Simba na Yanga zinaua mpira wa Tanzania na kinachosubiriwa ni kifo tu cha soka. Kila idara inayohusu soka kuna mwana simba au yanga anayetaka timu yake ipate upendeleo au anatumia mamlaka yake vibaya kuzipendelea. Matokeo yake ni kuwa timu zingine zinanyimwa haki na hazipati manufaa ya uwekezaji katika soka. Na kama Azam wamejiingiza katika mkumbo wa kuhonga waamuzi basi ujue soka limeoza. Kuna haja gani ya kuwekeza katika mfumo rushwa? Nchi ya hovyo huishia kufanya vitu vya hovyo katika kila jambo
HIVI TUSEME MPAKA LINI ILI WATU WAELEWE??? Mimi nasema kwa ujasiri mkubwa tena sana nasema kwa ARI MPYA na NGUVU MPYA na KASI MPYA
Simba na Yanga zinaua mpira wa Tanzania na kama TFF na wadau wasipo stukia hili tutazika soka letu moja kwa moja . Kuna mifano mingi inajidhihirisha katika ARGUMENTS zangu.
>>>Moja kwa kipindi kirefu tumeshuhudia jinsi marefa wanayozibeba timu za simba na Yanga ( Na ndio maana siku hizi timu hizi zinaingia na kutolewa round ya kwanza tu!!!AIBU). Tofauti na zamani walau ushindi wao ulikuwa halali maana timu nyingi za mikoani zilikuwa za mashirika ya serikali hivyo zilikuwa zinatoa ushindani wa kutosha.
>>> Nijambo lisilopingika kuwa kwa miaka ya sasa mathalani kila idara inayohusu soka nchini Tanzania si ajabu kusikia kuna mwana simba au yanga anayetaka timu yake ibebwe!! ama ipate upendeleo. Mtu huyu atatumia kila aina ya ushawishi ama mamlaka yake ili kuibeba ama simba au yanga ambayo anaipenda. Matokeo yake soka linakuwa la Yanga na Simba tu. Hata mahala ambambo moja wapo ya timu hizi ni dhaibu bado utashanga bingwa ni Yanga ama Simba
>>> Kuna Mambo yanayotokea uwanjani ambayo tukiacha ushabiki wa Simba ama yanga lazima tuukemee
>>> Mathalani uchezeshaji mpira!! Marefa wengi wamekuwa wakizibeba Simba na Yanga
>>> Ni hivi Karibuni miezi michache iliyopita kocha wa Mtibwa TOM OLABA aliwahi kulalamika kwamba Simba na Yanga zinabebwa na marefa tena akatoa onyo kali kwama ugonjwa huu ukiachwa kuendelea ipo siku TANZANIA TUTAUWANA KAMA KENYA mwisho wa kumnukuu''' Sasa tujiulize hivi kweli mpaka mtu atoe maneno makali namna hiyo bado tu hatuamini kuwa kuna ukweli wa yasemwayo? Naishauri TFF ifuatilie mambo haya na kutoa onyo kali kwa marefa
>>> Ngoja nitoe Mifano michache ambayo nimeshuhudia hivi karibuni ya jinsi marefa wanavyozibeba Simba na Yanga
1. Katika Mechi ya Yanga na Villa Goli la yanga lilikuwa TATA kabisa wala hakuna ubishi Mchezajiwa Yanga alimrukia kipa akiwa ameshika mpira ukamponyoka Yanga wakachukua wakapasiana wakafunga refa kakubali!!!! AIBU sana hii
2. Simba na Mtibwa ....Kulikuwa na move upande wa kushoto sasa beki wa mtibwa alipokuwa anafuata mpira mchezaji wa Simba akamkwatua refa akapeta ...ajabu alivyopeta na simba kuchukua mpira mchezajiwa simba akaguswa kidogo tofauti hata na alivyoguswa wa Mtibwa refa kapiga filimbi Simba wakapoga faulo na kufunga Huu ni unyama
>>> Hivi Tanzania soka ni Simba na Yanga tu kwanini timu zingine zinanyimwa haki na hazipati manufaa ya uwekezaji katika soka.
NAPENDA KUSEMA KUWA HILI HALIKUZI BALI LINAUA SOKA LETU
'''''Nchi ya hovyo huishia kufanya vitu vya hovyo katika kila jambo.....mwisho wa kunukuu'''