Satfa
New Member
- Aug 14, 2021
- 1
- 2
Changamoto tunazokabiliana nazo mpaka kufikia ndoto zetu, Ni vitu vingi sana tunakumbana navyo katika hazarakati/safari zetu za Maisha mpaka kufikia ndoto tulizokuwa tunaishi nazo kwenye fikra zetu(akilini) na kutamani kuona zimefikia hatima zikiwa na mafanikio tele hususani katika nyanja za kiuchumi /kipato imekuwa ni mtambuka.
Watu kujua ni ipi njia sahihi ya kutoboa kimaisha au kufikia ndoto aliyekuwa nayo kichwani kwa mda mrefu imekuwa shughuli, Lakini siku zote uthubutu ndio NGAO ya USHINDI ya Maisha yetu, wengi wanaogopa kuthubutu kitu kwasababu ya kuwa na fikra/dhana potofu alizojijengea kwenye mfumo wa akili yake.
Je, ni vitu gani hivyo?
Watu wengi wanapotaka kujaribu kitu huwaza mambo mengi sana ikiwemo; je' nikifanya labda watu watanionaje/fikra za watu wengine, kuwa na dhana ya kushindwa/siwezi akilini mwake, kukatishwa tamaa na wengine/fikra potofu za watu na fikra binafsi Kama labda inaweza kugharimu muda mwingi Bila mafanikio na hata pia kuogopa hasara baada ya uthubutu.
Amini usiamini "penye nia pana njia", hivyo siku zote unapotaka kufanya kitu chanya au Cha kimaendeleo binafsi usipende sana kushirikisha watu wengine/wengi kwani hakuna binadamu anayependa maendeleo/mafanikio ya mwenzie ila ni wachache sana. Na ukitaka kushirikisha basi angalia watu wanaofaa kuomba/kuombwa ushauri na rika zao.
Je, ni akina nani hawo, Kuna wazee wenye busara, vijana wenye fikra chanya(wapambanaji), na hata watoto pia wenye fikra za kimaisha.
Baada ya kupata mawazo/fikra kutoka kwa wadau mbalimbali kaa chini kwanza uoanishe mawazo ya watu na yako kwani siku zote "akili za kuambiwa changanya na zako" na ukishachambua ndipo uthubutu/jaribu ukiwa na imani la kufanikiwa na si vinginevyo.
Kwani watu wengi wanaweza kuthubutu jambo lakini hana imani na anachokifanya hukatisha/huachilia njiani lakini katika Maisha haiko hivyo, kukata tamaa mapema ni adui wa mafanikio ya badae.
Unaweza kuona mfano mzuri wa wafanyabiashara wakubwa au wawekezaji(entrepreneurs) huwekeza kiasi kikubwa cha pesa katika nyanja tofauti tofauti na wakiwa na imani la kufanikiwa na ndo maana siku zote wanakuwa ni watu wenye kuendelea na kuwa na maendeleo makubwa. Hivyo kwao hawagopi sana hasara na huamini zaidi kwenye mafanikio na mara zote huthubutu.
Pia kwa wanachama wote wa JAMIIFORUMS waliojaribu kuandika 'stories of change' naweza nikasema ni mfano mzuri wa uthubutu kwani wameandka wakiwa na imani la kufanikiwa na ishara nzuri ya upambanaji na uzalendo. Hivyo wameandika wakiwa na maana ya kuelimisha watu au JAMII zaidi na sio tu kuhusu kushinda/kuwa mshindi wa mashindano haya.
Hivyo basi nawaasa vijana wenzangu wawe na dhana ya kuthubutu kitu ambacho anajua kitakuwa na faida kwake na hata familia yake au JAMII kwa ujumla. Na wawe wazalendo wataifa letu na kuyaenzi maagizo ya maendeleo ya viongozi wetu pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo na mahala popote kwa imani la maendeleo na mafanikio tele kwani mkono mtupu haulambwi jaribu kuthubutu/kujaribu Kuna wazalendo wapenda maendeleo watakao kushika mkono na kukuinua zaidi na kuweza kuzifikia ndoto zako.

Upvote
1