UTI wa mgongo wa wamtesa Sabaya, kesi yake yaahirishwa tena

UTI wa mgongo wa wamtesa Sabaya, kesi yake yaahirishwa tena

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
753
Reaction score
1,812
Mahakama ya hakimu mkazi Arusha imeahirisha kwa mara nyingine shauri la uhujumu Uchumi linalomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai ole Sabaya na wenzake sita baada ya mshitakiwa Sabaya kuendelea kuwa mgonjwa.

Jana Novemba 3 mwaka huu mahakama hiyo iliahirisha shauri hilo baada ya kuarifiwa kuwa mshtakiwa namba moja (Sabaya)anaumwa na hakuweza kufika mahakamani na kupanga kesi hiyo kuendelea Leo (jana), ambapo shahidi wa saba wa jamhuri ambaye ni Ofisa wa Tehama wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Jofrey Nnko angeendelea kutoa ushahidi wake.

Akizungumza mahakamani hapo, Wakili wa utetezi Mosses Mahuna aliieleza mahakama kuwa mtuhumiwa huyo wa kwanza bado ni mgonjwa na kuwa ametoa ruhusa kesi hiyo iendelee kusikilizwa bila yeye kuwepo.

Naye wakili wa utetezi Faudhia Mustapha akihojiwa nje ya mahakama ameeleza kuwa jana jioni alienda kumjulia hali Mteja wao katika Gereza kuu Arusha Kisongo na Kuzungumza nae pamoja na daktari anaemtibu na kuelezwa kuwa anasumbuliwa na Ugonjwa wa vidonda vya tumbo alivyovipata akiwa Gerezani na anasumbuliwa na Uti wa mgongo tatizo alilolipata kabala ya kwenda gererezani.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho siku ya tarehe 4/11/2021 ambapo mahaka imetaka mawakili wa utetezi kuja barua ama ruhusa ya maandishi ya Lengai ole Sabaya kuwaruhusu waendelee na Kesi hiyo kusikilizwa bila uwepo wake.
 
Back
Top Bottom