Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Mwanangu umetisha sana ..hii idea ngoja nipite nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MREJESHO

Habari wakuu
Hope mko salama na tuendelee kuchukua tahadhari za ugonjwabwa corona

Niende kwenye mada kama mjuavyo mm n mnufaika namba mbili Wa hili shindano naendelea kuleta mrejesho Wa Yale tuliyokubaliana au niliyoahidi

Kifupi biashara inaenda vizuri kiasi pamoja na changamoto za hapa na pale hasa hili janga LA corona niliwah kueleza juu ya kuuguza kwa ndugu Yangu hapo awali lakn nashukuru amepona wiki iliyopta karuhusiwa hivyo muda mwingi niliutumia huko hvyo jion ndyo nilikuwa nafanya biashara sifichi kiasi nilikuwa napata faida kidogo ndyo iliyonisaidia kupata nauli na mambo madogo japo mtaji ulibaki palepale

Pia nilifanikiwa kununua kuku watano Wa kienyeji nilinunua wakiwa wadogo lakni sasa niwakubwa kias bado nahtaji kuwaongeza zaidi kwani nimeona upande huu ndio unamatumaini mazuri zaidi

Nimehama sehemu niliyokuwa nakaa kwa sasa nimepata hisani kidogo ya kaka Yangu amabaye yupo masomoni nje hvyo kaniachia .nyumba yake na inaeneo kubwa hvyo nitafanya ufugaji Mkubwa zaidi kwa kadiri iwezekanavyo nitaambatanisha na picha za kuku ninaoanza kuwafuga kwa sasa

Nikiri janga LA corona limeanza kidogo kuniyumbisha s kama mwanzo lakn nitakomaa hadi kieleweke

Cc@siliconvalley@bondelabaraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Kila la heri mzee baba
 
Mkuu anzisha hii kitu tena watu waeleze namna ya kuitumia 500000 katika biashara
 
Hongera sana Mkuu tunahtaji watu kama nyie ambao mnaonesha kweli una nia na unachokifanya uthubutu Wa kuja hapa kutueleza juu ya utekelezaji wako

Mimi nakuahid kukupush katiaka project yako ya kuku kwakukupa kuku watano makoo (jike) wadogo kama hao baada ya wiki mbili zijazo kwan nilionao bado wadogo kidogo

Kwa vile unapatikana hapa dar bas nicheki pm Mkuu

Hongera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante Mkuu nshakupm
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…