Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Nakumbuka kuna kipindi Marehemu Mzee Mengi alikuwa anashindanisha mawazo ya kibiashara na kutoa 1M kila mwezi nadhani
Naunga mkono hoja MaBillionaire ni watu wa hovyo kabisa.

How come, MO ana utajiri wa Trillion 4 roundly hivi akitenga only 1B tu sawa na million 1000/= akawawezesha vijana kwa vigezo purposefully 1M kila mmoja sawa na vijana 1000 Tz kwa 1B moja tu ambayo haitekenyi hata itajiri wake Hell.

Hell.

Portfolio | 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inakujaaa inakataaa,inakujaaa inakataaa..

On a serious note mm imekataa kuclick...! Kuna mama hapa anapika hizo mambo kila siku mfuko mzima anatoa hizo idad za maandaz na half cake .anatumia sukari 3kgs..aliomba nimpgie faida nikapga kwa uaminifu mkubwa ikaonekana anapata faida ya 8000!..hajalipa mkandaji..dishi moja analipa 2000!anakanda dishi 4daily!mafuta anatmia lita 5!ingawa yanabaki kiasi!all in all apambane tu kiume
 
Uko mkoa gani
Nina Hotel ambayo inatoa huduma ya Chakula Ila hakuna Vinywaji asilia na Bahati nzuri jirani yangu ambae pia Ni rafiki yangu ana deep freezer. Niazime hiyo Elfu hamsini Ninunue Blender ya sh.45,000 Matunda ya 3000 na Sukari Nusu pamoja na Viungo vingine nitengeneze Juice hapa niuze Glass Moja 500, ambapo kwa Matunda hayo ninauwezo wa kupata Vikombe 20 kwa wastani jumla inakua 10,000, nikiwekeza faida 2500 kila siku huku 2500 ingine nakuza Mtaji nitakua na uwezo wa kuirudisha hiyo Pesa in two weeks. Kwa sababu za kiusalama Namba sitaweza kuweka Ila Kama utapendezwa PM yangu ipo wazi.. Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe
Asante mkuu,ila mshindi sio Mimi,Mimi nimeingia kwenye tatu bora tu.maziwa nimeshafanya research,unauza kwa order,unavyotoa unapeleka moja kwa moja kwa wateja kwa order.order ni nyingine Sana ,maziwa ni deal mjini.hayawezi kubaki.usichanganye na maji tu ,utajiharibia soko.pia in case yakibaki unazalisha ya mgando.nayo Ni bei kuliko fresh.mtaji ukiwa mkubwa unafungua kifrem kabisa.na unanunua vifaa Kama Yale matank ili maziwa yasigande
Kuna jamaa YANGU anawazo kama lako la maziwa au ndiyo wewe....maelezo yako na YAKE yanafanana kwa kiasi kikubwa....au ni wewe unaisha kibaha picha ya....?
 
MREJESHO
Wakuu habari ya leo,
Tumshukuru mungu kwa wale tulio na afya njema, na kwa wale wenzetu wenye shida mbalimbali basi mungu awafanyie wepesi.

Kama nilivyoanza na kichwa cha habari hapo juu nimeleta mrejesho wangu wa kinyang'anyiro hiki kilichokuwa kinaendelea kwa siku kadhaa hapa jukwaani, na wengi wetu kutoa mawazo yetu mbalimbali.

Mleta mada jana usiku wa saa sita aliahidi kumleta mshindi wa hili shindano,ambalo miongoni mwa orodha ile nami nilikuwepo na kuibuka na ushindi mnamo saa sita na dakika mbili usiku.

Akanifuata pm tukawasiliana usiku ule na akaahidi leo akishatoka ibadani, basi atakamilisha lile dhumuni lake. Na ilipofika saa 11:42am alinitumia hiyo pesa ikiwa kamili na ya kutolea.

Shukrani zangu za dhati ni kwa mwenyezi mungu kwanza,halafu wale wote tulioshiriki kutoa mawazo yetu hapa, sababu yatanufaisha watu wengi.

Bwana Bonde la Baraka mungu akuzidishie baraka zaidi kama unavyojiita, kwani umekuwa faraja kubwa sana kwetu,na naomba na wengine wenye uwezo mjitokeze zaidi ili kuweza kusogeza gurudumu hili la maendeleo hasa kwetu vijana.
Mungu awabariki sana.

NB:Si mwandishi mzuri kwa hiyo tuvumiliane kwa hili.
View attachment 1367006

Sent using Jamii Forums mobile app
Nje ya mada
MLeta shindano ni ke au me?
 
Back
Top Bottom