Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

faida yake ndogo sana na inaumiza yani box moja unapata 1,500/= but gud idea though!!
 
Hongera kwa wazo lako pia shukrani kwa kuutambua mchango wangu mpaka kuuweka kwenye top ten yako,,
Hongera kwa mshindi na waliotoa mawazo yao kwa uwazi bila choyo

Nishauri tu hii kitu iwe endelevu na watakaofanyia kazi baadhi ya mawazo yaliyotolewa humu walete mrejesho, hata kama itakuwa negative ili tuzijue changamoto za mawazo husika maana tunajua kuandika wazo na kulitekeleza mara nyingi havifanani

Mi nitaendelea kuandika fursa kadri nitakavyokuwa nakutana nazo huko mahangaikoni
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thanks a lot
 
Hongera kwa ushindi mkuu, ningependa kufahamu namna unavyouza hayo maziwa, ni kwamba unakuwa na kijiwe unaweka kambi au unawafuata watu vijiweni unakuwa unawauzia kama vile wanavyouza wale jamaa wa kahawa...


Na hayo maziwa yanakuwa ni fresh au mtindi, kama siyo mtindi yanapokuwa hujauza yote yanayobaki unafanyaje, na kama ni ya mtindi unafanya vipi kuyaweka katika hali ya ubaridi. Nitashukuru nikipata ufafanuzi
 


Jinsi alivyoandika inaonekana ameamua kushare .sio kitu anachofanya...nimewaza hvyo!na mshindi ilisemekana ni yule anayetaka anza na sio aliye na business!
Hongera@zwangedaba
 
Ongera kwa mshindi, Ni wakati wake sasa kuchukua wazo kuliingiza kwenye Field,

Changamoto na Vikwazo ni mapito tu yasikukatishe tamaa, focus kwa kile unachokifanya naamini utaleta mrejesho Chanya hapa.


Cc Zero iq

Sent using Jamii Forums mobile app
 
faida yake ndogo sana na inaumiza yani box moja unapata 1,500/= but gud idea though!!
Faida ni ndogo kwa box moja lakin angalia mchanganuo, pia biashara inahitaji uvumilivu mpaka ikae sawa wengine huanza na hasara.

Kuna jamaa anafanya hyo biashara, alinunua freezer na akatafuta vijana akawasambaza katika mashule na matokeo yake ni mazuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MREJESHO
Wakuu habari ya leo,
Tumshukuru mungu kwa wale tulio na afya njema, na kwa wale wenzetu wenye shida mbalimbali basi mungu awafanyie wepesi.

Kama nilivyoanza na kichwa cha habari hapo juu nimeleta mrejesho wangu wa kinyang'anyiro hiki kilichokuwa kinaendelea kwa siku kadhaa hapa jukwaani, na wengi wetu kutoa mawazo yetu mbalimbali.

Mleta mada jana usiku wa saa sita aliahidi kumleta mshindi wa hili shindano,ambalo miongoni mwa orodha ile nami nilikuwepo na kuibuka na ushindi mnamo saa sita na dakika mbili usiku.

Akanifuata pm tukawasiliana usiku ule na akaahidi leo akishatoka ibadani, basi atakamilisha lile dhumuni lake. Na ilipofika saa 11:42am alinitumia hiyo pesa ikiwa kamili na ya kutolea.

Shukrani zangu za dhati ni kwa mwenyezi mungu kwanza,halafu wale wote tulioshiriki kutoa mawazo yetu hapa, sababu yatanufaisha watu wengi.

Bwana Bonde la Baraka mungu akuzidishie baraka zaidi kama unavyojiita, kwani umekuwa faraja kubwa sana kwetu,na naomba na wengine wenye uwezo mjitokeze zaidi ili kuweza kusogeza gurudumu hili la maendeleo hasa kwetu vijana.
Mungu awabariki sana.

NB:Si mwandishi mzuri kwa hiyo tuvumiliane kwa hili.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…