Uteuzi & Kumpangia Balozi kituo cha kazi: Stephen Simbachawene apangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil

(v) Balozi Dkt. Stephen John Simbachawene amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil. Balozi Dkt. Simbachawene anachukua nafasi ya Balozi Prof. Adelardus Kilangi ambaye amepangiwa majukumu mengine;
Huyu ni ndugu na yule Waziri
 
Attachments

  • images (13) (1)~2.jpeg
    images (13) (1)~2.jpeg
    16.3 KB · Views: 4
Ni kweli kwamba hali ya uteuzi wa majaji na mahakimu katika mfumo wa sheria ni nyeti sana, na inahitaji umakini wa hali ya juu.

Uteuzi wa watu wenye tuhuma za ufisadi au ubadhirifu wa mali za umma unaleta wasiwasi kwa jamii, na kama ulivyosema, haki za watu zinaweza kuwa hatarini.

Mambo Muhimu ya Kuangazia:

1. Utaftaji wa Ukweli: Ni muhimu kwa mchakato wa uteuzi uwe na ufuatiliaji wa kina. Hii inamaanisha kuwa viongozi wanapaswa kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kubaini iwapo wana rekodi nzuri ya utendaji kazi.

2. Vetting ya Wazi: Mchakato wa vetting unapaswa kuwa wazi na kujumuisha wananchi. Hii itawapa wananchi fursa ya kutoa maoni yao kuhusu wateule na kutangaza ushahidi wowote wa tuhuma walio nao.

3. Mifumo ya Kisheria: Kuimarisha mifumo ya sheria na kanuni zinazohusiana na uteuzi wa viongozi wa mahakama. Hii inaweza kusaidia kuondoa malalamiko na kusisitiza uwajibikaji.

4. Elimu na Uhamasishaji: Wananchi wanapaswa kuhamasishwa kuhusu haki zao na jinsi ya kushiriki katika mchakato wa uteuzi. Hii itawawezesha kuelewa umuhimu wa kuchagua viongozi waadilifu.

5. Taasisi Huru: Kuanzisha taasisi huru zinazoweza kuchunguza na kutoa mapendekezo kuhusu uteuzi wa majaji na mahakimu. Hizi taasisi zinapaswa kuwa na mamlaka ya kutosha ili kuhakikisha uwazi na haki.

Hitimisho

Rushwa ni adui wa haki, na inahitaji juhudi za pamoja kutoka kwa serikali, jamii, na taasisi za kiraia ili kukabiliana nayo.

Kuweka mchakato wa uteuzi wazi na wa uwajibikaji ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa viongozi wa mahakama wanaaminika na wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na haki.
kwa mfano huyo jaji Latifa mansoor aliyeteuliwa kuwa Jaji wa rufani, ana makandokando yake mengi. kungekuwa na vetting ya wazi kabla ya uteuzi huu hata mimi ningeweza kujitokeza hadharani na kuanika ushahidi na uthibitisho wote ili kuthibitisha Ukweli kuhusu suala hili, sijui ilikuwaje hadi akateuliwa kuwa jaji huyu dada.
 
hivi yule kamishina wa polisi Susan Kaganda si aliteuliwa ubalozi kaishia wapi
Anasubiri kituo lazima upate kituo na uombe ckearance nchi husika......hakuna shida...atakaa hadi nafasi ipatikane....
 
na huo muda anaokaa kusubiri si atakuwa analipwa mshahara na marupurupu ya ubalozi.?
 
Gari iko nje home masaa yote na driver....na magazeti.....serikali...haina hasara atiii wako wengi sana wa hivyo....nenda Polisi HQ na wizarani hasa tamisemi na utumishi....Dotto James yuko wizarani kimya style hiyooooo
 
Mama kaamua kuipanga safi yake tiifu ili ajilie Nchi atakavyo
 
Hivi huyu Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu bi Sharifa alipatikanaje baada ya Zuhura Yunus kupigwa chini?
 
Gari iko nje home masaa yote na driver....na magazeti.....serikali...haina hasara atiii wako wengi sana wa hivyo....nenda Polisi HQ na wizarani hasa tamisemi na utumishi....Dotto James yuko wizarani kimya style hiyooooo
daah.! hii nchi kuna haja ya kupata rais mkali na mzalendo ili afumue system nzima ya nchi na hizo sheria za ovyo za kulipana mapesa mengi eti wale viongozi na watumishi waliotumbuliwa au kuachishwa kazi miaka iliyopita hadi leo wanaendelea kulipwa hela sawa na aliyeko ofisini leo kisa kuna sheria imesema walipwe hv utalipaje mapesa mengi kwa lundo la viongozi zaidi ya kumi waliopita kwenye nafasi moja..na huu ndio ubovu wa sheria zetu eti akistaafu au kutumbuliwa anaendelea kubaki na status ya kile cheo wakati inatakiwa aliye ofisini ndie anapaswa kuwa na status ya cheo ! sasa ni nani atakuja kubadili au kufuta sheria hizi maana karibu asilimia 60 ya makusanyo ya pesa zetu zinaishia matumboni mwa wanasiasa na viongozi.!
 
Ni kweli kwamba hali ya uteuzi wa majaji na mahakimu katika mfumo wa sheria ni nyeti sana, na inahitaji umakini wa hali ya juu.

Uteuzi wa watu wenye tuhuma za ufisadi au ubadhirifu wa mali za umma unaleta wasiwasi kwa jamii, na kama ulivyosema, haki za watu zinaweza kuwa hatarini.

Mambo Muhimu ya Kuangazia:

1. Utaftaji wa Ukweli: Ni muhimu kwa mchakato wa uteuzi uwe na ufuatiliaji wa kina. Hii inamaanisha kuwa viongozi wanapaswa kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kubaini iwapo wana rekodi nzuri ya utendaji kazi.

2. Vetting ya Wazi: Mchakato wa vetting unapaswa kuwa wazi na kujumuisha wananchi. Hii itawapa wananchi fursa ya kutoa maoni yao kuhusu wateule na kutangaza ushahidi wowote wa tuhuma walio nao.

3. Mifumo ya Kisheria: Kuimarisha mifumo ya sheria na kanuni zinazohusiana na uteuzi wa viongozi wa mahakama. Hii inaweza kusaidia kuondoa malalamiko na kusisitiza uwajibikaji.

4. Elimu na Uhamasishaji: Wananchi wanapaswa kuhamasishwa kuhusu haki zao na jinsi ya kushiriki katika mchakato wa uteuzi. Hii itawawezesha kuelewa umuhimu wa kuchagua viongozi waadilifu.

5. Taasisi Huru: Kuanzisha taasisi huru zinazoweza kuchunguza na kutoa mapendekezo kuhusu uteuzi wa majaji na mahakimu. Hizi taasisi zinapaswa kuwa na mamlaka ya kutosha ili kkuhakikisha uwazi na haki.

Hitimisho

Rushwa ni adui wa haki, na inahitaji juhudi za pamoja kutoka kwa serikali, jamii, na taasisi za kiraia ili kukabiliana nayo.

Kuweka mchakato wa uteuzi wazi na wa uwajibikaji ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa viongozi wa mahakama wanaaminika na wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na haki.
Acknowledge "Kwa Msaada wa AI"
 
daah.! hii nchi kuna haja ya kupata rais mkali na mzalendo ili afumue system nzima ya nchi na hizo sheria za ovyo za kulipana mapesa mengi eti wale viongozi na watumishi waliotumbuliwa au kuachishwa kazi miaka iliyopita hadi leo wanaendelea kulipwa hela sawa na aliyeko ofisini leo kisa kuna sheria imesema walipwe hv utalipaje mapesa mengi kwa lundo la viongozi zaidi ya kumi waliopita kwenye nafasi moja..na huu ndio ubovu wa sheria zetu eti akistaafu au kutumbuliwa anaendelea kubaki na status ya kile cheo wakati inatakiwa aliye ofisini ndie anapaswa kuwa na status ya cheo ! sasa ni nani atakuja kubadili au kufuta sheria hizi maana karibu asilimia 60 ya makusanyo ya pesa zetu zinaishia matumboni mwa wanasiasa na viongozi.!
sheria kali huwa zinaletwa na wananchi Wala siyo rais wa nchi
 
Wakuu,

View attachment 3197733
View attachment 3197734

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Wenyeviti wa Bodi na kumpangia kituo cha kazi Balozi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

(i) Jaji Latifa Alhinai Mansoor ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Mansoor alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi, Morogoro;

(ii) Jaji George Mcheche Masaju ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Masaju alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mshauri wa Rais, Sheria;

(iii) Jaji Dkt. Deo John Nangela ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Dkt. Nangela alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga;

(iv) Jaji Dkt. Ubena John Agatho ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Dkt. Agatho alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam;

Pia soma: Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

(v) Balozi Dkt. Stephen John Simbachawene amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil. Balozi Dkt. Simbachawene anachukua nafasi ya Balozi Prof. Adelardus Kilangi ambaye amepangiwa majukumu mengine;

(vi) Bw. Uledi Abbas Mussa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kipindi cha pili; na

(vii) Prof. Zacharia Mabubu Mganilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE). Prof. Mganilwa anachukua nafasi ya Prof. Wineaster Anderson ambaye amemaliza muda wake.

Aidha, uapisho wa Majaji wa Mahakama ya Rufani walioteuliwa utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Nafikiri Sasa umefika wakati muafaka kabisa kwa Tanzania na Wananchi wa nchi hii kufanya TATHMINI YA KINA juu ya TIJA, FAIDA na HASARA ambayo Wananchi wengi zaidi wa Nchi hii wanayopata kutokana na hizi TEUZI za mara kwa Mara zinazofanywa na Mkuu wa nchi.
Teuzi ni nyingi sana kupita kiasi, Je, hizi Teuzi zina maslahi gani yaliyo mapana zaidi kwa Wananchi wengi zaidi wa Nchi hii?
Upembuzi Yakinifu wa kina unapaswa kufanyika ili kujua Hasara halisi na Faida halisi zitokanazo na TEUZI hizi za mara kwa mara
 
Back
Top Bottom