Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Katika zoezi la kusaka vyeti bandia, kuna watu wanashindwa kutofautisha kati ya vyeti bandia na majina bandia, Vyeti vya Mwigulu Nchemba sio vyeti bandia, yaani vyeti fake, ni vyeti halali na halisi kabisa, bonafide genuine, ila majina ya Mwigulu Nchemba ndio majina bandia!.

Cheti Bandia ni Cheti Gani?.
Cheti bandia ni cheti ambacho
1. Ama sio cheti cha kweli, ambacho ni cheti cha kutengeneza tuu kwenye secretarial lakini hakipo kabisa hivyo kimetengezwa cheti fake kwa forgery, mwenye cheti hicho hakusoma wala sio cheti cha kweli.
2. Ama ni cheti cha kweli kabisa na kimetolewa kihalali cha shule/chuo husika na jina kwenye cheti hicho ni la mhitimu wa ukweli aliyehudhuria masomo hayo na kuhitimu lakini anayekitumia sii mwenyewe halisi mwenye cheti chake, hivyo anayekitumia ni mtu mwingine, anatumia cheti cha mtu mwingine kwa kufoji cheti cha mtu mwingine, hili ni kosa la jinai na huu ni wizi na forgery!.

Jina Bandia ni Jina Gani?
Kama ilivyo kwenye vyeti bandia, na jina bandia ni vivyo hivyo
1.Jina bandia ni jina ambalo sio jina lako la ukweli, ni jina lolote tuu la kubuni, au kutumia majina ya kuunga unga ambayo sio majina yako halisi,
2. Jina ni jina la kweli ambalo ni jina halisi na halali, ila anayelitimia ni mtu mwingine, sio huyo mwenye hilo jina.

Cheti Halali chenye Jina Bandia

Hiki ni cheti cha halali kabisa, cha mtu anayetumia majina ya bandia, lakini aliyeingia darasani kusoma ni yeye mwenyewe kwa kusoma kupitia majina bandia, aliyehitimu ni yeye mwenyewe, hivyo hicho cheti ulichokipata ni cheti halali na sio cheti bandia ila jina alilolitumia kusomea, ndilo jina bandia, mtu wa aina hii anakuwa anatumia tuu majina ya bandia la ni mhitimu wa ukweli na cheti chake ni cheti cha ukweli, ni cheti halali, ila majina tuu ndio ya bandia, sio kosa kisheria kutumia majina yoyote ya bandia katika shughuli zozote.

Nimesoma utetezi wa Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kuhusu tuhuma za kuwa na cheti bandia, nimejiridhisha kabisa tena pasi shaka kuwa vyeti vya Mhe. Mwingulu Nchemba sio vyeti fake ila majina ya Mwigulu Nchemba ndilo jina bandia.

Sio kila jina bandia ni forgery, kuna majina bandia yanayoitwa Nick Names sio forgery bali ni just given names. Given names hizo zinapokuwa registered kwenye vyeti, vyeti hivyo ni halali ila jina la mwenye cheti ndilo jina bandia ambalo halina kosa lolote kisheria.

Uthibitisho huu ni kufuatia utetezi huu wa Mhe. Mwingulu Nchemba umethibitisha jina la Mwigulu Nchemba ni jina bandia la mtu halisi mwenye given name ya Lameck Madelu Mkumbo ambaye hata majina hayo,hakuna jina lolote la wazazi wake wala jina la ukoo wake, kama anavyojieleza yeye mwenyewe.

Mkuu Mhe. Mwigulu, kwa vile hili bandiko nimelikutia page 33, na sijaweza kusoma mabandiko yate ya nyuma, hivyo siwezi kujua kama ulijibu haya, ila kwanza kwa heshima na taadhima, nakupongeza sana kujitokeza kujibu tuhuma, ila very unfortunately, majibu yako, hayajitoshelezi kabisa!, hakuna kitu chochote ulichojibu hapa, you leave more questions than answers and there is something fishy!.

Majina yana formula ya majina, na hayawezi kuijiibukia tuu hivi hivi, na formula hiyo ni universal, dunia nzima.

Formula ya Majina
.
Majina yote kwenye usajili wowote yanatumia a universal formula diniani kote ni majina matatu
1.Jina la kwanza ni given name, yaani jina ulilopewa wewe ile siku unazaliwa, hili given name linaweza kuwa moja au hata kumi, haijalishi, kwenye given name, ni lile jina unaloitwa, liwe la utoto, ubatizo, etc, Kiingeza linaitwa fist name!, hakuna limit number ya given names, mtu unaweza kupewa hata majina kumi, lakini kwenye any official registration, unaruhusiwa kutumia jina moja tuu!.

2. Jina la pili, ni second name, or middle name or Initials, hili ni lazima liwe ni jina la mzazi wako, na hapa hakuna excuse. Kwenye kutumia majina ya wazazi, uko huru kutumia hata majina yote ya mzazi wako, ila jina la pili ni jina lazima liwe ni jina la mzazi wako, wa kiumeni, yaani jina ka baba yako, hii haina excuse popote!.

3. Jina la tatu ni sir name, hili ni jina la ukoo wenu ambalo ni jina la mwisho la babu yako, yaani baba wa baba yako. Hii maana yake kwenye official names lazima utumie majina matatu, jina lako, jina la baba yako na jina la ukoo wako au la babu yako.

Majina Yote Matatu ya Mwigulu Nchemba ni Bandia!
Kwenye majina yako, sijaweza kuona jina la mzazi na jina la ukoo, huwezi kutumia majina yote ya given name bila jina la mzazi na jina la ukoo!.

Katika maelezo yako yanamisi details muhimu sana hizi 3
  1. Ulizaliwa lini, wapi, na ulipozaliwa ulipewa majina matatu yapi?
  2. Ulianza shule lini, wapi, na uliandikishwa kwa majina matatu yapi?
  3. Ulimaliza shule darasa la saba lini, na ulimaliza kwa majina matatu yapi?.
Naomba wenye acess na immigration, fatulieni DN ya Mhe. Mwigulu Mchemba muone imeandikwaje, kwa sababu bila jina la mzazi na jina la ukoo mtu huwezi kuandikishwa shule wala kupata passport kwa majina ya kuokotezwa!.

This is the begining of opening a pandora box, we have to reach to the bottom of this, ila asante sana kujitokeza na kujibu, kwa sababu uwongo, ukisemwa sana na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hugeuka kuwa ni ukweli.

Kwa kuwasaidia wengine wasio jua, hakuna kosa lolote la jinai kujiita jina lolote la bandia na kuitumia popote.

Japo jina la Mwigulu Nchemba ni jina bandia ila vyeti vyake vyote ni vyeti halali.

Kutumia jina bandia, given name sio kosa kisheria na hakuna jinai yoyote! .

Hata mimi Pasco wa JF naweza kuisajili kama Mashokolokubangashe na nikatambulika kama Mashokolokubangashe na vyeti vyangu vyote vikasomeka Mashokolokubangashe na nikawa sijafanya kosa lolote la jinai, ila ikitokea kwenye ujazaji wa fomu zozote za kisheria kama hati ya kusafiria au cheti cha kuzaliwa lazima nitaonyesha majina halisi ya wazazi wangu, na ikitokea kule nako nimejiorodhesha jina la Mashokolokubangashe kuwa ni moja ya majina ya wazazi wangu, then hivyo inageuka forgery, cheating na ni kosa la jinai.

Hivyo natoa wito kwako wanaomtuhumu Mwigulu kudanganya vyeti wapate uthibitisho toka NIDA na Uhamiaji, watayaona majina halisi wazazi wa Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba.

Finally, wewe mwana Ilboru mwenzangu, ujege mara moja moja humu jf sio mpaka tuu kuja kujibu tuhuma, na ile shule iliokufikisha hapo uikumbukege!.
NB. Tukilimaliza vizuri hili zoezi la vyeti bandia, tunaweza kuamua kuanzisha msako wa wenye majina bandia, na kisha hata kwenye asili za watumishi wa umma, maana kuna a very interesting story ya kijana mmoja wa kabila la Kihaya, mwenye jina la Katto.
Asante.
Pasco
Rejea, kati ya wagombea wote wa urais wa CCM, Mhe. Mwingulu, ndie aliye ni impress sana kuliko wote kwa kuwa the most genuine kumbe...
Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President ...
 
Mwigulu kapiga sana chenga kwenye majibu yake na kuacha maswali kadhaa. Maana inatia shaka kwamba hiyo zamani yake mtu akirudi shule kutoka machungani, unaweza kutumia jina la nesi basi ukapata usajili. Kuna walakini bado hapo. Yupo Mwigulu mwenye jina hili.
 
haya umeeleweka....naomba nitoe ombi mjadala huu ufungwe na viongozi wengine wakubwa tu nao wawe na utaratibu wa kuja Hapa kujibu tuhuma kama hizi maana zikiachwa hewani mwisho wa siku zaweza kugeuka kuwa ukweli...mfano kuna Uzi humu unamchafua Mbowe eti hakufika hata form four! so inabidi aje tu alete utetezi wake maana uongo ukirudiwa Mara nyingi bila utetezi unageuka kuwa ukweli...
 

Hapo nimekuelewa mkuu na huu ndio ukweli
 
jina linamiliki vyeti,hivyo basi,mwenye jina ndio mwenye vyeti,mwenye jina akiamua kufuatilia particulars zake shule ya msingi akute taarifa zinaonyesha alifaulu,akaenda chuo lazima alalamike,alalamikie impersonation.

Mbona waliochukua vyeti vya watu leo wanahenyeshwa? kuchukua cheti ni kuchukua jina pia
 
Pasco hebu tueleze sababu za msingi za mtu kuacha kutumia majina yake sahihi na atumie majina feki pamoja na kuwa unayaita bandia? Haya majina bandia ni ya nani? Na kwa nini yatumike??
 
Mkuu Iparamasa, ni kweli kutumia jina la mtu mwingine ni kufoji ila hayo majina ya Mwigulu Nchemba sio majina ya mtu yoyote ni just given names, kama alivyoeleza mwenyewe, siku mtoto anapoandikishwa shule huwa kuna fomu ya majina ya wazazi, kwenye fomu zile za kumuandikisha shule huyu kijana wa Kinyiramba Lameck Madelu Mkumbo, wazazi wake walimuandikisha kwa majina yao kabisa ya Kinyiramba ila wakaomba utawala wa shule kumuandikisha mtoto wao kwa given names za Nesi wa Kisukuma Mwigulu Nchemba na hapo hakuna jinai yoyote kwa sababu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mtu unaruhusiwa kutumia jina lolote mfano Pasco wa JF ni Mashokolokubangashe as long as sio impersonation ya Mashokolokubangashe original.
Pasco
 
kweli kabisa......naona dalili za nchi kupata kihiyo mwingine
 
Pasco hebu tueleze sababu za msingi za mtu kuacha kutumia majina yake sahihi na atumie majina feki pamoja na kuwa unayaita bandia? Haya majina bandia ni ya nani? Na kwa nini yatumike??
Okoso majina ni kitu given, mtu uko huru kutumia given names zozote, na kwenye registration unaruhusiwa kuji register kwa majina yoyote ili mradi kwenye ile fomu majina halisi ya wazazi wako lazima yawepo na hakuna sheria ya kulazimisha kuyatumia ila Polisi, Uhamiaji na Nida ni lazima majina ya wazazi yawepo na yatajwe with given names hata kama ni majina kumi. Hivyo ukweli wa majina halisi ya wazazi wake yapo shule alipoandikishwa, yapo immigration na Nida ambayo yanaonyesha Mwigulu Nchemba ni given names.
Pasco
 

Bungeni wanaruhusu kutumia majina bandia? Vipi kuhusu serikalini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…