Professor Matthew Luhanga unamuita mpuuzi?
Hakika una matatizo ya kuongea juu ya watu usiowajua.
Prof. Matthew Luhanga ni Mwalimu wangu, miaka kadhaa kabla hajawa Chief Academic Officer wala Vice Chancellor wa University of Dar es Salaam.
Huyu msomi mahiri yupo kwenye kundi dogo sana la Watanzania ambao Mungu amewajalia 'bongo' iliyozidi kiwango.
Std 12 alipata, kwa viwango vya sasa, 'A' masomo yote.
Std 14 alipata 'A' zote.
Chuo Kikuu cha California, Marekani, shahada ya kwanza ya Uhandisi Umeme alipata 'B+' moja, nyingine zote 'A', kuanzia mwaka wa kwanza mpaka mwaka wa nne.
Kwa hakika, kwangu mimi Mwanafunzi wa Prof. Luhanga, nimekwazika kwa kitendo chako cha kukosa heshima na kutumia maneno yasiyofaa juu ya Msomi Mahiri sana.