Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli

Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli

Mkuu Pasco, somites unajishushiaga credit humu. Hivi hujui kua hayo majina bandia ni kwamba Mh alikua akijitetea tu? Yaani mzazi umpeleke mwanzo shule halafu uombe walimu wamwandikishe kwa majina bandia? Walikua walimu gani hao?Hapa ni blaa blaa nyingi ila jamaa alimaliza shule akafeli darasa la saba akaenda sekondari kwa jina mtu. Tuulize sisi tuliokulia jirani na shule ya msingi aliyosomea! Tena wenzetu wazazi wetu wamefundishia shule alikosoma tunalijua hili sana tu sema hua tunapiga pini tu.
Mkuu Mahanju, Mhe. Mwingulu Nchemba ni verified member humu na trusted source hivyo alichosema humu ndio ukweli wenyewe halisi. Wewe ndio unadanganya.
Pasco
 
Kuna watu wameshindwa elewa kuwa hayo majina "feki" ya Nchemba ndo aliyofanyia mitihani yote na kupata vyeti vyake, ni nini kigumu hapa kuelewa? Sioni tatizo lolote maana vyeti vyote ni halali yake kwa jina alilotumia.
Mkuu Barafu, hii ndio essence ya bandiko hili kuwa kuna cheti bandia na jina bandia. Cheti bandia ni forgery, jina bandia ni cheating. Sio kila jina bandia ni cheti bandia, na sio kila jina bandia ni forgery or cheating, ref ni mimi Pasco wa JF ndie Mashokolokubangashe.
Pasco
 
Mkuu Iparamasa, ni kweli kutumia jina la mtu mwingine ni kufoji ila hayo majina ya Mwigulu Nchemba sio majina ya mtu yoyote ni just given names, kama alivyoeleza mwenyewe, siku mtoto anapoandikishwa shule huwa kuna fomu ya majina ya wazazi, kwenye fomu zile za kumuandikisha shule huyu kijana wa Kinyiramba Lameck Madelu Mkumbo, wazazi wake walimuandikisha kwa majina yao kabisa ya Kinyiramba ila wakaomba utawala wa shule kumuandikisha mtoto wao kwa given names za Nesi wa Kisukuma Mwigulu Nchemba na hapo hakuna jinai yoyote kwa sababu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mtu unaruhusiwa kutumia jina lolote mfano Pasco wa JF ni Mashokolokubangashe as long as sio impersonation ya Mashokolokubangashe original.
Pasco

kama nakuelewa, ishu ni kua mwigulu alifaulu la 7 then hakufaulu kwa jina la mwigulu ila lingine ambalo ndilo analitumuia hadi leo kwenye vyeti, ila hilo mwigulu alipewaga tuu kama nick names
 
jina linamiliki vyeti,hivyo basi,mwenye jina ndio mwenye vyeti,mwenye jina akiamua kufuatilia particulars zake shule ya msingi akute taarifa zinaonyesha alifaulu,akaenda chuo lazima alalamike,alalamikie impersonation.

Mbona waliochukua vyeti vya watu leo wanahenyeshwa? kuchukua cheti ni kuchukua jina pia
kwamba nimewekewa sifa nisizostahili. kuwa nimefika chuo kikuu. Hii ni impersonation. ...it's ,really, drawing high order attention.
 
Mwigulu kapiga sana chenga kwenye majibu yake na kuacha maswali kadhaa. Maana inatia shaka kwamba hiyo zamani yake mtu akirudi shule kutoka machungani, unaweza kutumia jina la nesi basi ukapata usajili. Kuna walakini bado hapo. Yupo Mwigulu mwenye jina hili.
Umeonae! Afu anataka kutuaminisha kwa kasoma zamani sana kiasi kulikuwa na Ujinga mwing sana, wakat siyo kabsa mwigulu ni Juzi hata kama amezid kiumri, na wakati wake uwelewa ulikuwepo sana tu, Labda kama tatizo hili lingempata mzaz wake tungesema inaweza kuwa kweli, alafu na mzazi gan ambae atakubali abadilishe majina yote matatu mpaka la ukoo lisiwepo, daa hapana Mwigulu ni Muongo sana
 
Pasco acha kujishushia hadhi kirahisi namna hii.
Kosa la mwigulu siyo uhalali wa majina!!
Laa hasha, wala hatugombani na ubora wa akili yake kimasomo.
Tunapambana na UDANGANYIFU.
Sisi tunafahamu kuwa mtu ajulikanaye kwa jina la Lameck Mkumbo alifanya mtihani wa darasa la saba mwaka (.. ) katika kituo cha mtihani cha shule ya msingi (.....) akafeli
Halafu mtu yule tunayemfahamu kwa jina la Lameck Mkumbo anafanya tena mtihani wa darasa la saba mwaka (.....) katika kituo cha mtihani cha shule ya msingi (....) this time kwa jina la Mwigulu Nchemba, Akafaulu!!!!!

AMELIONGOPEA TAIFA.
Anaweza kuwaongopea wanyaturu
Hawezi na haitawezekana awaongopee wanyiramba wa kata nzima ya kyengege!!!!!

Kwa ucha MUNGU wao, wakazi hawa dhamira zinawasuta kuona huu mwendelezo wa kulidanganya taifa.

Labda kama uongo sio kosa kwa namna yoyote.

Sikutaja majina ya shule na miaka kama wito kwa Mwigulu Aliombe radhi taifa kwa uongo ule
TAIFA KAMA TAIFA LIKO TAYARI KUMSAMEHE ONCE AND FOR ALL.
Aisee wewe jamaa ndio umeelezea vizuri sasa...
 
Pasco umechanganya mambo kuhusu mfumo au utaratibu wa majina. Kwa sehemu kubwa duniani kuna mifumo miwili ya majina, kuna huu wa nchi za magharibi ambao kutokana na ukoloni ndiyo na sisi tumeurithi na upo wa nchi za mashariki. Huu wa magharibi huwa unaanza na "first name" au kama ukipenda "forename" halafu ukimalizia na "surname" yaani jina la ukoo. Unaweza pia kuwa na jina au majina ya kati "middle name/s". Mfano ni Juma Maharage au Juma Pasco Maharage.
Ule wa mashariki huanza na jina la ukoo halafu likaja la kwako au pengine ukawa na jina la kati. Mfano Wachina; ukisikia anaitwa Xi Jinping basi ujue "Xi" siyo first name bali ndiyo jina la ukoo halafu "Jinping" ndiyo la kwake. Kwa maana nyingine kama Juma Maharage angekuwa Mchina basi angeitwa "Maharage Juma".
Sasa basi utaratibu sahihi hata kwa hapa kwetu kwa mfano ni mtu kuitwa jina lolote la kwanza (first name) au hata la kati (middle name) kama wazazi wake watakavyopenda ila jina la ukoo (surname) linabaki lile lile ambalo linatumika kifamilia. Hili linatakiwa liwe la "kilugha" sababu hakuna ukoo wa Kitanzania au Kiafrika wenye jina la kizungu, yote yanapaswa kuwa ya kikwetu.
Kuna utaratibu mbovu hapa kwetu ambapo mtu anayeitwa kwa mfano "Steven Paul Mkama" anazaa mtoto halafu badala ya kumuita mfano "Judith Mkama" au "Judith Roselyn Mkama" utasikia anamuita "Judith Steven" au "Judith Steven Mkama".
Haya ni makosa maarufu sana. Kwa mfano huu, huyu mtoto ni Judith Roselyn, hayo ndiyo majina yake sahihi. Jina pekee analoazima ni "Mkama" ambalo ni la ukoo. "Steven" na "Paul" hapaswi kabisa kuyatumia kwa sababu haya ni "personal names" za baba yake kama vile yeye alivyo na personal names zake mbili yaani Judith Roselyn. Atakapokuwa anatumia personal name yoyote ya baba yake tayari anapoteza huo ukoo. Hili tatizo linajitokeza mara nyingi mno hapa Tanzania.
Kuhusu "nicknames", haya ni majina ya utani ambayo hayachukuliwi kuwa rasmi, mfano yule beki wa Yanga anayeitwa "Canavarro", hakuna mtu yeyote anayeamini kwamba hilo ndiyo jina lake na wala hawezi kulitumia "officially" popote. Yapo pia majina yanayoitwa "stage names" ambayo hutumiwa sana na wanamuziki au wacheza sinema na wengine huamua kuyatumia rasmi kisheria kama majina yao. Mfano mwanamuziki maarufu wa Uingereza anayefahamika kama "Elton John" jina hili ni stage name ambayo amelirasimisha. Majina yake ya kuzaliwa ni Reginald Kenneth Dwight.
Kwa leo niishie hapa.
 
Mkuu Mahanju, Mhe. Mwingulu Nchemba ni verified member humu na trusted source hivyo alichosema humu ndio ukweli wenyewe halisi. Wewe ndio unadanganya.
Pasco
Kwahiyo unaamini kua mtuhumiwa hata siku atajisemea ukweli? We Pasco vipi bhana? Kwa akili yako ndio umemuelewa?
 
Pasco acha kujishushia hadhi kirahisi namna hii.
Kosa la mwigulu siyo uhalali wa majina!!
Laa hasha, wala hatugombani na ubora wa akili yake kimasomo.
Tunapambana na UDANGANYIFU.
Sisi tunafahamu kuwa mtu ajulikanaye kwa jina la Lameck Mkumbo alifanya mtihani wa darasa la saba mwaka (.. ) katika kituo cha mtihani cha shule ya msingi (.....) akafeli
Halafu mtu yule tunayemfahamu kwa jina la Lameck Mkumbo anafanya tena mtihani wa darasa la saba mwaka (.....) katika kituo cha mtihani cha shule ya msingi (....) this time kwa jina la Mwigulu Nchemba, Akafaulu!!!!!

AMELIONGOPEA TAIFA.
Anaweza kuwaongopea wanyaturu
Hawezi na haitawezekana awaongopee wanyiramba wa kata nzima ya kyengege!!!!!

Kwa ucha MUNGU wao, wakazi hawa dhamira zinawasuta kuona huu mwendelezo wa kulidanganya taifa.

Labda kama uongo sio kosa kwa namna yoyote.

Sikutaja majina ya shule na miaka kama wito kwa Mwigulu Aliombe radhi taifa kwa uongo ule
TAIFA KAMA TAIFA LIKO TAYARI KUMSAMEHE ONCE AND FOR ALL.
Mkuu Jogi, Mhe. Mwingulu Nchemba ni verified member humu hivyo alichosema yeye ndicho ukweli, wewe ni just a pen name kama mimi na unachosema wewe ni uongo wa mchana kweupe! .

NB. Hii mada ni kama ya utani utani lakini tungekuwa nchi za wenzetu hapa kuna mtu akaondoka but not Tanzania. Kwa sababu kutaleta a very bad Precedence na watu kama kina Katto sijui itakuwaje.
Pasco
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Pasco umechanganya mambo kuhusu mfumo au utaratibu wa majina. Kwa sehemu kubwa duniani kuna mifumo miwili ya majina, kuna huu wa nchi za magharibi ambao kutokana na ukoloni ndiyo na sisi tumeurithi na upo wa nchi za mashariki. Huu wa magharibi huwa unaanza na "first name" au kwa ukipenda "forename" halafu ukimalizia na "surname" yaani jina la ukoo. Unaweza pia kuwa na jina au majina ya kati "middle name/s". Mfano ni Juma Maharage au *******************.
Ule wa mashariki huanza na jina la ukoo halafu likawa la kwako au pengine ukawa na jina la kati. Mfano Wachina; ukisikia anaitwa Xi Jinping basi ujue "Xi" siyo first name bali ndiyo jina la ukoo halafu "Jinping" ndiyo la kwake. Kwa maana nyingine kama Juma Maharage angekuwa Mchina basi angeitwa "Maharage Juma".
Sasa basi utaratibu sahihi kwa hapa kwetu kwa mfano ni mtu kuitwa jina lolote la kwanza (first name) au hata la kati (middle name) kama wazazi wake watakavyopenda ila jina la ukoo (surname) linabaki lile lile ambalo linatumika kifamilia. Hili linatakiwa liwe la "kilugha" sababu hakuna ukoo wa Kitanzania au Kiafrika wenye jina la kizungu, yote yanapaswa kuwa ya kikwetu.
Kuna utaratibu mbovu hapa kwetu ambapo mtu anayeitwa kwa mfano "Steven Paul Mkama" anazaa mtoto halafu badala ya kumuita mfano "Judith Mkama" au "Judith Roselyn Mkama" utasikia anamuita "Judith Steven" au "Judith Steven Mkama".
Haya ni makosa maarufu sana. Kwa mfano huu, huyu mtoto ni Judith Roselyn, hayo ndiyo majina yake sahihi. Jina pekee analoazima ni "Mkama" ambalo ni la ukoo. "Steven" na "Paul" hapaswi kabisa kuyatumia kwa sababu haya ni "personal names" za baba yake kama vile yeye alivyo na personal names zake mbili. Atakapokuwa anatumia personal name yoyote ya baba yake tayari anapoteza huo ukoo. Hili tatizo linajitokeza mara nyingi mno hapa Tanzania.
Kuhusu "nicknames", haya ni majina ya utani ambayo hayachukuliwi kuwa rasmi, mfano yule benki wa Yanga anayeitwa "Canavarro", hakuna mtu yeyote anayeamini kwamba hilo ndiyo jina lake na wala hawezi kulitumia "officially" popote. Yapo pia majina yanayoitwa "stage names" ambayo hutumiwa sana na wanamuziki au wacheza sinema na wengine huamua kuyatumia rasmi kisheria kama majina yao. Mfano mwanamuziki maarufu wa Uingereza anayefahamika kama "Elton John" jina hili ni stage name ambayo amelirasimisha. Majina yake ya kuzaliwa ni Reginald Kenneth Dwight.
Kwa leo niishie hapa.
Huyu Pasco naona keshaanza kuzeeka.
 
Back
Top Bottom