Uteuzi wa wazee waliostaafu umewafanya watumishi wa umma kutojiandaa kustaafu; viongozi wana matumizi mabaya ya fedha wakiamini watateuliwa wakistaafu

Uteuzi wa wazee waliostaafu umewafanya watumishi wa umma kutojiandaa kustaafu; viongozi wana matumizi mabaya ya fedha wakiamini watateuliwa wakistaafu

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Nchi yetu wakuu wa taasisi na vyombo vya ulinzi kwa miaka ya karibuni awastaafu ila wanabadili kazi. Wanastaafu leo kesho anateuliwa mjumbe wa bodi au balozi.

Matokeo ya mfumo huu hakuna kiongozi wa taasisi anayestaafu akiwa na biashara visible au kampuni inayoajiri hata vijana watano. Wao pesa zao zote wanafanyia starehe kwa sababu wameumbwa kufanya kazi hadi wafikishe miaka 75.

Kutokustaafu wazee hawa na wao kutoanzisha kampuni au biashara kumepelekea waajiri nchni kupungua. Wanaotakiwa waajiri nao wameziba nafasi za waajiriwa.

Kwanini kama nchi tusitunge sheria ya kukataza waliostaafu kurudi serikalini kwa mgongo wa nyuma? Mtu anateuliwa kwenye bodi anaambiwa nenda katulie uzeeke vizuri . Au unasikia nimekuteua ukatulie uwasikilize vijana.

Kwanini kama hawa wazee ni potential kwanini wasipewe ujumbe wa bodi kwenye private sector? Kama kwenye private sector wanakataliwa, wataweza kuivusha serikali ?

Ifike wakati mtu akifika miaka 60 ajue ameondoka serikalini hakuna kurudi, tukifanya hivyo hawa wazee watakuwa na displine ya fedha na watajiandaa na kazi binafsi.
 
Back
Top Bottom