Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Mbona vijana wengi wa kitanzania mna mawazo mazuri sana ya biashara pita pita kwenye post nimegundua mawazo hayo ni kutoboa kabisa, shida ni mnakosa mitaji, muwe mnakopa basi bank, na bank zipo kwaajili yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi si tajiri ila nataka kuwafundisha utu na ubinadamu matajiri walioko JF.

Nataka kijana mwaminifu mmoja kutoka Jf nimwazime 50 na airejeshe baada ya mwezi mmoja au miwili ili nimwazime mwingine.

Changanua wazo lako na weka namba ya simu kama utapenda kuiweka hapa Kisha members wengine watanisaidia kumchagua mtu sahihi.

Please huu sio mkopo kwa wanaojiweza kwa sababu hauna riba na utakuwa umedhulumu haki ya mwingine.

Masharti na vigezo vitazingatiwa. Mshindi atatakiwa kusubmit some of his/ her details PM.

Pesa nitamtumia au kumkabidhi Ijumaa 21/ Febuari/2020.

Shindano litadumu kwa siku 3 tu.

UPDATES
23:15 Jumatano, nimefunga shindano
Nashukuru kwa mliojitokeza kuwania hichi kiasi kidogo cha 50.
Niko busy kidogo na majukumu na washiriki ni wengi.
Ninaomba Jumamosi weekend ndio nipitie post to post ili kuleta haki.
Mshindi atatangazwa na nitampa pesa mkononi kama yuko Dar na kama yuko mkoani nitamtumia na ya kutolea.
Kila mwezi nitafanya kitu hichi na atakayetengeneza faida kubwa zaidi nitampa Pesa nyingi zaidi.

UPDATES
JUMAMOSI SAA 2:50 ASUBUHI
Nimeanza kufanya sorting, niko page number 3. Leo hii hii mshindi atatangawa.

UPDATES
09:15 AM
Nimemaliza uchambuzi wa awali na kupata post 22 zenye nguvu zaidi.
Nakunywa chai kisha nimalizie kusort na kupata vijana 3 nitakaowaleta mbele yenu, asanteni.

Updates
09:48 am
Saturday
Nimepata watu hawa, na uchambuzi unaendelea miongoni mwao.
Kama kuna mtu hajatendewa haki anaruhusiwa kuleta malalamiko within one hour.
Walioingia kwenye kinyang'anyiro ni;
1.Zero IQ post no.29
2.Zwenge Ndaba post no.
3.Noelia, post no.170
4.CONTROLA post no.175
5.Davie post no.236
6.Naipenda Familia yangu, post.#57
7.Peramiho Yetu post #30
8.FK21 post #147.

Updates
1930 hrs
Ninaomba radhi kwa kuchelewesha matokeo ya mwisho.
Sikuwa hewani kwasababu zilizo nje ya uwezo.
But nikitulia nitamaliza kazi leo hii hii na mhusika atapewa chake kwa kadri tutakavyokubaliana njia ya kumfikishia Pesa yake.

Updates
23: 50
Nawashukuru washiriki wote wa shindano hili dogo.
Ninatamani kila mshiriki nimpe pesa nyingi kwaajili ya wazo lake ila kamba yangu ni fupi.
Nawashukuru pia wasomaji na wachangiaji wa Uzi huu.
Washindi ni hawa wafuatao;
3: Zwenge Ndaba, katika post yake #208 inayoelezea biashara ya maziwa kutoka Chalinze kwenda Kibaha au Dar es salaam.
2.Peramiho Yetu, katika post yake #30 anaelezea biashara ya Mahindi mabichi ya kuchoma kutoka Stereo Temeke .
1:Napenda Familia Yangu, katika post yake #57 ameelezea biashara ya maandazi na half cake .
Mimi kwasasa nitaanza na kutoa zawadi kwa mshindi nambari 1.
Kwa atakayekuniunga mkono anaweza kuungana nami kuwapa mtaji washindi nambari 2 & 3 au kumwongezea mtaji mshindi nambari moja.

Note:
Nitaendeleza hili jambo kila baada ya mwezi mmoja na ninawashauri watakaokosa wajaribu tena.
Mshindi anione pm
Kwa akl zang ndogo za std7.... Nmegundua unatka bzness idea za watu.... Na huu uzi umeuleta as shortcut to achieve ur goals [emoji3578][emoji3578][emoji3578]
 
Shukran mkuu

Kwa wasiojua huyu ndye aliyenifinance huu mtaji


Niende kwenye mada nikweli mkuu miradi inahitaji usimamizi mkubwa naanza na hyo miradi

MRADI WA MAHINDI CHOMA

Hapo juu nimeeleza jinsi huu mrad ulivyonipa mtaji wa kufungua miradi miwili ambayo n ufugaj wa kuku 20 ambao wameongezeka had kufikia 118 kwa maana ya 20 kuku nilionunua na 98 vifaranga ambao wametotolewa mradi wa pili ndio huu ambao nipo nao huku KIkoshiradi wa Viatu vya watoto na wa dada

Mradi huu wa mahind nimempa mdogo wangu ili naye aweze kuendesha maisha n MTU wangu wa karbu amenisaidia kwa mengi bahat mbaya naye mambo hayakumuendea vizuri hvyo kwakuwa mm nimeanza biashara nyingne nimeona bora naye apate kwakujshkiza HVYO HUU MRADI SIUMILIKI

MRADI WA KUKU.

Hapa ndipo roho Yangu ilipo wakuu ndio maana nikamtafuta na mtaalam kabisa wa fani husika ili anisaidie mawazo ya kitaalam Usimamizi wa mrad huu kwa sasa si mgumu sana kwa vile bado sjaanza kufanya biashara nna utaratbu wa kijua idadi ya kuku. Wangu kupitia daftar maalum ambacho nimeliandaa na kama mjuavyo kuku wanahesabika sio kama sukar au chumvi n rahs kijua kama kuku wamepungua hapo nitakapoanza kuvuna nitakuwa making zaidi kwan biashara ya viatu n ya msimu tu

BIASHARA YA VIATU

Hii n ya msimu tu kwan had kufika septemba mwishon itakuwa imejifunga kabisa nam nitarud nyumban kupambana na biashara ya kuku lakn pia kama fursa nyingne itajitokeza sitasita kuingia huko ilimrad mtaji wangu isikae mda mrefu bila kujizungusha maana njaa ya mafanikio kwangu n kubwa sana

Nikutoe hofu juu ya usimamizi

CHANGAMOTO

Dah wakuu changamoto n nyingi baadhi n kutapeliwa na member wa humu jf wakati nachoma mahind tandka alinieleza ana mzigo wa mahindi hvyo huko uzaramuni kisarawe nimtumie nauli tu ya kusafirishia mzigo kama tsh 10000/= mwamba akapotea mazima

Wakopaji hawakosekan hao nao wakishakopa Mara mbil tatu na njia wanabadilisha tena unakuta unamdai tsh 800 tu

Kuchukuliana poa kuna nadharia kuwa ss wachuuzi yaan wafanya biashara ndondogo n watu tusioenda shule tumefel maisha hasa mabint so inahtaji uchukulie kawaida na upambane ukiwa blaza meni biashara utaiona ngumu hapa mm nakutana na wenzangu ambao nimemaliza nao chuo lakn nakaza roho tu nikiamin IPO simu

Biashara kukosa Wateja hii n kawaida siku nyingne unaweza ukarud na nusu ya mzigo kwakukosa Wateja hiyo n kawaida na mwenzako jiran akamaliza mzigo wote ukiwa na roho nyepesi waweza tafuta mganga ili umroge mwenzio

Mwisho ushawishi wa imani za kishirikina mfano kuna siku nilikuta hirizi inapumua kijiwen kwangu pamoja na naz iliyovunjwa ikiwa na maandishi ya kiarabu lakn nilichukulia kawaida

MWISHO

Mkuu silicon valley nikupe pongez sana kwakuniinua na Mungu akupe moyo huo huo wa kusaidia wengine
Kamanda mwenyezi Mungu akusaidie wewe ni maana halisi ya mpambanaji hasa mwenye kiu na uchu wa maendeleo . #Alutacontinue!!

Pole pia kwa changamoto maana hizo haziepukiki
 
Back
Top Bottom