Uteuzi wa nafasi mbalimbali TAMISEMI

Uteuzi wa nafasi mbalimbali TAMISEMI

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2019
Posts
1,042
Reaction score
2,005
Naamini kwa uwezo wa maanani mpo vyema na mnaaendelea vizuri na kulijenga taifa letu pendwa la Tanzania.

Huko Tamisemi kwa Katibu mkuu huwa kuna nafasi za uteuzi anazifanyaga mfano wakuu wa idara n.k. Kwa upande wa idara yetu ya elimu huku kwenye halmashauri kuna nafasi kama afsa elimu taaluma wilaya au mkoa, afisa takwimu wilaya, afisa elimu mwenyewe wilaya au mkoa kwa kurugenzi zote mbili.

Swali langu ni kwamba hizo nafasi kuna kitengo Tamisemi kipo kwa ajili ya kufanya huo uteuzi au huyo KM anafanyaje teuzi za nafasi kama hizo?

Kuna jamaa yangu juzi ameniambia kuwa kuna mtu amesema anataka amfanyie mpango wa uteuzi lakini akamwambia ampe kiasi cha fedha awapelekee waliopo kwenye kitengo wachakate suala hilo ili walipeleke kwa KM na then atafute fedha nyingne ya KM.

Sasa wasiwasi wake akaniauliza na mimi majibu sina kwa kuwa sina utaalam nalo. Mwenye kujua jamani mchakato unavyoenda atueleze ili jamaa asije akatapeliwa na maisha ni magumu mnoo kwa sasa.
 
Hizo nafasi ulizotaja hapo ni za kuajiriawa, sio kuteuliwa.
 
Bila shaka wew ni ticha jamaa wanataka kukupiga kwa kukuahid kuwa afusa elimu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tumeongea chemba unakuja kuleta JF. We jamaa ushazingua sahau uteuzi
 
Kuna jamaa yangu juzi ameniambia kuwa kuna mtu amesema anataka amfanyie mpango wa uteuzi lakini akamwambia ampe kiasi cha fedha awapelekee waliopo kwenye kitengo wachakate suala hilo ili walipeleke kwa KM na then atafute fedha nyingne ya KM.
Pesa ngapi anatakiwa kuwasilisha?
Kwamba hizo nafasi sasa ni bidhaa, zinauzwa na kununuliwa🙄
 
matapeli naona wana rejea kwa kasi sanaaaa... wapo accurate sanaaaa...
 
Uafisa elimu ni sawa na nyampara kuwasimamia wafungwa wenzie haipunguzi adhabu ya kifungo zaidi ya kula ugali mkubwa na kulalia godoro la peke yake.....afisa elimu taaluma sijui afisa elimu msingi mshahara ni uleule haubadiliki..
 
Mkuu hapa umedanganya. Kuna uwezekano hujui maana ya ukuu wa idara. Ukuu wa idara hauwezi kuota nyasi eti kwa kuwa mkurugenzi amebadilishwa. Uongo huu
Mkuu mbona mkugurenzi wa wilaya fulani alipohamishwa na wakuu wa idara walitinduliwa?....
 
Uafisa elimu ni sawa na nyampara kuwasimamia wafungwa wenzie haipunguzi adhabu ya kifungo zaidi ya kula ugali mkubwa na kulalia godoro la peke yake.....afisa elimu taaluma sijui afisa elimu msingi mshahara ni uleule haubadiliki..
Siku hizi Idara ya Elimu uongozi una posho.

Mkuu wa shule anapata Tsh 200,00 ( msingi ) na Tsh 250,000 ( Secondary na mratibu ).

Sasa nadhani Afisa Elimu watakuwa wanapata zaidi ya hizo.
 
Naamini kwa uwezo wa maanani mpo vyema na mnaaendelea vizuri na kulijenga taifa letu pendwa la Tanzania.

Huko Tamisemi kwa Katibu mkuu huwa kuna nafasi za uteuzi anazifanyaga mfano wakuu wa idara n.k. Kwa upande wa idara yetu ya elimu huku kwenye halmashauri kuna nafasi kama afsa elimu taaluma wilaya au mkoa, afisa takwimu wilaya, afisa elimu mwenyewe wilaya au mkoa kwa kurugenzi zote mbili.

Swali langu ni kwamba hizo nafasi kuna kitengo Tamisemi kipo kwa ajili ya kufanya huo uteuzi au huyo KM anafanyaje teuzi za nafasi kama hizo?

Kuna jamaa yangu juzi ameniambia kuwa kuna mtu amesema anataka amfanyie mpango wa uteuzi lakini akamwambia ampe kiasi cha fedha awapelekee waliopo kwenye kitengo wachakate suala hilo ili walipeleke kwa KM na then atafute fedha nyingne ya KM.

Sasa wasiwasi wake akaniauliza na mimi majibu sina kwa kuwa sina utaalam nalo. Mwenye kujua jamani mchakato unavyoenda atueleze ili jamaa asije akatapeliwa na maisha ni magumu mnoo kwa sasa.

TAMISEMI walitakiwa watangaze hizo nafasi ili wativwenyevsifa waombe na wafanye interview ila ni kugawana kwa rushwa na kujuana.​

Back
Top Bottom