Wanabodi,
Katika zoezi la kusaka vyeti bandia, kuna watu wanashindwa kutofautisha kati ya vyeti bandia na majina bandia.
Cheti bandia ni cheti ambacho ama hakipo kabisa hivyo kimetengezwa cheti fake kwa forgery ama ni cheti cha kweli lakini anayekitumia sii mwenyewe mwenye cheti halisi, hivyo kufoji cheti cha mtu mwingine, hili ni kosa kubwa la jinai na huu ni wizi!.
Jina bandia ni kutumia majina ya kuunga unga ambayo sio majina yako halisi, lakini aliyeingia darasani kusoma ni wewe, aliyehitimu ni wewe, hivyo hicho cheti ulichokipata ni cheti halali na sio cheti bandia ila jina ndilo jina bandia.
Nimesoma utetezi wa Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kuhusu tuhuma za kuwa na cheti bandia, nimejiridhisha kabisa tena pasi shaka kuwa vyeti vya Mhe. Mwingulu Nchemba sio vyeti fake ila majina ya Mwigulu Nchemba ndilo jina bandia.
Sio kila jina bandia ni forgery, kuna majina bandia yanayoitwa Nick Names sio forgery bali ni just given names. Given names hizo zinapokuwa registered kwenye vyeti, vyeti hivyo ni halali ila jina la mwenye cheti ndilo jina bandia ambalo halina kosa lolote kisheria.
Uthibitisho huu ni kufuatia utetezi huu wa Mhe. Mwingulu Nchemba umethibitisha jina la Mwigulu Nchemba ni jina bandia la mtu halisi aitwae mwenye given name ya Lameck Madelu Mkumbo ambaye hata majina hayo,hakuna jina lolote la wazazi wake wala jina la ukoo wake, kama anavyojieleza yeye mwenyewe.
Mkuu Mhe. Mwigulu, kwa vile hili bandiko nimelikutia page 33, na sijaweza kusoma mabandiko yate ya nyuma, hivyo siwezi kujua kama ulijibu haya, ila kwanza kwa heshma na taadhima, nakupongeza sana kujitokeza kujibu tuhuma, ila very unfortunately, majibu yako, hayajitoshelezi kabisa!, hakuna kitu chochote ulichojibu hapa, you leave more questions than answers and there is something fishy!.
Majina yana formula ya majina, na hayawezi kuijiibukia tuu hivi hivi, na formula hiyo ni universal, dunia nzima.
Jina lina given name, yaani jina ulilopewa wewe, hili given name linaweza kuwa moja au hata kumi, haijalishi, kwenye given name, ni lile jina unaloitwa, liwe la utoto, ubatizo, etc, Kiingeza linaitwa fast name!.
Jina la pili, ni lazima liwe ni jina la kwanza la mzazi wako, na hapa hakuna excuse, kama mwanzo kwenye given name, umetumia jina la nyumbani, la kilugha, then jina la pili lazima liwe jina la ubatizo, ukitangulia na jina la ubatizo, then jina la pili au liwe ni jina la kwanza, la mzazi wako, au ukitumia fast name ya majina mawili yote ya kwako, then jina la tatu ni lazima liwe ni jina la kwanza la mzazi wako!, na jina la nne ni lazima liwe ni jina la ukoo wenu yaani sir name.
Kwenye majina yako, sijaweza kuona jina la mzazi na jina la ukoo, huwezi kutumia majina yote ya given name bila jina la mzazi na jina la ukoo!.
Naomba wenye acess na immigration, fatulieni DN ya Mhe. Mwigulu Mchemba muone imeandikwaje, kwa sababu bila jina la mzazi na jina la ukoo mtu huwezi kupata passport kwa majina ya kuokotezwa!.
This is the begining of opening a pandora box, we have to reach to the bottom of this, ila asante sana kujitokeza na kujibu, kwa sababu uwongo, ukisemwa sana na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hugeuka kuwa ni ukweli.
Kwa kuwasaidia wengine wasio jua, hakuna kosa lolote la jinai kujiita jina lolote la bandia na kuitumia popote.
Japo jina la Mwigulu Nchemba ni jina bandia ila vyeti vyake vyote ni vyeti halali.
Kutumia jina bandia, given name sio kosa kisheria na hakuna jinai yoyote! .
Hata mimi Pasco wa JF naweza kuisajili kama Mashokolokubangashe na nikatambulika kama Mashokolokubangashe na vyeti vyangu vyote vikasomeka Mashokolokubangashe na nikawa sijafanya kosa lolote la jinai, ila ikitokea kwenye ujazaji wa fomu zozote za kisheria kama hati ya kusafiria au cheti cha kuzaliwa lazima nitaonyesha majina halisi ya wazazi wangu, na ikitokea kule nako nimejiorodhesha jina la Mashokolokubangashe kuwa ni moja ya majina ya wazazi wangu, then hivyo inageuka forgery, cheating na ni kosa la jinai.
Hivyo natoa wito kwako wanaomtuhumu Mwigulu kudanga wapate uthibitisho toka NIDA na Uhamiaji, watayaona majina halisi wazazi wa Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba.
Finally, wewe mwana Ilboru mwenzangu, ujege mara moja moja humu jf sio mpaka tuu kuja kujibu tuhuma, na ile shule iliokufikisha hapo uikumbukege!.
NB. Tukilimaliza vizuri hili zoezi la vyeti bandia, tunaweza kuamua kuanzisha msako wa wenye majina bandia, na kisha hata kwenye asili za watumishi wa umma, maana kuna a very interesting story ya kijana mmoja wa kabila la Kihaya, mwenye jina la Katto.
Asante.
Pasco
Rejea, kati ya wagombea wote wa urais wa CCM, Mhe. Mwingulu, ndie aliye ni impress sana kuliko wote kwa kuwa the most genuine kumbe...
Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President ...