Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Naamini kwa dhati kabisa kile alichosema Sabaya, kwamba matendo ya kihalifu aliyofanya Arusha ilikuwa maagizo toka mamlaka iliyomteua na alipaswa kutii. Sabaya ameenda mbali, akasema haikuwa mara ya kwanza kupewa maagizo kama hayo.
Na ni wazi kwamba Sabaya kama Mkuu wa Wilaya nje ya Arusha, asingekuwa na uthubutu wa kwenda kutenda mambo kama hayo nje ya mkoa wake. Kwa hiyo lazima kujiamini huko kulitokana na kufanya mambo kwa amri ya Raisi.
Jambo la msingi ni kwamba, ni wangapi waliagizwa kufanya matendo kama haya ya Sabaya na mamlaka zilizowateua? Na je, kuna walioamrishwa kuua raia? Kupotea kwa baadhi ya Watanzania kama kina Ben Saanane na wengineo, ni dalili tosha kwamba inawezekana kuna wengine kama Sabaya waliagizwa kuvunja haki za binadamu na mamlaka za juu zilizowateua, na hata kupoteza haki za watu kuishi.
Tukirudi nyuma kidogo, twapaswa kujiuliza, kwa nini hii mamlaka ya juu ilitoa amri kwa watu kama Sabaya ikijua wazi amri hizo zilikiuka haki za binadamu na hata kuwakosesha watu haki ya kuishi? Ni wazi tatizo liko kwenye Katiba yetu ambapo mamlaka hii ya juu ilitambua haiwezi kamwe kushitakiwa hata ingefanya jambo gani!
Sasa turudi kwa Raisi wetu wa sasa Samia na chama chake CCM. Hawaoni kwamba huu ni upungufu mkubwa sana katika Katiba yetu, kuwa na mamlaka ya juu ambayo yana uhuru wa kutoa maagizo ya kuvunja haki za binadamu na hata kuua kwa kiburi tu cha kujua mamlaka ya juu haiwezi kuwajibishwa kisheria kwa lolote?
Inatutia wasiwasi basi sababu za msingi kwa nini Raisi Samia na CCM wanapinga kwa nguvu zote mabadiliko ya Katiba. Hivi tuingie shaka kwamba Raisi Samia hataki Katiba mpya kwa sababu na yeye angependa kuwa na uwezo wa kutoa maagizo kama aliyopewa Sabaya na wengineo ambao mambo ya kutisha waliyofanya bado hayajawekwa wazi, ili yeye na wengine katika CCM kama Spika, Mwanasheria Mkuu nk wasije wakawajibishwa kisheria hapo baadae?
Kwa msingi huu, utetezi wa Sabaya kwamba alifanya aliyofanya kwa sababu yalikuwa ni maagizo toka mamlaka iliyomteua ni kengelea yenye sauti kubwa kwamba Katiba ya Tanzania ni lazima ifanyiwe mabadiliko.