Uteuzi wa tarehe 21 Julai 2024 waleta utata kuhusu kuvunjwa tena kwa katiba.

Uteuzi wa tarehe 21 Julai 2024 waleta utata kuhusu kuvunjwa tena kwa katiba.

Acha ujinga wewe. Anaitwaga mbunge mteule. Huwezi kuchukuliwa kuwa na nafasi fulani hasa hizi za kisiasa bila kula kiapo husika.

Ndo mana Rais anaitwa Rais mteule. Hawezi kusaini nyaraka yeyote ile hadi anapoapishwa.

Kiutaratibu Rais alipaswa kumteua kuwa mbunge. Then leo asubuhi anaapishwa na Spika au Naibu Spika kuwa mbunge then ndo anateuliwa kuwa Waziri.

Ngozi nyeusi mmezoea kukiuka taratibu ndo mana hamstaarabiki
Endelea kulialia mwenzio kesho anakula kiapo Ikulu 🐼
 
anakwambia suna
GTCZKVbWMAAFEMQ.jpg
 
Na katiba inasema hivyo hivyo ulivyoandika? Au ni ufafanuzi nje ya misingi ya katiba kwa matakwa ya mtu na si katiba?.
Kwani Katiba ni nini unadhani?

Nenda hapo Kenya uone kama Cheo cha Mudavadi kimeandikwa popote 😂😂
 
Lakini ili uwe waziri ni lazima uwe kwanza mbunge. Na ili uwe mbunge lazima ule kiapo bungeni (kuthibitishwa kama mbunge).

Hivyo basi kuteuliwa kuwa waziri kabla hujathibitishwa kama mbunge ni kosa kimantiki.

Logic.
Ikulu washauri wa Raisi kuna shida sio Siri
Nini hiki kimefanyika?
Je kuna watu wanataka Raisi aonekane hopeless mbele ya public au?

Kuna mtu au watu huko ikulu wanatakiwa kuwajibishwa kwa hili

Na raisi naye hasomi katiba au?
 
Raisi ina maana hasomi hata kifungu tu cha katiba kinachoongelea uteuzi ili ajue kinachohitajika? Asivunje katiba?
 
Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk 21.07.2024 alijiuzulu ubunge wa kuteuliwa na Rais, akiwa Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Jumapili, 21.07.2024 usiku, Balozi Mahmoud Thabit Kombo akateuliuwa kuwa Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 55(4) inaeleza “Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa wabunge.”

Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ameteuliwa kuwa WAZIRI kabla ya kuteuliwa kuwa MBUNGE. Kinyume na Uteuzi wa Mawaziri, Sheria ya 1984 Na. 15

Nini kinaanza? Kiapo cha ubunge au kiapo cha uwaziri? Katiba ya JMT haipo kimya. Katiba ya JMT imeweka masharti, mbunge atakula kiapo katika bunge.

Katiba ya JMT Ibara yake ya 68 inasema “Kila Mbunge ataapishwa katika Bunge la JMT kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki shughuli za Bunge”

Kiapo cha utii kwa wabunge kimetajwa katika kanuni za kudumu za bunge 24(1) zilizotungwa chini ya Ibara ya 89(1) ya Katiba ya Tanzania, Sura ya pili.

Kwa maoni yangu, RAIS amevunja KATIBA ya TANZANIA. Katiba ambayo aliapishwa kuhifadhi, kuilinda, kuitetea kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa.

Au vinginevyo, tuoneshwe kwamba Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk baada ya kujiuzulu UBUNGE, aliteuliwa kuwa MBUNGE na akateuliwa kuwa WAZIRI.

Kama tunataka MAWAZIRI wasiotokana na UBUNGE, RAIS aanzishe kuanzisha mchakato wa KATIBA MPYA, aachane na wabunge kuwa MAWAZIRI.

I stand to be corrected. Karibu.

Martin Maranja Masese, MMM.View attachment 3048994
Mbona hakuna kipengele kimekiukwa, uteuzi umeanza kwa kumpa nafasi ya kuwa mbunge wa kuteuliwa na kisha nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje.
Barua haitajatamka kama ameanza majukumu mara moja kama bali imeacha nafasi kwa taratibu zingine kufanyika kabla ya kiapo cha Uwaziri.
Na ninavyofahamu baada ya kiapo kukamilika ndiyo zile entlitlements za kuwa Waziri huwa granted kwa muhusika, ikiwepo kutumia gari yenye address ya Wizara anayoenda kuitumikia na kuingia ofisini kuanza majukumu.
Umeharakisha sana kukosoa kabla ya kosa halijatendeka, maana hapo ulichofanya ni kutahadharisha kuwa kosa linaweza kutendeka ilihali bado halijatendeka.
Kaa kwa kutulia watu wapo makini hawajakutukupa kama vile wewe umekurupuka.
 
Back
Top Bottom