Pasco, ni kwa maslahi ya kisiasa ya Mwingulu mwenyewe kusafisha hili wingu la majina fake kwa sababu pia ana ambition kubwa katika safari yake ya kisiasa. Kinachotakiwa hapa siyo uhalali kisheria wa kutumia hayo majina, bali yalipatikanaje. Na muhimu zaidi hiki ni kipimo cha ukweli na uaminifu wa Mwingulu kama kiongozi wa kitaifa. Kadhalika huu ni mtihani wa kupima umahiri wake katika kujibu tuhuma au maswali yanayomhusu. Utetezi wake umezidisha utata kwa sababu hauko straight; na maelezo yake yana makosa mengi ya kisarufi na kiuandishi (poor grammar, phraising, punctuation and capitalization) na hivyo hayaeleweki kirahisi. Hii haiendani na hadhi yake.