Uteuzi wa Job Masima kuwa Balozi Israel ni ishara ya Rais Magufuli kuinoa na kuiimarisha TISS

ni muda sasa umepita tokea tupate uhuru, nchi za wenzetu ikiwemo china waliwatumia wanausalama wao kujiimarisha kiuchumi lakini kama hawa Tiss hawapo chini ya chama kilichopo madarakani ni lipi walilolifanya kutuimarisha kiuchumi?

Hapana, labda hujafuatilia jinsi China ilivyochukua maamuzi magumu kufikia hapo ilipo leo.

Ni chama cha kikomunisti cha China ndicho chanzo na kichocheo cha China uionayo leo.
 
Ungeipenda nchi yako unavyosema usingelaumu kwa hiyo style. Typically wewe ni antagonist na hata ufanyiwe nini utalalamika tu kama mlivozoea. Pia nakusihi usipende kusema unaipenda nchi yako ili kufurahisha watu au keyboard warriors. Kuipenda nchi kwa watu wengine ina maana kubwa so please dont make it look so cheap.
 
Makala ndefu ila hukuweka ataisadiaje na utayari wa israel katika hilo.
Mimi nadhani njia nzuri ni kuweka bajeti ya kuwapeleka vijana kusoma nchi mbali mbali kutokana na hitajio.
Huwezi ukautoa usalama wa nchi kwa taifa moja na kusaidiwa...
Ukumbuke israel ni kama US haina rafiki wa kudumu wao wanaweka maslahi yao kwanza..
Na pia isreal wanatania ya kupandikizw chuki pale nchi ikiwa ina dini mbili hizi...
Ni vizuri kuwa na uhusiano ndio utandawazi lakini kama taifa uasalama wetu ni wetu wenyewe haihusu taifa jengine.
Sasa hivi hii Tiss inatakiwa iwe na vijana wabobezi wa investigation katika mamno ya uchumi , makampuniya kimataifa, mfumo wa biashars za maguta na gesi..
Yuwe na vijana ambao ukiwapa file kuhusu kampuni fulani inayo taka kuja kuwekeza wanakupa data zote mesani...
Au vijana ambao ukitaka kumchagua mtu kuwa kiongozi wanakuoa data za uhakika kuanzia kolomije mpaka moshi ushirika...
 
Tanzania tayari ina mahusiano ya kibalozi na Marekani, UK, Russia, France, China, Germany na kadhalika na kadhalika.

Israel ni cha mtoto katika kila eneo ukiilinganisha na hayo ma nchi, mbona hiyo TISS ya Bongo miaka yote hiyo haijasaidiwa?

Haya ni ma imani ya the Christian right wanaoamini biblia is literally true. Kama unaamini biblia is literally true basi Israel ni nchi ya ahadi, taifa teule ambalo ndio bingwa wa kila kitu ulimwenguni.

Theological baloney. Mashudu!
 

Tuko pamoja mkuu maana kabla ya serikali ya awamu ya 5 huko nyuma kwenye kutiliana saini mikataba mwekezaji anaweza kusema ana assets au hiki na kile huko watokako.

Lakini kama huna vijana na nyenzo za kufuatilia kampuni zinazotaka kuingia mikataba kama ya uchimbaji madini basi yanatokea sasa hivi kwenye suala la makontena ni kielelezo tosha kwamba kuna mahitaji katika hilo.

Pia, hata suala la ulinzi wa viwanja vya ndege ni wazi kuwa vijana wamepwaya sana kwenye kuchunguza aingiaye na atokae nchini mwetu awe na madini au mchanga.
 
Asante hii ni fursa njema kama taifa kuvuna ujuzi wa intelligence kutoka kwa hawa wenzetu
 

Nadhani hujasoma na kuelewa kwa undani nilichokieleza, yaani pengine unahitaji akili za ziada.

Mtu unaweza kuwa una shahada ya chuo kikuu lakini katika kujadili masuala ya msingi na muhimu kabisa ambayo mara nyingi yanahitaji kutumia welevu au "intelligence" ukajikuta unafeli.

Na kutumbuliwa kwa profesa Ntalikwa leo pale wizara ya nishati na madini ni mfano tosha wa ninachomaanisha.

Security is a subject that can be taught theoretically, but nothing is a substitute for a real hands-on experience and we've got lots of it."-
 


Anhaa, mimi nahitaji akili za ziada? Okay.

Kwanza acha ku speculate na kutudanganya sababu ya Profesa Ntalikwa kutumbuliwa Nishati, hujui! Nobody knows, msomi hafanyi fanyi ma wild speculation kama hayo kwamba Ntalikwa ameshindwa ukatibu mkuu kwa sababu hawezi kujadili masuala muhimu japo kasoma. Such ridiculous, wild and woolly conclusions.

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Tanzania basi unatakiwa kujua kwamba teua-tengua za utawala huu ziko erratic and inexplicable, hazielezeki, and sometimes vindictive, visasi, kama Nape. TRA, kwa mfano, ina mabosi wangapi toka JPM achukue nchi, kwa nini hafanyi thorough vetting and prior perfomance evaluation of his nominees?

Hakuna teuzi za JPM ambazo ni thought through and strategic. Balozi wa Israel kachaguliwa kwa mtindo wa random draws.

Israel ni nchi ya kawaida tu, ila nyinyi ambao mnasema the bible is literally true then of course Israel ndio mwisho wa kila kitu. Incredibly feeble mind.


 

Hii ndio intellegency tunayoihitaji sio ile ya kutoa kucha watu wanaosema ukweli!
 
Ni kweli Israel inaongoza katika teknnologia na ukiangalia tech security companies za Israel ndizo zenye tenda nyingi sana Ulimwenguni. Ushauri wangu waanze na mradi wa NIDA ambao naamini kwa kuwa Modestus anaufahamu fika ni eneo ambalo mchango wao unaweza kuwa wa manufaa sana kwetu. Mradi huu una impact kubwa sana kwenye ustawi wa Uchumi wa nchi yetu kwa ujumla. Pili kwenye kilimo na Umwagiliaji wako mbali sana. Israel ni almost jangwa lakini huwezi kuamini mazao ya kilimo yanayotoka kwenye jangwa hilo. Ukiona swimming pools zilizoko Tel Aviv utafikiri hawa jamaa wana mito kama huku kwetu. Tatu ni kuhusu Elimu, maandalizi yafanywe kuanza kuwaandaa wanafunzi kusoma na kujua Kiyahudi kwani ukitaka kupata Elimu nzuri Israel ni kwenye vyuo vyao ambavyo sharti moja kubwa ni ujue kiyahudi.
 

Hii story yako ulitaka kutueleza nini?/? Maana hujaeleweka

Nyie vijana Wa Lumumba very bogus kabisa

Aliwafundisha nini?
 
Naona kama imani yako ni mlengo wa kigaidi.acha kudharau imani za watu we mzee wa kitabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…