Uteuzi & Kumpangia Balozi kituo cha kazi: Stephen Simbachawene apangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil

(v) Balozi Dkt. Stephen John Simbachawene amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil. Balozi Dkt. Simbachawene anachukua nafasi ya Balozi Prof. Adelardus Kilangi ambaye amepangiwa majukumu mengine;
Huyu ni ndugu na yule Waziri
 
kwa mfano huyo jaji Latifa mansoor aliyeteuliwa kuwa Jaji wa rufani, ana makandokando yake mengi. kungekuwa na vetting ya wazi kabla ya uteuzi huu hata mimi ningeweza kujitokeza hadharani na kuanika ushahidi na uthibitisho wote ili kuthibitisha Ukweli kuhusu suala hili, sijui ilikuwaje hadi akateuliwa kuwa jaji huyu dada.
 
hivi yule kamishina wa polisi Susan Kaganda si aliteuliwa ubalozi kaishia wapi
Anasubiri kituo lazima upate kituo na uombe ckearance nchi husika......hakuna shida...atakaa hadi nafasi ipatikane....
 
Anasubiri kituo lazima upate kituo na uombe ckearance nchi husika......hakuna shida...atakaa hadi nafasi ipatikane....
na huo muda anaokaa kusubiri si atakuwa analipwa mshahara na marupurupu ya ubalozi.?
 
na huo muda anaokaa kusubiri si atakuwa analipwa mshahara na marupurupu ya ubalozi.?
Gari iko nje home masaa yote na driver....na magazeti.....serikali...haina hasara atiii wako wengi sana wa hivyo....nenda Polisi HQ na wizarani hasa tamisemi na utumishi....Dotto James yuko wizarani kimya style hiyooooo
 
Mama kaamua kuipanga safi yake tiifu ili ajilie Nchi atakavyo
 
Hivi huyu Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu bi Sharifa alipatikanaje baada ya Zuhura Yunus kupigwa chini?
 
Gari iko nje home masaa yote na driver....na magazeti.....serikali...haina hasara atiii wako wengi sana wa hivyo....nenda Polisi HQ na wizarani hasa tamisemi na utumishi....Dotto James yuko wizarani kimya style hiyooooo
daah.! hii nchi kuna haja ya kupata rais mkali na mzalendo ili afumue system nzima ya nchi na hizo sheria za ovyo za kulipana mapesa mengi eti wale viongozi na watumishi waliotumbuliwa au kuachishwa kazi miaka iliyopita hadi leo wanaendelea kulipwa hela sawa na aliyeko ofisini leo kisa kuna sheria imesema walipwe hv utalipaje mapesa mengi kwa lundo la viongozi zaidi ya kumi waliopita kwenye nafasi moja..na huu ndio ubovu wa sheria zetu eti akistaafu au kutumbuliwa anaendelea kubaki na status ya kile cheo wakati inatakiwa aliye ofisini ndie anapaswa kuwa na status ya cheo ! sasa ni nani atakuja kubadili au kufuta sheria hizi maana karibu asilimia 60 ya makusanyo ya pesa zetu zinaishia matumboni mwa wanasiasa na viongozi.!
 
Acknowledge "Kwa Msaada wa AI"
 
sheria kali huwa zinaletwa na wananchi Wala siyo rais wa nchi
 
Nafikiri Sasa umefika wakati muafaka kabisa kwa Tanzania na Wananchi wa nchi hii kufanya TATHMINI YA KINA juu ya TIJA, FAIDA na HASARA ambayo Wananchi wengi zaidi wa Nchi hii wanayopata kutokana na hizi TEUZI za mara kwa Mara zinazofanywa na Mkuu wa nchi.
Teuzi ni nyingi sana kupita kiasi, Je, hizi Teuzi zina maslahi gani yaliyo mapana zaidi kwa Wananchi wengi zaidi wa Nchi hii?
Upembuzi Yakinifu wa kina unapaswa kufanyika ili kujua Hasara halisi na Faida halisi zitokanazo na TEUZI hizi za mara kwa mara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…