Uteuzi: Suleiman Abubakar Mombo Ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Siwa amestaafu

Uteuzi: Suleiman Abubakar Mombo Ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Siwa amestaafu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Rais Samia afanya uteuzi wa Mkurugenzi Wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ambapo bwana Abubakar Mombo Ateuliwa baada ya ndugu Siwa kustaafu.

IMG_20240711_190737_151.jpg

20240711_193413.jpg


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Mululi Majula Mahendeka, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua na kumuapisha Bw. Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mombo alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu. Bw. Mombo amechukua nafasi ya Balozi Ali Idi Siwa ambaye amestaafu.

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
20240711_193413.jpg


Pia Soma
Tetesi: - Mombo Seleman kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (TISS). Aliyepo anafukuzwa muda wowote
 
Kila siku uteuzi mpya nafasi moja, hivi hata wewe Samia sisi tungekuwa kama wewe Kila siku tunabadili Rais, Leo upo wewe, kesho tunamuweka makamba, keshokutwa Halima mdee, nchi haiwezi kwenda. Halaf kama hao unaoteuwa unasemaga viatu haviwatoshi, je wewe umejipima na kuangalia viatu kama vinakutosha.

Kama unajua wewe mwenyewe hutoshi, basi acha kutumbua tumbua bianadamu c wakamilifu
 
Hata picha yake tu hamna???
Japo nilishawah kupata hiz hearsaybkwamba hawa wakurugent wanaotangazwa pale tiss ninkama boshen tu ila kuna wanyama ambao hao hutawasikia ndio haswa wenye tiss yao. Hao hawatangazwagi na mtu
Mkurugenzi yeye ni kama IGP tu. Kazi zinafanywa na ma RPC. IGP hupewa tu taarifa
 
Hata picha yake tu hamna???
Japo nilishawah kupata hiz hearsaybkwamba hawa wakurugent wanaotangazwa pale tiss ninkama boshen tu ila kuna wanyama ambao hao hutawasikia ndio haswa wenye tiss yao. Hao hawatangazwagi na mtu
Alokwambia hivyo kakudanganya,mkurugenzi mkuu ndiyo ana clearance level ya juu kabisa ambayo hao miamba wako hawana,naamini wajua clearance level ni nini
 
Kwenye uteuzi haangaliwi mtu Imani yake ya dini huangaliwa utendaji wake wa kazi,Eliimu na uziefu acha fitina.
Kwa Tanzania ni kigezo cha kwanza kabla ya vigezo vya utendaji.

Utendaji ni subjective, mimi naweza kusema wewe ni mtendaji mwingine akasema sio mtendaji.

Na bongo unaweza kua mtendaji na bado ukaondolewa, mfano ni Kidata wa TRA, rais alisema ni mtendaji mzuri sana ila amemuondoa kwa sababu ya utendaji kazi wake mzuri.

So bongo ni dini kisha sifa nyingine.
 
Back
Top Bottom