Uteuzi: Yusuf Juma Mwenda ateuliwa kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar

Uteuzi: Yusuf Juma Mwenda ateuliwa kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Yusuf Juma Mwenda kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), kuanzia leo Machi Mosi, 2022

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu mkuu kiongozi wa l iliyotolewa kwa vyombo vya habari kabla ya uteuzi huo Yusuf Juma Mwenda alikuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Yusuf Mwenda pia aliwahi kuwa diwani wa Mikocheni na Meya wa Kinondoni kuanzia mwaka 2010/ 2015

4307ED08-C40A-466E-A334-DA64D41FE715.jpeg
 
Sawa..ila wanachangia kiasi gani kwenye bajeti kuu ya JMT?

#MaendeleoHayanaChama
 
Jamaa yuko vizuri sana. Wamepata mtu sahihi.
 
Kazi ya Charles Hillary ni nini hasa? Taarifa ya Uteuzi inatolewa kwa maandishi na Katibu mkuu Kiongozi!
 
Huyu si alikuwa meya wa kinondoni na mmoja wa walioshiriki kumuibia kura Rasheed wa Kawe. Kifupi sio muadilifu ni mbadhilifu anakaa karibu na shule ya Hindu Mandali
 
Majukumu haswa ya Charles Hillary ni yapi jamani?...nauliza ili nipate kujua.
 
Umewahi kufanya nae kazi??.
Nilipata nafasi ya kufanya nae mikutano kadhaa zaidi ya mara 8 kati ya TRA LTD na wateja, tulikua tukimuuliza maswali na aliyajibu kwa ufasaha yale aliyoona ni changamoto zao TRA wenyewe alikubali na kwenda kuyafanyia kazi na kutekeleza.
 
Hongera kwake kwa uteuzi na kuaminiwa na Mhe. Rais hivyo kinacho takiwa afanye kazi kwa bidii na ubunifu wa kiwango cha juu.
 
machogo hili mmelinyamazia kimya huyu jamaa kama alikuwa nikimuona kinondoni na makaburasha ya Chama cha CCM ni Raia wa Tanganyika,au mnasemaje .
 
Huyu si alikuwa meya wa kinondoni na mmoja wa walioshiriki kumuibia kura Rasheed wa Kawe. Kifupi sio muadilifu ni mbadhilifu anakaa karibu na shule ya Hindu Mandali

Haupo sahihi
Yusuf Juma Mwenda Mwaipopo,mnyakyusa wa Kyela kijiji cha Tenende ni mtu mwadilifu na hana makuu!
Ni kijana mchapa kazi na mara nyingi akija kijiweni hapa Kasyungutini Tenende Kyela vijijini tunakaa kijiweni tunapata kahawa kidogo pamoja!
Mama yake tumezika hapa kijijini mwaka juzi,ni kijana wetu
 
Back
Top Bottom