Yani mimi najibu hoja zako halafu wewe kwa sababu zako binafsi tu unaamua kukataa majibu yangu, kwa kisingizio kwamba sijajibu au unataka nijibu vile unavyotaka wewe, hebu acha huu ujinga kama umeishiwa hoja sema usilazimishe kuandika pumba mradi tu usionekane umeshindwa na huna majibu
Bi Jadda Wewe sio Muadilifu Kabisa Wewe Umesema Wanawake Wengi Nimekwambia Wengi Inamaanisha Sio Wote. Umeshindwa kuleta Hoja unaruka ruka Plus Malalamiko.
Sasa ni kanuni gani inayoamua kwamba binadamu mwenye macho mazima ni bora zaidi ya kipofu, na ana mamlaka ya kumtawala kipofu kwa sababu tu ya hizo tofauti za kimaumbile, na hayo unayoyaita maandiko matukufu ni kwa mujibu wa nani
Wapi Mimi nimesema Kipofu atawaliwe na Anaeona Mbona Unachanganya Mambo.
Maandiko Matukufu kwa Mujibu wa Nani?? Mbona Swali lako halieleweki. Anyways Kwa Mujibu Wa Mungu.
Sasa ni nature ya aina gani inayoamua kwamba utawala utokane na maumbile ambayo mtawaliwa hana na hakupenda kutokuwa nayo na mbaya zaidi hafurahii huo utawala,
Hoja Umekosa Umebaki kujigonga gonga. Nature Ndo Imeamua Mwanamke Awe Dhaifu (kwa maana no external force) Sasa Unaponiuliza Ni Nature Gani!! Nashindwa Kuelewa unataka nikutajie Jina La Nature hiyo?? (Bi Jadda Umefirisika Hoja)
hebu acha porojo zenu hao wanyama tuna uwezo wa kuwatawala na kuwadhibiti ikiwa tu tunawafuga na kuwahudumia au wewe nenda kaingie kwenye msitu wa wanyama wakali na silaha zako (ambazo unahisi ndio zitakupa jeuri) halafu uone kama watakutii, kitakachokukuta ndio utajua kwamba hizo propaganda zenu hazifanyi kazi kwenye uhalisia au wewe ulimaanisha hawa wanyama kama paka, mbwa, sijui ng'ombe na mbuzi tu ambao nao lazima uwahudumie au nenda kajaribu kuvamia nyumba yenye mbwa wakali halafu uone kama hao mbwa watakupa utii
Umeongea mambo Kinyume kabisa na Uhalisia Yaani INASIKITISHA kusoma Hiki Ulichokiandika.. Leo Mimi Nikiwakuta Ng'ombe Barabarani hata kama Siwajui Ni wa Nani Ila Nikwafukuza Lazima Watiii. We Jadda unaonekana Unaongea Mambo Kutumia Nadharia pekee. Unasikitisha.
Manyanyaso ni nini na unayatafsiri vipi, sasa hivi ambao hawana furaha na amani kwenye ndoa ni wanaume kwa sababu hawataki kukubaliana na ukweli kwamba wanawake hawapendi kutawaliwa na ndio maana siku hizi malalamiko mengi kwenye ndoa yanatoka kwa wanaume kuliko wanawake,
Bi Jadda Unafurahisha kwa kweli Hivi hujui Wanaoteseka Mitaani ni Single Mothers na Wale wa Mikopo kausha Damu hujui kuwa Wanawake wanaojiuza na Kudanga wanazidi kuwa wengi Inaonekana wewe Huijui Jamii.
achilia mbali mimi tu hivi kuna mtu yeyote ambaye anafurahia kuitii serikali yake bila sababu au kuna mtu ambaye anafurahia kumtii boss wake bila sababu sijui hata kama unaelewa ulichouliza au ndio tayari umechanganyikiwa kwa kukosa hoja
Acha kupindisha Hoja Mimi nimesema Sio kila Anaetawaliwa Anakuwa Hana Furaha. Hatujazungumzia Suala la Kufaidika au kutofaidika.
Sasa kama hakuna aliyeamua mwanaume kuzaliwa madhubuti na mwanamke kuzaliwa dhaifu kwanini ninyi mjiamulie kwamba utawala utokane na hizo sifa za umadhubuti tu na si sifa nyinginezo,
Nilishakwambia Kila Kitu kina vigezo Vyake Na Haviingiliana Utawala Umejengwa katika misingi ya Nguvu na Umadhubuti na Uwezo. Hili ni Muhimu ili uwe unaweza Kumuwajibisha Unaemtawala itapo bidi.
mnawashawishije hao mnaotaka kuwatawala ili wakubali kutawaliwa mind you lazima kuwe na sababu ya kumshawishi huyo unayetaka kumtawala akubali kutawaliwa huwezi kumtawala hivi hivi tu bila sababu yoyote, hakuna utawala wa aina hiyo narudia hakuna mtu anayekubali kutawaliwa bila faida yoyote anayopata toka kwa huyo anayemtawala hili ndio nalisikia kwako na mbaya zaidi haujui kulitetea kwa hoja
Bi Jadda Unalazimisha Usielewe Na Unapinga Yale yale Tuliyoyatolea Maelezo mazuri kabisa. Nilishwakwambia Utawala wa mwanaume Kwa Mwanamke umekuja Automatically na Hakuna katika Historia kwamba Wanaume Wali install Utawala wao kimabavu au Kuna Wanawake Waligoma Utawala ulipoanzisha Na ndio maana Tunasema Nature. Haya ya Feminism yamekuja Miaka mingi sana Na Watu Wenye malengo mabaya na Ulimwenguni na Hata Sio Hao wanawake unadai Walistuka Sijui walikuwa na Akili.
Si ndio nilikuambia wazungu walithibitisha hilo kupitia maandiko ya kwenye biblia kuhusu watoto wa Nuhu ambao ni Shem, Ham, na Jafet, kama wewe ni wa dini nyingine basi inabidi tukubaliane kuacha kutumia references toka kwenye vitabu vya dini kwa sababu hatutaelewana, hapo nilikuwa nakuonesha jinsi mifumo ya hii dunia inavyofanya kazi kwa propaganda na si nature kwahiyo huo mfano nilioutoa wa ukoloni ni relevant kabisa hata ukibisha
Huo mfano sio Relevant kwa sababu Sisi Tunasema Nature kwa Sababu zenye Mashiko na Zinazokubalika kuwa ni kweli Zimetokana na Nature. Usinipeleke kwenye Mada isiyonihusu nilishwambia Hao wazungu ndio Wathibitishe Mimi sio Mzungu. Sasa unatakiwa ufungue mjadala na Wazungu Mjadili. Mimi hapa najadili Wanaume na wanawake.
Mimi nimekuuliza kuhusu feminism halafu wewe unaniletea habari za atheism na homosexuality hivi unaona kuna uhusiano kati ya swali langu na hilo jibu lako kweli, yani ni sawa mimi nikuambie unifafanulie kuhusu physics halafu wewe uniambie kwamba physics, chemistry na biology ni ndugu wa familia moja kwa sababu tu zote ni science, au ni sawa nikuambie unifafanulie kuhusu mahakama halafu wewe uniambie kwamba mahakama, bunge na utawala ni ndugu wa familia moja kwa sababu tu yote ni mihimili ya serikali hivi unaona kuna uhusiano hapo
Uelewa wako Mdogo Ulitakiwa Uniulize Kuna Uhusiano gani kati ya Vitu Hivyo na Jee kivipi Vinatafsiri Feminism. Ila Sababu unapenda tuu kibisha bila hoja unaleta Mifano Irrelevant.
Nimekujibu hivi bila kupepesa macho kama mke ndiye anayemhudumia mume basi mume hana budi kumtii huyo mke je sikukujibu hivyo wewe, kama unaona hilo haliwezekani waulize wale wanaume wanaoitwa mamarioo sijui vibenten wanaohudumiwa na wanawake kwamba kati yao ni nani anayemtawala mwenzake,
Unataka kutuambia kuwa Uongozi katika Familia ni dynamic leo Baba anaongoza kesho Mama Kama baba akishindwa kuhudumia. Nadharia zako ni za ajabu mno.
ndio maana mimi tangu mwanzo hoja yangu ni kwamba ili kuepuka hayo yote ni heri kila mmoja ajitawale mwenyewe na kujifanyia maamuzi juu ya maisha yake kusiwe na wa kumtawala mwenzie regardless of majukumu..
Kila mtu ajitawale mwenyewe kama Nyie Sio wanandoa(Sio Familia) Ila Mkishakuwa Familia Lazima Kuwe na Kiongozi. Lazima kuwe na wa kupanga Mambo na kusimamia Familia. Napata wasi wasi Kuhusu Uzoefu wako katika maisha ya Familia Ya Baba Mama na Watoto alafu eti kusiwe na Kiongozi yaani kila mtu anajiamulia mwenyewe aisee Ajabu.
haya nijibu swali langu je kama mke ni mama wa nyumbani na mume akakwama kiuchumi anafanyaje
Wewe Huna Uzoefu na Familia Nina Wasiwasi Na Umri wako Au Malezi yako. Yaani Unamaanisha Huzijui Familia Zilizoweza Kuishi Baada ya Baba kufukuzwa kazi au Kupata ajali au Kuumwa na Ilihali Mama ni Mama tuu wa Nyumbani Hujawai Kuziona Hujawai kuona Waliwezaje Ku survive?? Unataka nikufundishe Maisha ya Kijamii namna Jamii Zinavyosaidiana katika matatizo??
Ndio wazungu walishathibitisha sasa kwamba huo utawala ni nature na upo kibiblia, kwahiyo hata watu weusi hatukutakiwa kupinga ukoloni wala kudai uhuru tulitakuwa tuwaache wazungu waendelee kututawala kwa sababu kwa mujibu wao hiyo ni nature,
Mimi sio Mzungu Bi Jadda Huo Mijadala Mimi haunihusu Tafuta Wazungu. Mimi Ongelea Masuala ya wanawake na wanaume.
wewe mpaka sasa bado hujaelezea msingi wa hiyo nature zaidi ya kuniletea habari zilizo kwenye maandiko na tamaduni huku ukichanganya na hisia zako binafsi..yani kwa kifupi hadi sasa hakuna swali lolote ulilojibu zaidi ya kupuuzia hoja zangu na kutoka nje ya mada
Umefirisika maneno na Hoja Bi Jadda. Naendelea kukazia Mimi Nilisema Kigezo Ni Nguvu uwezo na Umadhubuti. Na Tunasema ni Nature kwa Sababu Hakuna Alieamua Mwanamke Awe Dhaifu na Mwanaume awe Strong it Just Happen that way na ndio maana ya Nature.
Sasa wewe Huamini Maandiko Ya Mungu Utaamini Maneno Yangu mimi. Kazi ipo yaani Mtu Yupo Tayari akane imani ili tuu Kudhibitisha Kuwa Yeye ni Sawa na Mwanaume kuna Fikra ni hatari Mno.
Ni mungu yupi sasa unayemzungumzia maana kuna miungu zaidi ya 1000 kulingana na dini zilizopo duniani kwa sasa, wewe unao ushahidi gani kwamba hayo maandiko yalishushwa kwa mitume kutoka kwa mungu na ni wapi huyo mungu mwenyewe alisema hivyo,
Ndio Maana Nilihusisha Feminism na Atheism Vyote ni Mipango ya Watu wenye Fikra za Kishetani. Na haya Maneno yako Yanathibitisha hilo.
Maandiko ni Maneno ya Mungu alafu unaniuliza ni wapi huyo Mungu kasema!!!. Ajabu.
feminism ni matokeo ya watu kuwa open minded na unprejudiced na kukataa kukubaliana na kila porojo wanazo mezeshwa na wanaume na mfumo dume
Feminism Ni mfumo wa Watu wenye Nia Mbaya Kwa Lugha Kali Tunasema Wenye Nia za kishetani. Feminism haikuanzishwa Purely na Wanawake Kuna Watu Walikuwa Nyuma Wanasuka Hayo Mambo na Ndio Hao Wanatoa Support. We unadhani eti wanawake tuu From no where Wangefika wapa walipofika??
Ushahidi wa hili
Wewe probably ni mvulana kwa sababu ungekuwa mwanaume ungekuwa unafikiria kama wanaume, mind you uvulana au uanaume siyo suala la umri bali akili, kitendo cha kupinga uhalisia ambao hata tamaduni zetu zinaufahamu kinadhihirisha hilo
Wewe ndio mwenye Fikra za Kisichana Hujawai kuyaishi maisha ya Familia Unafikiria Maisha yako Katika Mahusiano ni ndio hayo hayo katika Ndoa. So sad.
Hapana wewe ndio ulitakiwa ujue kwamba utii siyo suala la nature na hili nimeshalifafanua, na ndio maana mwanamke ukiwa unamhudumia ndio atakubali umtawale ila ukiwa humhudumii basi usitegemee utamtawala,
Unatuchanganyia Utii Wa wanawake na Wajibu wa mwanaume hivi ni vitu Viwili tofauti kila kimoja kinahukumiwa kwa Vigezo vyake.
yani huo ndio uhalisia utii hauji tu hivi hivi huletwa na jambo fulani na mara nyingi huyo anayetii anakuwa anapenda na si kulazimishwa
Utii hauji hivi hivi ndio Tunakubali Na ndio maana sisi tuliweka vigezo vya Utii kuwa Ni Uwezo Nguvu na Umadhubuti Sio kwamba utii unakuja From no where. Suala la Wajibu wa mwanaume kuitunza Familia yake Ni Jambo lengine kabisa na linahukumiwa Kivyake.
Ndoa za zamani zilikuwa na furaha
Nashukuru umekubali kuwa Ndoa za Zamani zilikuwa na Furaha. Sasa ndio Ujue Walioleta Feminism hawakuitaka hii Furaha iendelee na Wamefanikiwa Now ndoa hazina Furaha.
kwa sababu tu wanawake hawakuwa na sauti wala uhuru wa kujieleza na kusema mabaya yanayowakumba
Sio kweli Wanawake Walikuwa wanaweza kushitaki kwa Wazee kama kuna Jambo baya anatendewa. Mind you serikali za kijadi zilikuwa zinatatua migogoro katika familia. Usitutengenezee Jamii ambayo haikuwepo.
tofauti na sasa hivi ambapo wanawake wana elimu na uhuru wa kujieleza hivyo wakiyasema mabaya yenu mnawaona kama maadui na kuwaita feminists,
Nyinyi mmesoma ila badala muelimike Elimu yenu yote mnawekeza ku prove kuwa Mpo Sawa na Wanaume.
ni sawa na kuchukulia mfano wa nchi yenye utawala wa dikteta na kusema kwamba wananchi wa hiyo nchi wana furaha sana kwa sababu wanaitii na hawaipingi serikali yao ila kumbe kiuhalisia wameufyata tu kwa sababu hakuna demokrasia wala uhuru wa kujieleza maana wanajua wakifanya hivyo watashughulikiwa na vyombo vya dola,
Kwa hapa umethibitisha kuwa utii au Utawala Upo based on Nguvu na Uwezo. Ila Mimi Nilisema Sio kila Anaetawaliwa Anakuwa Hana Furaha. Siku sema Wote.
kama kweli unaona wanawake walikuwa na furaha kwa sababu tu ndoa zao zilikuwa zinadumu kwahiyo unataka kusema kwamba hata kukeketwa napo wanawake walikuwa wanapenda
Sasa Swala la Kukeketwa Linahusika Vipi hapa. Mbona unaongelea Mambo tofauti tofauti. (Umefirisika Hoja)
(bila shaka unajua mwanamke akikeketwa hakuna raha yoyote anayoipata kwenye tendo) walikuwa wanakeketwa ili tu wasichepuke wawalindie waume zao kwahiyo unataka kusema hili nalo wanawake walilifurahia na kama hawakufurahia kwanini hawakuresist tangu mwanzo kabisa
Mimi Sijasema Kwamba wanawake waliifurahia kila Jambo. Mimi Nimesema Sio Kila Anaetawaliwa Anakua hana furaha. (Usinipeleke kujadili tamaduni zisizo faa katika jamii hatupo katika Mada hii).
Kama kweli mwanamke anatakiwa kumtii mwanaume bila sababu yoyote ya msingi
Bi Jadda Upo wapi wewe!!! nani Kasema Mwanaume anatiiwa bila sababu ya Msingi?? Sisi tumeshataja Sababu kuwa ni Nguvu uwezo na Umadhubuti Sasa unaposema bila Sababu ya Msingi Mbona Unatusikitisha.
maana yake hata mwanaume anatakiwa kumpenda mwanamke bila sababu yoyote ya msingi,
Mbona unatuchanganyia Mambo Mbona hapa hatujadili Vigezo vya Kupendana Tunajadili Vigezo vya Utii. (Unatoka Katika Mada.)
kwa vile umerejea maandiko basi kumbuka imeandikwa mwanaume anatakiwa ampende mkewe na mwanamke anatakiwa amtii mumewe, kwahiyo nakuuliza ina maana hata kama mwanamke hataki kutimiza majukumu yake mfano kufanya za nyumbani au hataki kuzaa watoto muda mumewe anaotaka unataka kusema huyo mume anatakiwa aendelee kumpenda tu huyo mke regardless of what hebu nijibu hapo bila kujizungusha
Kwanza inanisikitisha WEWE ILISHAYAKATAA MAANDIKO ALAFU TENA UNAYAJENGEA HOJA. HAPA HATUJADILI KUHUSU MUME KUMPENDA MKEWE (FUNGUA UZI MWENGINE TUJADILI HILO KAMA UNATAKA) HAPA TUNAJADILI UTII NA UTAWALA BAKI HAPA. MIND YOU HAKUNA ALIESEMA MWANAUME ANATIIWA BILA KIGEZO CHOCHOTE TUMESHALIELEZEA HILI VYA KUTOSHA.
Ni nani anayeamua kwamba hivyo vigezo ndio viwe vigezo vya utawala mbona unakwepa kunijibu hapa kwani una shida gani,
MAJIBU TULISHAYATOA MBONA KWAMBA KILA KITU KINA KIGEZO CHAKE KAMA VILE ILI UWE MZURI LAZIMA UWE NA VIGEZO FULANI UKIWA NAVYO TUU AUTOMATICALLY UNAKUWA MZURI ILI UWE MPOLE UWE NA VIGEZO FULANI (NATUMIA MIFANO MEPESI MNO) SASA UTAWALA NAO UNA VIGEZO VYAKE NA TULISHAVITAJA NA VINAKUBALI SEHEMU ZOTE. ILA KIGEZO CHAKO CHA HUDUMA KINAKATAA NA SIO KIGEZO CHA UTIIFU.
je huyo unayemtawala naye akili yake automatically inamtuma kukubali kutawaliwa na wewe kiasi cha yeye kufurahia hilo na mambo kuflow smoothly au ndio hadi utumie nguvu kubwa,
Mimi nilikuuliza na hukujibu
UNA USHAHIDI WA KIHISTORIA KUWA WANAUME WAKI INSTALL UTAWALA WAO KIMABAVU??
mimi nataka uniambie vigezo hivyo ni kwa mujibu wa nani na mwanamke anapotawaliwa anapata faida gani kiasi cha kukubali kirahisi
Vigezo kwa mujibu wa nature tumelisema hili mara nyingi sana.
Mwanamke Kuna mengi anayapata ndani ya Ndoa na Ndio Mana Licha ya kudai kuwa Bibi zetu Walikuwa hawana furaha sijui walikuwa wananyanyaswa ila Mabinti walikuwa wanatamani na ilikuwa ni Fahari kwa Binti Kuolewa na Hata leo Wanawake wanatamani (wale ambao sio Manipulated kama wewe) waolewe.
Hapo umezunguka tu ila kiuhalisia sababu kubwa inayofanya mtu amtii boss wake ni kwa sababu tu analipwa mshahara na anaogopa asipotii kibarua kitaota nyasi,
Umerudi kule kule Ndo maana nilikwambia Kwenye kila Utii kuna aina furani ya Uoga. Unachekesha Bi Jadda.
hakuna mtu anayekubali kuajiriwa kwenye taasisi fulani halafu akafanye tu kazi na kufuata maelekezo ya maboss bure bure bila maslahi ya kiuchumi narudia hayupo labda wewe peke yako ndio unaweza hilo, na ndio maana taasisi nyingi pale watumishi wanapokosa mishahara yao huweza hata kuandamana na kuwagomea hao maboss wao unaodhani kwamba wanapewa utii kwa sababu tu ya nguvu au mamlaka walizonazo
Kulipa mshahara sio ndio uwezo tunaouzungumzia sisi au wewe unahisi tunaposema nguvu ni kwamba Ni Physical strength pekee??
Hiyo tafsiri ya two bulls ni yenu na ni subjective, inawezekana kabisa mkaishi bila kutawalana ndani ya nyumba wote mkaishi kwa kushirikiana na kusikilizana, utofauti kwenye maumbile siyo lazima uweke utofauti hadi kwenye haki na wajibu
Hili jambo halipo Hakuna Familia Hiyo Acha Maigizo Nasisitiza Hili Jambo Halipo acha kutufanya Sisi ote hatujui maisha ya familia kama wewe.
Sasa hiyo nguvu na uwezo inachangiwa na nini, yani from nowhere tu Tanzania tuwatii Iran kwa sababu tu wametuzidi nguvu na uwezo, ilihali hatufaidiki nao kiuchumi
Haya ni malalamiko.
Hivi ni kwamba hujui maana ya nature au, nature ni kitu chochote ambacho hakijatengenzwa na binadamu bali kilikuwepo kipo na kitaendelea kuwepo, sasa hiyo mifumo yote ya kiutawala siyo nature bali imetengenezwa tu na binadamu
Bi Jadda Unajichanganya Mno. Sisi Tulisema Mwanaume ni Strong due to nature Na kwa Ulivyotafsiri hapo umelithibitisha hilo. Sasa Kitu Strong lazima kitawale kitu Dhaifu kwa sababu kitu dhaifu hakiwezi kukitawala kitu strong pia kitu strong hakiwezi kikawa sawa sawa na kitu dhaifu nature inakataa hilo. kama ilivyo kwa Survival of fittest.
Sasa kama umeshaona mtu amekuzidi nguvu na uwezo kuna haja gani ya kujaribu kumpinga wakati unajua kabisa hata ukifanya hivyo wewe ndio utashindwa, kwahiyo obviously wanaume waliitumia hiyo advantage kujipa mamlaka
Kwanini Wanawake Hawakujipa utawala wao kwanza ndo Ujue Strong must rule weak.
sababu walijua wanawake hawana uwezo wa kuwapinga, sasa jambo ukishalifanya kwa kulazimisha kaa ukijua siyo watu wote watalikubali lazima watatokea tu ambao watalipinga hata kama itawagharimu maisha yao yote
Utawala wa wanaume haukulazimishwa kama unaushahidi wa kihistoria Juu ya installment ya Huo utawala nipe.
Sasa maandiko yanaamuliwa na nani na ushahidi uko wapi
Wewe ulishayakana maandiko sina la kukushawishi hapa.
Hivi unajua kwamba unavyonasibisha utii na uoga ndivyo unavyozidi kujifunga na kuenda mbali na uhalisia, kama kweli kwenye kila utii kuna aina fulani ya uoga basi ndio unazidi kuthibitisha ile hoja yangu kwamba utii siyo natural bali ni man made
Utii ni Natural na Uoga ni Natural Lazima ujue hivyo. Leo wewe ukimuona Simba Hutalazimishwa kuogopa Na Pia ukiona Sungura Hata uweje Huwezi kuogopa hata ukilazimishwa Hiyo ndio maana ya Nature. Una kichwa kigumu sana.
, yani hiyo aya yako imebatilisha yale yote uliyokuwa unabisha kule juu na ni kama umeniunga mkono kwamba utii lazima ujengwe na misingi fulani na hiyo misingi isipokuwepo basi hata huo utii nao hauna budi kutokuwepo tena, kama unadai kwamba utii wa mwanamke kwa mwanaume umejengwa katika msingi wa nguvu basi nijibu hili swali langu kwamba je mama au shangazi au dada nao wanatakiwa wawatii ndugu zao wa kiume kwa sababu tu wamewazidi nguvu na wana uwezo wa kuwacharaza makofi, na je unamaanisha mwanamke anatakiwa kutii amri ya mwanaume yeyote yule hata anayekutana naye barabarani kwa sababu tu ni mwanaume na ana nguvu na uwezo wa kumcharaza makofi huyo mwanamke siyo
Hapa unaongea mambo ili kupindisha Maneno.
Hatusemi Mwanamke Amtii hata Mwanaume wa barabarani Sasa kwanza anamtii kwa lipi Tunazungumzia Utiifu wa mwanamume na Mwanamke kwenye maisha ya Familia(Ndoa).
Na Hatusemi Boss wa kike Amtii Mfanyakazi wake wa kiume Hatuzungumzii haya.
Malalamiko gani acha visingizio wewe unajua maana ya malalamiko, we sema tu umeishiwa hoja unatafuta namna ya kukwepa mada, hilo liko wazi wala haihitaji uwe na elimu ya rocket science ili kuliona hilo
Leo Umezungumza Porojo tuu na Kupindisha pindisha Maneno.