UTEUZI: Jaffar Haniu ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu); amrithi Gerson Msigwa

hamna shida ni bora apange na kupangua kadiri anavyotaka na kujaaliwa, ili hapo baadae isije ikatuwa lawama kwa waliokuwepo kwamba hawakuwa chaguo lake,ifike siku tujue ameishaclear vilivyoachwa na sasa ni vyake ili tufaidi mambo yake .
Very true . . wakati utaongea
 
Kwa nini msemaji mkuu wa serikali awe tofauti na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu?
Tofauti yake ni kubwa sana mzee japo wanaweza kuonekana wako sawa but things are quiet different mkuu.
Presidential communication ni kwa ajili ya mawasiliano ya rais pekee. Yaani ni sawa na kumwita
Presidential aide on Communications kama Marekani wanavyomwita.
Msemaji mkuu wa serikali ana portfolio kubwa zaidi ya usemaji. Anaisemea serikali katika sekta zote. Sio umeme, sio mambo ya nje, sio ulinzi, msemaji ni yeye. Huyu ndiye anasema msimamo wa serikali (kwa maelekezo ya serikali) kuhusu jambo fulani.
 
Jana tu nilikuwa nasoma waraka wa Msigwa wa teuzi, nikasema huyu Rais Hassan kaamua kuonesha urais ni taasisi, anaendelea na Msigwa hajataka kaweka mtu wake.

Yale mawazo yangu yakawa kama yamekorofisha mitambo Ikulu huko.
Hahahahaaaaaa . . yaani nimecheka saanaaaa
 
Na bado kuna the "quango jungle"
 
Mtu mmoja atawezaje kuisemea serikali kwenye mambo mengi hivyo?

Huyo msemaji wa serikali huwa ni mtaalamu wa mambo yote ya serikali? Yaani anajua kuhusu uchuro, ulinzi, afya, siasa, sanaa, nk?
 
Uzuri kazi hizi za kuteuliwa ni za muda na kutesa kwa zamu tu. Acheni walioteuliwa wakati huu nao wamege keki ya taifa.....ndo maisha yalivyo. "Nothing is permanent" ata mteuaji naye muda wake utaisha atakuja mwingine naye atakuja na team yake. Kwanza hawa jamaa wanatakiwa kuwa wanaondoka wote ikulu na Rais anayemaliza muda wake hili wasiwe wanaondolewa na ajaye kutunza heshima kwa watu. Ikulu wawe wanabaki wale wanaojulikana kwamba wao kazi yao miaka yote ni pale. Nadhani uanzishwe huo kama nchi za magharibi. Mambo ya mtu kusubiri mpaka Rais Mpya aje kumuondoa si poa.
 
wataenda wapi na wakati hawana issue?
 
Maumivu yakizid muone daktar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…