Uteuzi wa Prof. Kabudi Mara ya 3 Sheria Japo Umefanywa na Binadamu tu, Una Roho wa Mungu. Je, Prof Kabudi Atatimiza Mapenzi ya Mungu au ya Binadamu?

Uteuzi wa Prof. Kabudi Mara ya 3 Sheria Japo Umefanywa na Binadamu tu, Una Roho wa Mungu. Je, Prof Kabudi Atatimiza Mapenzi ya Mungu au ya Binadamu?

Namuomba mwalimu wangu Prof. Palamagamba Kabudi atimize mapenzi ya Bwana Mungu wake, na amini nawaambia, kama hawatatimiza mapenzi ya Mungu kuhusu huu ubatili wa katiba yetu, na ubatili wa sheria yetu ya uchaguzi kabla uchaguzi mkuu ujao wa 2025, Mungu atafanya kitu na mimi nitarejea humu kuja kuwashuhudia Mungu amefanya nini!.
Dah!...Ccm hawaogopi hili aiseee au umewasahau....?
 
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la leo
View attachment 3072962

Uteuzi wa Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Sheria kwa Mara ya tatu, japo umefanywa na Rais Samia ambaye ni binadamu, Rais Samia ameongozwa na Roho wa Mungu kumuona Prof. Kabudi!. Hii maana yake Mungu ana makusudi fulani na Tanzania kwenye mambo fulani yanayohusu Katiba, sheria na haki. Swali ni Je Prof. Kabudi atatimiza mapenzi ya Mungu aliyemteua kupitia kwa binadamu Rais Samia au atatimiza mapenzi ya binadamu aliyemteua?.

Paskali
Hili swali limeanza kupata majibu, sikiliza mahojiano haya na Sudi Mnete wa DW
Kwa hisani ya Mkuu brazaj
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kwenye mahojiano na mtangazaji Sudi Waziri huyo kuondoka mwishoni mwa mahojiano hayo bila kuaga.
Si kweli, nimeisikiliza clip, Prof. Kabudi aliaga!.

Ujio wa social media umefanya kila mtu kuwa a journalist, a reporter wa citizens journalism.

Msingi mkuu wa tasnia ya habari ni "Tell nothing but the truth".
Kwenye mahojiano hayo mtangazaji Sudi Mnete alimuuliza Kabudi kuhusu kitendo cha serikali kuzuia maandamano ya CHADEMA, ripoti mpya iliyotoka ya Human Rights Watch na hali ya siasa ilivyo nchini.
Kabudi alijibu vizuri na kuusemaukweli, hao HRW ni waongo, wazushi na wazandiki.
Kabudi alipoulizwa kuhusu kitendo cha serikali ya Tanzania kufungia The Citizen, Kabudi alidokeza kuwa Mwananchi na The Citizen walifungiwa kwa mujibu wa sheria za nchi na kwamba kama kituo hicho kingekuwa hakijaridhishwa na maamuzi ya TCRA kilikuwa kinaruhusiwa kukata rufaa.
True
ilipofika dakika ya 9 ya mahojiano Kabudi aliomba udhuru kwamba anaingia kwenye kikao kingine ambapo mara baada ya mtangazaji kuanza kumuuliza Waziri huyo kuhusu hali tete ya kisiasa hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Waziri huyo alikataa simu.
Hii pia sii kweli, Waziri alikata simu mara baadaya kumaliza kujibu na aliaga ana kikao kingine.

Kiukweli Prof. Kabudi amejibu vizuri sana, na amemtendea haki Sudi na kuitendea haki DW, kumpata waziri impromptu kwa mahojiano ya dakika 9 is not a joke!.

Viongozi wetu wanaheshimu sana media za kibeberu na kutudharau media za nyumbani. Maombi yangu kumhoji JPM yameozea ikulu hadi anatwaliwa, sikuwahi kupata chance zaidi ya kulazimisha kama pale ikulu.

Ile Samia ameingia tuu, maombi yangu mezani kwake, nae itakua kama JPM!.
Thanks for this.
Hivi ndivyo mawaziri wote wanatakiwa kuwajibu hizi media za kibeberu, msiwaogope BBC, DW, VOA au media zozote za kibeberu.
P
 
Wanabodi

Uteuzi wa Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Sheria kwa Mara ya tatu, japo umefanywa na Rais Samia ambaye ni binadamu, Rais Samia ameongozwa na Roho wa Mungu kumuona Prof. Kabudi!. Hii maana yake Mungu ana makusudi fulani na Tanzania kwenye mambo fulani yanayohusu Katiba, sheria na haki. Swali ni Je Prof. Kabudi atatimiza mapenzi ya Mungu aliyemteua kupitia kwa binadamu Rais Samia au atatimiza mapenzi ya binadamu aliyemteua?.

Paskali
mara paap News Alert: - Rais Samia afanya uteuzi: Masauni apigwa chini Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais kaondolewa!
P
 
Back
Top Bottom