Hiyo 50k mafanyia biashara ya matunda naenda hapo kilombero nanunua vitu vifuatavyo;
TIKITI kubwa-6000
Maembe-1500
Ndizi mbivu-1000
Matango-500
Apple 2@1000-2000
STRAWBERRY pkt 1-2000
Mananasi 3@1000-3000
Umma pkt 1- 1500
Percels(kontena zile)@300×20=6000
Tuishi 1-1000
Nauli -1000
JUMLA = 25,500
So kwenye hiyo 50k nitabakiwa na 24,500 kama akiba yangu.
Hapo tayari nina visu, karai kubwa, vitambaa kwa ajili ya kufuta kontena, meza kubwa ..
Naosha matunda vizuri kwa maji ya moto, napaki kwenye kontena kwa bei tofauti.
Kontena kumi naweka Apple, STRAWBERRY na matunda mengine, bei yake ni tsh 2000.
Kontena kumi naweka matunda yote kasoro apple na STRAWBERRY, bei yake ni tsh 1500.
Hivyo kwenye kontena kumi za 2000 nitapata tsh 20000 kama 'mauzo'
Kwenye kontena kumi za 1500 nitapata 15000 kama 'mauzo'
JUMLA itakuwa 35000 nikitoa 25,500 ya manunuzi nabakiwa na tsh 9500 kama faida khalisi ..nikifanya hii bizi kwa siku sita tu nazalisha tsh 50000 na kichele kama faida.
Hapo bado kuna 24,500 niliweka kama akiba[emoji3][emoji3]
NB: HII NDIO BIASHARA NINAYOFANYA SASA.
Asante.
[emoji1666][emoji1666]
Sent from my SM-A305F using
JamiiForums mobile app