Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli

Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli

Pasco mwiguru mchemba ni mwalifu katika taratibu za usajili wa mtu duniani kwani amekonfuse jamii, yaani ni kama amepoteza vinasaba (DNA) kama ukitokea ghafla ujamtafuta huwezi kujua pa kuanzia; kiumri alisoma akiwa mtu mzima sana kiasi kwamba alitakiwa atambue kuwa kujipoteza na kujipotosa ni kosa kwani ukipata ajali ukafa unaweza kukuta umezikwa mwanza wakati kwako singida .pia utaratibu wa sensa waweza kupata itilafu kwani ubini una utata, kitu kingine anamweka wasiwasi mamake mzazi kuwa uenda alimwibia siri kuwa sio mzaliwa halali wa kinyailamba ndio maana katika maelezo yake wakati anatafuta ubunge alipata shida kuyatambulisha haya majina ndio akaongezea lamerk madelu yani mtu mwenye madevu ndipo wakampa kura, je ikitokea babayake akataka wapime DNA si ndio kuhaibika zaidi. Tunataka sababu makini sio visababu vya kuokoteza
 
f69377dcef34bc88463f029bdd4da5ca.jpg
kafanya tukio kama ili. Najua umelipwa ili umtetee.
Hili ni kosa tuu la photo misplacement ni kosa la kawaida sana kwenye printing wakati wa designing au type setting ila hilo ni tangazo moja la mtu mmoja yule yule walichanganya tuu picha, wale mnaojua mambo ya matangazo, someni advert control number yenye maandishi madogo chini ya picha upande wa kulia. Wakarekebisha na kurudiwa kutangazwa.

Pasco
 
Wanabodi,
Katika zoezi la kusaka vyeti bandia, kuna watu wanashindwa kutofautisha kati ya vyeti bandia na majina bandia.

Cheti bandia ni cheti ambacho ama hakipo kabisa hivyo kimetengezwa cheti fake kwa forgery ama ni cheti cha kweli lakini anayekitumia sii mwenyewe mwenye cheti halisi, hivyo kufoji cheti cha mtu mwingine, hili ni kosa kubwa la jinai na huu ni wizi!.

Jina bandia ni kutumia majina ya kuunga unga ambayo sio majina yako halisi, lakini aliyeingia darasani kusoma ni wewe, aliyehitimu ni wewe, hivyo hicho cheti ulichokipata ni cheti halali na sio cheti bandia ila jina ndilo jina bandia.

Nimesoma utetezi wa Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kuhusu tuhuma za kuwa na cheti bandia, nimejiridhisha kabisa tena pasi shaka kuwa vyeti vya Mhe. Mwingulu Nchemba sio vyeti fake ila majina ya Mwigulu Nchemba ndilo jina bandia.

Sio kila jina bandia ni forgery, kuna majina bandia yanayoitwa Nick Names sio forgery bali ni just given names. Given names hizo zinapokuwa registered kwenye vyeti, vyeti hivyo ni halali ila jina la mwenye cheti ndilo jina bandia ambalo halina kosa lolote kisheria.

Uthibitisho huu ni kufuatia utetezi huu wa Mhe. Mwingulu Nchemba umethibitisha jina la Mwigulu Nchemba ni jina bandia la mtu halisi aitwae mwenye given name ya Lameck Madelu Mkumbo ambaye hata majina hayo,hakuna jina lolote la wazazi wake wala jina la ukoo wake, kama anavyojieleza yeye mwenyewe.


Mkuu Mhe. Mwigulu, kwa vile hili bandiko nimelikutia page 33, na sijaweza kusoma mabandiko yate ya nyuma, hivyo siwezi kujua kama ulijibu haya, ila kwanza kwa heshma na taadhima, nakupongeza sana kujitokeza kujibu tuhuma, ila very unfortunately, majibu yako, hayajitoshelezi kabisa!, hakuna kitu chochote ulichojibu hapa, you leave more questions than answers and there is something fishy!.

Majina yana formula ya majina, na hayawezi kuijiibukia tuu hivi hivi, na formula hiyo ni universal, dunia nzima.

Jina lina given name, yaani jina ulilopewa wewe, hili given name linaweza kuwa moja au hata kumi, haijalishi, kwenye given name, ni lile jina unaloitwa, liwe la utoto, ubatizo, etc, Kiingeza linaitwa fast name!.

Jina la pili, ni lazima liwe ni jina la kwanza la mzazi wako, na hapa hakuna excuse, kama mwanzo kwenye given name, umetumia jina la nyumbani, la kilugha, then jina la pili lazima liwe jina la ubatizo, ukitangulia na jina la ubatizo, then jina la pili au liwe ni jina la kwanza, la mzazi wako, au ukitumia fast name ya majina mawili yote ya kwako, then jina la tatu ni lazima liwe ni jina la kwanza la mzazi wako!, na jina la nne ni lazima liwe ni jina la ukoo wenu yaani sir name.

Kwenye majina yako, sijaweza kuona jina la mzazi na jina la ukoo, huwezi kutumia majina yote ya given name bila jina la mzazi na jina la ukoo!.

Naomba wenye acess na immigration, fatulieni DN ya Mhe. Mwigulu Mchemba muone imeandikwaje, kwa sababu bila jina la mzazi na jina la ukoo mtu huwezi kupata passport kwa majina ya kuokotezwa!.

This is the begining of opening a pandora box, we have to reach to the bottom of this, ila asante sana kujitokeza na kujibu, kwa sababu uwongo, ukisemwa sana na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hugeuka kuwa ni ukweli.

Kwa kuwasaidia wengine wasio jua, hakuna kosa lolote la jinai kujiita jina lolote la bandia na kuitumia popote.

Japo jina la Mwigulu Nchemba ni jina bandia ila vyeti vyake vyote ni vyeti halali.

Kutumia jina bandia, given name sio kosa kisheria na hakuna jinai yoyote! .

Hata mimi Pasco wa JF naweza kuisajili kama Mashokolokubangashe na nikatambulika kama Mashokolokubangashe na vyeti vyangu vyote vikasomeka Mashokolokubangashe na nikawa sijafanya kosa lolote la jinai, ila ikitokea kwenye ujazaji wa fomu zozote za kisheria kama hati ya kusafiria au cheti cha kuzaliwa lazima nitaonyesha majina halisi ya wazazi wangu, na ikitokea kule nako nimejiorodhesha jina la Mashokolokubangashe kuwa ni moja ya majina ya wazazi wangu, then hivyo inageuka forgery, cheating na ni kosa la jinai.

Hivyo natoa wito kwako wanaomtuhumu Mwigulu kudanga wapate uthibitisho toka NIDA na Uhamiaji, watayaona majina halisi wazazi wa Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba.

Finally, wewe mwana Ilboru mwenzangu, ujege mara moja moja humu jf sio mpaka tuu kuja kujibu tuhuma, na ile shule iliokufikisha hapo uikumbukege!.
NB. Tukilimaliza vizuri hili zoezi la vyeti bandia, tunaweza kuamua kuanzisha msako wa wenye majina bandia, na kisha hata kwenye asili za watumishi wa umma, maana kuna a very interesting story ya kijana mmoja wa kabila la Kihaya, mwenye jina la Katto.
Asante.
Pasco
Rejea, kati ya wagombea wote wa urais wa CCM, Mhe. Mwingulu, ndie aliye ni impress sana kuliko wote kwa kuwa the most genuine kumbe...
Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President ...
Maelezo yako ni mazuri lakini kama ulivyokili, Mwigulu ameacha maswali zaidi kuliko majibu!!

Ila kwa upande wangu ninafikiri ni lazima zoezi la vyeti liendane na la majina bandia. Ni kweli kabisa Mwigulu amepata vyeti vile kiahalali ila hiyo ya kuacha shule na kurudi baada ya miaka miwili anatuchomekea!! Na hapo ndipo utata ulipo!? Kwa nini aliporudi aliamua kutumia majina tofauti. Je jina lake lilikuwa limeshaondolewa kwenye roster!(register book)!? Kwa sisi tuliosoma miaka ile hii inawalakini mkubwa sana. Watu wengi waliokuwa wanafail darasa la saba walikuwa wanarudia darasa la tano kwa kuwa kwa kutumia majina ya watu walioacha shule. Na ilikuwa rahisi darasa la tano kuliko la sita kwa kuwa record za mwanafunzi kwa ajili ya mtihani wa darasa la saba zilikuwa hazijapelekwa huko juu (Mkoani ...nk.). Hata uhamisho kuanzia darasa la sita ulikuwa ni mgumu sana, la saba ilikuwa almost impossible!!

Off course issue ya Mwigulu ni bit complected kwa vile ni jasho lake ingawa inawezekana kwa jina la mwingine. Ila kama ni kweli ametumia jina la any drop out basi ni forgery kama forgery nyingine. Kwa nini nasema hivi? Kuna watu vile vile wametumia vyeti vya watu wengine may form four wakaenda wakasoma high school au vyuoni kwa kutumia akili zao na kufaulu vizuri tu na wanafanya kazi vizuri tu. Hili kundi halina tofauti na Mwigulu. Labda tofauti yao moja alifanya akiwa Primary school na mwingine baada ya secondary school.

On the other hand, naona kama hili zoezi lingeweza kufanyika tofauti kidogo. Badala ya kulenga vyeti kwanza wangelenga kwenye utendaji. Hii ni kwa sababu hili tatizo lilikuwa ni la kitaifa na ninaamini kila moja wetu walau anajua at least mtu moja mwenye hili tatizo. Inawezekana hata Rais awawafahamu watu au marafiki zake wa enzi zile. Hata Afrika ya Kusini walipopata uhuru waliamua kufanya reconciliation. Hii ilikuwa ni kusamehe yaliyotokea huko nyuma.

Off course kuna lile kundi ambalo wao wamechukua vyeti tu na kuvitumia kupata kazi moja kwa moja bila kuingia darasani. Hawa lazima waondolewe.
 
Mtaumiza vichwa sana. Ukweli ni kwamba Lameck Madelu Mkumbo alifanya mtihana wa darasa la saba akashindwa.

Baada ya kushindwa darasa la saba mara ya kwanza, Lameck Madelu Mkumbo akaamua kurudia shule ya msingi. Kwakuwa miaka hiyo kurudia shule ya msingi ilikuwa hairuhusiwi, ndipo Lameck Madelu Mkumbo, akachukua jina la Mwigulu Nchemba, kijana wa kisukuma aliyekuwa ameacha shule wakati huo akiwa darasa la tano.

Hivyo Lameck Madelu Mkumbo akasoma darasa la tano kwa kutumia jina la Mwigulu Nchemba hadi darasa la saba na akafaulu mtihani kwa jina hilo la Mwigulu Nchemba.

Hivyo Mwigulu Nchemba aka Lameck Madelu Mkumbo hakuiba cheti cha mtu bali alisoma kwa kutumia jina la mtu mwingine aliyekuwa ameacha shule wakati huo kwasababu zake.
 
Mkuu Yohana Mbatizaji utakuwa hujui. Mimi namfahamu Paskali vizuri sana kwa sababu mimi na yeye ni mapacha wa tumbo moja. Msemaji wa pale alikuwa awe ni yule jamaa wa Mtanzania, msaidizi wake ni huyu jamaa wa DW aliyepo, Paskali yeye angekula tuu tenda za production ya vipindi vya TV kupitia kampuni yake ya PPR.
Pasco
Umenifurahisha sana Mkuu
 
kachukua jina la dactari kasome tena.
swissme
Mkuu Swiss Me, jina la dakitari, hakujichukulia yeye, bali mama alipokwenda hospitali, dakitari akashindwa kulielewa jina la mama, hivyo mama akatoa kibali kwa dakitari, basi mpe wewe jina, dakitari akatoa majina, hakuna tatizo lolote hapo!.
Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja.
Mwigulu,
Japo ni very interesting!.

Pasco
 
Sidhani kama ni lazima jina la pili liwe la mzazi, mfano mimi jina langu la pili na tatu yote ni ya babu zangu, situmii jina la mzazi wala la ukoo! Wakati mwingine inasaidia sana kukuepusha na mambo mengi!
 
nyie mnamtetea mwigulu muna hoja nzuri naza kuvutia......lakini mwigulu mwenyewe hana hoja....hawezi kujitetea...kwanini hawezi kujitetea na kujenga hoja zilete mashiko?????????????/
yeye ndo anaejua ukweli..nahisi kuna uforgery fulani wa kutumia kacheti ka mwigulu OG wa vijijini
 
Mkuu Swiss Me, jina la dakitari, hakujichukulia yeye, bali mama alipokwenda hospitali, dakitari akashindwa kulielewa jina la mama, hivyo mama akatoa kibali kwa dakitari, basi mpe wewe jina, dakitari akatoa majina, hakuna tatizo lolote hapo!.
Japo ni very interesting!.

Pasco
Jaribuni kujenga hoja sio kukurupuka.soma kipande kimoja kimoja cha lameck au nikusaidie kukata vipande hili ujue jamaa kaamua tena kudanganya


swissme
 
Mimi namfahamu kwa jina la gulo shumbi
Mkuu wewe kumfahamu kwa jina lolote hakujalishi, mtu anaweza kufahamika mahali fulani kwa jina fulani, la mahali pengine kwa jina jingine, kinachomatter ni jina lake halisi la ukweli ni nani!.

Pasco
 
Chabruma na Kigwa please, jitokezeni hapa kujibu tuhuma zinazowakabili. Pongezi kwake Mh. Lameck Madelu Mkumbo kwa ufafanuzi wake.
 
haya umeeleweka....naomba nitoe ombi mjadala huu ufungwe na viongozi wengine wakubwa tu nao wawe na utaratibu wa kuja Hapa kujibu tuhuma kama hizi maana zikiachwa hewani mwisho wa siku zaweza kugeuka kuwa ukweli...mfano kuna Uzi humu unamchafua Mbowe eti hakufika hata form four! so inabidi aje tu alete utetezi wake maana uongo ukirudiwa Mara nyingi bila utetezi unageuka kuwa ukweli...
Ngoja tumalizane na hawa waliyoko serikarilini, kisha tutahamia kwenye vyama vya siasa.
 
Back
Top Bottom