Utii wa wanawake wa kisasa

Unajua tulielewana mwanzo ila kuna kitu nimekiona kwako, wewe una narcissistic behaviours! Wewe upo sahihi ila kuna kama kaushindani flani unako unataka ku prove kuwa wanawake wapo sawa na wanaume in all aspects, hilo halipo usawa upo ila majukumu tunatofautiana. In terms of family matters manaume anatake charge, haiwezekani mwanamke aka huku kijiti, kwenye swala la ku provide. Mimi nakwambia uhalisia ambao unautaka mwanamke anahaki ni reciever hawezi kuprovide, period. Imagine all infrastructures zimetengenezwa na wanawake? They're not that physical strong hio ni kigezo cha nyie kukubali mwanamme kutake charge.

Hiki ambacho unapigania trust me utakuja kugundua you're wasting your time while it's too late. Kubali wewe mwanamke, jua strengths and weaknesses zenu alaf ishi. Usi complicate maisha utateseka sana
 
Haya ni malalamiko.
Huna hoja wewe
Wahindu Ng'ombe ni mungu sio symbol ya Mungu,, wanaoabudu Moto (Zoroastrianism) kwao Moto ni Mungu sio symbol ya Mungu pia yale Masanamu ya Buddha ni miungu kwao na sio Symbol ya Mungu. (Jitahidi uelewa).
Enhe sasa mbona huendelei unaishia hapo hapo tu kwenye hizo dini au hizo ndio dini pekee zilizopo duniani, vipi mbona huongelei ukristo, uislamu, uyahudi na dini nyingine ambazo zote zinaamini miungu yao iko mbinguni, kwahiyo bado narudi pale pale kwenye hoja yangu thibitisha kwamba ni mungu wa dini yako tu ndio yuko mbinguni
Unatudanganya majibu gani umetoa Bi Jadda??
Kasome tena comment yangu acha kutafuta visingizio
Nimekuuliza ukijitegesha ili upate mimba alafu asipatikane mwanaume utapata hiyo Mimba??
Hivi unaelewa maana ya mwanamke kujitegesha ili apate mimba au ni kiswahili ndio kimekupiga chenga hapo, nimemaanisha mwanamke anaweza akajitegesha kwa kufanya na mwananaume akiwa kwenye siku za hatari bila mwanaume kujua, au wewe hujawahi sikia kuna wanawake wanajibebesha mimba ya wanaume ambao hawakuwa na mpango wa kuzaa nao watoto
Aliesema Majukumu ya Baba ndio yanamfanya awe kiongozi ni nani??
Oohh kwahiyo tunakubaliana kwamba kinachofanya mwanaume awe kiongozi siyo majukumu yake, basi nisione tena huko mbele umehusianisha majukumu ya mwanaume na kuwa mtawala, tuende taratibu mwisho wa siku mbivu na mbichi zitajulikana tu
Nanufaika nayo ila wewe ulisema tunaonufaika ni sisi pekee kana kwamba familia hainufaiki.
Ni wapi niliposema mwanamke hanufaiki na hayo majukumu hebu uwe unasoma ili uelewe siyo unasoma ili ubishe, nilisema hayo majukumu yanamnufaisha mwanaume mwenyewe zaidi kuliko mwanamke, halafu kuna mahali nilikuuliza kwamba unapofanya hayo majukumu kama kuchimba visima sijui kupigana vita, hufanyi kwa ajili ya mkeo tu bali unafanya kwa ajili ya ndugu na jamaa zako na jamii yako kwa ujumla, sasa kwanini hao wengine wote wasikutii kwa sababu hiyo ila mkeo tu ndio anatakiwa akutii kwa sababu hiyo nijibu
Kwani Mada ni Kufuga wanyama Zoo au Utii wa Wanawake wa kisasa?? Naona nikiendela kukujibu katika hili unapata vichaka zaidi vya kujaza risala.

Haya ngoja nikichome hiki kichaka.
Kama umeshindwa hoja unasema tu siyo unajifanya unachoma vichaka, vichaka vyenyewe uliviotesha mwenyewe, ila baada ya kuona vimekushinda unanisingizia eti mimi ndio nimejifichia humo..pathetic!!
Suala la malalamiko ni kwa Pande zote kwa sababu Wanawake wana vituko vyao na wanaume kadhalika sijui wewe unakusudia nini??
Oohh kwahiyo sasa hivi unakubali kwamba wanalalamika sasa mbona mwanzo ulijifanya kukataa kwamba eti wanaume hawalalamiki, mimi hoja yangu ni kwamba wanaoongoza kwa hayo malalamiko ni wanaume kuliko wanawake na siku zote malalamiko ni ishara ya kuumizwa na jambo fulani, kwahiyo kitendo cha wanaume kulalamika zaidi kuliko wanawake kinadhihirisha kwamba ni wao ndio wanaumia zaidi kihisia kuliko wanawake
Pili kuathirika kisaikolojia ni kwa wote bali kwa wanawake ni zaidi kwa sababu you're too emotional.
Okay naona hapa tunazunguka sana ila ngoja nikusaidie tu na naomba hizi aya zinazohusu hii hoja uzisome kwanza zote ndio ujibu usikimbilie tu kujibu vipandevipande bila kuelewa maana nzima ya hii comment, ni hivi wanaume ndio wanaoathirika zaidi kisaikolojia na tabia mbovu za wanawake kuliko wanawake wanavyoathirika na tabia mbovu za wanaume hii ni kwa sababu maisha ya mwanaume yanarevolve around wanawake, yani mwanaume siku zote furaha yake iko kwa mwanamke kwa maana kwamba mwanaume siku zote anategemea mwanamke ndio ampe furaha hawezi kutafuta furaha nje ya hapo

Na wanaume ndio wanaopenda zile kauli za faraja na mahaba kama "pole na uchovu mpenzi" au "karibu chakula mume wangu" na kauli nyingine kama hizo maana zinawafanya wajisikie vizuri, na kama nilivyokuambia kwenye comments zilizopita kwamba mwanaume tangu zamani hajafundishwa kuvumilia maovu ya mwanamke mwanaume siku zote anategemea mwanamke awe ni kiumbe mwenye tabia njema hilo ndio linamfanya mwanaume awe na furaha, kwahiyo mwanaume akikosewa au akivurugwa na mkewe anachanganyikiwa na anakosa furaha anaanza kuona nyumba chungu kiasi cha kumfanya aanze kuchelewa kurudi nyumbani

Na atafikia hatua atapunguza hata ufanisi kwenye shughuli zake za utafutaji na hata kwenye tendo la ndoa na mwisho wa siku ataenda kutafuta faraja kwa mchepuko ambaye naye ni mwanamke, mwanaume anaweza kuwa bilionea lakini hawezi kuwa na furaha hadi atumie hizo pesa na wanawake kuna msemo unasema "kadiri mwanaume anavyozidi kupata pesa ndivyo anavyotamani kuwa na wanawake wengi zaidi, ila kadiri mwanamke anavyozidi kupata pesa ndivyo anavyotamani kuwa mbali na wanaume" na wanaume wengi matajiri hukiri kwamba moja ya faida za utajiri ni kuwa na wanawake

Lakini tukija kwa mwanamke yeye furaha yake haiko kwa mwanaume pekee mwanamke ana uwezo wa kutafuta furaha kwa watu wengine kama wazazi, watoto, ndugu na jamaa nk yani mwanamke tangu zamani alifundishwa kuvumilia maovu ya mwanaume, kwahiyo mwanamke hata akikosewa au akivurugwa na mumewe siyo rahisi kuchanganyikiwa au kuchepuka kuenda kutafuta furaha kwa mwanaume mwingine kwa sababu mwanamke hata usipomtamkia zile kauli za kimahaba kama nilizozisema hapo juu kwake ataona kawaida tu, mwanamke akipata pesa cha kwanza hawazi kutumia na wanaume bali atawaza kuzitumia na watoto na wazazi kisha watafuata ndugu na jamaa na wengine hata wazazi wengi wenye watoto wa jinsia zote husema kwamba watoto wao wakishaanza kujitegemea wa kike ndio huwa wanawakumbuka zaidi wazazi wao kuliko wa kiume ambao ahadi na kalenda zinakuwa nyingi

Hiyo ni kwa sababu wanaume wakipata pesa cha kwanza wanawaza kuhonga na kutumia na washikaji kisha ndio watawakumbuka wazazi na hao wengine ndugu na jamaa na kingine ambacho kinafanya wanaume waumie zaidi kisaikolojia kuliko wanawake ni kile kitendo cha kuhudumia, yani unakuta mwanaume kahangaika kuhudumia mwanamke halafu huyo mwanamke anakuja anamsaliti au anamuacha kirahisi tu ndio maana cases za wanaume kuua wapenzi wao ni nyingi ila za wanawake kuua wapenzi wao ni chache, sababu wanaume huwa wanahisi kama ndio wanapoteza zaidi kuliko wanawake ambao wao wakiwa kwenye mahusiano hakuna cha maana wanachooffer zaidi ya ngono na vitu vidogo vidogo huku wanaume ndio wakioffer vingi zaidi na hii ndio inawafanya wanaume waumizwe zaidi kisaikolojia na maovu ya wanawake kwahiyo usiwe unabisha bila kureason
Sio kweli,,, Kesi zaidi ya hizo zipo katika madawati ya jinsia.
Hizo kesi huwa zinahusu nini na ni ngapi kulinganisha kesi za kudai huduma za kiuchumi
Pili wanaopeleka kesi za huduma za kiuchumi Ni Huduma zipi hizo??
Huduma za kiuchumi kwa watoto wao au unataka kudanganya hapa kwamba huko kwenye madawati wanajaa wanawake wasio wa watoto, kwa taarifa yako huko asilimia kubwa wanaoenda ni wanawake wenye watoto waliotelekezwa, hivyo wanaenda kutafuta haki ya kutaka wanaume wahudumie hao watoto wao lakini hawaendi kulalamikia tabia mbovu za hao wababa
Tabia zisizo faa zipo kwa wote Bi Jadda.
Inanisikitisha kusikia kutoka kwako kwamba Umuhimu wa Mwanaume kwa Mwanamke ni Huduma za kiuchumi tuu(pesa) Wanaume Ni Walinzi wenu And Women are more comfortable with Men.
Sasa mbona umeandika kana kwamba hao wanaume hiyo kazi yao ya ulinzi wanaifanya vyema hivi ni kwamba huwajui wanaume wa kizazi hiki, wanaume wa kizazi hiki hawana kingine cha kuoffer zaidi ya pesa na mali basi na wanawake wameshaliona hilo ndio maana siku hizi kwenye mahusiano wanafuata hayo tu, wanaume wenyewe siku hizi wengi hawajielewi kwenye mahusiano wanafuata ngono na muonekano unategemea wanawake wataona umuhimu wa wanaume hapo
Hiki kichaka pia nakichoma.
Bora umeamua kuvipunguza hivyo vichaka mwenyewe, maana ningefanya hivyo mimi ungesema nakimbia hoja, mimi naenda sambamba na wewe huwa sikimbii hoja
Oohh kwahiyo sasa hivi kuna feminism yenye afadhali na feminism yenye misimamo mikali, mbona unabadili gia angani tena wewe si ulikuwa unaitukana feminism hapa oo ni upumbavu sijui ni takataka, sasa hivi ndio unajua kwamba kuna stages za feminism hebu kuwa na msimamo mmoja basi feminism inafaa au haifai
Nimekwambia Ndoa nyingi hizi leo zinazovunjika ni Zile za wanawake wajuaji wanaoishia Kuwa single mothers Na kujidai they don't care.
Sasa si ndio nikakuambia ulete takwimu na ushahidi kuwa ndoa nyingi zinazovunjika ni zenye feminism
Hapa tena umebadili gia angani mwanzo ulisema wanawake wajuaji hawaolewi sasa hivi unasema eti wanaolewa ila wakileta ujuaji wanaachika, hivi unaelewa hata unachokisimamia na unachokitetea kweli mbona hujiamini na hoja zako unahamahama tu, kwahiyo wanawake wote wanaofanya hayo ndio hawaachiki na una uhakika ndoa zote zinazodumu ni zenye wanawake wa aina hiyo tu
We jamaa unachekesha na unasikitisha sana hivi unajua maana ya feminism kwahiyo feminism ni wanawake kubandika kucha, kupost mitandaoni, kutumia contraceptives na huo ujinga mwingine ulioandika, yani muda wote unaitajataja feminism nikajua unajua hata maana yake kumbe hata maana yake yenyewe huijui unakuja kuleta nadharia zako hapa
Hizi Tamaduni unaziona hazina faida wewe. Sasa usilazimishe Kila uanchokiona wewe kibaya na kwa mwenzio nacho kiwe kibaya. Mind you German Ushoga ni Jambo zuri Sana na wanatushangaa sisi tunaopinga Mambo hayo.
Sasa mbona unaniambia mimi kana kwamba mimi ndiye niliyeanzisha feminism ni hivi hakuna mwanamke anayefurahia hizo tamaduni kwa utashi wake narudia HAYUPO, kitendo cha feminism kuanzishwa na wanawake kuikubali kinaonesha kwamba ni wanawake wengi waliona hizo tamaduni ni mbaya na hazina faida kwao bali zina faida kwa wanaume tu, hapa usiniongelee mimi ongelea mitazamo ya wanawake wote kwa ujumla toka feminism ilipoanzishwa hadi hapa ilipofikia
Ulevi na Usaliti ndio uanaume nani kakwambia It seems like umezungukwa na Wanaume wa aina furani hivi.
Hivi kweli unaweza kusimama hadharani ukasema Ulevi ndio Uanaume alafu ukaeleweka???
Wewe ni either unaishi kwenye nyumba za ibada na hupiti sana mitandaoni ndio maana unaishi kwa nadharia au uhalisia unaujua ila hapa unafanya makusudi tu kujitoa ufahamu ili mradi utetee uongo wako, ni mara ngapi wanaume wanajitetea kwamba mwanaume kuchepuka ni nature kwa sababu mwanaume ameumbwa na tamaa na hatosheki na mwanamke mmoja tena wenyewe ndio huwa wanasema ukiona mwanaume hachepuki ujue ni shoga au masikini au hana nguvu za kiume, hata kwenye ulevi wanaume huwa wanajitetea kwamba mwanaume lazima akae baa na washikaji zake maana ndio sehemu nzuri za kupeana madili na michongo ya pesa na biashara wanadai mwanaume hutakiwi kila siku kuwahi kurudi nyumbani mkeo atakuzoea sana..hayo ni maneno ya wanaume wenzio vijiweni na mitandaoni halafu unasema eti mimi nimezungukwa na wanaume wa aina fulani mbona unapenda kuishi kwa kukariri
Personal attack kivipi!!. Kwani Si mnajivunia kutokuolewa Kwa sababu mnasimamia mambo yenu wenyewe no need of man.
Anyway kama nimesema uongo( kwamba ndoa unayo) prove me wrong kama nipo sahihi then hiyo sio attack ni reality.
Yani unataka niprove kwako kwamba mimi nina ndoa hivi una akili kweli wewe sasa personal issues zangu zinakuhusu nini wewe umeona kuna mahali mimi nimekuuliza kama una ndoa, jitahidi kwenye public discussions kama hizi usiwe unapenda kuingiza personal issues kwa sababu inachukuliwa kama defensive mechanism na ni ishara ya kushindwa na kukwepa hoja, marital status yangu haihusiani na michango yangu ninayoitoa kwenye hii mijadala kwa sababu humu tunajadili uhalisia uliopo kwenye jamii hatujadili kulingana na hali zetu binafsi za maisha kwahiyo wewe jikite kwenye hoja
Nilikuuliza kuwa jee wewe Bibi yako amekwambia Alikuwa hana Furaha na maisha yake ya ndoa na Babu yako chini ya mfumo mnaouita mfumo dume?? (Jaribu kujibu)
Hili mbona jibu lake lipo kwenye ile comment yangu na linajieleza nenda kanisome tena
Nadharia gani Ninyi wanawake wanaharakati mnajua kupika?? Na hizo kucha mnapikaje?? Huo Muda wa kupika mnapata wapi?? Wakati Mkirudi kutoka Ofisini Mmechoka mnamkolomea Aunt awahishe Chakula.
Wewe haujui maana ya feminism, yani bado unashikilia kwamba mwanamke kubandika kucha ni feminism, nani aliyekuambia kwamba mwanamke kubandika kucha ni feminism
Ndio maana nikakuuliza kwahiyo ina maana hiyo miaka watu walikuwa hawatibiwi au bidhaa zilikuwa hazitengenezwi, au ni wapi mimi nimesema kwamba hizo kazi zilikuwa zinafanyika kama zinavyofanyika miaka ya sasa, mimi nilimaanisha kwanini wanawake walikuwa hawapewi hiyo elimu kulingana na teknolojia hiyo hiyo iliyokuwepo miaka hiyo
Nasisitiza Utii unachunga Mahusiano yaliyopo baina ya Watu husika. Nakazia tena.
Nami nasisitiza kama ni hivyo basi msingi wa utii wa mwanamke kwa mwanaume siyo kuzidiwa nguvu na umadhubuti, kwa sababu hicho kigezo hakichagui aina ya mahusiano maana siku zote mwanaume yeyote ana nguvu kuliko mwanamke yeyote, hapo umechemka hauna hoja
Sasa ndio uone kwamba hicho kigezo chako cha nguvu na umadhubuti ni batili kwa sababu mtoto wa kiume kumzidi mama yake nguvu hakumfanyi awe mtawala, mimi niliitetea hoja yangu vizuri kabisa kwamba msingi wa mtoto kumtii mzazi (bila kujali jinsia) ni kwa sababu hao wazazi wamemzaa na wanamhudumia na hicho kigezo cha kumzaa ndio chenye nguvu, ila wewe ukasema tu kwamba kigezo cha mwanaume kumtawala mwanamke ni nguvu na umadhubuti sasa kiuhalisia hicho kigezo hakichagui aina ya mahusiano, wewe ndio unalazimisha kwamba hicho kigezo kinachagua aina ya mahusiano ila si kweli halafu mbona umeng'ang'ania hayo mahusiano ya mama na mtoto tu, kwani hukuona hayo mengine ya shangazi na dada na ndugu wengine wa kike wa mwanaume je nao wanatakiwa kumtii kwa sababu tu kawazidi nguvu na umadhubuti
Hahahaha defensive mechanism. Unapopataka wapi??

Unachotaka kusema kuwa Wanaume wana Nguvu Sawa na Wanawake na Wanauwezo sawa katika hayo Mambo uliyoyataja??
Hiyo siyo hoja hoja ni kwamba wanawake wanaweza kufanya ambayo wanaume wanaweza huo utofauti wa kuyahimili unaletwa na binadamu wenyewe, kwa sababu hata ninyi kuna majukumu ya wanawake ambayo mnaweza kuyafanya ila hamuwezi kuyafanya kwa ufanisi kama wanawake mfano kulea watoto lakini hutasikia wanawake wakijiit watawala kwa hilo, halafu kwanza kule juu umeuliza swali la kuashiria kwamba kinachomfanya mwanaume kuwa mtawala siyo majukumu yake kwahiyo sitegemei tena utahusisha haya majukumu na utawala wa mwanaume
Kwanza hoja Ilikuwa sio Hii. Umepindisha Hoja. Wewe ulisema kazi za nyumbani Wanaume hawawezi kuzifanya Mnaweza ninyi kwaiyo You're Strong for that. Poor you.
Ni wapi nimesema kwamba mwanamke ni strong kwa sababu ya kufanya kazi za nyumbani hebu paquote halafu nioneshe nasisitiza nioneshe, mimi nilisema mwanamke ni strong kwa maamuzi aliyonayo juu ya uzazi tu yani wewe ukiishiwa hoja unalazimisha kunipandikizia maneno ili upate sababu ya kuendelea kujaza magazeti, kazi za nyumbani siyo majukumu ya kimaumbile hivyo hata wanaume wanaziweza tena kwa ufanisi kabisa ila swali langu ni kwamba kwanini hawapendi kuzifanya wanataka mpaka wanawake wawafanyie tena wanadai eti ni majukumu ya kike
Pili mgawanyo wa majukumu ndio unaoongoza mambo hayo Baba Anaenda kutafuta Mahitaji Muhimu kwa ajili ya familia kutokana na Maumbile yake ya Nguvu na Umadhubuti na Mama anasimamia Majukumu ya hapo nyumbani pamoja na Malezi Nyumbani.
Sasa kumbe unajua kwamba huo mgawanyo wa majukumu uliwekwa kwa sababu ya utofauti wa kimaumbile tu na si kigezo cha kumfanya mmoja awe mtawala kwa mwenzie, yani ni kama vile mnajaribu kusema kwamba majukumu ya mwanaume ndio ya muhimu na magumu zaidi kuliko ya mwanamke wakati ugumu au urahisi wa jukumu unatokana na maumbile ya mhusika, kama kuna mtu anaona kama majukumu yake ndio ya muhimu na magumu zaidi kuliko ya mwenzie kiasi cha kutaka kumtawala mwenzie basi aishi peke yake na afanye hayo majukumu yote peke yake ikiwemo hayo anayoyaona marahisi bila kuhitaji msaada wa jinsia nyingine
Sasa kama shida ni watoto maana yake wanawake wasitoke kabisa wasiende hata kutafuta pesa wawe wamama wa nyumbani tu, lakini siyo kusingizia eti mitoko ya mara moja moja ndio chanzo cha watoto kuharibiwa wakati mke huyo huyo anashinda kwenye kazi au biashara siku tano au zote za wiki, na hilo suala la wanawake kuwa wamama wa nyumbani ni mada nyingine kabisa na ni kitu ambacho siyo jamii tu bali hata serikali hazitakubali kurudi huko kwa sababu huo mfumo wa maisha ni adui wa mapato na maendeleo ya nchi ila kwa sababu wanaume ni wabinafsi mnawaza maslahi yenu ya kipuuzi tu
Ujerumani na Ulaya kwa Ujumla ushoga Unalazimishwa?? au unakusudia Huku Afrika??
Ushoga duniani kote unalazimishwa ndio maana hata wanaoupinga wengi ni wanaume ambao ndio jinsia yao inahusika, lakini pia wengi wanaoipinga feminism ni hao hao wanaume siyo wanawake ambao jinsia yao ndio inahusika unadhani ni kwanini, jiulize kwanini wanawake wameifurahia feminism ambayo inahusu jinsia yao ila wanaume hawajaufurahia ushoga ambao unahusu jinsia yao halafu ndio utajua kipi kinalazimishwa na kipi hakilazimishwi
Aiseee kwani wewe huoni namna wamama wanavyowalea watoto wao wa kiume siku hizi hadi wanaume wanalalamika kwamba wanawake siku hizi wanaharibu watoto wa kiume, kwa taarifa yako wamama wengi wanajitahidi kuwalea watoto wao kiume kuwa gentlemen ninyi wababa ndio mnalea watoto wa kiume kuwa na ubabe wa kipumbavu mnadai eti ndio uanaume kwamba asipokuwa hivyo wanawake watampelekesha, wamama wengi huwa wanawalea watoto wao wa kiume katika misingi ya kwamba mwanamke ni mwenza wako na siyo mtumwa wako wote mnatakiwa kusaidiana kuheshimiana na kusikilizana
Binti yangu kuwa house wife Mtiifu kwa Mumewe ni jambo zuri kwangu kuliko kuwa degree holder Employed kiburi kwa mumewe. Mind you Kiburi Baada ya kusoma Ni maamuzi ya mtu kutokana na watu aliokutana nao katika safari yake ya kusoma.
Ndio maana nikakuambia hapa unaandika tu majibu ambayo yatakuwa upande wa hoja zako mradi tu utetee uongo wako ila hali halisi tunaiona namna wanaume wa siku hizi wanavyopambana kulea na kusomesha mabinti zao ili wasije kuwa watumwa wa wanaume kisa huduma za kiuchumi, kuna uzi uliwahi kuanzishwa humu jf kuwauliza wanaume kwamba "je utakubali binti yako aolewe na mwanaume mwenye matendo kama unayomfanyia mkeo", aise comments nyingi za wanaume ziliashiria hawako tayari kwa hilo na huo ni mfano tu kati ya mifano mingi inayoonesha jinsi gani wanaume wana ubinafsi juu ya wanawake wanaotaka kuwaoa tu
Huo mfano hautoshi?? Mbona unamun'gunya maneno unajidai kama vile unayajua maisha mengine Tofauti na yale anayoyasema Mwenyewe. (Prove)
Yani unataka niprove hilo ndio hoja iwe na ukweli we jamaa huna akili wewe inaonekana hata siku ukisikia mchungaji au shehe kafumaniwa au kabaka (maana hayo mambo yapo), utapinga kwa sababu tu ni mtu ambaye anasimama madhabahuni anahubiri mema na yeye anaonekana ni mtenda mema, ninyi msiojua ukweli mtamuona mtakatifu lakini sisi tunaoujua ukweli hatuwezi kuyatilia maanani hayo mahubiri yake maana mbele ya macho yetu tunamuona kama mnafiki tu
Sasa kama mnavumilia mbona mnaoongoza kulalamika ni nyie na kuvunja ndoa kila siku
Kwani huoni Ndoa zinazovunjika nyingi ni za Mafeminist baada ya kushindwa kuendelea kuficha makucha yao. Na wale Wanawake wanaowaiga Wanawake kama ninyi bila kujua kuwa wengi wenu mnazungumzia ndoa wakati ninyi hamjaolewa.
Wewe una data na ushahidi gani juu ya hili
Kwaiyo Wananchi wengeshirikishwa Kipengele kingetolewa??
Ndio
Eti Kijana it's okay Sio shida
But Walioweka hiko kipengele ni katika Kuchunga heshima kwa kiongozi wa nchi na sidhani kama kuna nchi Ulaya yenye demokrasia kubwa ambapo Rais anaweza kushitakiwa akiwa madarakani.
Hapa hoja siyo lengo la kuwekwa hiko kipengele, bali hoja ni kwamba wananchi hawawezi kufurahia hicho kipengele endapo rais ana makosa, na ndio maana nchi nyingine raia wanaandamana au majeshi yanapindua serikali
Unaweza kujitengenezea mambo ukahisi unakuwa psychological tortured kumbe ni expectations zako tuu. Kama ninyi mnavyoiga maigizo ya kizungu.
Wewe kwanini umpangie mtu ni kipi kinachompa furaha na kipi kinachompa huzuni, kama mtu anaona kwamba jambo fulani kwake linampa psychological torture kwanini wewe umkatalie kwani wewe ndio umeshikilia hisia zake, na mbaya zaidi eti kauli kama hizo zinatoka kwa huyo huyo anayekupa hiyo psychological torture unategemea nini lazima tu atatetea upande wake kwa maslahi yake
Nilikuwa nataka uniambie Hizo Ndoa chache zilizokuwa na furaha. Furaha ilitoka wapi?? wakati Mwanamke hakuwahi kuwa na furaha chini ya Mfumo Dume.????
Si ndio maana nikakuambia kulikuwa na few exceptions za wanaume ambao hawakuwa na hizo tabia ambazo zilikuwa common kwa wanaume wengi, una uelewa mdogo sana kiasi kwamba umeshindwa kuelewa huo mfano wangu unamaamisha nini hapo, au unahisi mimi sijui ninachokisimamia na ninachokitetea kama wewe unavyohamahama
Hakuna hoja unajenga na Unaandika ili ubishe tuu to infinity.
Wewe ungekuwa siyo mbishi tusingefikia hapa, hata wewe pia ni mbishi tena bora mimi nabisha kwa facts, wewe unabisha kwa mihemko mradi tu usionekane umeshindwa huu mjadala kirahisi
Maandiko sio Nature acha kulazimisha.
Ndio mimi nasema maandiko siyo nature, ila watu wa dini ndio wanadai kwamba maandiko ni nature, sasa kwa hiyo kauli yako maana yake unaniunga mkono mimi
Uhuru wa Kuendelea na mahusiano mengi bila kuulizwa na yeyote.
So
Nani kazungumzia starehe hapa??
Sasa kuruka viwanja ni nini ni basic need au
Jee Sababu zipi zenye mashiko Mwanaume anaweza kumzuia mkewe kutoka?? Au hakuna kumzuia kabisa??
Sababu zenye mashiko ni zile ambazo zinatakiwa kuapply hata kwa mwanaume mwenyewe, siyo hizo sababu azitoe kwa mwanamke tu halafu yeye ajiexclude kwenye hizo sababu, kama sababu ni madhara basi hayo madhara yawe yale ambayo yanaweza kumpata yeyote kati yao endapo atafanya jambo fulani au ataenda sehemu fulani
Nani kaweka utofauti??
Si ninyi mnaodai kwamba kwa sababu mwanaume na mwanamke hawako sawa kwenye maumbile tu basi hawatakiwi kuwa sawa kwenye mambo mengine yote
Hakuna maisha ya namna hii.
Ndio mhakikishe hamkwami kiuchumi sasa
Kama umeamua kutumia maandiko basi usichague yale yanayofavour jinsia yako tu, haya naomba niletee na maandiko ya mwanaume kula kwa jasho na kulisha na kutunza familia, halafu uniambie kwanini mwanamke hakuambiwa hayo
Nimeshajibu.

Aisee!!!

Kwanza nikuulize wewe unafurahia talaka kuwa nyingi!! una Shida Kubwa. Mind you dada zako ndio wanaachika Na kuwa single mothers.
Ni wapi nimesema nafurahia talaka mimi naandika hali halisi iliyopo tu, kwani ni uongo kwamba watu hawapeani talaka kila siku, we vipi mbona unalazimisha kunipandikizia maneno
Hakuna uhusiano na hii mada yetu acha porojo.
Ndio kuna uhusiano jamii nyingi bibi zetu walikeketwa kwa sababu babu zetu walioa wake wengi na wakati mwingine walishindwa kuwaridhisha ipasavyo, hivyo kwa kuhofia kuwa watawasaliti wakaanzisha utamaduni wa wanawake kukeketwa ili wasiwe wanapata hamu ya tendo hata kama hawajakutana na waume zao kwa muda mrefu, hivyo hiyo ingewafanya kushindwa kuchepuka na kubaki waaminifu kwa waume zao tu
Una ushahidi juu ya hili??

Hahahha eti wanaume wanaojielewa Wanapatikana kwa wingi Mkoa Gani??
Kwamba kujielewa ni kabila, hadi watu wanaojielewa wapatikane mkoa fulani, we jamaa mbona unafurahisha sana
Sasa mara kwamba unayajua Ya chinichini mara yeye sio kielelezo cha Wanawake wote Hueleweki.
Yote hayo ni majibu acha kukwepa hoja, nasisitiza rais samia siyo kielelezo cha namna wanawake wote duniani wanavyotakiwa kuwa, huo ni mtazamo wake binafsi na siyo sheria na wala haumfanyi kuwa sahihi au kuwa na akili kuliko wanawake wengine wote
Aisee Kwaiyo Unaolewa na Una guarantee utii katika Pesa zikikosekana unaonyesha uhalisia wako (Changamoto).
Siyo kuguarantee utii katika pesa bali huo ndio msingi wa utii wa mwanamke kwa mwanaume, yani wewe mtu hujamuumba wala hujamzaa unataka akutii kwa lipi, hivi hata kwa akili ya kawaida tu wewe unaona hiyo inaingia akilini kweli..anyway wewe lazima ikuingie akilini kwa sababu ina maslahi kwako huwezi kutumia common sense kwenye jambo linalokufavour hata kama ni baya kwa mwingine au kwa ujumla
Jike dume kama ilivyo literally.
Sijui ulishawahi kujiuliza kwanini Wewe tukikwambia una Tabia za kiume kiume Haitakuwa shida sana and may be Uta feel proud ila Mwanaume tukimwambia ana tabia za kike kike Hiyo ni Vita imeanzishwa hatokubali.
Sasa hilo suala la mtu wa jinsia fulani kufurahia au kuchukia kupewa sifa za jinsia nyingine limekujaje hapa, anyway kwakuwa mimi sikimbii hoja acha nikujibu kwamba hayo yote ni kutokana na fikira tu zilizojengeka kwenye jamii, lakini huwezi kusema moja kwa moja kwamba kumuita mtu wa jinsia fulani kwa jinsia nyingine ni vizuri au vibaya labda useme inategemea
Usitoe majibu mepesi katika hoja ngumu.
Wewe kuna hoja gani ngumu umeweka hapo hebu jistukie
Mwanaume akiwa na sababu ya msingi anaruhusiwa kumzuia mkewe akitaka kutoka??
Ndio endapo hiyo sababu itakuwa applicable to both parties hilo nimeshaeleza
Kwani tulikuwa tunajadiri Waarabu au Jamii yetu ya Zamani??
Duuh kwahiyo informal education, inakuwa defined kulingana na maisha ya jamii zetu za kiafrika tu, aise yani unapuyanga hadi unatia huruma
Aaah kwanini umetanguliza "bila mshahara" Defensive mechanisms zako Hovyo kabisa.
Anyways Tufanye hunyimwi mshahara jee Kumtii boss wako unakosa furaha??
Aiseee hivi we jamaa unasoma comments zangu zote hadi mwisho kweli au ukifika katikati tu basi unakimbilia kujibu, si nimekuambia hapo kwamba hakuna anayefurahia kumtii boss wake ila watu wanakubali kwa sababu tu ya mshahara, nikakutolea na mfano kwamba ndio maana watu wengi wenye uwezo huwa wanaanzisha biashara zao kwa sababu wanaona ajira ni utumwa
Uongo.

Nadharia.

Hueleweki.
Huna hoja wewe
Na wazee.
Okay kwahiyo mfano huyo mwanaume anamuwajibisha mkewe, na huyo mkewe hasikii bado anaendelea, je huyo mwanaume bado anatakiwa kuendelea kumpenda huyo mke wake
Maneno yako ni sahihi kwamba uliposema Mshahara ni Huduma ulikuwa sahihi??
Kwanza ni wapi niliposema kwamba mshahara ni huduma nioneshe
Hahahaaaa

Unajua unachokiandika kweli??

Kwamba wale pet dogs na puppies ni hatari??
Aise kwahiyo wewe unajua hao tu ndio mbwa pekee wenye mionekano mizuri, nikikuambia unitajie aina za mbwa unazijua kweli au ndio kwa hisani ya google, ndio maana nikakuambia usiishi kwa kukariri wapo mbwa wenye mionekano mizuri na ni hatari
Cheo kina nini kwanini unamtii??
Ni kwa sababu wananchi wenyewe ndio wamemchagua na wamempa kile cheo na yuko pale kuwatumikia wananchi, pia unaweza kumtii kwa sababu unamuogopa lakini si kwa sababu eti umependa kumtii, hili kila wakati nakujibu lakini unajitia kukaza kichwa nishakuambia utii unaoletwa na uoga siyo nature
Maandiko katika Utii wa Mke kwa Mumewe hayana Tofauti.
Sawa mbona huongelei na maandiko ya mume kumpenda na kumhudumia mkewe na kwanini mwanamke hakuambiwa afanye hayo kwa mumewe
Aise sasa mbona hujajibu swali langu, yani muda wote unaniambia nisubiri kwamba utakuja na jibu ila hapa ndio unaona umekuja na jibu kweli, yani umekimbilia kuniambia habari za waves za feminism wakati mimi nilikuuliza kwamba

Kama kila mwanamke anazaliwa na fikira za kutaka kutawaliwa na mwanaume, na hakuna mwanaume anayezaliwa na fikira za kutaka kutawaliwa na mwanamke (maneno ambayo ulisema mwenyewe), je feminism ilianzishwa na nani na kwa faida ya nani hebu nijibu kwanza hilo

Kuhusu waves za feminism mbona nilikuambia kwamba lengo kubwa la feminism ni wanawake kuanza kuwa na access ya elimu na ajira, na kumiliki pesa na mali sawa na wanaume hayo mengine yote ni matokeo ya wanawake kuwa na hivyo nilivyovitaja, kwahiyo nijibu swali langu acha kutafuta vichaka vingine vya kujifichia
 
Hivi unaelewa maana ya narcissistic behaviours mkuu au umeamua tu kuliweka hapo ili mradi utetee hoja yako mimi sishindani ila naongea uhalisia uliopo kwenye jamii haya siyo mawazo yangu, mimi sijakataa kwamba mwanaume hatakiwi kumtawala mwanamke ila hoja yangu ni kwamba msingi wa mwanaume kumtawala mwanamke upo katika huduma za kiuchumi tu na si vinginevyo, hayo majukumu ya kimaumbile siyo kigezo cha mwanaume kuwa mtawala kwa sababu mwanamke hana nguvu na uwezo kama mwanaume huwezi kujipa utawala kwa kigezo ambacho mwenzako hajaumbwa nacho na hakupenda au hakuchagua kutokuwa nacho sijui kama unanielewa
 
Naelewa vizuri, ndo maana nikasema, wewe unaile dhana ya kutumia logic kama mwanaume kupinga vitu ambavyo unavihisi japo unajua fika who you really are! Toka kipindi kile nilikuambia usi base kwenye negative side ya utawala lkn kumbe hukunielewa. Naomba fuatilia vizuri akina nani wanaoumia zaidi in this era of feminism! Sawa wanaume hasa vijana wadogo imewa affect ila at the end of the day wanainuka as mens wanasonga mbele, nyie ndo mnaishia kuwa single mnatapatapa tu mnatumika then mnaaachwa! Wanawake wanaojifanya mafeminists wanaishiga pabaya, you'll learn this, ila mpk yakukute ndo ujue...

Umesema sjui uchumi, haya hivi wakina nani wanao run huo uchumi? Wakina nani wanao fanya kazi kuhakikisha society ina thrive? Wakina nani wanao hakikisha usalama wa taifa, jamii na familia kwa ujumla kama sio waume? Je hvyo vinahitaji pesa vyote? Mifano midogo kama hii ndo itakupa jawabu kama mwanamke kujua position yako. Kuna vitu vingine kukaa unabisha ni kupoteza muda tu. Neno utawala lisikutishe as long as hakuna baya litakalo kukuta, ku submit kwa mwanaume ndo nature yako.
 
Naelewa vizuri, ndo maana nikasema, wewe unaile dhana ya kutumia logic kama mwanaume kupinga vitu ambavyo unavihisi japo unajua fika who you really are! Toka kipindi kile nilikuambia usi base kwenye negative side ya utawala lkn kumbe hukunielewa. Naomba fuatilia vizuri akina nani wanaoumia zaidi in this era of feminism! Sawa wanaume hasa vijana wadogo imewa affect ila at the end of the day wanainuka as mens wanasonga mbele, nyie ndo mnaishia kuwa single mnatapatapa tu mnatumika then mnaaachwa! Wanawake wanaojifanya mafeminists wanaishiga pabaya, you'll learn this, ila mpk yakukute ndo ujue...

Umesema sjui uchumi, haya hivi wakina nani wanao run huo uchumi? Wakina nani wanao fanya kazi kuhakikisha society ina thrive? Wakina nani wanao hakikisha usalama wa taifa, jamii na familia kwa ujumla kama sio waume? Je hvyo vinahitaji pesa vyote? Mifano midogo kama hii ndo itakupa jawabu kama mwanamke kujua position yako. Kuna vitu vingine kukaa unabisha ni kupoteza muda tu. Neno utawala lisikutishe as long as hakuna baya litakalo kukuta, ku submit kwa mwanaume ndo nature yako.
 
Khaaaaaa umeandika binti...zaidi ya thread 7
 

Na wewe naona hoja zako ni kama za huyo ninayebishana naye tu okay hiyo negative side ya utawala unayosema ni ipi na positive side ni ipi hebu fafanua hapo, hayo mnayosema ya kurun uchumi sijui kufanya society ithrive kumbuka hamyafanyi kwa faida ya wake zenu tu bali pia mnayafanya kwa faida ya jamii nzima wakiwemo wazazi, walezi, ndugu na jamaa zenu ila mbona hamdai utii kutoka kwa hao bali mnadai utii kutoka kwa wake zenu pekee, kuhusu kina nani wanaoumia zaidi in this era nafikiri wote tunajionea hali halisi huku mitandaoni na huko kwingine ni jinsia gani inaongoza kwa kulalamikia maovu ya jinsia nyingine
 
Unachekesha sana ujue! Yaani unapenda kurudi kwenye circle ileile ambayo wanawake wasiojitambua hupenda, mmekuwa manipulated na elimu uchwara! Nimekueleza utii au mwanamke kutawaliwa na mwanaume ni protection kwenu biologically women need that, hakuna mwanamke duniani anayetaka mwanaume asiyeweza kukidhi mahitaji au kumuhudumia. Hata wanyama dume imara ndo ata win jike. So mko intrinsically created kutawaliwa sasa hii generation ya nyoka na u feminism ndo mnajifanya na nyie wanaume lol 😂, huwa nacheka sana kuona mwanamke anapinga hii kitu, mme base kwenye utii wenye negative outcomes ambao ni kama kivuli tu kuwapumbaza. Skia we men don't give a f*ck all we need is a woman, mafeminist mtabaki kulialia tu.

Kingine unataka iweje labda maana una bisha kila kitu. Ungetoa maoni yako unavyotaka iwe instead of arguing, maana ni kama unajifurahisha for no reason, hii kitu ni serious na ina madhara makubwa kama utaichukulia juu juu tu. Wanawake ndo mnaathrika sana, because hamna sauti na ile kudangadanga mnatuliza maumivu ila hamna hope hata kidogo. Ili swala inabidi miliangalie kwa jicho la tatu, mwanamke ndo anayeumia.
 
Mbona mtoa mada hajaongelea hayo uliyoandika
 
Kijana mbona una mihemko sana halafu hakuna cha maana unachoandika zaidi ya kurudia yale yale tu hebu acha kunipandikizia maneno kwani ni wapi ambapo haujaelewa, nimekuambia hivi msingi wa mwanamke kumtii mwanaume uko katika mwanaume kumhudumia mwanamke yani kama mwanamke anahudumiwa basi hana budi kutii, nimekuuliza hivi hiyo negative side ya utawala ni ipi na positive side ni ipi badala ya kunijibu maswali yangu unaniletea mikwara mbuzi na hasira zako juu ya feminists..chillax bro i am not the cause of your problems!!
 
Hizo dini ulizozitaja ni kweli Wao wenyewe wanadai Mungu wao Yupo mbinguni na ni Dini ambazo zina Uhusiano furani Wa kimaandiko Kuhusu Dini Nyengine sidhani kama nazo Zinadai Mungu wao yupo mbinguni.
Hoja sio yeye Kujua fertile days zake hoja ni kuwa Kama asipopatikana Mwanaume hakuna namna Mwanamke anaweza Kupata mimba.
Oohh kwahiyo tunakubaliana kwamba kinachofanya mwanaume awe kiongozi siyo majukumu yake, basi nisione tena huko mbele umehusianisha majukumu ya mwanaume na kuwa mtawala, tuende taratibu mwisho wa siku mbivu na mbichi zitajulikana tu
Unachanganya Mambo Tulishasema Kigezo cha Mwanaume kuwa Kiongozi ni Nguvu uwezo na Umadhubuti wake Ukilinganisha na Mwanamke Hatukusema kuwa Mwanaume ni kiongozi kwa Sababu ya Majukumu yake( kuhudumia Familia)
Ni wapi niliposema mwanamke hanufaiki na hayo majukumu hebu uwe unasoma ili uelewe siyo unasoma ili ubishe, nilisema hayo majukumu yanamnufaisha mwanaume mwenyewe zaidi kuliko mwanamke,
Sio kweli Majukumu ya mwanaume kuhudumia Familia ni Beneficial kwa Familia yake Hata kuliko kwake yeye mwenyewe. Wanaume Wanaweza Kununua Mavazi kwa Watoto na Mkewe na asijali kama yeye Hana.
Utii unazingatia mipaka. Kama ilivyo Rais ni Mtawala wa nchi nzima Lakini na yeye ana wazazi na Ndugu zake Wakubwa. Urais wake Kwa Watu hao(Wazazi wake) Sio Sawa na Urais Wake Kwa akina Sisi(Raia Wengine )Na Hii haimaanishi kuwa Kwa kufanya hivyo anakuwa sio Rais kamili.
Kama umeshindwa hoja unasema tu siyo unajifanya unachoma vichaka, vichaka vyenyewe uliviotesha mwenyewe, ila baada ya kuona vimekushinda unanisingizia eti mimi ndio nimejifichia humo..pathetic!!
Shida unanifanya nijadili Mambo kulingana na Upeo wako wa akili kuna vitu nikivijadili kisha akija mtu Mwengine kusoma ataona Na mimi pia sina akili kwa sababu naenda mbali kabisa na Mada na ndio maana nalazimika Kuchoma hivi vichaka.
Oohh kwahiyo sasa hivi unakubali kwamba wanalalamika sasa mbona mwanzo ulijifanya kukataa kwamba eti wanaume hawalalamiki,
Asili ya Maneno ni ya wanawake na asili ya vitendo ni kwa wanaume. Mwanaume Ni kiumbe makini.
Wewe ni Ushahidi wa namna gani wanawake wakiumizwa kihisia Maumivu hayo hudumu muda mrefu. POLE.
Hii Risala ulitakiwa uwape wadogo zako wajue Nafasi zao katika Jamii. Unaandika Vitu vizuri ambavyo Wanawake wa siku hizi hamtaki tena kuvifanya Mnachoona cha maana Ni kushindana na Wanaume Mitaani na Kwenye mitandao. Poor
Hizo kesi huwa zinahusu nini na ni ngapi kulinganisha kesi za kudai huduma za kiuchumi
Kesi za kupigwa na kufanyia ukatili hujawahi kuzisikia??
Single mothers unamaanisha??
Sasa mbona umeandika kana kwamba hao wanaume hiyo kazi yao ya ulinzi wanaifanya vyema hivi ni kwamba huwajui wanaume wa kizazi hiki,
Unawazungumzia Wanaume gani hapa.?? Kwanini Baadhi ya wanaume ambao wapo around you wanakufanya uone Wanaume wote tupo hivyo??

Kinachonisikitisha ni kwamba hampo fair Mnateka ajira zote na fursa za kiuchumi kisha vijana wa kiume wanakosa ajira wakipata Mashangazi wa kuwalea mnakuja kuwasema Wanaume wa siku hizi hamna kitu ni wanalelewa tuu. It's not fair.
Hii sio fair,,, Tabia za Wanawake kutanguliza pesa na kukosa upendo na kuona miili yao ni mtaji wa kupata pesa ndicho kilichotufikisha katika Jamii hii ya Sasa.
Bora umeamua kuvipunguza hivyo vichaka mwenyewe, maana ningefanya hivyo mimi ungesema nakimbia hoja, mimi naenda sambamba na wewe huwa sikimbii hoja
Shida yako Ninapotoa majibu ya hoja moja unatafuta kaupenyo kwenye lile jibu ndo unakomalia hapo unasahau kuwa Kuna Hoja tulikuwa tunaijadili kabla. Akili yako ni ya kijinga.
Feminism ni kama Ilivyo kwa waumini wa Dini kuna walioshika Sana dini na kuna wale wa kawaida alafu kuna wale wafia dini kabisa.

For your information Kuna Feminists Ambao wao Tendo la ndoa Baina ya mwanaume na Mwanamke Hawalikubali kwa sababu kuna aina furani ya submission anaitoa Mwanamke kwa mwanaume Ile Kubinuka sijui kukaa hivi na vile ni kama anajishusha Furani kwa mwanaume. Wao Ni bora wakasuguane wenyewe ila sio Kumbinukia Mwanaume kisha amchezee mwili wake. SIJUI KAMA LEVEL HIZI WEWE UMEFIKA??
Sasa si ndio nikakuambia ulete takwimu na ushahidi kuwa ndoa nyingi zinazovunjika ni zenye feminism
Hilo lipo wazi wadada wa haki sawa ndio Wengi ndoa zinawashinda.
Mdada mjuaji ambae anadhihilisha ujuaji mapema kama wewe ni Ngumu kuoelewa. Ila kuna wale Wanaoficha makucha wanaonekana Wife material Wanaolewa Siku wakiyatoa makucha yao Mwanaume Rijali hawezi kuvumilia.
Wewe ndio hujui mengi kuhusu feminism. Hizo ni sifa ambazo wadada kama ninyi lazima muwe nazo. Kwa sababu mnaambiwa mnatakiwa kuwa free with your sexuality.
Moja Jambo kukubaliwa sio hoja Kwa sababu Hata ushoga kuna Watu wanaukubali bali hata serikali zinaukubali.

Pili Feminism ilipoanzishwa haikuwa na lengo la kumfanya Mwanamke ni sawa na Mwanaume kwamba hakuna wa kumtawala mwenzake hili Lengo limekuja baada ya miaka mingi na ndio Ufeminism tunaoukataa.
Unakutana na wanaume wa Hovyo always nina mashaka hata kazi unayofanya. Haya unayoyasema Sio normal katika jamii ya kawaida hakuna mtu ambaye atajisifia mbele ya watu wake wa heshima kuwa yeye ni mlevi sijui ni malaya. Hayo ni kwa hao wanaume unaokutana nao wewe na sijui unakutanaga nao wapi!!!!
Yani unataka niprove kwako kwamba mimi nina ndoa hivi una akili kweli wewe sasa personal issues zangu zinakuhusu nini
Huna ndoa Hilo mbona linajulikana. Na kwako sio shida kwa sababu ndoa sio kipaumbele si ndio mnasemaga hivyo???
Sasa utazungumziaje Jambo la ndoa ambalo hujawahi kuli Experience.???

Upele wa jirani unakuwashia nini??
Hili mbona jibu lake lipo kwenye ile comment yangu na linajieleza nenda kanisome tena

Wewe haujui maana ya feminism, yani bado unashikilia kwamba mwanamke kubandika kucha ni feminism, nani aliyekuambia kwamba mwanamke kubandika kucha ni feminism
Wewe ndo hujui uhusiano wa feminism na female sexuality.
Ndio maana nikakuuliza
Acha uongo Jadda umeniuliza wapi?? Akili yako ya kijinga sana.
Waganga wa kienyeji Wanawake walikuwepo.
Jibu la swali lako hili umelitoa mwenyewe kwenye maelezo yako ya chini.
Chukua haya Maelezo peleka kule kwenye hoja yangu.
kigezo cha kumzaa ndio chenye nguvu,
Sasa mbona mimi nikisema utii unazingatia mahusiano yaliyopo baina ya pande mbili unakataa. Tatizo
ila wewe ukasema tu kwamba kigezo cha mwanaume kumtawala mwanamke ni nguvu na umadhubuti sasa kiuhalisia hicho kigezo hakichagui aina ya mahusiano,
Kwani kigezo cha huduma Kinachagua Mahusiano.?? Basi wazazi wamtii mtoto wao atakapokuwa anawahudumia.
Naomba unijibu hapa MTOTO AKIWA ANAWAHUDUMIA MAMA ZAKE NA SHANGAZI ZAKE SIJUI BIBI ZAKE. JEE HAO WANATAKIWA KUMTII HUYO KIJANA WAO??
Hiyo siyo hoja hoja ni kwamba wanawake wanaweza kufanya ambayo wanaume wanaweza huo utofauti wa kuyahimili unaletwa na binadamu wenyewe,
Unamaanisha Wanawake wanaweza kufanya physical works kama Wanaume??
kwa sababu hata ninyi kuna majukumu ya wanawake ambayo mnaweza kuyafanya ila hamuwezi kuyafanya kwa ufanisi kama wanawake mfano kulea
Nashukuru kujua kuwa Wanawake ni wafanisi katika kulea naomba nikuulize huo ufanisi umetokana na nini??. Na jee Jamii ya zamani iliposema kuwa Mwanamke abaki nyumbani kulea kosa lao lilikua wapi???
watoto lakini hutasikia wanawake wakijiit watawala kwa hilo, halafu kwanza kule juu umeuliza swali la kuashiria kwamba kinachomfanya mwanaume kuwa mtawala siyo majukumu yake kwahiyo sitegemei tena utahusisha haya majukumu na utawala wa mwanaume
Moja Kama Kulea ni Sifa ya kuwa Mtawala basi tangu enzi hizo jamii ingekubali kwamba Wanawake ndio watawala wa dunia kwa sababu wanalea na wanazaa watoto lakini haikuwa hivyo.

Pili kuna kitu umekisema majukumu sisi hakuna sehemu tumesema mwanaume anatawala kwa sababu ya majukumu yake aliyonayo TUMESEMA NI KWA SABABU YA NGUVU UWEZO NA UMADHUBUTI WAKE.
JAMII ILIKUBALIANA KUWA WANAWAKE WAFANYE KAZI ZA NYUMBANI KWA SABABU NI LIGHT WORKS NA WANAUME WAENDE NJEE KUFANYA KAZI NGUMU AMBAZO WANAWAKE AIDHA HAWATAZIWEZA AU WATAZIWEZA KWA TAABU.
UNALALAMIKA NINI??
Sasa kama shida ni watoto maana yake wanawake wasitoke kabisa wasiende hata kutafuta pesa wawe wamama wa nyumbani tu, lakini siyo kusingizia eti mitoko ya mara moja moja
Unapozungumzia mitoko ya mara moja moja unakusudia kule kwenda ofisini saa kumi na moja asubuhi na kurudi saa 12 jioni??
Wanawake ni wafanisi katika malezi ya watoto kama ulivyosema. Jee Mkitoka Na kwenda Kutafuta pesa malezi atasimamia nani??
Kukubalika kwa jambo sio hoja. Inategemea na huyo aliyelikubali akili yake ni kubwa Kiasi gani??
Moja ni Uongo kwamba wanawake Mafeminist wanalea Watoto wao Ninyi mpo busy kutafuta pesa watoto wanalelewa na Televisheni na mitandao.

Pili vitoto vya kiume vya single mom Feminist ukiziona vinatia huruma ni kama vitoto vya kike vile. Na vingi huishia kuingia kwenye Ushoga. Mnatuharibia vizazi kwa upumbavu wenu.
Malalamiko.
Akili yako MBOVU sana.
Sasa kama mnavumilia mbona mnaoongoza kulalamika ni nyie na kuvunja ndoa kila siku
Waonee Huruma wanawake wenzako wanaokuwa single mothers. Siku hizi nimesikia Wanaume hawaoi Walioachika.
Huna hoja.
Kila mtu anachokiwaza kiheshimiwe sio ndio?? Hata kama ni upumbavu.
Unataka kutuambia kuwa Kulikuwa na Wanaume ambao familia zao hazikuwa na Mfumo dume yaani kila Mmoja anajitawala??
Wewe ungekuwa siyo mbishi tusingefikia hapa, hata wewe pia ni mbishi tena bora mimi nabisha kwa facts, wewe unabisha kwa mihemko mradi tu usionekane umeshindwa huu mjadala kirahisi
Tatizo unahisi unajadiliana na underground.
Ndio mimi nasema maandiko siyo nature, ila watu wa dini ndio wanadai kwamba maandiko ni nature, sasa kwa hiyo kauli yako maana yake unaniunga mkono mimi
Kumbuka Tulipotoka hadi tumefikia hapa kisha Jenga hoja.
So

Sasa kuruka viwanja ni nini ni basic need au
Hakuna hoja ya msingi hapa.
Mwanaume akimzuia mkewe kutoka kwa sababu yenye mashiko na huyo mkewe akakataa je Mwanaume afanye nini??
Si ninyi mnaodai kwamba kwa sababu mwanaume na mwanamke hawako sawa kwenye maumbile tu basi hawatakiwi kuwa sawa kwenye mambo mengine yote
Poor
Ndio mhakikishe hamkwami kiuchumi sasa
Ona akili yako sasa. How can you guarantee Economic stability?? Wanawake kama ninyi Mna akili za maisha ya kinadharia mno. Mumeo asikwame kabisa!!!. Na ndio maana wengi mnaishia kuwa madanga.
Kama umeamua kutumia maandiko basi usichague yale yanayofavour jinsia yako tu, haya naomba niletee na maandiko ya mwanaume kula kwa jasho na kulisha na kutunza familia, halafu uniambie kwanini mwanamke hakuambiwa hayo
Tuanze na Maandiko hayo Usikimbie nimekuuliza unayazungumziaje hayo maandiko??

Hayo mengine wewe ndio unatakiwa uyalete kisha tuyajadili.
Ni wapi nimesema nafurahia talaka mimi naandika hali halisi iliyopo tu, kwani ni uongo kwamba watu hawapeani talaka kila siku, we vipi mbona unalazimisha kunipandikizia maneno
Sasa huoni kwamba kukua kwa feminism kunaendana na kukua kwa Talaka??
Umeongea Uongo wa kipuuzi.

Sexual arousal ni Hormonal vipi inahusiana na kukeketwa???
Kwamba kujielewa ni kabila, hadi watu wanaojielewa wapatikane mkoa fulani, we jamaa mbona unafurahisha sana
Hao wanaume mnaowataka ninyi Hawapo hakuna mwanaume ambae mkewe Atajipangia mwenyewe pakwenda na Cha kufanya alafu yeye atulie tuu labda kama unamlea.
Yote hayo ni majibu acha kukwepa hoja, nasisitiza rais samia siyo kielelezo cha namna wanawake wote duniani wanavyotakiwa kuwa, huo ni mtazamo wake binafsi na siyo sheria na wala haumfanyi kuwa sahihi au kuwa na akili kuliko wanawake wengine wote
Sasa wewe ulisema HAKUNA kwa herufi kubwa Mwanamke msomi akubali kuwa chini ya mumewe.
Siyo kuguarantee utii katika pesa bali huo ndio msingi wa utii wa mwanamke kwa mwanaume, yani wewe mtu hujamuumba wala hujamzaa unataka akutii kwa lipi
Anitii kwa sababu Mwanaume amefanywa kiongozi katika familia.
, hivi hata kwa akili ya kawaida tu wewe unaona hiyo inaingia akilini kweli..anyway wewe lazima ikuingie akilini kwa sababu ina maslahi kwako huwezi kutumia common sense kwenye jambo linalokufavour hata kama ni baya kwa mwingine au kwa ujumla
Jambo la Mwanamke kumtii mumewe lina Ubaya gani??
Wewe kuna hoja gani ngumu umeweka hapo hebu jistukie
Hujajibu hoja yangu yoyote kikamilifu hadi sasa.
Ndio endapo hiyo sababu itakuwa applicable to both parties hilo nimeshaeleza
Nakuliiza upande wa pili jee Mwanamke anatakiwa amkataze mumewe akitaka kutoka kama akiwa na sababu ya msingi?? Na jee huyo mwanaume akikataa Mwanamke anatakiwa afanye nini??
Duuh kwahiyo informal education, inakuwa defined kulingana na maisha ya jamii zetu za kiafrika tu, aise yani unapuyanga hadi unatia huruma
Informal Education ya Tanzania sio hiyo hiyo ya Amerika. Information Education is more related with culture and norms.
Huo sio uhalisia Waajiriwa wa serikali Wote hawana furaha kwa saabu Wanawatii maboss zao?? na wale wa sekta binafsi nao Hawana Furaha kwa sababu Wanawatii Wakubwa zao??. Akili yako ipo sawa sawa??
Huna hoja wewe

Okay kwahiyo mfano huyo mwanaume anamuwajibisha mkewe, na huyo mkewe hasikii bado anaendelea, je huyo mwanaume bado anatakiwa kuendelea kumpenda huyo mke wake
Mwanamke akiadabishwa asiposikia anapewa talaka huenda atajivunza akienda kwa Mwengine. Hoja yako ni ipi ??
Kwanza ni wapi niliposema kwamba mshahara ni huduma nioneshe
Unakataa tena??
Aise kwahiyo wewe unajua hao tu ndio mbwa pekee wenye mionekano mizuri, nikikuambia unitajie aina za mbwa unazijua kweli au ndio kwa hisani ya google, ndio maana nikakuambia usiishi kwa kukariri wapo mbwa wenye mionekano mizuri na ni hatari
Lete jina La specie hiyo tuone.

Pili kwani Google sio source ya information??
Unamuogopa kwa nini??
Sawa mbona huongelei na maandiko ya mume kumpenda na kumhudumia mkewe na kwanini mwanamke hakuambiwa afanye hayo kwa mumewe
Yalete hayo maandiko hapa tuyajadili sisi hatuamini maneno yako tunataka Maandiko kama mimi nilivyo nukuu maandiko.
Poor you hujaelewa nimetoa elimu kubwa may be kuliko Uwezo wako wa ku digest in short feminism haikuanzishwa mwaka 1848 kwa lengo la kumfananisha mwanaume na Mwanamke na nimeshafafanua tayari haya tunayoyaona ni gradual evolutional changes baada ya watu kuona Wanaweza kuipeleka jamii sehemu Furani kupitia Kuvuli cha feminism.
Haya hayakuwa malengo ya kuanzishwa kwa feminism mwaka 1848 kama unaushahidi ulete hapa.
 
watawatii vipi wakati nyi ndomnawapigia magoti badala ya wao ndo wawapigie magoti wakati wa kufunga ndoa,hamjui kuwa ile inanguvu kiroho?
 
Ulitumia nguvu nyingi sana kwa mtu ambaye ulipaswa kumjibu kwa comments mbili tu na kuachana nae....!!

Huyu mama anaonekana kabisa ni wale third wave feminists ambao wako kwenye denial.
 
Naona tayari umekuwa triggered lol! Kwani hujui positive and negative outcomes mpaka sasa, si tulisha maliza kipindi kile! Mbona unanirudisha nyuma? Mwanamke anatawaliwa ili afeel Secure mwanamke ni kama uwa you know what I mean? Ila kutokana na mentality iliyopo nowadays wanawake hamjui hata nature yenu, mnataka na nyie muwe masculine, so mna align kutawaliwa na utii ambao ni vitu viwili tofauti, feminists mna shida sana mnapenda kupinga vitu msivyovijua vimetengenezwa kama silaha kuwaangamiza.

Haya nimekujibu na wewe niambie what do you need out of this? Maana unataka sjui usawa ambao basically nature yenyewe haina usawa. Kuna polarity ambazo zinaifanya I survive. Wewe na wengine ambao bado mnacheza huo mchezo wa kupinga vitu natural huwa nawashangaa sana. So unataka mwanamke naye awe masculine ama? Unataka mwanamke awe na amri ndani ya nyumba? Unataka iweje labda?
 
Ulitumia nguvu nyingi sana kwa mtu ambaye ulipaswa kumjibu kwa comments mbili tu na kuachana nae....!!

Huyu mama anaonekana kabisa ni wale third wave feminists ambao wako kwenye denial.
Anashida kubwa sana huyo, yaani ni kama anatafta jibu la kwa nini ulimwengu una exist. Kuna vitu hadi scientists wamenyoosha mikono, kadri wanavyotafta wanazidi kuchanganyikiwa ila ukija kuangalia vipo na vina exist through generations.
 
Jambo la Mwanamke kumtii mumewe lina Ubaya gani??
Hapohapo ndo umemnasa, huyo anahisi utii ni udhaifu! Kuna kitu ambacho wanawake wa dizaini hii huwa wamepandikizwa psychologically na ufeminism wanashindwa kuona kuwa it's a natural thing. Ndo maana hakuna stability kwenye ndoa na mambo yanazidi kuwa mabaya kadri siku zinavyoenda. Mbona mabibi zetu hawakuwa hivi?
 
Hizo dini ulizozitaja ni kweli Wao wenyewe wanadai Mungu wao Yupo mbinguni na ni Dini ambazo zina Uhusiano furani Wa kimaandiko Kuhusu Dini Nyengine sidhani kama nazo Zinadai Mungu wao yupo mbinguni.
Zina uhusiano fulani wa kimaandiko lakini zinatofautiana kwenye mapokeo na kulingana na mapokeo hayo ukiangalia sifa za mungu wa kila dini kati ya hizo utagundua kwamba wanatofautiana, yani Jehova wa wakristo, Yahweh wa wayahudi, Allah wa waislamu na Jah wa rastafarians ni miungu minne tofauti na kila dini inadai kwamba mungu wao ndio superior na ndio yuko mbinguni, sasa ndio nikakuambia unatakiwa uthibitishe pasi na shaka kwamba mungu wa dini yako ndio yuko mbinguni na si wa dini nyingine
Hoja sio yeye Kujua fertile days zake hoja ni kuwa Kama asipopatikana Mwanaume hakuna namna Mwanamke anaweza Kupata mimba.
Ndio maana nikakuambia suala la wanaume wa kuzalisha kutopatikana ni nadharia, kwa sababu wanaume hawajawahi na hawawezi kukataa kuzalisha siku zote mwanaume huona fahari kuongeza na kuacha uzao wake bila kujali hali yake ya kiuchumi ndio maana hata wanaume masikini wana watoto, ndio nikakutolea na mfano kwamba huko ulaya ambako population inakuwa kwa kasi ndogo kwanini viongozi wao wanawabembeleza wanawake tu ndio wazae kwanini wasiwabembeleze na wanaume wakati hiyo process inahusisha wote
Unachanganya Mambo Tulishasema Kigezo cha Mwanaume kuwa Kiongozi ni Nguvu uwezo na Umadhubuti wake Ukilinganisha na Mwanamke Hatukusema kuwa Mwanaume ni kiongozi kwa Sababu ya Majukumu yake( kuhudumia Familia)
Ndio maana nikakuambia hicho kigezo cha nguvu na umadhubuti kinakataa hapo
Sio kweli Majukumu ya mwanaume kuhudumia Familia ni Beneficial kwa Familia yake Hata kuliko kwake yeye mwenyewe. Wanaume Wanaweza Kununua Mavazi kwa Watoto na Mkewe na asijali kama yeye Hana.
Acha kubadili gia wewe mwanzo ulinitajia majukumu ya kupigana vita na kuchimba visima ndio nikakuambia kwamba hayo majukumu hayana faida kwa familia yake tu bali pia kwa mwanaume mwenyewe na jamii nzima, kwa sababu kupigana vita ni kujilinda wewe mwenyewe na jamii yako na kuchimba visima ni kwa matumizi yako mwenyewe na jamii au familia yako, hayo mambo ya mavazi ndio umeyaibua sasa hivi na hata hivyo umekuwa too specific, kununua mavazi mara kwa mara inajulikana siyo kipaumbele kwa mwanaume haijalishi ana familia au hana kwanini usiongelee kiujumla tu kwamba zile pesa na mali anazotafuta, zina faida zaidi kwake mwenyewe kuliko kwa familia yake maana hata yeye mwenyewe mwanaume anazitumia au unataka kusema mwanaume akiwa hana familia ndio hatafuti pesa na mali
Wewe mbona unalazimisha kufananisha utii wa raia kwa rais na utii wa mwanamke kwa mwanaume wewe unaona hivyo vitu vinafanana kweli, nimekuambia kinachofanya watu wamtii rais ni kile cheo chake alichonacho (siyo jinsia) na huo utii unaletwa na uoga kwamba wasipotii vyombo vya dola vinaweza kuwashughulikia, lakini si kwamba hao watu wanakuwa wamependa kutii bali wamelazimika tu na bado nasisitiza kwamba utii wa aina hiyo siyo nature
Shida unanifanya nijadili Mambo kulingana na Upeo wako wa akili kuna vitu nikivijadili kisha akija mtu Mwengine kusoma ataona Na mimi pia sina akili kwa sababu naenda mbali kabisa na Mada na ndio maana nalazimika Kuchoma hivi vichaka.
Acha usanii wewe hakuna cha akili wala nini hivyo unavyoviita vichaka umevichoma baada ya kuona umeishiwa hoja, mbona mwanzo ulivikomalia kama kweli unaona hoja inatoka nje ya mada kwanini usiachane nayo tangu mwanzo, yani mwanzo unakomaa nayo unaishushia magazeti weee halafu ukiona umefika sehemu umekwama ndio unajua kwamba nimetoka nje ya mada unajifanya kuachana nayo
Asili ya Maneno ni ya wanawake na asili ya vitendo ni kwa wanaume. Mwanaume Ni kiumbe makini.
Sasa hizi porojo zako zinahusiana nini na hiyo hoja yangu hapo
Wewe ni Ushahidi wa namna gani wanawake wakiumizwa kihisia Maumivu hayo hudumu muda mrefu. POLE.
Hahaha masikini yani hii ndio defensive mechanism pekee mnayoitumia pale mnapoona mmeshindwa hoja baada ya kuambiwa ukweli mchungu, itoshe tu kusema wewe bado hujaijua saikolojia ya wanawake unalazimisha mawazo yako ndio yawe uhalisia, na mbaya zaidi hata saikolojia ya jinsia yako nayo bado hujaijua vizuri you lack a lot of information hata mimi ambaye siyo mwanaume nafahamu mambo mengi kukuzidi
Hii Risala ulitakiwa uwape wadogo zako wajue Nafasi zao katika Jamii. Unaandika Vitu vizuri ambavyo Wanawake wa siku hizi hamtaki tena kuvifanya Mnachoona cha maana Ni kushindana na Wanaume Mitaani na Kwenye mitandao. Poor
Ndio ifike mahali wanaume mjiulize kwanini wanawake hawataki tena kukaa kwenye hizo so called nafasi zao, yani wanaume wanakimbia majukumu halafu wanawake wakiamua kujiongeza mnaanza tena kulalamika kwamba hawakai kwenye nafasi zao, sasa kama jamii yenyewe imejaa wanaume wasiojielewa mnataka wanawake waendelee kukaa kwenye hizo nafasi zao kwa sababu zipi
Kesi za kupigwa na kufanyia ukatili hujawahi kuzisikia??
Zipo ndio maana nikasema asilimia kubwa ni kesi za huduma za kiuchumi kwa watoto wao waliotelekezwa, halafu hao wanaoenda kuripoti hizo kesi hayo ni malalamiko dhidi ya hao wanaume husika ili wawajibishwe, haya ninyi wanaume ambao hampigwi wala hamfanyiwi ukatili mbona malalamiko yenu ndio yamejaa humu mitandaoni kuliko ya wanawake
Single mothers unamaanisha??

Unawazungumzia Wanaume gani hapa.?? Kwanini Baadhi ya wanaume ambao wapo around you wanakufanya uone Wanaume wote tupo hivyo??
Wewe unajuaje kwamba mimi naongelea wanaume wanaonizunguka, hivi kwa dunia ya leo hii ambayo taarifa nyingi unaweza kuzipata kiganjani mwako unahitaji hadi uzungukwe na watu wa aina fulani ndio ujue kwamba watu wa aina hiyo wapo kweli, kwahiyo kama mimi sijawahi kukutana na shoga basi maana yake sitakiwi kuamini kwamba mashoga wapo ilihali taarifa kuhusu mashoga zimejaa humu mitandaoni..what kind of reasoning is this!!
Kinachonisikitisha ni kwamba hampo fair Mnateka ajira zote na fursa za kiuchumi kisha vijana wa kiume wanakosa ajira wakipata Mashangazi wa kuwalea mnakuja kuwasema Wanaume wa siku hizi hamna kitu ni wanalelewa tuu. It's not fair.
Duuh naona sasa umetoka kwenye hoja umeanza kulialia hizo ajira na fursa wanawake wamezitekaje kwamba wanafika tu kwenye hayo maofisi wanajipa hizo fursa na ajira na kwamba wanaume hamzipati au mko wachache humo maofisini kuliko wanawake au vipi, kwani wanawake si wanapitia michakato yote ya kupata hizo ajira na fursa au wao kazi zikitangazwa huwa wanaitwa tu moja kwa moja hawafanyiwi interview wala vetting, kwahiyo kama kuna wanawake wana vigezo kuliko wanaume unataka waachwe kwa sababu tu ni wanawake kwani hujui kwamba huu ni ulimwengu wa kibepari karibu kila kitu ni competition ninyi si mnadai kwamba mmewazidi wanawake akili na nguvu sasa mnashindwa nini kuziteka hizo ajira kwa kutumia hizo akili na nguvu zenu mlizonazo badala yake mnaishia kulialia..yani unajustify midume mizima kulelewa na mishangazi kwa visingizio vya kipuuzi halafu wanawake wasipowaheshimu mnadai eti wanashindana na ninyi..stupid!!
Hii sio fair,,, Tabia za Wanawake kutanguliza pesa na kukosa upendo na kuona miili yao ni mtaji wa kupata pesa ndicho kilichotufikisha katika Jamii hii ya Sasa.
Kama kuna jinsia ambayo haipo fair kwa nyenzie basi ni wanaume tena wenyewe huwa mna msemo wenu eti "everything is fair in war and love", mbona husemi tabia ya wanaume kuingia kwenye mahusiano kwa lengo la kupata ngono tu (wenyewe wanaita kupiga na kusepa) halafu baada ya hapo wanakuja kuwatukana wanawake kuwa hawafai kuolewa maana wametumika sana kwahiyo wanawake wanachofanya ni kureciprocate tu kulingana na tabia zenu, maana hili suala la wanawake kutanguliza pesa na kukosa mapenzi wala halina miaka mingi limeshika hatamu karne hii tu na wanawake wameamua kufanya hivyo sababu wameona hata wanaume wengi nao hawana mapenzi ya kweli na wanawake ndio walioonekana kulose sababu eti wanaume jinsia yao inawafavor
Shida yako Ninapotoa majibu ya hoja moja unatafuta kaupenyo kwenye lile jibu ndo unakomalia hapo unasahau kuwa Kuna Hoja tulikuwa tunaijadili kabla. Akili yako ni ya kijinga.
Hebu fuatilia huu mjadala halafu uone ni nani anayekomalia hoja za nje ya mada, mimi ninachofanya ni kutoa mifano ambayo inaendana na mada, ila wewe ukiona hoja imekushinda unakimbilia kusema eti nimetoka nje ya nada
Feminism ni kama Ilivyo kwa waumini wa Dini kuna walioshika Sana dini na kuna wale wa kawaida alafu kuna wale wafia dini kabisa.
Sasa wewe mwanzo uliicondemn feminism kama feminism, hakuna mahali ulipospecify kwamba feminism ya aina hii ni nzuri na ya aina hii ni mbaya, au umesahau ulipotoa zile kauli kwamba feminism ni upumbavu mara sijui feminism ni takataka..kuwa makini unapojenga hoja zako maana hadi sasa umeshapindisha maneno mara nyingi
Nani kakudanganya kwamba hiyo character ni feminism hivi wewe mbona unapenda kutunga nadharia zako unapata faida gani kupotosha, kwa taarifa yako hiyo ni sexual orientation tu haihusiani na feminism na haipo kwa wanawake tu, hata wanaume wapo ambao hawapendi kufanya ngono sasa hao nao tuwaite feminists au

Watu wa aina hiyo wanaitwa asexuals huwa hawana kabisa hisia za kingono hao wanaosuguana wenyewe ni lesbians na hiyo haihusiani na feminism, kwa sababu wasagaji wengi tu huwa wana wanaume zao na wana sifa zote za uanamke ikiwemo kuwatii waume zao, hao wasagaji wengi wao wanadai hufanya hiyo michezo sababu ndio wanafika sana kileleni maana wanaume zao hawawaridhishi sasa hiyo ni mada nyingine

Na pia kwa wanawake kutokuwa tayari kusubmit kwa wanaume kwenye suala la sex kuna makala kadhaa niliwahi kusoma kwamba hilo linahusiana na kuwa na uwezo mkubwa wa akili, yani mwanamke wa hivyo anakuwa anatumia logic zaidi kuliko hisia kwenye kila jambo yani yeye kila kitu lazima areason hafanyi jambo kwa sababu tu kila mtu anafanya, sasa habari kama hizi zimezagaa mitandaoni unashindwa kufuatilia ili uwe na taarifa sahihi unaishia kutunga nadharia zako
Hilo lipo wazi wadada wa haki sawa ndio Wengi ndoa zinawashinda.
Lipo wazi kwenye kichwa chako wewe na siyo uhalisia, nimekuambia usinilazimishe nijadili mawazo yako mufilisi, kama huwezi kujadili uhalisia basi katika vile vichaka ulivyojificha ambavyo unadai unachoma usisahau kuchoma na hiki
Mdada mjuaji ambae anadhihilisha ujuaji mapema kama wewe ni Ngumu kuoelewa. Ila kuna wale Wanaoficha makucha wanaonekana Wife material Wanaolewa Siku wakiyatoa makucha yao Mwanaume Rijali hawezi kuvumilia.
Mwanaume rijali ni nani kwa mtazamo wako
Wewe ndio hujui mengi kuhusu feminism. Hizo ni sifa ambazo wadada kama ninyi lazima muwe nazo. Kwa sababu mnaambiwa mnatakiwa kuwa free with your sexuality.
Hebu nioneshe ni wapi panaposema kwamba feminism ni wanawake kubandika makucha na kujipost mitandaoni, nikikuuliza wewe ulishawahi kuniona wapi kiasi cha kujua kwamba na mimi nina sifa kama hizo za kubandika makucha na kujipost mitandaoni, kwa sababu kama umeweza kuandika huu uongo wako kuhusu mimi ilihali hunifahamu sasa utakuwa umeandika uongo kuhusu mangapi kwenye hii mada
Moja Jambo kukubaliwa sio hoja Kwa sababu Hata ushoga kuna Watu wanaukubali bali hata serikali zinaukubali.
Hoja siyo kukubaliwa tu bali umekubaliwa na nani kama ushoga ungekuwa umekubaliwa kiasi hicho basi wanaume wengi mngeukubali kama ambavyo wanawake wengi wameikubali feminism, na kama kweli ushoga ungekuwa umekubaliwa kiasi hicho basi wanaume msingeupinga nilitegemea upingwe zaidi na wanawake kama ambavyo wanaopinga zaidi feminism ni wanaume, wewe unalazimisha kuzifananisha kwa kigezo kimoja tu kwamba eti zote ni agenda zinazofadhiliwa na wazungu na ndio maana nikakupa ule mfano kwamba ni sawa na kusema eti physics, chemistry, na biology ni kitu kimoja kwa sababu tu zote ni science sasa ndivyo namna wewe ulivyoijenga hiyo hoja yako
Pili Feminism ilipoanzishwa haikuwa na lengo la kumfanya Mwanamke ni sawa na Mwanaume kwamba hakuna wa kumtawala mwenzake hili Lengo limekuja baada ya miaka mingi na ndio Ufeminism tunaoukataa.
Wanawake walianza kudai usawa pale walipoanza kutoka kupata elimu na ajira na kuanza kuwa na uwezo wa kutafuta na kumiliki pesa na mali zao wenyewe, kwaiyo wewe unaona kwamba feminism haikuwa na lengo la kumfanya mwanamke awe sawa na mwanaume kwa sababu hawakudai elimu na ajira in the first place, na mimi hoja yangu ni kwamba mwanaume anatakiwa kuwa mtawala endapo mke wake ni mama wa nyumbani na yeye ndiye anayemhudumia kwa kila kitu kiuchumi
Hili nimeshakujibu kule juu wewe reasoning yako bado iko chini sana, hebu uwe unapitapita mitandaoni na kusoma upumbavu wa wanaume wenzio halafu ndio urudi hapa tuje tubishane kuhusu hili, maana hapa nahisi kama vile nabishana na mlugaluga wa kijijini asiyejua uhalisia ukoje kwenye jamii yani hata watu wakisoma hapa watajua nani anaongea uhalisia na nani anaongea kulingana na watu waliomzunguka au anaokutana nao tu
Huna ndoa Hilo mbona linajulikana. Na kwako sio shida kwa sababu ndoa sio kipaumbele si ndio mnasemaga hivyo???
Kama umeweza kunizushia kuhusu hili tena kwa ujasiri kabisa kana kwamba unanifahamu je utakuwa umezusha mangapi hapa, okay mimi kuolewa au kutokuolewa kunahusiana nini na hii mada kwani marital status yangu ndio inaamua kwamba hoja ninazoandika humu ni za ukweli au uongo, halafu nikikuambia unatafuta vichaka vya kujifichia unabisha wewe mbona mimi hakuna mahali nimekuongelea wewe kuhusu maisha yako binafsi umeona jinsi unavyotafuta njia za kukwepa hoja
Sasa utazungumziaje Jambo la ndoa ambalo hujawahi kuli Experience.???
Aise yani kwa dunia ya leo yenye utandawazi unataka kusema kwamba mtu kuzungumzia mambo ya siasa au sanaa ni mpaka awe mwanasiasa au msanii, au mtu kuzungumzia mambo ya kazi au biashara ni mpaka awe mfanyakazi au mfanyabiashara, your level of stupidity is out of proportion
Upele wa jirani unakuwashia nini??
Pathetic!!
Wewe ndo hujui uhusiano wa feminism na female sexuality.
Hadi sasa nina uhakika hata wewe mwenyewe kichwani mwako umeshajua ni anayejua na ni nani aisyejua, ila hapa lazima ujitutumie kubisha mradi tu usionekane umeshindwa hoja, lakini ni wazi huna hoja yoyote ya maana mpaka sasa unazidi kujivua nguo tu kwa kudhihirisha upeo wako mdogo wa kufikiri na kupambanua hoja
Acha uongo Jadda umeniuliza wapi?? Akili yako ya kijinga sana.

Waganga wa kienyeji Wanawake walikuwepo.
Sasa huo uganga wa kienyeji waliufanyia wapi na waliwafanyia kina nani
Hawatakiwi kumtii kwa sababu siyo jukumu lake kuwahudumia hao watu bali ni hiyari yake au unaweza ukaniambia ni wapi palipoandikwa kwamba ni lazima mtoto awahudumie wazazi wake au ndugu na jamaa zake, halafu sijajua ni huduma gani hiyo unayozungumzia maana usije ukawa unazungumzia ile ya kuwapa pesa kidogo mara moja moja kama ambavyo unaweza kumsaidia mtu yeyote yule hata rafiki tu, huduma inayohusika hapa ni ile ya wao kuwa chini ya himaya yako na kukutegemea kwa kila kitu kuanzia kula, kulala, kuvaa na matumizi mengine na kama ni hivyo basi hawatawajibika kukutii bali pia hawawezi kukutawala kwa maana ya wewe kulazimika kutii amri wanazokupa tofauti na wewe ukiwa unawategemea kwahiyo bado hakuna uhusiano na utawala wa mwanaume kwa mwanamke
Unamaanisha Wanawake wanaweza kufanya physical works kama Wanaume??
Ndio kwani wewe hujawahi kuwaona wanawake wa aina hiyo
Nashukuru kujua kuwa Wanawake ni wafanisi katika kulea naomba nikuulize huo ufanisi umetokana na nini??. Na jee Jamii ya zamani iliposema kuwa Mwanamke abaki nyumbani kulea kosa lao lilikua wapi???
Kosa siyo mwanamke kubaki nyumbani kulea, kosa ni kulazimisha kumtawala kwa kisingizio kwamba yeye anabaki nyumbani kulea tu, yani ni kana kwamba jukumu la kulea ni jukumu duni
Moja Kama Kulea ni Sifa ya kuwa Mtawala basi tangu enzi hizo jamii ingekubali kwamba Wanawake ndio watawala wa dunia kwa sababu wanalea na wanazaa watoto lakini haikuwa hivyo.
Ni kwa sababu wanaume walitumia hiyo advantage ya kuwazidi nguvu wanawake kuwatawala na kuweka vigezo ambavyo vingewafavour wao kuwa watawala, na hakuna mahali nimesema kwamba kuzaa lazima iwe sifa ya kuwa mtawala hebu acha kuwa na kichwa kigumu asee, mimi nilisema siyo sawa kujipa utawala kwa kuzingatia vigezo vya kimaumbile ambavyo mwenzako hana na hakuchagua kutokuwa navyo, ndio nikasema kwamba ninyi kuona eti mnastahili kuwa watawala kwa sababu ya nguvu za mwili (ambalo ni kimaumbile) ni sawa na wanawake nao kusema wanastahili kuwa watawala kwa sababu ya kubeba mimba na kuzaa, sasa kama mnaona hicho kigezo hakimake sense basi hata hicho kigezo chenu pia hakimake sense vile vile
Pili kuna kitu umekisema majukumu sisi hakuna sehemu tumesema mwanaume anatawala kwa sababu ya majukumu yake aliyonayo TUMESEMA NI KWA SABABU YA NGUVU UWEZO NA UMADHUBUTI WAKE.
Sasa hicho kigezo chako automatically kinakataa, mwanaume anamtawala mwanamke kwa kigezo cha jukumu la kuhudumia familia tu, na si hayo majukumu mengine ya kutafutiza eti kupambana na majambazi sijui kupigana vita
JAMII ILIKUBALIANA KUWA WANAWAKE WAFANYE KAZI ZA NYUMBANI KWA SABABU NI LIGHT WORKS NA WANAUME WAENDE NJEE KUFANYA KAZI NGUMU AMBAZO WANAWAKE AIDHA HAWATAZIWEZA AU WATAZIWEZA KWA TAABU.
Ndio lakini huo mgawanyo ulitokana na utofauti wa kimaumbile jambo ambalo ni natural na ndio maana nikasema ugumu au urahisi wa kazi unategemea na maumbile ya mtu, kama wanawake nao wangekuwa na maumbo yenye nguvu kama wanaume basi bila shaka nao wangefanya hizo kazi sawa sawa na wanaume na hata hizo kazi ambazo unadai ni light works kwa wanaume ni ngumu mfano kulea watoto, ndio maana nikasema siyo sawa kujipa utawala kwa kuzingatia mgawanyo wa majukumu unaotokana na maumbile ambayo mwenzako hana yani kufanya hivyo maana yake unayaona majukumu yako ndio ya muhimu kuliko ya mwenzako
UNALALAMIKA NINI??

Unapozungumzia mitoko ya mara moja moja unakusudia kule kwenda ofisini saa kumi na moja asubuhi na kurudi saa 12 jioni??
Hapa hata wewe mwenyewe sijui kama umeelewa hiki ulichoandika
Wanawake ni wafanisi katika malezi ya watoto kama ulivyosema. Jee Mkitoka Na kwenda Kutafuta pesa malezi atasimamia nani??
Vipi na baba akiwatelekeza au akifariki huduma za watoto atasimamia nani
Kukubalika kwa jambo sio hoja. Inategemea na huyo aliyelikubali akili yake ni kubwa Kiasi gani??
Oohh kwahiyo wewe ndio unayeamua kiwango cha akili ya mtu kulingana na fikira ulizozijenga wewe juu ya kile anachokikubali
Moja ni Uongo kwamba wanawake Mafeminist wanalea Watoto wao Ninyi mpo busy kutafuta pesa watoto wanalelewa na Televisheni na mitandao.
Acheni hizi propaganda mnaexaggerate sana haya mambo tangu lini kutafuta pesa kukawa sababu ya kushindwa kulea watoto, kwani hao wazazi wanapoenda kutafuta hizo pesa huwa wanapotelea huko huko maofisini hawarudi majumbani au, jukumu la kulea watoto wakiwa wadogo ni la mama ila jukumu la kushape tabia na maadili ya watoto ni la wote, lakini cha ajabu wanaume mmewasukumizia hili jukumu wanawake kwa visingizio vya kipumbavu halafu watoto wakiharibikiwa mnawatupia lawama wanawake ilihali miaka yote mnaishi nyumba moja na watoto wenu, ukiachilia mbali wale wapumbavu wengine ambao wanaamua kukimbia majukumu na kutelekeza kabisa watoto
Pili vitoto vya kiume vya single mom Feminist ukiziona vinatia huruma ni kama vitoto vya kike vile. Na vingi huishia kuingia kwenye Ushoga. Mnatuharibia vizazi kwa upumbavu wenu.
Aise kwahiyo mashoga wote wamelelewa na feminists na kwamba watoto wa kiume wote waliolelewa na feminists wamekuwa mashoga siyo, vipi na ile mitoto milevi, mivibaka, mijambazi, mizinzi, nk ambayo imelelewa na wazazi wote wawili, au kwenu ushoga pekee ndio mbaya hayo maovu mengine yote yanayoharibu jamii hamyaoni
Malalamiko.

Akili yako MBOVU sana.

Waonee Huruma wanawake wenzako wanaokuwa single mothers. Siku hizi nimesikia Wanaume hawaoi Walioachika.
Si unaona sasa unaanza hivi hivi halafu baadaye ukiona umebanwa unakuja kubadili gia angani, kuna wanawake kila siku wanaachika na wanaolewa tena hasa waislam ambao wanadai dini yao inaruhusu talaka, basi hapa utakuja kusema kwamba wanaolewa ila wakigundulika waliachika basi wanaachika tena maana wanaume rijali hawawezi kuvumilia wanawake walioachika..hahahaaa!!
Huna hoja.

Kila mtu anachokiwaza kiheshimiwe sio ndio?? Hata kama ni upumbavu.
Ndio kama nyie mnavyotaka upumbavu wenu wa kulazimisha wanawake wawatii uheshimiwe
Unataka kutuambia kuwa Kulikuwa na Wanaume ambao familia zao hazikuwa na Mfumo dume yaani kila Mmoja anajitawala??
Hapana bali hao wanaume ni wale ambao hawakuwa na tabia za hovyo kama walizokuwa nazo wanaume wengi mfano ulevi na unyanyasaji, pamoja na kwamba zamani ilikuwa kawaida wanaume kuoa wake wengi ila kuna few exceptions ambao walioa mke mmoja, na kuna ambao walikuwa wanaishi vizuri tu na wake zao wala hawaleti ubabe wa kijinga eti kwa sababu tu ni wanaume so kwa wanaume kama hao ndio wanawake walikuwa na furaha
Tatizo unahisi unajadiliana na underground.
Wewe ndiye unahisi unajadiliana na underground yani kwa kifupi ulipoanza kubishana na mimi ulinichukulia poa, mimi siku zote ninapoanza kubishana na mtu huwa namchukulia kama anajua mengi kuhusu hiyo mada ndio maana kaamua kuingia kwenye hayo mabishano, kadiri anavyozidi kuwasilisha hoja zake ndio itanionesha kama anafaa kuendelea kuwekwa kwenye kundi la wanaojua au ndio kavamia fani..sasa hata wewe mwanzo ulivyoanza kwa mbwembwe nilidhani unajua unachokiongelea ila kadiri ninavyozidi kubishana na wewe ndivyo ninavyozidi kuona jinsi gani ulivyo mweupe kichwani kuhusu mada kama hizi
Kumbuka Tulipotoka hadi tumefikia hapa kisha Jenga hoja.

Hakuna hoja ya msingi hapa.

Mwanaume akimzuia mkewe kutoka kwa sababu yenye mashiko na huyo mkewe akakataa je Mwanaume afanye nini??
Kama ni sababu yenye mashiko siyo rahisi mwanamke kukataa, ukiona mwanamke kakataa ujue hiyo sababu haina mashiko, hivyo hutakiwi kumfanya chochote zaidi ya kumuacha aende au kutoa sababu yenye mashiko ili akuelewe
Poor

Ona akili yako sasa. How can you guarantee Economic stability?? Wanawake kama ninyi Mna akili za maisha ya kinadharia mno. Mumeo asikwame kabisa!!!. Na ndio maana wengi mnaishia kuwa madanga.
Kwanza hujui hata unachokisimamia kule juu umetoka kusisitiza kwamba wanawake hawatakiwi kutoka kuenda kutafuta pesa bali wanatakiwa wabaki nyumbani wahangaike na malezi ya watoto, hapa tena umeandika kana kwamba mwanaume akikwama kiuchumi basi mwanamke ndio anatakiwa amsaidie kusukuma gurudumu la kutunza familia hadi pale mwanaume atakapokaa sawa, sasa kama unataka mwanamke akae nyumbani alee tu watoto hizo pesa za kumsaidia mumewe akikwama atazitoa wapi na hapo sasa ndipo tunarudi kwenye ile hoja yangu kwamba kama mwanamke ni mama wa nyumbani huyo mume akikwama kiuchumi anafanyaje
Tuanze na Maandiko hayo Usikimbie nimekuuliza unayazungumziaje hayo maandiko??
Sasa ni wapi nimekimbia kwani hayo maandiko si yapo kama yalivyo na yanaeleweka au ulitaka niyazungumzieje, yani hata ukikimbilia kwenye maandiko bado hoja yangu inabaki pale pale kwamba utawala wa mwanaume kwa mwanamke unaambatana na majukumu ya mwanaume kuhudumia familia, kama ambavyo mwanamke kaambiwa amtii mwanaume ndivyo mwanaume alivyoambiwa ale kwa jasho na ahudumie familia ndio maana nikakuuliza kwanini wanawake hawakuambiwa wafanye hayo
Hayo mengine wewe ndio unatakiwa uyalete kisha tuyajadili.

Sasa huoni kwamba kukua kwa feminism kunaendana na kukua kwa Talaka??
Kama ukuaji wa talaka unaendana na ukuaji wa feminism basi tatizo halipo kwa wanawake, tatizo lipo kwa wanaume kukataa kukubaliana na reality na kuendelea kuishi kwenye illusions, somebody needs to give you men a reality check and it's got to be women ninyi kushindwa kukubali ukweli ni tatizo lenu siyo tatizo la wanawake
Umeongea Uongo wa kipuuzi.

Sexual arousal ni Hormonal vipi inahusiana na kukeketwa???
Hebu acha kuongelea haya mambo kama huyajui unazidi kujiaibisha tu hapa, kiungo kinachochochea hamu ya tendo kwa mwanamke na kumfanya aenjoy tendo ni ile clitoris, ndio maana kuna hao wasagaji ambao wanafika kileleni kwa kusuguana hivyo viungo tu na hata baadhi ya wanaume husema kuna wanawake wanafika kileleni kwa kuchezewa hicho kiungo tu hata kabla ya kuingiziwa uume, kwahiyo wewe unadhani nje ya hiyo sababu ni ipi sababu iliyofanya wanawake wawe wanakeketwa hebu nitajie faida hata moja anayopata mwanamke aliyekeketwa
Hao wanaume mnaowataka ninyi Hawapo hakuna mwanaume ambae mkewe Atajipangia mwenyewe pakwenda na Cha kufanya alafu yeye atulie tuu labda kama unamlea.
Wapo wanaume wengi tu wa hivyo na wanajielewa wala hawalelewi jambo kama hujawahi kuliona au kulisikia haimaanishi kwamba halipo, au pengine unaweza ukawa unafahamu kwamba hilo jambo lipo ila hapa utajifanya kubisha ili tu utetee uongo wako, haya mfano ndio mkeo kapangiwa safari ya mkoani na boss wake na wewe hutaki aende unadhani hapo mkeo atamsikiliza nani
Sasa wewe ulisema HAKUNA kwa herufi kubwa Mwanamke msomi akubali kuwa chini ya mumewe.
Acha kunipandikizia maneno mbona nilisema kabisa kwamba "ukiona mwanamke ana elimu na ajira na amekubali kuwa chini ya mwanaume, ujue huyo mwanaume anatimiza majukumu yake ipasavyo bila kuhitaji msaada wa mke labda mke tu mwenyewe aamue kusaidia" au hukuona nilipoandika hivyo, pamoja na hilo bado nasisitiza kwamba huo mfano wa mama samia ni batili fullstop
Anitii kwa sababu Mwanaume amefanywa kiongozi katika familia.
Mwanaume amefanywa na nani kuwa kiongozi kwa hiko kigezo cha nguvu na umadhubuti
Jambo la Mwanamke kumtii mumewe lina Ubaya gani??
Kama lingekuwa zuri basi wanawake wasingepingana nalo, uzuri au ubaya wa jambo anaujua yule anayelifanya, wewe hutakiwi kumsemea lipi ni zuri au baya kwake kwa sababu naye ana hisia zake na utashi wake
Hujajibu hoja yangu yoyote kikamilifu hadi sasa.
Wewe kuamua kukataa majibu yangu kwa sababu zako binafsi haimaanishi kwamba mimi sijajibu hoja zako, actually ni wewe ndiye ambaye hujajibu hoja zangu hadi sasa yani unarukaruka tu kama bisi kikaangoni, nimekuambia tuende taratibu tu mwisho wa siku mbivu na mbichi zitajulikana
Nakuliiza upande wa pili jee Mwanamke anatakiwa amkataze mumewe akitaka kutoka kama akiwa na sababu ya msingi?? Na jee huyo mwanaume akikataa Mwanamke anatakiwa afanye nini??
Ndio kama mwanamke ana sababu ya msingi kwanini asimkataze mumewe kutoka, au wewe suala la kukatazana kuenda sehemu fulani unalichukuliaje, kama mwanaume akikataa basi ni either hajielewi au hiyo sababu siyo ya msingi kwahiyo mwanamke anatakiwa amuache aende tu
Informal Education ya Tanzania sio hiyo hiyo ya Amerika. Information Education is more related with culture and norms.
Informal education ni universal hakuna cha amerika wala tanzania, informal education ni ujuzi na maarifa kuhusiana na shughuli mbalimbali za kila siku, na rasilimali zilizopo kwenye mazingira yanayotuzunguka, hoja ni kwamba kwanini wanawake hawakupewa ujuzi na maarifa kama waliyokuwa wanapewa wanaume, mbona leo hii wanawake wanapewa ujuzi na maarifa sawa na wanaume na wanafanyia kazi vizuri tu
Huo sio uhalisia Waajiriwa wa serikali Wote hawana furaha kwa saabu Wanawatii maboss zao?? na wale wa sekta binafsi nao Hawana Furaha kwa sababu Wanawatii Wakubwa zao??. Akili yako ipo sawa sawa??
Si nimeshakuambia kinachowafanya wafurahie ni mshahara tu na si kingine, hakuna mtu anayeweza kumtii boss wake kama halipwi mshahara, na nasisitiza kwamba utii wa aina hiyo siyo nature
Mwanamke akiadabishwa asiposikia anapewa talaka huenda atajivunza akienda kwa Mwengine. Hoja yako ni ipi ??
Hoja yangu ni kwamba kama maandiko yanavyosema kuwa mwanamke amtii mumewe ndivyo vivyo hivyo pia yanasema mwanaume ampende mkewe, na wewe umesema kwamba utii wa mwanamke kwa mwanaume ni nature na kwa mantiki hiyo basi maana yake hata upendo wa mwanaume kwa mwanamke ni nature, kwahiyo hata kama mwanamke ni mjeuri na hatimizi majukumu yake mumewe anatakiwa aendelee kumpenda tu sasa akimpa talaka si maana yake hampendi tena na kumbuka maandiko yanasema mungu anachukia kuachana
Unakataa tena??

Lete jina La specie hiyo tuone.

Pili kwani Google sio source ya information??
Mimi nimesema kwamba utakuwa huzijui species za mbwa hadi uconsult google hakuna sehemu nimesema kwamba google siyo source ya information, nikikutajia majina ya hao mbwa una uhakika utakubaliana na mimi kwamba hao mbwa ni wazuri au ndio utabisha kwamba wewe kwa mtazamo wako unawaona ni wabaya (maana kumbuka uzuri upo machoni mwa mtazamaji), na kwa kuzingatia hilo suala la subjectivity kwenye uzuri basi siyo mbwa tu bali kuna wanyama wengi ambao ni wazuri lakini ni hatari
Unamuogopa kwa nini??
Hili tayari nimeshafafanua
Yalete hayo maandiko hapa tuyajadili sisi hatuamini maneno yako tunataka Maandiko kama mimi nilivyo nukuu maandiko.
Kama kweli ungekuwa unaijua dini na unayajua maandiko kama unavyojinasibu, basi usingesema kwamba hayo ni maneno yangu, nimeanza kuwa na mashaka hata na hiyo elimu yako ya dini

Kasome Mwanzo 3 : 17-19

Kasome 1 Timotheo 5 : 8
Yani unasingizia umetoa elimu kubwa ambayo mimi nimeshindwa kudigest wakati umekwepa swali langu ambalo kila nilipokuuliza ulisema nisubiri unakuja na majibu, cha kushangaza unakuja na mambo ya waves za feminism kana kwamba mimi nilikuambia siyajui hayo huku ukiacha kujibu swali langu nililokuuliza halafu nikikuambia unakwepa hoja na kutafuta vichaka vya kujifichia unakataa, bado nasisitiza ulisema kwamba "kila mwanamke anazaliwa na fikira za kutaka kutawaliwa na mwanaume ila hakuna mwanaume anayezaliwa na fikira za kutaka kutawaliwa na mwanamke na kwamba hiyo ni nature" sasa swali langu ni je kama ni hivyo feminism ilianzishwa na nani na kwa faida ya nani hili hujajibu hadi sasa
 
Duuh kwahiyo mwanamke kukataa kutawaliwa maana yake ndio anataka kuwa masculine, kijana hebu acha kukaza fuvu nimekuambia utii wa mwanamke kwa mwanaume umejengwa katika msingi wa huduma za kiuchumi tu na si nje ya hapo sasa ambacho huelewi ni nini, kama wanawake wangekuwa wanafeel hiyo security kwanini waanze kuresist kutawaliwa kwani wenyewe wanawake hawana hisia na utashi wa kujua kipi kinawapa furaha na kipi kinawapa huzuni maishani mwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…