Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

apo penyewe apo[emoji122][emoji122][emoji122]
Naomba na mimi lisinipite hili . .
Mimi idea yangu kuuza sambusa na kacholi mashuleni (msingi na secondari ) na mtaani.
Gharama .
kalai lipo tayari
Deli lipo tayari
Viazi 2@5k
Ngano 2@1300
mafuta 2@2000
Nyanya kwa siku , pilipili, chumvi rangi ya kacholi (2000) =2000+ 5000= 7k
Jumla ni 24k
Sales
sambusa 100@100 =10k
kacholi 100@100=10k
Mauzo Jumla 20k kwa siku
20×siku 6 = 120k
120k-22k=98k

Haha kama hauna Deli na Kalai (au ukaazima )bado kuna uwekan0 ukatengeneza pesa ya kutosha said ya 50 kwa wiki .
Hili ni wazo ninalo liishi
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwanangu ulivyoeleza naona kabisa kwa sasa kichwa changu kimepanuka kias flan, bimaana kwa mazingira ambayo nipo mm ni location ya watu kabisaaaa pamechngamka lakini hivyo vitu hakuna, ngoja nijikongoje na mm nikafanye yangu, shukraan sana mtoa mada mana vitu kama hivi tusingevipata, mkono wa shukran pia kwako...zero IQ...
Mkuu kwa sasa nafikiria kupata fedha kiasi kadhaa niboreshe hilo wazo,

Kwanza nataka niuze mishikaki vizuri siyo local tena kama mwanzo,
Nataka nitafute sehemu nzuri niweke meza flani hivi nilishadizine,
Then kwa juu naweka katent flani hivi na bango kubwaa,

Hapo itakuwa ni mishikaki ya Nundu plus Nyama ,
Then pembeni kutakuwa na ndizi za kuchoma pamoja na kukaanga ,chachandu flani hivi ya kuvutia,

Mavazi ,nitakuwa na mavazi flani special Tshirt ya kuprint yenye logal mbele na maandishi Nyuma,chini laba flani hivi na jinsi Nyeusi ya kuchomekea(lengo kuwa Nadhifu muda wote wa kazi)

Nje ya meza kutakuwa na Viti vya kudizine vitakavyowezesha kukaa watu nane tu (kila upande watu wanne,)

Yaani nataka niifanye kiaina flani hivi ambayo ata wewe mwenye Suti yako usione Aibu kushuka kwenye gari yako kuja kununua mishikaki ,

hapo kwa haraka haraka mchanganuo wangu mpaka sasa ulikuwa hivi.

Hiyo meza niliyodizine nilishaongea na fundi inacost kama 300k (ni ya chuma alafu itakuwa na umbo kama L )

Carpet yake ya kutandika meza (vile ninavyotaka mimi)35.

Majiko mawili 80k (kubwa 45k, dogo la karahi 35k)

Karahi 1. 9k

Meza na viti vile navyotaka kudizine vitanicost 150k,

Chuma nne za kusimama 120k (kila moja 30k)
Za juu 40k ,turubahi la kuweka 30k (hapo tent ) fundi sijajua bado

So hapo kwa haraka haraka 800k - 900k inatosha Biashara itakuwa kama vile ninavyotaka mimi,

Nilishaweka kiasi kadhaa na bado nazidi kuweka Akiba, wazo langu halina haraka sana nategemea kuanza ikifika mwezi wa Sita hivi ,

Eneo ninalotegemea kuweka ni mapito ya watu wa aina tofauti

Biashara yenyewe.
Nitakapoanza biashara nategemea kuanza kwa bei ya kawaida tu ,
Kila mshikaki utauzwa shilingi 500,
Ndizi ya kuchoma shilingi 500,
Na ndizi ya kukaanga shilingi 400,

Pembeni ya jiko kutakuwa na mishikaki pia midogo ya shilingi mia 2, mia 2 kwa ajiri ya wanafunzi na watoto.

Ongezeko la bidhaa itaongezeka kulingana na ongezeko la wateja watakaokuwa wanakuja mfano.

Naweza kuweka mihogo,maziwa fresh kwa Jioni, maini na firigisi za kuku Nk.

ila tu sitaweka chipsi nataka nidili na hivyo Vitu tu na nitasimamia mwenyewe.

Nb.
Kwenye banda langu la kiepe kama kawa watu wapo wa kufanya kazi mimi binafsi nataka nigeukie huko kwanza

Cc Zero IQ

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa kufikiria njia njema ya kupata wazo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kuna watu wana moyo wa kusaidia tu na si vinginevyo,huwezi amini mie pia nadhani mbele ya safari nitatoa kwa washindi.

Wengine tuna vimitaji vya hapa na pale lakini tumetingwa kiasi kwamba ni ngumu kufanyia kazi kila idea.

Unaweza iona Tsh 50,000/= ni pesa ndogo sana lakini kuna mtu anaisaka hiyo afanyie biashara haioni.
 
Mkuu wapi hapo huzo ndiz zinauzwa bei hiyo naomba kujua
Kuna sehemu wale wakaanga ndizi kwenye mabanda ya chips huwa wanapata tabu kuzipata zile ndizi ndefu kubwa(mzuzu),,, sasa Kuna mahala zile zinapatikana kwa wingi, na huko zinanunuliwa sh 50 kila moja mara usafiri na vingine zinafika sokoni kwa sh 80 mpaka 90 kwa kila moja, na huwa zinachukuliwa kwa bei ya jumla 200 mpaka 250 kila moja.... Kwahiyo mtu hapo anaweza kutengeneza hiyo elfu 50 sio mwezi Bali tuchukulie wiki mbili tu maximum

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wapi hapo huzo ndiz zinauzwa bei hiyo naomba kujua

Yaani wewe kama unaweza kwenda Mbingu Ifakara nenda ukajionee maajabu ya bei za mzuzu!..sema barabara mbovu..sijui km wametengeneza sasa hv...!kule ni mbingu kwel
 
Mkuu kuna watu wana moyo wa kusaidia tu na si vinginevyo,huwezi amini mie pia nadhani mbele ya safari nitatoa kwa washindi.

Wengine tuna vimitaji vya hapa na pale lakini tumetingwa kiasi kwamba ni ngumu kufanyia kazi kila idea.

Unaweza iona Tsh 50,000/= ni pesa ndogo sana lakini kuna mtu anaisaka hiyo afanyie biashara haioni.
Safi sana mkuu..ila msibague..na sisi tuweke mawazo yetu tushinde!
 
Weka tu mkuu..

Mimi nimekua nikijaribu sana biashara lakini usimamizi unanifelisha kutokana na nature ya kazi yangu nabanwa sana na sipo tayari kuacha kazi kwa sasa.

Natumai siku nikisaidia watu wawili watatu kwa plan ya mleta mada na wakafanikiwa kusimama wenyewe nafsi yangu itasuuzika kupita maelezo.
 
Be blessed mkuu!huo ni utu kutoka moyoni mwako utabarikiwa sana sana!
 
Mimi si tajiri ila nataka kuwafundisha utu na ubinadamu matajiri walioko JF.

Nataka kijana mwaminifu mmoja kutoka Jf nimwazime 50 na airejeshe baada ya mwezi mmoja au miwili ili nimwazime mwingine.

Changanua wazo lako na weka namba ya simu kama utapenda kuiweka hapa Kisha members wengine watanisaidia kumchagua mtu sahihi.

Please huu sio mkopo kwa wanaojiweza kwa sababu hauna riba na utakuwa umedhulumu haki ya mwingine.

Masharti na vigezo vitazingatiwa. Mshindi atatakiwa kusubmit some of his/ her details PM.

Pesa nitamtumia au kumkabidhi Ijumaa 21/ Febuari/2020.

Shindano litadumu kwa siku 3 tu.

UPDATES
23:15 Jumatano, nimefunga shindano
Nashukuru kwa mliojitokeza kuwania hichi kiasi kidogo cha 50.
Niko busy kidogo na majukumu na washiriki ni wengi.
Ninaomba Jumamosi weekend ndio nipitie post to post ili kuleta haki.
Mshindi atatangazwa na nitampa pesa mkononi kama yuko Dar na kama yuko mkoani nitamtumia na ya kutolea.
Kila mwezi nitafanya kitu hichi na atakayetengeneza faida kubwa zaidi nitampa Pesa nyingi zaidi.

UPDATES
JUMAMOSI SAA 2:50 ASUBUHI
Nimeanza kufanya sorting, niko page number 3. Leo hii hii mshindi atatangawa.

UPDATES
09:15 AM
Nimemaliza uchambuzi wa awali na kupata post 22 zenye nguvu zaidi.
Nakunywa chai kisha nimalizie kusort na kupata vijana 3 nitakaowaleta mbele yenu, asanteni.

Updates
09:48 am
Saturday
Nimepata watu hawa, na uchambuzi unaendelea miongoni mwao.
Kama kuna mtu hajatendewa haki anaruhusiwa kuleta malalamiko within one hour.
Walioingia kwenye kinyang'anyiro ni;
1.Zero IQ post no.29
2.Zwenge Ndaba post no.
3.Noelia, post no.170
4.CONTROLA post no.175
5.Davie post no.236
6.Naipenda Familia yangu, post.#57
7.Peramiho Yetu post #30
8.FK21 post #147.

Updates
1930 hrs
Ninaomba radhi kwa kuchelewesha matokeo ya mwisho.
Sikuwa hewani kwasababu zilizo nje ya uwezo.
But nikitulia nitamaliza kazi leo hii hii na mhusika atapewa chake kwa kadri tutakavyokubaliana njia ya kumfikishia Pesa yake.

Updates
23: 50
Nawashukuru washiriki wote wa shindano hili dogo.
Ninatamani kila mshiriki nimpe pesa nyingi kwaajili ya wazo lake ila kamba yangu ni fupi.
Nawashukuru pia wasomaji na wachangiaji wa Uzi huu.
Washindi ni hawa wafuatao;
3: Zwenge Ndaba, katika post yake #208 inayoelezea biashara ya maziwa kutoka Chalinze kwenda Kibaha au Dar es salaam.
2.Peramiho Yetu, katika post yake #30 anaelezea biashara ya Mahindi mabichi ya kuchoma kutoka Stereo Temeke .
1:Napenda Familia Yangu, katika post yake #57 ameelezea biashara ya maandazi na half cake .
Mimi kwasasa nitaanza na kutoa zawadi kwa mshindi nambari 1.
Kwa atakayekuniunga mkono anaweza kuungana nami kuwapa mtaji washindi nambari 2 & 3 au kumwongezea mtaji mshindi nambari moja.

Note:
Nitaendeleza hili jambo kila baada ya mwezi mmoja na ninawashauri watakaokosa wajaribu tena.
Mshindi anione pm
Kwa utaratibu huu huu wako nakuunga mkono kwa huyo mshindi no. 2 Peramiho kwa hiyo post yake #30 ani PM apate mtaji wake ikiwezekana aweke na namba yake ya simu. pia awe tayari kurudisha mrejesho wa kupokea huo mtaji na baadae maendeleo yake ya biashara husika...
 
oya Peramiho yetu amka huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa utaratibu huu huu wako nakuunga mkono kwa huyo mshindi no. 2 Peramiho kwa hiyo post yake #30 ani PM apate mtaji wake ikiwezekana aweke na namba yake ya simu. pia awe tayari kurudisha mrejesho wa kupokea huo mtaji na baadae maendeleo yake ya biashara husika...
Safi sana mkuu.
Ujumbe umempata bila shaka
 
Mkuu kwa sasa nafikiria kupata fedha kiasi kadhaa niboreshe hilo wazo,

Kwanza nataka niuze mishikaki vizuri siyo local tena kama mwanzo,
Nataka nitafute sehemu nzuri niweke meza flani hivi nilishadizine,
Then kwa juu naweka katent flani hivi na bango kubwaa,

Hapo itakuwa ni mishikaki ya Nundu plus Nyama ,
Then pembeni kutakuwa na ndizi za kuchoma pamoja na kukaanga ,chachandu flani hivi ya kuvutia,

Mavazi ,nitakuwa na mavazi flani special Tshirt ya kuprint yenye logal mbele na maandishi Nyuma,chini laba flani hivi na jinsi Nyeusi ya kuchomekea(lengo kuwa Nadhifu muda wote wa kazi)

Nje ya meza kutakuwa na Viti vya kudizine vitakavyowezesha kukaa watu nane tu (kila upande watu wanne,)

Yaani nataka niifanye kiaina flani hivi ambayo ata wewe mwenye Suti yako usione Aibu kushuka kwenye gari yako kuja kununua mishikaki ,

hapo kwa haraka haraka mchanganuo wangu mpaka sasa ulikuwa hivi.

Hiyo meza niliyodizine nilishaongea na fundi inacost kama 300k (ni ya chuma alafu itakuwa na umbo kama L )

Carpet yake ya kutandika meza (vile ninavyotaka mimi)35.

Majiko mawili 80k (kubwa 45k, dogo la karahi 35k)

Karahi 1. 9k

Meza na viti vile navyotaka kudizine vitanicost 150k,

Chuma nne za kusimama 120k (kila moja 30k)
Za juu 40k ,turubahi la kuweka 30k (hapo tent ) fundi sijajua bado

So hapo kwa haraka haraka 800k - 900k inatosha Biashara itakuwa kama vile ninavyotaka mimi,

Nilishaweka kiasi kadhaa na bado nazidi kuweka Akiba, wazo langu halina haraka sana nategemea kuanza ikifika mwezi wa Sita hivi ,

Eneo ninalotegemea kuweka ni mapito ya watu wa aina tofauti

Biashara yenyewe.
Nitakapoanza biashara nategemea kuanza kwa bei ya kawaida tu ,
Kila mshikaki utauzwa shilingi 500,
Ndizi ya kuchoma shilingi 500,
Na ndizi ya kukaanga shilingi 400,

Pembeni ya jiko kutakuwa na mishikaki pia midogo ya shilingi mia 2, mia 2 kwa ajiri ya wanafunzi na watoto.

Ongezeko la bidhaa itaongezeka kulingana na ongezeko la wateja watakaokuwa wanakuja mfano.

Naweza kuweka mihogo,maziwa fresh kwa Jioni, maini na firigisi za kuku Nk.

ila tu sitaweka chipsi nataka nidili na hivyo Vitu tu na nitasimamia mwenyewe.

Nb.
Kwenye banda langu la kiepe kama kawa watu wapo wa kufanya kazi mimi binafsi nataka nigeukie huko kwanza

Cc Zero IQ

Sent using Jamii Forums mobile app

Njo Pm mkuu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Naomba na mimi lisinipite hili . .
Mimi idea yangu kuuza sambusa na kacholi mashuleni (msingi na secondari ) na mtaani.
Gharama .
kalai lipo tayari
Deli lipo tayari
Viazi 2@5k
Ngano 2@1300
mafuta 2@2000
Nyanya kwa siku , pilipili, chumvi rangi ya kacholi (2000) =2000+ 5000= 7k
Jumla ni 24k
Sales
sambusa 100@100 =10k
kacholi 100@100=10k
Mauzo Jumla 20k kwa siku
20×siku 6 = 120k
120k-22k=98k

Haha kama hauna Deli na Kalai (au ukaazima )bado kuna uwekan0 ukatengeneza pesa ya kutosha said ya 50 kwa wiki .
Hili ni wazo ninalo liishi
Asante
Unapikia kwa kutumia nishati gani hivi vitu?

Mvua ikinyesha au jua Kali unakaa wapi kufanya biashara yako?

Rudia tena mchanganuo wa hesabu zako Mr Finest
 
Kwa utaratibu huu huu wako nakuunga mkono kwa huyo mshindi no. 2 Peramiho kwa hiyo post yake #30 ani PM apate mtaji wake ikiwezekana aweke na namba yake ya simu. pia awe tayari kurudisha mrejesho wa kupokea huo mtaji na baadae maendeleo yake ya biashara husika...
Nimekupm Mkuu sorry nimechelewa nilikuwa nauguza Mdogo wangu hvyo sikuwa na muda Wa kuingia jf

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom