UKIWA NA SIFA ZOTE HAPO JUU NI NGUMU WATU KUKUTUMIA KATIKA MAMBO AMBAYO SI MEMA NA WATAKUTOA KWNY SYSTEM MAPEMA SANA ILA UKIWA KINYUME NA SIFA ZA HAPO JUU WATAKUTUMIA NA KUKUTUPA MAPEMA SANA SBB WANAJUA WEWE SIO MUAMINIFU.
Maisha ni kupanga na kuchagua.
 
Hawezi kutoka wilaya moja na kwenda wilaya nyingine bila mwenye mamlaka katika wilaya husika au eneo hilo kuwa na taarifa 'trust me' siri ndio iko hapo lakini kwa wataalama wakiruhusiwa kuunganisha vijiini vya matendo utaamini hicho ndico kilicho tokea huyui katoswa tu kwa sababu ya nyota iling'ara kupindukia kiasi cha kutisha mamlaka.

Kwa usalama zaidi hii kesi itagota na kulazimisha kutogota.......
 
Theoretically yes lakin practically kwa nyakati zile nani ndani ya hicho chama angemkatalia Jiwe mwenye mamlaka ya kimungu ya kikatiba? Labda mpinzani lakin siyo mwanassm.
Ndo maana nimesema, kama mtu alishindwa kukataa kwa kuheshimu mamlaka, bado alikuwa na mwanya wa kuachia ngazi!! Hiki ndicho kinachofanyika hata huko kwa wenzetu, na wala usidhani viongozi wa huko hawatoi maagizo ya hovyo hovyo!!

Kinachotushinda sisi ni kutokuwa tayari "kuachia" ugali!
Unajua haya makosa ya dogo ukiiyaangalia kiuhaki kabisa si yake, na wala si ya mwendasake, bali ni ya katiba. kwa asilimia karibu 95 mateso ya watanzania, hasa wanayopewa na wanasiasa, yanatokana na katiba mbovu na dhaifu
Tuna-overrate sana suala la katiba pale tunapodhani kila tatizo linatokana na katiba mbovu na kwahiyo solution ni katiba mpya!! Tatizo kubwa la Miafrika ni IMMORALITY...

Jamii nyingi kama sio zote za Kiafrika zimeoza sana kimaadili!!

Watu tunaendekeza sana njaa!!!
 
Uthibitisho atatoa tu.
Atautolea wapi?!!

Narudia, ushahidi ambao ungeweza kumsaidia ni wa kimaandishi but there's no way hizo nyaraka eti zinaweza kuelekeza `afanye aliyofanya!! Ndo maana nimesema nyaraka bila shaka zitakuwa na clean instruction lakini akapigiwa simu achukue "hatua zaidi when necessary"!
Kwa hiyo kama alipewa maagizo ya ziada yasiyo fuata sheria si ndo maana tunasema wote mtoaji na mpokeaji ni vululuvululu!!
Hiyo ni assumption, na hoja hapa ni kwamba, hata kama alipewa hayo maagizo bado msalaba utabaki kuwa ni wa kwake! Mosi, I doubt kama atakuwa na huo uwezo wa kuthibitisha! Pili, mamlaka ya uteuzi kwa nafasi yake ni ex-president ambae amefariki lakini hata kama angekuwa hai bado isingemsaidia!!
Nijiulize mara ngapi wakati hilo tumelisema sana wakati wa uhai wa JPM?!

Narudia, tuna-overrate sana umuhimu wa katiba mpya pale tunapodhani kila tatizo solution yake ni katiba mpya na kudhani lau kama tungekuwa na katiba mpya tayari basi tatizo husika lisingetokea!

Katiba mpya ni muhimu sana, tena sana lakini tuna-overrate mno umuhimu wake!!!

Tena kama katiba mpya yenyewe ndo hizi za kufanya miongoni mwa wajumbe kuwa wabunge waliopo huku bunge lenyewe likiwa na over 95% CCM ndo wala usitarajie chochote cha maana!!

Padri au Sheikh hawatakiwi kumuogopa polisi au umma ili wasifanye maovu bali wanatakiwa kumuogopa Mungu kutokana na maandiko matakatifu yanavyosema!

Hata hivyo, nao bado ni miongoni mwa watenda maovu!!! Na wanapochelea kutenda uovu wanaogopa sana mamlaka za kidunia au jamii kuliko kuogopa makatazo ya maandiko takatifu!!

Hiyo ndo jamii tuliyonayo, na ndo maana, wakati Kenya inapata katiba mpya tuliisifia kweli kweli lakini hadi kesho uovu wa viongozi upo pale pale!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…