Uthibitisho wa uwepo wa roho na ulimwengu wa roho ni ndoto

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
8,774
Reaction score
13,566
Kila mtu anapo lala usingizi kuna kitu hutokea kinaitwa rapid eye movement (REM) macho kuzunguka kwa haraka.
Hutokea baada ya saa 1 hadi masaa 2 katika usingizi.
Ndipo utaanza kupata ndoto au maono ambayo ni kama jambo halisi nala kawaida.

Wengi wenu manapokua kwenye ndoto, ndoto hizo huja na hisia nyingi na kuonekana kama ni kweli lakini ukishituka unajisemea asante Mungu kumbe ilikua ni ndoto tu

Mtu unaota umekufa au unaota ukizikwa na unapiga kelele na kulia lakini utakapo amka unagundua ilikua ni ndoto tu.

Macho kuzunguka hiyo ni hatua ya mwisho hatua ya Nne.
1. Hatua ya kwanza
Mtu unapofumba macho na kuamua kulala unaanza na kufikiri.
Lazima kuwa na muda mchache wa kutafari ndipo usinzie,
sasa kama utakua na vitu vingi vinavyokusumbua utatumia muda mwingi kufikiria hadi uje upate usingizi.

2. Hatua ya pili
Hatua ya pili ni pale ubongo wako utaacha kufanya kazi, utaacha kufikiri na ubongo utakua umetulia.
unaweza kusikia yanayoendelea mahali ulipo lakini kwa hisia za mbali kidogo.
mfano wakati umelala chumbani ulihisi kuna mtu kaingia na kutoka kwenye chumba ulicholala.

3. Hatua ya Tatu.
Hii hatua unakua hujui chochote kinachoendelea katika ulimwengu wa mwili.

4. Ndipo unaingia hatua ya nne.
Ni hatua ya mwisho macho yanakua yanazunguka kwa kasi..

mfano:
kuna baadhi yenu ambao mmewahi kukaa pembeni ya mtu amelala na ukagundua huyo mtu alikuwa katika ndoto.
Utaona anaweweseka uso, wakati macho yanazunguka kulia na kushoto na kichwa kinaweweseka.

Kama ni ndoto mbaya unaweza kugundua, na kama ni ndoto nzuri unaweza kugundua.
Wangapi umewahi kukaa na mtu kalala na anaota na usoni anaanza kufurahi na kucheka na wakati mwingine kuongea. Hiyo ni ndoto.
Na kuna wengine hawaongei, wala hawafurahi wala kucheka lakini jinsi macho yanavyozunguka unaweza kuona kwa kumwangalia usoni katika macho aliyoyafumba.

Hii umaanisha kwamba kuna mawasiliano, kuna mawasiliano yanaendelea, kuna shughuli inaendelea katika ulimwengu mwingine.

Sio kila kinachotokea katika ndoto muhusika akiamka ataweza kukumbuka kila ndoto, lakini ndoto hutokea sana kwa kila mtu.

Kinachotokea kama ndoto itakutia hofu, basi ndoto hiyo inatunzwa katika subconscious mind na utakapo amka ni lazima utaikumbuka ndoto hiyo.

Kuna mwingine anakumbuka kabisa nilipata ndoto, lakini haikumbuki inasemaje, kwa sababu hana uwezo wa kupokea taarifa katika ulimwengu wa roho kuja ulimwengu wa mwili.
japo anakua anajua wazi niliota ndoto lakini haikumbuki.

Kutokujua maana na ndoto haina maana kwamba ulichokiona na kusikia katika ndoto hakina umuhimu.

Uthibitisho ni huo kama umewahi kumshuhudia mwenzio katika hali hiyo.
Tafsiri ya ndoto,
Kwanini tunapata ndoto,
na ndoto hutoka wapi sio somo letu la Leo.

OUR DESIRE IS HAPPINESS.
 
Mtu kashalala hayo macho yake unaonaje yanazunguka
 
Ndoto yeyeto yenye ujumbe ni lazima utaikumbuka ukiamka hata zaidi ya siku tatu utaendelea kuikumbuka.
Ndoto za kujirudia mara kwa Mara ni ujumbe nenda kwa wafasiri wakupe maana.
 
Usingizi ni nusu ya kifo,roho huwa inaacha mwili inatoka ukilala Ina uwezo wa kufika mahali hata ndani ya sekunde tatu na kushiriki vingi katika ulimwengu wa roho.
Thus ukimstua mtu aliyelala Huwa anakurupuka kabla, roho Ina sense na mwili thus ndani ya sekunde ukimstua au mgusa mtu anapata uwezo wa kuamka.
Roho inaweza ikakamatwa na nguvu zingine mfano wachawi na viumbe vingine katika roho na ikashindwa kurejea kwenye mwili,hii inaitwa kifo Cha usingizini,alilala hakuamka Tena yaan kafia usingizini.
 
Upo uwezekano wa kurudia ndoto kwa kuwa na eneo geni zaidi ya Mara moja labda mji fulani ambao haujawahi kuufika ile inakuwa ni real upo ugenini katika mji usiowahi kuwepo.
 
Roho inaweza ikakamatwa na nguvu zingine mfano wachawi na viumbe vingine katika roho na ikashindwa kurejea kwenye mwili,hii inaitwa kifo Cha usingizini,alilala hakuamka Tena yaan kafia usingizini.
Haya mambo mliyathibitisha wapi?
 
Nyie atheist piteni kushoto hizi elimu ni kubwa sana kwenu
Akili kubwa huwa hawana assumption za mihemko mtu anapohitaji kupata maarifa.

Swali lipo straight, hizi habari zimethibitishwa wapi wewe unakuja na mihemko.
 
Kupitia wenye elimu kuhusu ndoto
 
Imani na uthibitisho havikai sehemu moja. Ukishathibitisha unaacha kuamini, unaanza kujua.
 
Back
Top Bottom