Nakushukuru kwa fikra nzuri Zing!
1.Kilimo ndicho tumekuwa tukiambiwa ni uti wa mgongo wa Taifa hili tangu enzi! japo bado njaa inazidi kutishia amani! Wakati mwingine tunaagiza vyakula toka nje ya nchi kufidia upungufu! na mfumuko wa bei ya vyakula unatesa wananchi wengi! NACHANGANYIKIWA KAMA KWELI HUU NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA HILI.
2.Madini yetu yamekuwa yakichakachuliwa kwa mikataba mibovu yenye maslahi duni kwa wazawa wazalendo. Gawiwo la faida halikidhi hata upungufu wa Bajeti na bado tunaenda omba misaada kwa hao hao wanaochukua madini yetu!!!!!!!! NACHANGANYIKIWA KAMA KWELI HUU NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA HILI.
3.Utalii haujatangazwa vya kutosha kuwavutia watalii wa ndani na nje katika vivutio vyetu, Na Utalii huu umejikita ktk Mbuga za Wanyama tu na kusahau vivutio vingine kama makumbusho. Japo wanajitahidi kutangaza lakini bado NACHANGANYIKIWA KAMA KWELI HUU NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA HILI.
4.Viwanda bado ni vichache sana na vimejikita zaidi katika kuzalisha bidhaa za mlaji (Consumer goods) mfano biskuit, soda, majani ya chai nk, na kusahau sana Kuzalisha bidhaa za Mzalishaji (Producer goods) mfano Mashine za kusaga, injini mbalimbali nk. Hii inawafanya wajasiliamali wazalishaji kuagiza mitambo toka nje kwa gharama kubwa na kusababisha Unfavourable balance of Payment/ Trade. Yaani Tunalipa zaidi kwa Ku-import kuliko tunachopata ktk ku-export, bado NACHANGANYIKIWA KAMA KWELI HUU NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA HILI.
INATUBIDI KUFIKIRIA UPYA AU KUWEKA MSISITIZO NA BAYANA JUU YA NINI UTI WA MGONGO WA TAIFA HILI