Utii wa wanawake wa kisasa

Utii wa wanawake wa kisasa

Haisaidii kwa upande wako sababu wanaodhurika mwisho wa siku ni wanawake. Tazama maisha ya kitaa kwasasa ni akina nani wanateseka na maisha magumu ya kitaa?

View: https://www.instagram.com/reel/C5CXj6FseYu/?igsh=MWJ0ZWU0YjB1em42bw==

Yaani we mpumbavu na wapumbavu wenzio mnaojiita wanaume na mna tabia kama za kwenye hiyo post hapo, submission mtaiskia kwenye radio. Wanaume wengi hamna akili! Oneni huyu mpuuzi mwenzenu kachukua savings za mkewe kaenda kununua gari na hata bongo mpo wenye akili hizi ndo maana hatutaki mtuongoze vilaza wakubwa!
 
Naona mnawapigia mbuzi gitaa, waacheni watakutana nayo huko mbele,nchi ya ulaya wamejaza kibao tiktok wanalamika " wanaume wamepunguza kutongoza........wanaume wanawaogopa..........mara hawana bahati............" ila hajui tatizo ni wao.US ishatabiriwa ikifika 2030,zaidi ya asilimia 50 ya wanawake watakuwa single na hawana watoto,sababu ni zile zile ujuaji,heshimaless nk.Kuna wanawake na hela zao 30+ wanatafuta hata mwanaumee wa kumwambia pole ,pindi apitiapo magumu ila hawamuoni.

Maisha yao huishiaga kutembea na waume za watu, vijana wadogo huku wakihudumia penzi kwa hela zao na vijana wakipiga wanakaa kidogo wanasepa.
 
Mbona Unanisingizia yale unayoyafanya wewe. Uzuri hapa kila Mtu anaona Kwamba nani Anatoa Hoja Na Nani Anatunga Maneno.
Kama kuna mtu ataona kwamba wewe ndiye unayetoa hoja hapa basi naye ni either hana akili kama wewe, au ndio wale wazee wa kutetea lolote linalohusu wanaume hata kama ni ujinga, maana mpaka sasa kuna sehemu nyingi sana nimeshakukosoa na hujajibu tena na nyingine unarudia kujibu yale yale
Nithibitishe Kwa Namna Gani Tena Nimekwambia Wahindu Ng'ombe kwao ni Mungu Jee Ng'ombe Yupo Mbinguni?? Kuna watu Mungu wao ni Moto Je Moto uko mbinguni?? Hao Waroma Unawazushia Maneno na Wanakushangaa Wao wenyewe. (Aibu)
Sasa mbona hujajibu swali langu kwahiyo hapo ndio umeshathibitisha kwamba mungu wako ndio yuko mbinguni, waroma nawazushia kivipi wakati wewe kwa mujibu wako ni kwamba kama dini inaabudu sanamu basi mungu wao hayuko mbinguni, unashindwa kujua kwamba kwa wengine hayo masanamu ni symbol ya miungu yao tu
Hakuna Hoja Hapa.

kama mwanamke Akitaka Watoto watatu alafu Mume akataka wawili itakuaje??
Hivi si nimekuambia uwe unasoma kwanza aya nzima hadi mwisho kisha ndio ujibu, unaona kama hapo umeuliza swali ambalo jibu lake lilikuwepo kwenye hiyo hiyo aya kwa chini yake, unajaza magazeti bure kwa maswali ya kipuuzi ambayo majibu yake nimeshakupa na yanaeleweka vizuri tu
Nasisitiza Suala la kuzaa ni Jukumu Shirikishi. Hakuna anaeweza kulifanikisha Pekee yake.

Nadharia.

Nadharia.

Hahahaha kwaiyo ukijitegesha Alafu nikiondoka Utapata Mimba??
Ukishaondoka kuenda wapi
Tatizo lako wewe ulilisema jambo la kuzaa kana kwamba Mwanaume Hausiki kabisa. Sisi hatukatai kuwa Mama ana Play role kubwa katika Suala la Kuzaliwa Watoto. Na ndio maana Tangu mwanzo tulishasema Jambo Hili linafanya Kina Mama wapendwe zaidi na watoto wao ila sio kigezo cha kuwa kiongozi.
Sasa kwanini hilo jukumu kubwa la mama kuzaa haliwezi kumfanya awe kiongozi, kwani hao watoto anajizalia yeye mwenyewe hadi useme kwamba anatakiwa tu kupendwa na watoto wake, kwanini na majukumu ya baba yasimfanye apendwe na watoto kwanini yenyewe ndio yamfanye awe kiongozi
Kwani nani amesema haina athari??

Unageuka tena wewe si ulisema Majukumu ya mwanaume yanamnufaisha zaidi yeye mwenyewe??
Ndio kwani unapofanya hayo majukumu wewe hunufaiki nayo au
Aisee kazi ipo.
Hapa tunazungumzia kitendo cha wewe kuwa na uwezo wa kumtoa polini na kumuweka Zoo. Bila yeye kufanya lolote. Masuala ya huduma yamekujaje?? Kwani hao wanyama Usipowapa hizo huduma Hapo zoo watafanyaje??? Watakupiga?? Unachekesha.
Hebu jaribu kumuweka mnyama zoo halafu umnyime chakula na mengineyo uone atakufanyaje, maana naona sasa unauliza maswali ya kipumbavu ambayo hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kuuliza, wewe huchekeshi tu bali pia unasikitisha sana
Hakuna mnyama ambae hawezi kuwekwa zoo.. kwanza hapa hatuongelei masuala ya wanyama mana naona umehama kabisa. Mind you Zoo sio yale mabanda ya kufungia tumbili pekee acha ujuha.
Wewe akili yako ndio inakutuma kwamba zoo ni yale mabanda maana mimi hakuna sehemu nimesema hivyo, nani kakudanganya kwamba hakuna wanyama ambao hawawezi kuwekwa zoo hebu acha uvivu wa kufikiri fanya research ndio uje uongee huu uongo wako, sasa hivi nikiona unabisha jibu langu na kuleta jibu lako la uongo nakuacha unless uthibitishe kwa hoja usinilazimishe nijadili mawazo yako
Wanaowasakama wanawake wasipoolewa ni Wanaume? Wanaowasakama wanawake wakiachika ni Wanaume?? Hivi unatujua Sisi wanaume.!!! (Sisi huwa hatuna muda na mambo ya kipuuzi)
Huwa mnajifanya hamna muda na mambo ya kipuuzi ya wanawake, ila pita humu mitandaoni uone mada za kuwatukana na kuwadhalilisha wanawake zinatoka kwa jinsia gani, hayo yote ni kwa sababu mnajua mwanamke akiwa na tabia mbovu inamuathiri mwanaume kisaikolojia kama utabisha na hili basi rudi darasani
Mi nachojua kesi nyingi katika madawati ya kijinsia ni za wanawake alafu unatuambia mmeacha malalamiko. Ajabu.
Hivi unaelewa unachoandika kweli sasa kwani kesi za wanawake kwenye madawati zinahusu tabia mbovu za wanaume, si huwa zinahusu huduma za kiuchumi au mgawanyo wa mali na hilo linadhihirisha kwamba umuhimu wa mwanaume kwa mwanamke uko hapo tu huko kwingine mnadanganywa tu, mimi hapa naongelea malalamiko ya jinsia fulani dhidi ya tabia mbovu za jinsia nyingine ni wanaume ndio wanaongoza wewe unaniletea habari za madawati
Huu ni udhaifu na sio jambo la kawaida.
Siyo udhaifu hiyo ndio saikolojia ya binadamu hata wagonjwa wa ukimwi wanaposimangwa na kutengwa na jamii, huwa wanaanza kujiona hawafai lakini si kwamba ni kweli hawafai bali ni watu wanaowazunguka ndio wanawafanya wajione hivyo, sasa ndivyo na wanawake hao wenye experience kama hizo wanavyojiona
Ndoa za Mafeminist ndio zinavunjika kwa wingi(mfano ulaya).
Wewe una takwimu gani zinazoonesha kwamba ndoa zinazovunjika kwa wingi ni za feminists tu, halafu sijui hata kama unajua kwamba feminists hawapo wanawake bali hata wanaume pia wapo feminists, na sijui kama umeshawahi hata kutembelea huko ulaya achilia mbali kuishi au na wewe ndio wale wazee wa "niamini mimi" maana hoja zako ndio zimejikita hapo
Huo ndio ukweli siku hizi wanawake wajuaji kama wewe mnazalishwa tuu.

Mind you ndoa zitaendelea kufungwa kwa sababu sio wanawake wote ni Wajuaji kama wewe pia hata Watu wajuaji kama wewe wakifika Umri wa jioni akili zinawaingia. (Kwaiyo hata wewe Tunakupa muda)
Sasa kama wanawake wote siyo wajuaji na ninyi mnaoa wanawake ambao siyo wajuaji kwanini sasa hizo ndoa hazina amani na nyingine zinavunjika, mimi nilitegemea kwamba kwa sababu mnaoa wanawake wife material kisha mnawaacha hawa wajuaji basi ndoa zenu zitakuwa na uhakika wa kudumu ila matokeo yake talaka kila siku, na kwanini wanawake waanze kutamani ndoa katika umri wa jioni kwanini wasitamani katika umri wa asubuhi kama ninyi wanaume unaweza kunipa jibu lililonyooka hapa
Sasa furaha ni kitu gani?? Bibi zetu tumeshuhudia maisha yao wakiwa na Furaha na kulidhika wewe unasema hiyo sio furaha sasa furaha kwako ni kitu gani??
Hapa umeamua tu kujitoa ufahamu
Sio kweli.

Tamaduni za Masuala ya mwanamke Pia walitunga Wanaume!!! au unahisi yale Wanayofundisha Kwenye unyago ni Vitabu vilitungwa na Wanaume?? (Tatizo hujapita kwenye Unyago ndio maana umekuwa Mjuaji)
Duuh hata kama historia huijui hivi kwa akili ya kawaida tu, unadhani wanawake wangeweza kujitungia tamaduni ambazo zinawaumiza na hazina faida yoyote kwao kwa lengo la kuwafurahisha wanaume tu, we jamaa mbona kama hata common sense tu inakushinda kuitumia
Swali lako hili na mengine kama hilo nitajibu.

Subiri.
Nasubiri
Kwaiyo Jamii zote zilikuwa na mambo mabaya??
Hayo mambo mabaya ni tafsiri yako wewe ila hayo yalionekana ndio uanaume na mwanaume usipoyafanya hayo basi unaonekana dhaifu kwa mkeo, na kuna mengine hadi leo yanaonekana ndio uanaume mfano ulevi na usaliti ni mara ngapi watu wanasema mwanamke kulewa na kusaliti ni vibaya, ila mwanaume kulewa na kusaliti ni sawa tu wakati kiuhalisia hayo ni mambo mabaya kwa jinsia zote
Ndoa zenye Furaha ni zile Za Pure women. Au zile za Mafeminist waliowaoa wanaume wao (yaani mwanaume analelewa) ila Ndoa ya feminist na Mwanaume Rijali Haiwezi kutoboa. Labda utupe mfano wa ndoa yako ( kwanza uitoe wapi!!!)
Oohh kwahiyo na wale wanawake wanaovumilia usaliti na unyanyasaji nao wana furaha, narudia wewe sasa hivi huna tena hoja bali umeamua tu kujitoa ufahamu, na kwa vile umeishiwa hoja naona sasa umeanza kuleta ad hominem personal attacks kana kwamba unanijua
Aisee kazi ipo. So negative mdada.
Speaking of the reality and not negativity
Mabinti walikuwa wanafunzwa malezi,, wanafunzwa kupika,, wanafunzwa Tendo la Ndoa kwa umahili,,, wanafunzwa Usafi wao kiujumla na wafunzwa nafasi zao katika familia. (Ndo maana siku hizi hamjui kupika) ,,,,Huo utumwa Walifunzwa vipi??
Wewe unaishi wapi huko ambako watu hawajui kupika, we jamaa mbona umekaa kinadharia sana, wewe kwako kujua kupika maana yake nini
Sasa ulitaka mwanamke afanye Shughuli gani zaidi?? Embu nitajie mfano wa shughuli ambayo angeweza mwanamke wa zamani kuifanya out ya kazi za nyumbani?? Ulitaka aende vitani?? U feminism Mzigo.
Duuh kwahiyo wewe nje ya shughuli za nyumbani shughuli nyingine unayoijua wewe ni vita tu kana kwamba huko vitani wanaume walikuwa wanaenda kila siku wakati vita ni suala la once in a life time, tena kuna wengine tangu wanazaliwa hadi wanakufa uzeeni hawajawahi hata kuexperience hizo vita sasa hilo nalo kwanini ulihesabia katika majukumu ya kila siku ya mwanaume, unaniuliza nilitaka mwanamke afanye shughuli gani zaidi kwani huoni dunia ya leo wanawake wanafanya nini wapo kwenye kila nyanja madaktari, wahandisi, walimu, wahasibu nk wapo kwenye siasa, majeshi, sanaa, michezo nk na wanafanya vizuri tu sasa kwanini zamani hawakufundishwa hayo unaweza ukanipa sababu
Hakuna mafahali wawili katika zizi moja.
Aise kwahiyo mwanamke naye atakuwa ni fahali
Baba akifariki Kiongozi wa familia Anakuwa Kaka mkubwa hili lipo wazi. (Zingatia Familia gani unayokusudia maana Mashangazi wao ni wa familia nyengine na wanakaka zao wakubwa)
Dooh kwahiyo kila familia watoto wakubwa ni wa kiume tu hakuna familia ambazo watoto wakubwa ni wa kike, halafu kumbuka hapa tunaongelea suala la nguvu na umadhubuti hatuongelei aina ya familia, mtoto wa kiume ana nguvu na umadhubuti kuliko ndugu au jamaa yake yoyote yule wa kike kwanini asiwatawale na hao sasa
Sasa hili si ndio jibu kuwa Mtoto hawezi Kutaka utiifu kwa Mama ake kwa Sababu Uhusiano wao sio sawa na Mahusiano ya mke na Mume. Nashukuru kwa kuelewa.
Sasa suala la nguvu na umadhubuti linahusiana nini na aina ya uhusiano uliopo baina ya mwanaume na mwanamke, okay labda swali langu niliweke hivi kinachomzuia mwanaume kuwatawala wanawake wengine tofauti na mkewe ni kipi hasa, yani kwanini hilo suala la nguvu na umadhubuti liapply kwenye ndoa tu na siyo kwenye uhusiano wa aina nyingine nipe jibu lilinyooka hapa
Unajibu kisha unauliza tena swali hilo hilo.

Unachanganya tena Wakati nilishakufundisha Kwenda vitani,, Kuchimba Visima,, sio Majukumu ya Kimaumbile. (Elewa)

Moja, Majukumu ya kimaumbile ya mwanamke ni Kutengeneza mayai, kubeba mimba,kuzaa,kunyonyesha, na majukumu ya kimaumbile ya mwanaume ni Kutengeneza mbegu ku erect kupeleka mbegu kwenye njia ya uzazi.

Hayo majukumu Mengine sio Majukumu ya Kimaumbile usichanganye vitu.

Kuna majukumu ya kimaumbile(Biological mfano kuzaa ku erect ),,majukumu ya kitabia mf kutongoza,,, majukumu ya kiuwezo (Ability related Roles ambazo ni Naturally selected mf kwenda vitani),,, Na Majukumu ya Kimakubaliano mf. Majukumu ya Rais.
(Usichanganye vitu.)
Sasa umeanza kuja ninapopataka kwahiyo kumbe unajua kwamba hayo majukumu siyo ya kimaumbile na kwamba jinsia yoyote inaweza kuyafanya sasa kwanini mnataka kuwatawala wanawake kwa sababu ya hayo, by the way siku hizi kuna wanawake wengi wanaingia kwenye majeshi na wengine wanakuwa hadi makomando na wanapigana vita na pia kuna wanawake wanafanya hizo kazi ngumu kama kuchimba visima kubeba zege ila mbona hawajataka kuwatawala kwa sababu hiyo, kwahiyo wanaume kuzalisha mbegu na kutungisha mimba mnaona ndio jukumu kubwa kuliko kubeba mimba na kuzaa kiasi cha kuwafanya ninyi ndio muwe watawala
Pili kazi za nyumbani wanaume wanafanya hakuna kazi ya nyumbani ambayo mwanaume hawezi kufanya. (Kama ipo nitajie.)
Tofautisha kati ya kuwa na uwezo wa kufanya na kufanya wanaume wengi wana uwezo wa kufanya hayo majukumu ila hawataki kuyafanya, tena wengi husema eti hayo ni majukumu ya kike mwanaume aliyeoa hawezi kufanya hayo na ukiona anafanya hayo ujue ni mume bwege mke wake anampanda kichwani, sasa labda nikuulize kwanini wanaume wengi pamoja na kuweza kufanya hayo majukumu bado hawapendi kuyafanya na wanataka wanawake ndio wawafanyie
Feminist mko wengi kwa data ipi?? Maana hata mashoga na wasagaji(LGPTQ+ Members) nao Watakwambia wapo wengi.

Nasisitiza sio kila kinachopata wafuasi ni kitu Sahihi. Nchi kama Ujerumani ushoga ni jambo la kawaida mno na ukionekana unapinga ushoga Ujerumani utakuwa na wakati mgumu mno jee Mashoga waseme ushoga ni jambo zuri kwa sababu haulazimishwi??

Mimi sizungumzii usawa katika Idadi nazungumzia Ukuaji na uungwaji mkono.
Pia wewe unaposema haifiki nusu una Data umeegemea au na wewe ni mlopokaji??
Hata kwa kuangalia hali halisi tu unaona kabisa ushoga unalazimishwa, kwa sababu idadi ya mashoga bado ni ndogo kulinganisha na wanaume rijali hili lifanyie research mwenyewe, lakini kwa upande wa feminists wanawake idadi ni kubwa kuliko wanawake ambao bado wanaunga mkono mfumo dume

Kama unabisha hili jiulize kwanini hata wale wanaounga mkono ushoga hawako tayari watoto wao wa kiume wawe mashoga, lakini wale wanaopinga feminism wanasomesha mabinti zao ili waje kujitegemea wakiolewa wasiende kuwa wamama wa nyumbani, maana mlivyo wabinafsi mnataka wake zenu tu ndio wawe watumwa kwenu ila hamtaki mabinti zenu wakawe watumwa kwa waume zao huko

Au wewe unaona karne hii kuna baba ambaye hataki binti yake asome, kama kweli wanaume mnachukia feminism acheni kusomesha mabinti zenu hii formal education maana hilo ndilo lengo la kwanza la feminism kwahiyo ili kuikwepa kabisa feminism msisomeshe mabinti zenu, waacheni wawe housegirls huko majumbani kwenu halafu wakifika miaka 18 hadi 20 waozesheni wakawe housewives huko kwa waume zao halafu mrudi mtupe mrejesho
Sisi tunasikiliza maneno yake kama wewe unamjua kiundani Rais Hongera.

Aisee Hongera kumbe kuna za chinichini za Rais Unazijua!!! ,,, unayajua maisha ya Ndani ya Rais!!! Hongera.
Aiseee yani kama kila mtu angekuwa anasikiliza maneno tu mtu anayosema kuhusu yeye, basi hata huko mahakamani watu wangekuwa hawafungwi, anyway nimekuambia tuishie hapa tafuta mfano mwingine
Wewe ndio unatunga maneno hadi unajistukia. Una akili za kitoto mno.

Hhahaahaha aiseee!!!!

Ni laana?? Aisee we unazungumia Jamii gani??

Mabinti walikuwa wanataka Wenyewe waolewe kwa faida za ndoa walizokuwa wanaziona haya unayoyafunga yanastaajabisha. Labda kama unazungumzia zile Jamii chache ambazo huwezi ku conclude kwa jamii nzima.
Walitaka waolewe kwa faida gani za ndoa walizokuwa wanaziona unaweza ukanitajia hizo faida wewe ndio maana nakuambia huna hoja, ila umeamua tu kujitoa ufahamu na kuukataa ukweli yani mimi nakufafanulia kwa kina kwanini zamani ndoa zilidumu hata kama wanawake hawakuwa na furaha, halafu wewe unaendelea kukomalia tu kwamba walikuwa na furaha kwa cheap na shallow points kama hizo yani huna sababu yoyote yenye uhalisia zaidi ya mawazo yako tu
Suala la Kuvumiliana hilo jambo la kimaisha Sababu kila mmoja ana mapungufu yake usidhani ninyi Wanawake ni malaika na nyinyi mna Vituko vyenu ambavyo Wanaume wanavumilia.
Wanawake wa zamani walikuwa na mapungufu gani ambayo yalikuwa yanawaumiza wanaume moja kwa moja, na kama wanawake wana hayo mapungufu kwanini sasa mnaendelea kuwaoa kumbuka kwa tamaduni zetu anayeamua ndoa ni mwanaume, hakuna mwanaume anayelazimishwa kuoa au kumuoa mwanamke wa aina fulani sasa kwanini mnaendelea kuoa wanawake wenye mapungufu ina maana ninyi hampendi kuwa na furaha
As long as Sio wanawake wote ni ma Feminist basi ndoa zitaendelea kufungwa lakini Idadi ya Talaka inazidi kuwa juu kwa Wale wanaojidai wajuaji.
Unaona sasa shida ilipo yani mnadai kwamba siyo wanawake wote ni mafeminist na kwamba ninyi mnaoa wife material tu, ila cha ajabu kila siku kuna talaka na ndoa zilizobaki zina migogoro sasa mna uhakika huwa hao wanawake mnaooa ni wife material au ndio mikwara na vitisho tu, halafu una uhakika na ushahidi gani kama ndoa zote zinazovunjika chanzo ni wanawake kuwa mafeminist tu
Naona unapinga katiba sasa. Kwaiyo huko ulaya Rais anashitakiwa?? Maana ninyi Ulaya ndio role model.
Wapi nimeipinga katiba, mimi nimekuambia hizo katiba wanaozitunga ni hao viongozi wenyewe, huwa hawawashirikishi wananchi wote bali wananchi huwa wanalazimika kufuata tu hizo sheria
Kwaiyo wewe unahuzuni hapo sababu Katiba imesema Rais hashitakiwi. U Feminism ni uwendawazimu.
Kijana mbona unapenda kukurupuka wewe ulisema kama rais ana makosa na mimi pia nikakujibu kama rais ana makosa, sasa kama rais anafanya makosa na wananchi wanajua hawawezi kumshitaki unadhani kuna mwananchi atakuwa na furaha na hilo, wewe huoni ndio maana nchi nyingine zenye uthubutu watu wanaandamana kila siku na kwingine majeshi yanapindua nchi au hizo nchi hazina katiba..sasa feminism imeingiaje hapo
Aisee mbona unatutukania Babu zetu!!!!
kwamba Babu zetu wote walikuwa Wanyanyasaji Mbona sisi tumeishi Nao Hatujayaona hayo unayoyasema. Labda nikuulize Babu yako alikuwa anampiga na kumnyanyasa Bibi yako???
Dooh kwahiyo kwako wewe unyanyasaji ni kupiga tu mtu una safari ndefu sana asee, kwahiyo wewe ukisikia unyanyasaji wa kisaikolojia huwa unaelewa nini au hata hauelewi kitu, maana kwa yote hayo niliyoelezea mtu mwenye upeo mkubwa angeshaelewa ni unyanyasaji wa aina gani ninaozungumzia hapa
Uzuri Wanaofatilia huu Mjadala watakuwa wanajua Nani anatunga Maneno na nani anajenga Hoja.

Hizo few exceptions Zimekuwaje na furaha!!! Wakati wewe unasema Bibi yako amekuambia Ndoa zao zilikuwa hazina furaha.!!!!
In every general rule there is an exception but the exception does not invalidate the rule, mfano tunaposema wazungu na waarabu ni wabaguzi hatumaanishi wote kuna few exceptions ambao siyo wabaguzi ila hiyo haiondoi sifa yao ya ubaguzi kwa ujumla, au inaposemwa kwamba wanaume wana tamaa ya wanawake haimaanishi wote kuna few excpetions ila hiyo haiondoi ile sifa ya jumla ya wanaume kuwa na tamaa ya wanawake
Mind you Wanawake ndani ya Nyumba Huwa wana vituko vingi mno Na wanaume huwa Wanavumilia vitu vingi Sana. ( Kama mimi navyo vumilia Utoto wako unaouandika hapa). So Tabia mbovu zilikuwapo kwa wote.
Actually ni mimi ndiye ninayevumilia utoto wako hapa maana huna hoja na hata hizo unazoona unazo huwezi kuzitetea unabaki unarukaruka tu, wanaume huwa mnataka na mmezoea wanawake kukubali tu chochote mnachosema hata kama mnatetea upumbavu unaofanywa na jinsia yenu, sasa mnapokutana na wanawake kama sisi ambao hatukubali huo ujinga mnaanza kutuaddress majina yote mabaya na kutulabel tabia zote mbaya kumbe ninyi ndio hamjazoea kuambiwa ukweli mchungu mnapenda kusikia yale yanayowafurahisha tu
Watu wa Dini Wanaamini maandiko ni Nature kwa ushahidi upi maana na Mimi ni Mtu wa Dini Sasa Nashangaa unachokisema.
Nimesema hivi watu wa dini wanaamini kwamba maandiko ya vitabu vyao yanatoka kwa miungu yao na miungu ni nature, kama wewe hujui na hujawahi kusikia hilo basi itafakari upya hiyo imani yako juu ya dini yako, maana hiyo ndio imani ya waumini wa dini zote sasa labda kama wewe una dini yako na maandiko yako peke yako
Umeshaolewa unataka Uhuru wa kufanya nini??
Hivi wale wanaume wanaosema kwamba hawataki kuoa kwa sababu watakosa uhuru huwa wanamaanisha uhuru wa kufanya nini
Kwani watu huwa wanalazimishwa kuolewa?? Si huwa wanatia saini wenyewe kwenye kile cheti. Sasa umeolewa unataka uruke viwanja kama Wanawake wengine. Cha msingi Usiolewe.
Ulivyo na akili finyu umewaza mambo ya kuruka viwanja tu kwahiyo wewe unadhani kila mtu hapa duniani starehe yake ni kuruka viwanja tu, kwahiyo wewe unadhani mwanaume hawezi kumzuia mke wake kufanya mambo mengine mfano kufanya kazi au biashara fulani au pesa yake kuifanyia kitu au kuipeleka sehemu fulani, vile vile mwanamke anaweza kuwa anataka kuenda sehemu fulani ambayo kwake anaona ni ya muhimu na hakuna madhara yoyote akienda ila mwanaume kwa sababu zake binafsi zisizo na mashiko mfano wivu anaamua tu kumkataza unadhani huyo mwanamke atakuwa na furaha
Aisee Umefirisika kumbe ulikuwa hujasoma vizuri majibu yangu!!.(Uwe unasoma vizuri)

Majukumu ya kimaumbile unayoyakusudia ni yapi?? Na huko kwingine unakokusema ni kupi??
Nimesema utofauti wa kimaumbile siyo justification ya kuweka utofauti na kwenye mambo mengine kama elimu, ajira, haki na wajibu
Kwenye maisha kuna Kuanguka Mdada. Tatizo wanawake kama ninyi mnawaza pesa na Maisha ya Ulaya yaani mumeo akianguka kidogo Huwezi kumfariji katika kipindi hicho ila utaanza kumsimanga. (Hovyo kabisa)
Ni wapi nimesema kwamba mwanaume akianguka mwanamke anatakiwa kumsimanga hebu nioneshe, mimi nilisema mwanamke anapokuwa anamhudumia mwanaume basi huyo mwanaume naye akubali kufanya na kufanyiwa yale aliyokuwa anafanya na kufanyiwa mwanamke pindi yeye alipokuwa anamhudumia, kama unaona mtu kumtii mwenzie ni jambo zuri na rahisi kwanini ninyi wanaume mshindwe sasa maana yake utii ni jambo baya si ndio
Wewe hukusema Maandiko ni Maneno tuu ya watu??. Nikakuuliza Unaamini katika mungu ukaniuliza Mungu yupi??
Tuachane na Hayo Kama utanithibitishia kuwa wewe unayaamini maandiko basi nitaanza tena kuyatumia..
Mimi huwa najaribu kuwa considerate siwezi kujadili mada kama hizi kwa kutumia reference ya dini moja wakati dini ziko nyingi na kila dini ina mungu wake, labda kama wewe hujui ethics za public discussions kama hizi mimi kwenye mijadala kama hii hata dini yangu huwa naiweka pembeni (ila haimaanishi sina dini) kwa sababu naweza kuwa na najadiliana na mtu mwenye dini au imani tofauti na yangu, mimi natumia maandiko ya huku yeye analeta maandiko ya kule (na huwezi kuyatupilia mbali maandiko yake) sasa unadhani kutakuwa na kuelewana hapo na huo mjadala utaisha kweli au wewe unadhani maandiko ya dini zote yanalingana kwa kila kitu
Hilo "bila kujali" umeitoa wapi!! Kwani huu mjadala haukulenga Mume na Mke??.

Anyway kwani si nimesema hata katika ngazi ya jamii Mwanaume ndio kiongozi.

Nasisitiza utii unazingatia mahusiano yaliyopo baina yenu. Kama ni kaka na dada basi kaka ni Kiongozi kama ni shangazi na mjomba basi mjomba ni kiongozi kama ni baba na Mama basi Baba ni kiongozi kama ni babu na bibi basi babu ni Kiongozi.

Sasa usihamishe ukaniuliza Bibi na Kaka?? wakati unajua Mahusiano ya kaka na dada sio sawa na ya Kaka na Bibi.
Na hapo ndipo hoja yangu ilipo kwamba kama mahusiano hayafanani huoni kwamba hicho kigezo chako cha nguvu na umadhubuti automatically kinakataa hapo kwa sababu hicho kigezo hakichagui aina ya mahusiano, maana siku zote mwanaume yeyote yule huwa ana nguvu kuliko mwanamke yeyote yule hivyo kwa kuzingatia hicho kigezo chako, maana yake mwanaume yeyote ana uwezo wa kumtawala mwanamke yeyote bila kujali ni nani yake na mwanamke yeyote anatakiwa kumtii mwanaume yeyote bila kujali ni nani yake
Ukijibu langu nitajibu lako kwa sababu swali langu ndio la kwanza.
Hapo swali langu mimi ndilo la kwanza acha kukwepa hiyo hoja
As long as sio wanawake wote ni Wajuaji kama wewe basi ndoa zitaendelea kufungwa.
Lakini cha ajabu talaka nazo haziwezi kuisha
Aisee Sasa Suala la kuoa wake wengi limetoka wapi tena?? Hujajibu swali unaanzisha Mada nyengine.
Duuh kwahiyo ina maana hujui kwamba zamani suala la wanaume kuoa wake wengi lilikuwa ni kawaida, yani hapa napo unashindwa kuona uhusiano uliopo kati ya hili na hiyo hoja kiasi cha kuona kwamba hiyo ni mada nyingine, aloo hapa nina kibarua kizito sana cha kukuelewesha hebu fanya hivi kama kuna mahali unaona umeshindwa hoja na huna majibu basi achana napo nitakuelewa tu
Hujui na hutaki kujifunza kabla ya kuniita daktari uchwara ungefanya research kwanza. (Yaani usilopoke)
Kutahiriwa kwa mwanaume hakupunguzi utamu wa tendo acha uongo, mimi siropoki kama wewe nafahamu fika ninachopinga, wewe ndio unaleta porojo zako ili utetee uongo wako
Ukeketaji Ulianzishwa na wanaume kwa ushahidi upi?? U feminism Takataka.
Hilo nimeshalifafanua huko juu, hizo tamaduni zenu ndio takataka, feminism ni beneficial kwa wanawake na wanaume wanaojielewa
Wapo Wenye akili sio wanawake wote wasomi Hawana akili kama wewe. Nimekutolea mfano tuu Rais Samia.
Nimeshakuambia kwa mtu anayejua ukweli huo mfano ni uongo kwahiyo tafuta mfano mwingine, halafu kuwa rais hakumfanyi mtu kuwa na akili kuliko watu wote anaowaongoza weka akilini hilo, na pia mwanamke kuwa rais siyo kielelezo cha namna wanawake wote duniani wanavyotakiwa kuwa hivyo matendo yake binafsi siyo sheria, kwahiyo unataka kusema tafsiri ya kuwa na akili kwa mwanamke ni kuwa mtumwa wa mwanaume siyo, je tafsiri ya neno akili ni tofauti kulingana na jinsia vipi na kwa wanaume tafsiri ya kuwa na akili ni nini
Pili ikiwa Mwanamke msomi mwenye ajira hawezi kuwa chini ya Mwanaume inamaanisha hata ukimuhudumia hawezi kukutii kisa ni msomi ana ajira??
Si nilishakuambia kwamba ukiona mwanamke mwenye elimu na ajira anakubali kuwa chini ya mwanaume, ujue huyo mwanaume anatimiza majukumu yake ipasavyo bila kuhitaji msaada wa mke au hukuona mahali nilipokuandikia hivyo, na huyo mwanamke atakubali kwa sababu anahudumiwa na si kwa sababu nyingine yoyote siku hizo huduma zikikata ndipo hapo anapoanza kuonekana mjeuri kumbe ndio uhalisia ulivyo
Kwaiyo wanawake wema hawapo mmebaki ninyi Majike dume???
Wewe unajua tafsiri ya jike dume au umeamua tu kulazimisha tafsiri yako ifit kwenye uongo wako
Unatudhibitishia kuwa ninyi ni chui Sio Wanawake.
Duuh kwahiyo kinyume cha wanawake ni chui, naona hoja zimekuchanganya hadi unaandika pumba sasa, anyway endelea tu kudhihirisha uwezo wako kufikiri inanisaidia kujua nadeal na mtu wa aina gani
Nakumbuka nilikuwa namsikia Feminist mmoja akisema Yeye yupo na financial independence ndio mana Ameweza kutoka nyumbani bila kumuaga mumewe namnukuu akasema" unajua jeuri hii nimeitoa wapi?? Ni kwa sababu ya financial independence". Nikawa najiuliza kama suala la kutoka nyumbani bila kuaga ni jambo zuri kwa nini amesema "jeuri hii" mbona kama inaashiria hilo jambo hata kwake sio zuri ila Kwa Sababu ya mashindano amelazimisha ku prove umwamba.
Yeye alitumia hiyo kauli kwa sababu suala la mwanamke kutoka bila kumuaga mumewe tayari kwenye jamii limeshaonekana ni jeuri tofauti na kwa mwanaume kwahiyo yeye alikuwa analiongelea hilo suala kulingana na namna jamii inavyoliona, by the way binafsi sioni kama kutoka bila kumuaga mwenzio ni jambo zuri haijalishi ni mume au mke kwa sababu unaweza kupatwa na tatizo huko na mwenzio hajui kwahiyo hilo siyo suala la mashindano bali ni kwa faida ya huyo mtokaji mwenyewe labda uniambie kuomba ruhusa maana kuna tofauti kati ya kuaga na kuomba ruhusa, hapo kwenye kuomba ruhusa hata mimi siungi mkono kwa sababu kama nilivyosema huko juu mwanamke anaweza kuwa anataka kufanya jambo fulani au kuenda sehemu fulani ambayo yeye anaona ni muhimu kwake ila mwanaume bila sababu ya msingi anamkataza ila eti yeye akiamua kufanya au kuenda ni muda wowote sasa kwa mwanamke hilo lina faida gani
Informal Education ni jando na unyago full stop na hakukuwa na jamii usiyokuwa na Jando na Unyago kama unapinga njoo na ushahidi hapa.
Ndio maana nikakuambia fanya research acha ubishi na ujuaji wa kipumbavu, hiyo siyo maana ya informal education usinilazimishe nijadili hisia zako binafsi mimi najadili uhalisia, unaweza kuniambia kwenye jamii za wazungu na waarabu kwenye jando na unyago walikuwa wanafundishwa nini
Mimi sizungumzii haya nimekuuliza unapokuwa unamtii Boss wako unakuwa Huna furaha??? Jibu hili.
Ndio hakuna mtu anayefurahia kumtii boss wake pasipo mshahara kama wewe unafurahia basi baki na huo uongo na unafiki wako, wewe jiulize kwanini watu wengi wanasema hawawezi kuajiriwa kwa sababu ajira ni utumwa, kwa maana kwamba ukikubali kuajiriwa umekubali utumwa ila huna budi mradi tu mkono uende kinywani na ukiangalia huna biashara ya kueleweka ya kukufanya ukatae kuajiriwa na watu
Feminism hii ya leo (third wave) ni upumbavu.
Hakuna cha third wave wala ninth wave feminism ni feminism tu lengo la kuanzishwa kwake ni lile lile toka zamani hadi sasa, upumbavu ni wanaume kushindwa kukubaliana na uhalisia kwamba kinachowafanya wanawake wakubali kuwatii ni huduma za kiuchumi tu, upumbavu ni wanaume kuendelea kulazimisha kuwatawala wanawake kwa kisingizio cha either majukumu ya kimaumbile au majukumu ambayo hata wanawake wanayaweza
Kwaiyo umkute mtu Mtaa wa kongo kariakoo umuagize dukani. Aisee una umri gani wewe???
Kwamba hujui kuwa hilo linawezekana, yani wewe unaona ni jambo la ajabu mwanaume kumuagiza jambo, mwanamke aliyekutana naye randomly barabarani (si lazima iwe kumuagiza dukani), tena kwa mtu ambaye ameishi kwenye jamii zilizokumbatia ujamaa hilo wala siyo jambo la kushangaa, labda kama ungekuwa umezaliwa na kukulia kwenye jamii zilizokumbatia ubepari kidogo ningekuelewa
Unachekesha mimi nilihusianisha baina ya Feminism na Atheism Alafu unataka nikupe uhusianao njee ya dini. Ajabu..
Sasa kwanini ulazimishe kuhusianisha concepts ambazo, moja inaweza kuelezewa nje ya dini na nyingine haiwezi kuelezewa nje ya dini, huoni kama hilo tu ni uthibitisho tosha kuwa hivyo vitu havina uhusiano
Wanawake jeuri Walikuwa wanaadhibiwa na waume zao. Imeisha.
Vipi na wanaume jeuri walikuwa wanaadhibiwa na kina nani
Kwani si ni kweli kwamba umetumia maneno yasiyo sahihi sasa unalalamika nini??
Maneno niliyotumia ni sahihi na ndio niliyoyamaanisha, wewe ulielewa ila ulichofanya ni kunikosoa na kunitaka niandike vile unavyotaka wewe, yani ulitaka nitumie maneno rahisi ambayo yangeweza kueleweka hata na mtu mwenye kichwa kigumu na uelewa mdogo na finyu kama wako
Tatizo ujuaji mwingi.
Wewe ndio mjuaji halafu haujui
Umetetea vyema. Sasa katika suala la kuamini Mungu huyu tunaemuamini Sisi (sijui kama na wewe unamuamini) Hao wote wako sawa.
Wako sawa kivipi
Unatudanganya mdada. Miili yetu ni nature sasa sijui wewe Physical appearance unajua ni kitu gani??
Ni wapi nimesema kwamba physical appearance siyo nature hebu acha kukaza fuvu, mimi nimesema kuogopa kiumbe sababu ya physical appearance yake siyo nature, yani uoga wa aina hiyo siyo nature bali ni made
Aisee umeandika Ujinga.

Eeee kuna mnyama hatari mwenye muonekano mzuri(ambao hauwezi kukutisha) embu tutajie!!!!
Sasa inategemea wewe muonekano mzuri kwako ni upi maana uzuri upo machoni pa mtu, mimi kuna jamii ya mbwa ambao nawaona ni wazuri lakini ni hatari, hata hao nyoka unaosema kwamba wana muonekano wa kutisha kuna watu wanawaona ni wazuri
Nadharia.

Embu subili Jadda kwanza kwani Rais akikukuta Barabarani akakutuma. Utamtii kwa vigezo gani?? Japo naamini si Rahisi kiongozi akukute tuu barabarani alafu akutume hhahahahha aisee kazi ipo.
That is logical non sequitur mtu kumtii rais barabarani haihusiani na mwanamke kumtii mwanaume katika mazingira kama hayo, sijui kwanini unalazimisha kuhusianisha vitu kwa kuangalia category moja badala ya kuangalia hivyo vitu kwa ujumla, kumbuka huyo rais kinachoangaliwa hapo ni cheo chake na siyo jinsia yake
Nataka uniambie kama unayakubali maandiko ya kikristo (bible) au ya kiislamu (Quran) au ya kiyahud niambie nianze kuyatumia maana huko juu uliniambia nikuletee maandiko.
Tatizo ni kwamba unaleta maandiko bila uthibitisho unatakiwa ufahamu kwamba maandiko mengi yanakizana baina ya dini, kwahiyo unapoleta maandiko unatakiwa ulete uthibitisho kwamba maandiko ya dini fulani ndio ya kweli na ya dini nyingine ni ya uongo, vinginevyo bora usilete kabisa ni heri ujenge hoja zako nje ya dini kuliko kulazimisha na kunilisha maneno kuwa nimekana dini kana kwamba uliambiwa ukiniambia hivyo ndio utanitisha
 
Utii sio utumwa dada.

Samahan kusema hivi lakini Unaonesha ni muhanga wa mahusiano uliyopita.

Ana victim mentality huyo.

mkuu mtaani Kuna wanawake wengi sana wanaotii kuliko anayozungumza huyo dada,
Ni kuchagua vizuri tu mwenza wa Maisha.
Inategemea wewe unatafsiri utumwa ni nini, hao wanawake wanaotii huko mtaani inajulikana sababu ni maisha magumu ila si kwamba wanapenda, jua kali mtaani mkuu kwa mtu mvivu ukipata mtu wa kukuweka ndani na kukupa hata mahitaji yako ya msingi tu hakuna namna lazima umtii tu
 
Kwan umeambia hii ni assignment kwamba ina deadline lazima niijibu au kuiandika as per a certain date? [emoji848]

Acha kunichakachua.
Sasa ndio ukaamua uje uniquote kwenye comments mia kidogo, mtu mwenyewe huna hata hoja za maana unazojenga zaidi ya kuleta ubishi na ulalamishi tu, yani badala ya kusoma ili uelewe unasoma ili uje kubisha kutafuta ushindi..nah son not today!!
Sisi hatuongei hapa kwasababu hakuna wanawake wa kuoa. Tunaongea ili kuwasaidia wale mabinti ambao hawajitambui kama akina Jadda ili at least wapate a final fighting chance.

Kuhusu sisi wanaume kupata wanawake wa kututii wa kuoa hiyo hatiwezi kukosa abadani. Wamejaa tele ni kuchagua. Balaa ni ninyi sasa mnaotaka wanaume wa kuwatoa out kila weekend, wa kuwanunulia kila toleo la iphone likitoka, wakuwanunulia nguo za fashion kila mwezi, wa kuwajengea nyumba kubwa na kuwanunulia magari ya bei plus vacation kila mwaka nje ya nchi ndipo muweze kuwaheshimu, sijui hao wanaume tanzania wanapatikana kwa wingi wilaya gani ya mkoa gani.
Hahaha kwahiyo wanawake wa kuwatii wanaume wapo wengi ila wanaume wa kuwahudumia wanawake ndio hakuna, aiseee mnapenda sana kuwadanganya watu humu mitandaoni kwa nadharia zenu ila on the ground wote hali halisi tunaiona, leo hii vijiweni na mitandaoni wanaoongoza kulalamika kwenye ndoa kuhusu tabia mbovu za wenza wao ni wanaume huku wanawake wakiwa hawajali tena na wameshaamua kwamba liwalo na liwe
Haka kameshafeli. Ni swala la muda tu kaweze kuprove point.
To hell with your prophecies!!..nilianza kubishana na watu kama wewe humu jf tangu 2019 huu ni mwaka wa tano sasa waulize wanaonifahamu, wengi walikuwa wanaongea kauli kama hizi na kunitabiria kama hivi "oo wewe bado binti mbichi subiri miaka mitano ijayo utajutia hii misimamo yako na utarudi hapa kutuambia", haya miaka mitano hiyo ndio kwanza maisha yananinyookea na nazidi kujionea upumbavu wa wanaume (isipokuwa kwa wachache ambao wanajielewa), kama tukiendelea kuwa hai miaka mingine mitano ijayo nitarudi tena hapa na habari njema zaidi, huku wewe ukiendelea kujifariji na kusubiri niwe single mother na reject ili uthibitishe hizo tabiri zako na ujisikie vizuri
 
ni kabishi sana, hataki ashindwe mwanzo nilimuambia kama anaishi hivyo kupata mwanaume wa kumwelewa itakuwa shida, japo ana point ila ime base kwenye negativity mwanamke kaumbwa ku submit kwa mwanaume, ila wanawake wa sikuhizi wanaichukulia ni udhaifu
Wewe nilidhani umenielewa ila naona bado nimekuacha nyuma sana, anyway naelewa wanaume huwa lazima mteteane kwenye kila jambo linalowahusu hata kama ni ujinga, ila ifike pahala jitahidini msitumie sana mihemko na hisia zenu katika kujadili mambo kama haya yanayohitaji uhalisia
 
Kama kuna mtu ataona kwamba wewe ndiye unayetoa hoja hapa basi naye ni either hana akili kama wewe, au ndio wale wazee wa kutetea lolote linalohusu wanaume hata kama ni ujinga, maana mpaka sasa kuna sehemu nyingi sana nimeshakukosoa na hujajibu tena na nyingine unarudia kujibu yale yale
Haya ni malalamiko.
Sasa mbona hujajibu swali langu kwahiyo hapo ndio umeshathibitisha kwamba mungu wako ndio yuko mbinguni, waroma nawazushia kivipi wakati wewe kwa mujibu wako ni kwamba kama dini inaabudu sanamu basi mungu wao hayuko mbinguni, unashindwa kujua kwamba kwa wengine hayo masanamu ni symbol ya miungu yao tu
Wahindu Ng'ombe ni mungu sio symbol ya Mungu,, wanaoabudu Moto (Zoroastrianism) kwao Moto ni Mungu sio symbol ya Mungu pia yale Masanamu ya Buddha ni miungu kwao na sio Symbol ya Mungu. (Jitahidi uelewa).
Hivi si nimekuambia uwe unasoma kwanza aya nzima hadi mwisho kisha ndio ujibu, unaona kama hapo umeuliza swali ambalo jibu lake lilikuwepo kwenye hiyo hiyo aya kwa chini yake, unajaza magazeti bure kwa maswali ya kipuuzi ambayo majibu yake nimeshakupa na yanaeleweka vizuri tu
Unatudanganya majibu gani umetoa Bi Jadda??
Ukishaondoka kuenda wapi
Nimekuuliza ukijitegesha ili upate mimba alafu asipatikane mwanaume utapata hiyo Mimba??
Sasa kwanini hilo jukumu kubwa la mama kuzaa haliwezi kumfanya awe kiongozi, kwani hao watoto anajizalia yeye mwenyewe hadi useme kwamba anatakiwa tu kupendwa na watoto wake, kwanini na majukumu ya baba yasimfanye apendwe na watoto kwanini yenyewe ndio yamfanye awe kiongozi
Aliesema Majukumu ya Baba ndio yanamfanya awe kiongozi ni nani??
Ndio kwani unapofanya hayo majukumu wewe hunufaiki nayo au
Nanufaika nayo ila wewe ulisema tunaonufaika ni sisi pekee kana kwamba familia hainufaiki.
Hebu jaribu kumuweka mnyama zoo halafu umnyime chakula na mengineyo uone atakufanyaje, maana naona sasa unauliza maswali ya kipumbavu ambayo hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kuuliza, wewe huchekeshi tu bali pia unasikitisha sana
Kwani Mada ni Kufuga wanyama Zoo au Utii wa Wanawake wa kisasa?? Naona nikiendela kukujibu katika hili unapata vichaka zaidi vya kujaza risala.
Wewe akili yako ndio inakutuma kwamba zoo ni yale mabanda maana mimi hakuna sehemu nimesema hivyo, nani kakudanganya kwamba hakuna wanyama ambao hawawezi kuwekwa zoo hebu acha uvivu wa kufikiri fanya research ndio uje uongee huu uongo wako, sasa hivi nikiona unabisha jibu langu na kuleta jibu lako la uongo nakuacha unless uthibitishe kwa hoja usinilazimishe nijadili mawazo yako
Haya ngoja nikichome hiki kichaka.
Huwa mnajifanya hamna muda na mambo ya kipuuzi ya wanawake, ila pita humu mitandaoni uone mada za kuwatukana na kuwadhalilisha wanawake zinatoka kwa jinsia gani, hayo yote ni kwa sababu mnajua mwanamke akiwa na tabia mbovu inamuathiri mwanaume kisaikolojia kama utabisha na hili basi rudi darasani
Suala la malalamiko ni kwa Pande zote kwa sababu Wanawake wana vituko vyao na wanaume kadhalika sijui wewe unakusudia nini??

Pili kuathirika kisaikolojia ni kwa wote bali kwa wanawake ni zaidi kwa sababu you're too emotional.
Hivi unaelewa unachoandika kweli sasa kwani kesi za wanawake kwenye madawati zinahusu tabia mbovu za wanaume, si huwa zinahusu huduma za kiuchumi au mgawanyo wa mali na hilo
Sio kweli,,, Kesi zaidi ya hizo zipo katika madawati ya jinsia.
Pili wanaopeleka kesi za huduma za kiuchumi Ni Huduma zipi hizo??
linadhihirisha kwamba umuhimu wa mwanaume kwa mwanamke uko hapo tu huko kwingine mnadanganywa tu, mimi hapa naongelea malalamiko ya jinsia fulani dhidi ya tabia mbovu za jinsia nyingine ni wanaume ndio wanaongoza wewe unaniletea habari za madawati
Tabia zisizo faa zipo kwa wote Bi Jadda.
Inanisikitisha kusikia kutoka kwako kwamba Umuhimu wa Mwanaume kwa Mwanamke ni Huduma za kiuchumi tuu(pesa) Wanaume Ni Walinzi wenu And Women are more comfortable with Men.
Siyo udhaifu hiyo ndio saikolojia ya binadamu hata wagonjwa wa ukimwi wanaposimangwa na kutengwa na jamii, huwa wanaanza kujiona hawafai lakini si kwamba ni kweli hawafai bali ni watu wanaowazunguka ndio wanawafanya wajione hivyo, sasa ndivyo na wanawake hao wenye experience kama hizo wanavyojiona
Hiki kichaka pia nakichoma.
Wewe una takwimu gani zinazoonesha kwamba ndoa zinazovunjika kwa wingi ni za feminists tu, halafu sijui hata kama unajua kwamba feminists hawapo wanawake bali hata wanaume pia wapo feminists, na sijui kama umeshawahi hata kutembelea huko ulaya achilia mbali kuishi au na wewe ndio wale wazee wa "niamini mimi" maana hoja zako ndio zimejikita hapo
Globalization inatusaidia kuyajua Mambo Hata ya Ulaya bila kuishi huko. Ila huo ndio Uhalisia Japo Sababu nyengine zipo ila Ujue pia U Feminism sio lazima uwe wa msimamo mkali (radical) kama huu wako kuna wengine Wanachovya chovya. Wanafanya Vitu kwa kuiga na Kusikia tuu na hata hawajui kuwa kuna kitu kinaitwa Feminism.
Sasa kama wanawake wote siyo wajuaji na ninyi mnaoa wanawake ambao siyo wajuaji kwanini sasa hizo ndoa hazina amani na nyingine zinavunjika,
Nimekwambia Ndoa nyingi hizi leo zinazovunjika ni Zile za wanawake wajuaji wanaoishia Kuwa single mothers Na kujidai they don't care.
mimi nilitegemea kwamba kwa sababu mnaoa wanawake wife material kisha mnawaacha hawa wajuaji basi ndoa zenu zitakuwa na uhakika wa kudumu ila matokeo yake talaka kila siku,
Unarudia jambo lile lile Vidada vijuaji Huitafuta Ndoa kama kondoo kisha Baadae huwa chui then sio muda ndoa inakufa.
Lakini kwa wale waliooa wanawake watiifu Mwanamke Hatoki bila kukuomba ruhusa Ukirudi amepika Vizuri na Anakusubiri Ule kisha ukale Unamuacha Kwa lipi??.

Kazi Ninyi sasa Hutaki Upangiwe wapi unaenda na unaenda na nani pia Muda wa kurudi ni maamuzi yako. Kupika na hizo kucha zako za bandia ni Ngumu so atapika aunt Mumeo yupo kwa bed wewe upo na smart yako instagram unapost Ulivyokuwa Beach na Bikini. Sasa Usiachike kwa nini??
na kwanini wanawake waanze kutamani ndoa katika umri wa jioni kwanini wasitamani katika umri wa asubuhi kama ninyi wanaume unaweza kunipa jibu lililonyooka hapa
Wanawake Watiifu huoelewa Mapema angali vigoli. Ninyi Huwa hamna jinsi sasa mana una approach menopause na Huna Mume Mbaya hata Mtoto Huna Kizazi chenyewe Mtihani Zile contraceptives Chuo Zimeharibu kizazi unaona Yoyote tuu aje.
Hapa umeamua tu kujitoa ufahamu

Duuh hata kama historia huijui hivi kwa akili ya kawaida tu, unadhani wanawake wangeweza kujitungia tamaduni ambazo zinawaumiza na hazina faida yoyote kwao kwa lengo la kuwafurahisha wanaume tu, we jamaa mbona kama hata common sense tu inakushinda kuitumia
Hizi Tamaduni unaziona hazina faida wewe. Sasa usilazimishe Kila uanchokiona wewe kibaya na kwa mwenzio nacho kiwe kibaya. Mind you German Ushoga ni Jambo zuri Sana na wanatushangaa sisi tunaopinga Mambo hayo.
Hayo mambo mabaya ni tafsiri yako wewe ila hayo yalionekana ndio uanaume na mwanaume usipoyafanya hayo basi unaonekana dhaifu kwa mkeo, na kuna mengine hadi leo yanaonekana ndio uanaume mfano ulevi na usaliti ni mara ngapi watu wanasema mwanamke kulewa na kusaliti ni vibaya, ila mwanaume kulewa na kusaliti ni sawa tu wakati kiuhalisia hayo ni mambo mabaya kwa jinsia zote
Ulevi na Usaliti ndio uanaume nani kakwambia It seems like umezungukwa na Wanaume wa aina furani hivi.
Hivi kweli unaweza kusimama hadharani ukasema Ulevi ndio Uanaume alafu ukaeleweka???
Oohh kwahiyo na wale wanawake wanaovumilia usaliti na unyanyasaji nao wana furaha, narudia wewe sasa hivi huna tena hoja bali umeamua tu kujitoa ufahamu, na kwa vile umeishiwa hoja naona sasa umeanza kuleta ad hominem personal attacks kana kwamba unanijua
Personal attack kivipi!!. Kwani Si mnajivunia kutokuolewa Kwa sababu mnasimamia mambo yenu wenyewe no need of man.
Anyway kama nimesema uongo( kwamba ndoa unayo) prove me wrong kama nipo sahihi then hiyo sio attack ni reality.
Speaking of the reality and not negativity
Nilikuuliza kuwa jee wewe Bibi yako amekwambia Alikuwa hana Furaha na maisha yake ya ndoa na Babu yako chini ya mfumo mnaouita mfumo dume?? (Jaribu kujibu)
Wewe unaishi wapi huko ambako watu hawajui kupika, we jamaa mbona umekaa kinadharia sana, wewe kwako kujua kupika maana yake nini
Nadharia gani Ninyi wanawake wanaharakati mnajua kupika?? Na hizo kucha mnapikaje?? Huo Muda wa kupika mnapata wapi?? Wakati Mkirudi kutoka Ofisini Mmechoka mnamkolomea Aunt awahishe Chakula.
Duuh kwahiyo wewe nje ya shughuli za nyumbani shughuli nyingine unayoijua wewe ni vita tu kana kwamba huko vitani wanaume walikuwa wanaenda kila siku wakati vita ni suala la once in a life time, tena kuna wengine tangu wanazaliwa hadi wanakufa uzeeni hawajawahi hata kuexperience hizo vita sasa hilo nalo kwanini ulihesabia katika majukumu ya kila siku ya mwanaume,
Vita ni mfano tuu hata Wanaume walikuwa na Shughuli chache za kufanya Baada ya Shamba. Jamii yetu miaka ya tisini sio hii unayoiona leo iliyojaa pilika pilika.
unaniuliza nilitaka mwanamke afanye shughuli gani zaidi kwani huoni dunia ya leo wanawake wanafanya nini wapo kwenye kila nyanja madaktari, wahandisi, walimu, wahasibu nk wapo kwenye siasa, majeshi, sanaa, michezo nk na wanafanya vizuri tu sasa kwanini zamani hawakufundishwa hayo unaweza ukanipa sababu
Aisee Hizo kazi mbona kwa wakati huo pia zilikuwa hazijawa kama zilivyo sasa Ulitaka wanawake wawe wahandisi sijui madaktari mwaka 1930 Uko serious??
Aise kwahiyo mwanamke naye atakuwa ni fahali

Dooh kwahiyo kila familia watoto wakubwa ni wa kiume tu hakuna familia ambazo watoto wakubwa ni wa kike, halafu kumbuka hapa tunaongelea suala la nguvu na umadhubuti hatuongelei aina ya familia, mtoto wa kiume ana nguvu na umadhubuti kuliko ndugu au jamaa yake yoyote yule wa kike kwanini asiwatawale na hao sasa
Nasisitiza Utii unachunga Mahusiano yaliyopo baina ya Watu husika. Nakazia tena.
Sasa suala la nguvu na umadhubuti linahusiana nini na aina ya uhusiano uliopo baina ya mwanaume na mwanamke, okay labda swali langu niliweke hivi kinachomzuia mwanaume kuwatawala wanawake wengine tofauti na mkewe ni kipi hasa, yani kwanini hilo suala la nguvu na umadhubuti liapply kwenye ndoa tu na siyo kwenye uhusiano wa aina nyingine nipe jibu lilinyooka hapa
Nachoshangaa Hili jambo ulilitolea majibu wewe mwenyewe.
Nilikuuliza Mtoto akiwa Anajitegemea aache kuwatii wazazi wake kwa kuwa hawamuhudumii tena Ukasema hapana Sababu Mtoto anatakiwa Amtii Mama yake kwa kuwa yeye amemzaa. Hivyo uhusiano wa Mama na Mtoto ni Mmoja kamzaa Mwengine Japo Mmoja ni Mwanamke na Mmoja ni Mwanaume. Sasa kama ndivyo hivyo Unaonaje ukalichukua hilo katika upande huu pia. Uhusiano wa Mke na Mume ni Mmoja kamuoa Mwengine. Sio sawa na Ule wa mmoja Kamzaa Mwengine. (Jitahidi uelewe)
Sasa umeanza kuja ninapopataka
Hahahaha defensive mechanism. Unapopataka wapi??
kwahiyo kumbe unajua kwamba hayo majukumu siyo ya kimaumbile na kwamba jinsia yoyote inaweza kuyafanya sasa kwanini mnataka kuwatawala wanawake kwa sababu ya hayo, by the way siku hizi kuna wanawake wengi wanaingia kwenye majeshi na wengine wanakuwa hadi makomando na wanapigana vita na pia kuna wanawake wanafanya hizo kazi ngumu kama kuchimba visima kubeba zege ila mbona hawajataka kuwatawala kwa sababu hiyo, kwahiyo wanaume kuzalisha mbegu na kutungisha mimba mnaona ndio jukumu kubwa kuliko kubeba mimba na kuzaa kiasi cha kuwafanya ninyi ndio muwe watawala
Unachotaka kusema kuwa Wanaume wana Nguvu Sawa na Wanawake na Wanauwezo sawa katika hayo Mambo uliyoyataja??

Tofautisha kati ya kuwa na uwezo wa kufanya na kufanya wanaume wengi wana uwezo wa kufanya hayo majukumu ila hawataki kuyafanya, tena wengi husema eti hayo ni majukumu ya kike mwanaume aliyeoa hawezi kufanya hayo na ukiona anafanya hayo ujue ni mume bwege mke wake anampanda kichwani, sasa labda nikuulize kwanini wanaume wengi pamoja na kuweza kufanya hayo majukumu bado hawapendi kuyafanya na wanataka wanawake ndio wawafanyie
Kwanza hoja Ilikuwa sio Hii. Umepindisha Hoja. Wewe ulisema kazi za nyumbani Wanaume hawawezi kuzifanya Mnaweza ninyi kwaiyo You're Strong for that. Poor you.

Pili mgawanyo wa majukumu ndio unaoongoza mambo hayo Baba Anaenda kutafuta Mahitaji Muhimu kwa ajili ya familia kutokana na Maumbile yake ya Nguvu na Umadhubuti na Mama anasimamia Majukumu ya hapo nyumbani pamoja na Malezi Nyumbani.

Changamoto ni katika familia zenu wewe unatoka na Mumeo anatoka Watoto wenu mnaachia aunt Mtoto wako akifanyiwa vitendo vibaya Mnalalamika Wakati Binti mnamlipa laki moja.
Na Ndio mana Watoto wa Familia hizo za Baba Sharubu mama Sharubu Utaona Tabia zao zinavyokuwa.
Hata kwa kuangalia hali halisi tu unaona kabisa ushoga unalazimishwa, kwa sababu idadi ya mashoga bado ni ndogo kulinganisha na wanaume rijali hili lifanyie research mwenyewe, lakini kwa upande wa feminists wanawake idadi ni kubwa kuliko wanawake ambao bado wanaunga mkono mfumo dume
Ujerumani na Ulaya kwa Ujumla ushoga Unalazimishwa?? au unakusudia Huku Afrika??
Kama unabisha hili jiulize kwanini hata wale wanaounga mkono ushoga hawako tayari watoto wao wa kiume wawe mashoga, lakini wale wanaopinga feminism wanasomesha mabinti zao ili waje kujitegemea wakiolewa wasiende kuwa wamama wa nyumbani, maana mlivyo wabinafsi mnataka wake zenu tu ndio wawe watumwa kwenu ila hamtaki mabinti zenu wakawe watumwa kwa waume zao huko
Kipimo sio Feminist apate mtoto wa Kike Bali Apate Mtoto Wa Kiume kisha tumuulize atamfundisha Nini Mtoto wake wa kiume Juu ya Mkewe atakaemuoa???

Kwamba Awe gentleman asimpangia mkewe pa kwenda wala asimzuie akiamua kutoka asiwe mkali Akipewa taarifa na mkewe kuwa hatorudi Nyumbani kwa siku hiyo yupo kwa rafiki zake. Amuhudumie Mkewe Vizuri pesa yake ni ya kumuhudumia mkewe na familia ila pesa ya mkewe Ni kwa ajili ya send off na kitchen parties. Kwamba asifatilie Mienendo ya mkewe Hasa simu yake kila mtu yupo huru katika ndoa Hakuna wa kumuongoza mwenzake. Kila mmoja anajiongoza Mwenyewe.
Au wewe unaona karne hii kuna baba ambaye hataki binti yake asome, kama kweli wanaume mnachukia feminism acheni kusomesha mabinti zenu hii formal education maana hilo ndilo lengo la kwanza la feminism kwahiyo ili kuikwepa kabisa feminism msisomeshe mabinti zenu, waacheni wawe housegirls huko majumbani kwenu halafu wakifika miaka 18 hadi 20 waozesheni wakawe housewives huko kwa waume zao halafu mrudi mtupe mrejesho
Binti yangu kuwa house wife Mtiifu kwa Mumewe ni jambo zuri kwangu kuliko kuwa degree holder Employed kiburi kwa mumewe. Mind you Kiburi Baada ya kusoma Ni maamuzi ya mtu kutokana na watu aliokutana nao katika safari yake ya kusoma.
Aiseee yani kama kila mtu angekuwa anasikiliza maneno tu mtu anayosema kuhusu yeye, basi hata huko mahakamani watu wangekuwa hawafungwi, anyway nimekuambia tuishie hapa tafuta mfano mwingine
Huo mfano hautoshi?? Mbona unamun'gunya maneno unajidai kama vile unayajua maisha mengine Tofauti na yale anayoyasema Mwenyewe. (Prove)
Walitaka waolewe kwa faida gani za ndoa walizokuwa wanaziona unaweza ukanitajia hizo faida wewe ndio maana nakuambia huna hoja, ila umeamua tu kujitoa ufahamu na kuukataa ukweli yani mimi nakufafanulia kwa kina kwanini zamani ndoa zilidumu hata kama wanawake hawakuwa na furaha, halafu wewe unaendelea kukomalia tu kwamba walikuwa na furaha kwa cheap na shallow points kama hizo yani huna sababu yoyote yenye uhalisia zaidi ya mawazo yako tu
Defensive mechanism. Na malalamiko tuu.
Wanawake wa zamani walikuwa na mapungufu gani ambayo yalikuwa yanawaumiza wanaume moja kwa moja,
Binadamu wote tuna mapungufu na ndio maana migogoro baina yetu haishi hata wewe inawezekana watu wako wa karibu mlishwahi kukwaluzana. Wanawake wanayakwao Katika ndoa. Kama huyajui then basi wewe ni mgeni katika Masuala ya familia.
na kama wanawake wana hayo mapungufu kwanini sasa mnaendelea kuwaoa kumbuka kwa tamaduni zetu anayeamua ndoa ni mwanaume, hakuna mwanaume anayelazimishwa kuoa au kumuoa mwanamke wa aina fulani sasa kwanini mnaendelea kuoa wanawake wenye mapungufu ina maana ninyi hampendi kuwa na furaha
Mapungufu binadamu tunavumiliana na kuelekezana na kuadabishana inapobidi.
Unaona sasa shida ilipo yani mnadai kwamba siyo wanawake wote ni mafeminist na kwamba ninyi mnaoa wife material tu, ila cha ajabu kila siku kuna talaka na ndoa zilizobaki zina migogoro sasa mna uhakika huwa hao wanawake mnaooa ni wife material au ndio mikwara na vitisho tu, halafu una uhakika na ushahidi gani kama ndoa zote zinazovunjika chanzo ni wanawake kuwa mafeminist tu
Kwani huoni Ndoa zinazovunjika nyingi ni za Mafeminist baada ya kushindwa kuendelea kuficha makucha yao. Na wale Wanawake wanaowaiga Wanawake kama ninyi bila kujua kuwa wengi wenu mnazungumzia ndoa wakati ninyi hamjaolewa.
Wapi nimeipinga katiba, mimi nimekuambia hizo katiba wanaozitunga ni hao viongozi wenyewe, huwa hawawashirikishi wananchi wote bali wananchi huwa wanalazimika kufuata tu hizo sheria
Kwaiyo Wananchi wengeshirikishwa Kipengele kingetolewa??
Kijana mbona unapenda kukurupuka wewe ulisema kama rais ana makosa na mimi pia nikakujibu kama rais ana makosa, sasa kama rais anafanya makosa na wananchi wanajua hawawezi kumshitaki unadhani kuna mwananchi atakuwa na furaha na hilo, wewe huoni ndio maana nchi nyingine zenye uthubutu watu wanaandamana kila siku na kwingine majeshi yanapindua nchi au hizo nchi hazina katiba..sasa feminism imeingiaje hapo
Eti Kijana it's okay Sio shida
But Walioweka hiko kipengele ni katika Kuchunga heshima kwa kiongozi wa nchi na sidhani kama kuna nchi Ulaya yenye demokrasia kubwa ambapo Rais anaweza kushitakiwa akiwa madarakani.
Dooh kwahiyo kwako wewe unyanyasaji ni kupiga tu mtu una safari ndefu sana asee, kwahiyo wewe ukisikia unyanyasaji wa kisaikolojia huwa unaelewa nini au hata hauelewi kitu, maana kwa yote hayo niliyoelezea mtu mwenye upeo mkubwa angeshaelewa ni unyanyasaji wa aina gani ninaozungumzia hapa
Unaweza kujitengenezea mambo ukahisi unakuwa psychological tortured kumbe ni expectations zako tuu. Kama ninyi mnavyoiga maigizo ya kizungu.
In every general rule there is an exception but the exception does not invalidate the rule, mfano tunaposema wazungu na waarabu ni wabaguzi hatumaanishi wote kuna few exceptions ambao siyo wabaguzi ila hiyo haiondoi sifa yao ya ubaguzi kwa ujumla, au inaposemwa kwamba wanaume wana tamaa ya wanawake haimaanishi wote kuna few excpetions ila hiyo haiondoi ile sifa ya jumla ya wanaume kuwa na tamaa ya wanawake
Nilikuwa nataka uniambie Hizo Ndoa chache zilizokuwa na furaha. Furaha ilitoka wapi?? wakati Mwanamke hakuwahi kuwa na furaha chini ya Mfumo Dume.????
Actually ni mimi ndiye ninayevumilia utoto wako hapa maana huna hoja na hata hizo unazoona unazo huwezi kuzitetea unabaki unarukaruka tu, wanaume huwa mnataka na mmezoea wanawake kukubali tu chochote mnachosema hata kama mnatetea upumbavu unaofanywa na jinsia yenu, sasa mnapokutana na wanawake kama sisi ambao hatukubali huo ujinga mnaanza kutuaddress majina yote mabaya na kutulabel tabia zote mbaya kumbe ninyi ndio hamjazoea kuambiwa ukweli mchungu mnapenda kusikia yale yanayowafurahisha tu
Hakuna hoja unajenga na Unaandika ili ubishe tuu to infinity.
Nimesema hivi watu wa dini wanaamini kwamba maandiko ya vitabu vyao yanatoka kwa miungu yao na miungu ni nature, kama wewe hujui na hujawahi kusikia hilo basi itafakari upya hiyo imani yako juu ya dini yako, maana hiyo ndio imani ya waumini wa dini zote sasa labda kama wewe una dini yako na maandiko yako peke yako
Maandiko sio Nature acha kulazimisha.
Hivi wale wanaume wanaosema kwamba hawataki kuoa kwa sababu watakosa uhuru huwa wanamaanisha uhuru wa kufanya nini
Uhuru wa Kuendelea na mahusiano mengi bila kuulizwa na yeyote.
Ulivyo na akili finyu umewaza mambo ya kuruka viwanja tu kwahiyo wewe unadhani kila mtu hapa duniani starehe yake ni kuruka viwanja tu
Nani kazungumzia starehe hapa??
, kwahiyo wewe unadhani mwanaume hawezi kumzuia mke wake kufanya mambo mengine mfano kufanya kazi au biashara fulani au pesa yake kuifanyia kitu au kuipeleka sehemu fulani, vile vile mwanamke anaweza kuwa anataka kuenda sehemu fulani ambayo kwake anaona ni ya muhimu na hakuna madhara yoyote akienda ila mwanaume kwa sababu zake binafsi zisizo na mashiko mfano wivu anaamua tu kumkataza unadhani huyo mwanamke atakuwa na furaha
Jee Sababu zipi zenye mashiko Mwanaume anaweza kumzuia mkewe kutoka?? Au hakuna kumzuia kabisa??
Nimesema utofauti wa kimaumbile siyo justification ya kuweka utofauti na kwenye mambo mengine kama elimu, ajira, haki na wajibu
Nani kaweka utofauti??
Ni wapi nimesema kwamba mwanaume akianguka mwanamke anatakiwa kumsimanga hebu nioneshe, mimi nilisema mwanamke anapokuwa anamhudumia mwanaume basi huyo mwanaume naye akubali kufanya na kufanyiwa yale aliyokuwa anafanya na kufanyiwa mwanamke pindi yeye alipokuwa anamhudumia, kama unaona mtu kumtii mwenzie ni jambo zuri na rahisi kwanini ninyi wanaume mshindwe sasa maana yake utii ni jambo baya si ndio
Hakuna maisha ya namna hii.
Mimi huwa najaribu kuwa considerate siwezi kujadili mada kama hizi kwa kutumia reference ya dini moja wakati dini ziko nyingi na kila dini ina mungu wake, labda kama wewe hujui ethics za public discussions kama hizi mimi kwenye mijadala kama hii hata dini yangu huwa naiweka pembeni (ila haimaanishi sina dini) kwa sababu naweza kuwa na najadiliana na mtu mwenye dini au imani tofauti na yangu, mimi natumia maandiko ya huku yeye analeta maandiko ya kule (na huwezi kuyatupilia mbali maandiko yake) sasa unadhani kutakuwa na kuelewana hapo na huo mjadala utaisha kweli au wewe unadhani maandiko ya dini zote yanalingana kwa kila kitu
Unayazungumziaje Haya Maandiko.

1 Timotheo 2:11
[11]Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.

1 Timotheo 2:12
[12]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

1 Wakorintho 11:3,7,10

[3]Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.

[7]Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.

[10]Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.

Na hapo ndipo hoja yangu ilipo kwamba kama mahusiano hayafanani huoni kwamba hicho kigezo chako cha nguvu na umadhubuti automatically kinakataa hapo kwa sababu hicho kigezo hakichagui aina ya mahusiano, maana siku zote mwanaume yeyote yule huwa ana nguvu kuliko mwanamke yeyote yule hivyo kwa kuzingatia hicho kigezo chako, maana yake mwanaume yeyote ana uwezo wa kumtawala mwanamke yeyote bila kujali ni nani yake na mwanamke yeyote anatakiwa kumtii mwanaume yeyote bila kujali ni nani yake
Nimeshajibu.
Hapo swali langu mimi ndilo la kwanza acha kukwepa hiyo hoja
Aisee!!!
Lakini cha ajabu talaka nazo haziwezi kuisha
Kwanza nikuulize wewe unafurahia talaka kuwa nyingi!! una Shida Kubwa. Mind you dada zako ndio wanaachika Na kuwa single mothers.
Duuh kwahiyo ina maana hujui kwamba zamani suala la wanaume kuoa wake wengi lilikuwa ni kawaida, yani hapa napo unashindwa kuona uhusiano uliopo kati ya hili na hiyo hoja kiasi cha kuona kwamba hiyo ni mada nyingine, aloo hapa nina kibarua kizito sana cha kukuelewesha hebu fanya hivi kama kuna mahali unaona umeshindwa hoja na huna majibu basi achana napo nitakuelewa tu
Hakuna uhusiano na hii mada yetu acha porojo.
Kutahiriwa kwa mwanaume hakupunguzi utamu wa tendo acha uongo, mimi siropoki kama wewe nafahamu fika ninachopinga, wewe ndio unaleta porojo zako ili utetee uongo wako
Una ushahidi juu ya hili??
Hilo nimeshalifafanua huko juu, hizo tamaduni zenu ndio takataka, feminism ni beneficial kwa wanawake na wanaume wanaojielewa
Hahahha eti wanaume wanaojielewa Wanapatikana kwa wingi Mkoa Gani??
Nimeshakuambia kwa mtu anayejua ukweli huo mfano ni uongo kwahiyo tafuta mfano mwingine, halafu kuwa rais hakumfanyi mtu kuwa na akili kuliko watu wote anaowaongoza weka akilini hilo, na pia mwanamke kuwa rais siyo kielelezo cha namna wanawake wote duniani wanavyotakiwa kuwa hivyo matendo yake binafsi siyo sheria, kwahiyo unataka kusema tafsiri ya kuwa na akili kwa mwanamke ni kuwa mtumwa wa mwanaume siyo, je tafsiri ya neno akili ni tofauti kulingana na jinsia vipi na kwa wanaume tafsiri ya kuwa na akili ni nini
Sasa mara kwamba unayajua Ya chinichini mara yeye sio kielelezo cha Wanawake wote Hueleweki.
Si nilishakuambia kwamba ukiona mwanamke mwenye elimu na ajira anakubali kuwa chini ya mwanaume, ujue huyo mwanaume anatimiza majukumu yake ipasavyo bila kuhitaji msaada wa mke au hukuona mahali nilipokuandikia hivyo, na huyo mwanamke atakubali kwa sababu anahudumiwa na si kwa sababu nyingine yoyote siku hizo huduma zikikata ndipo hapo anapoanza kuonekana mjeuri kumbe ndio uhalisia ulivyo
Aisee Kwaiyo Unaolewa na Una guarantee utii katika Pesa zikikosekana unaonyesha uhalisia wako (Changamoto).
Wewe unajua tafsiri ya jike dume au umeamua tu kulazimisha tafsiri yako ifit kwenye uongo wako
Jike dume kama ilivyo literally.
Sijui ulishawahi kujiuliza kwanini Wewe tukikwambia una Tabia za kiume kiume Haitakuwa shida sana and may be Uta feel proud ila Mwanaume tukimwambia ana tabia za kike kike Hiyo ni Vita imeanzishwa hatokubali.
Duuh kwahiyo kinyume cha wanawake ni chui, naona hoja zimekuchanganya hadi unaandika pumba sasa, anyway endelea tu kudhihirisha uwezo wako kufikiri inanisaidia kujua nadeal na mtu wa aina gani
Usitoe majibu mepesi katika hoja ngumu.
Yeye alitumia hiyo kauli kwa sababu suala la mwanamke kutoka bila kumuaga mumewe tayari kwenye jamii limeshaonekana ni jeuri tofauti na kwa mwanaume kwahiyo yeye alikuwa analiongelea hilo suala kulingana na namna jamii inavyoliona, by the way binafsi sioni kama kutoka bila kumuaga mwenzio ni jambo zuri haijalishi ni mume au mke kwa sababu unaweza kupatwa na tatizo huko na mwenzio hajui kwahiyo hilo siyo suala la mashindano bali ni kwa faida ya huyo mtokaji mwenyewe labda uniambie kuomba ruhusa maana kuna tofauti kati ya kuaga na kuomba ruhusa, hapo kwenye kuomba ruhusa hata mimi siungi mkono kwa sababu kama nilivyosema huko juu mwanamke anaweza kuwa anataka kufanya jambo fulani au kuenda sehemu fulani ambayo yeye anaona ni muhimu kwake ila mwanaume bila sababu ya msingi anamkataza ila eti yeye akiamua kufanya au kuenda ni muda wowote sasa kwa mwanamke hilo lina faida gani
Mwanaume akiwa na sababu ya msingi anaruhusiwa kumzuia mkewe akitaka kutoka??
Ndio maana nikakuambia fanya research acha ubishi na ujuaji wa kipumbavu, hiyo siyo maana ya informal education usinilazimishe nijadili hisia zako binafsi mimi najadili uhalisia, unaweza kuniambia kwenye jamii za wazungu na waarabu kwenye jando na unyago walikuwa wanafundishwa nini
Kwani tulikuwa tunajadiri Waarabu au Jamii yetu ya Zamani??
Ndio hakuna mtu anayefurahia kumtii boss wake pasipo mshahara kama wewe unafurahia basi baki na huo uongo na unafiki wako, wewe jiulize kwanini watu wengi wanasema hawawezi kuajiriwa kwa sababu ajira ni utumwa, kwa maana kwamba ukikubali kuajiriwa umekubali utumwa ila huna budi mradi tu mkono uende kinywani na ukiangalia huna biashara ya kueleweka ya kukufanya ukatae kuajiriwa na watu
Aaah kwanini umetanguliza "bila mshahara" Defensive mechanisms zako Hovyo kabisa.
Anyways Tufanye hunyimwi mshahara jee Kumtii boss wako unakosa furaha??
Hakuna cha third wave wala ninth wave feminism ni feminism tu lengo la kuanzishwa kwake ni lile lile toka zamani hadi sasa, upumbavu ni wanaume kushindwa kukubaliana na uhalisia kwamba kinachowafanya wanawake wakubali kuwatii ni huduma za kiuchumi tu, upumbavu ni wanaume kuendelea kulazimisha kuwatawala wanawake kwa kisingizio cha either majukumu ya kimaumbile au majukumu ambayo hata wanawake wanayaweza
Uongo.
Kwamba hujui kuwa hilo linawezekana, yani wewe unaona ni jambo la ajabu mwanaume kumuagiza jambo, mwanamke aliyekutana naye randomly barabarani (si lazima iwe kumuagiza dukani), tena kwa mtu ambaye ameishi kwenye jamii zilizokumbatia ujamaa hilo wala siyo jambo la kushangaa, labda kama ungekuwa umezaliwa na kukulia kwenye jamii zilizokumbatia ubepari kidogo ningekuelewa
Nadharia.
Sasa kwanini ulazimishe kuhusianisha concepts ambazo, moja inaweza kuelezewa nje ya dini na nyingine haiwezi kuelezewa nje ya dini, huoni kama hilo tu ni uthibitisho tosha kuwa hivyo vitu havina uhusiano
Hueleweki.
Vipi na wanaume jeuri walikuwa wanaadhibiwa na kina nani
Na wazee.
Maneno niliyotumia ni sahihi na ndio niliyoyamaanisha, wewe ulielewa ila ulichofanya ni kunikosoa na kunitaka niandike vile unavyotaka wewe, yani ulitaka nitumie maneno rahisi ambayo yangeweza kueleweka hata na mtu mwenye kichwa kigumu na uelewa mdogo na finyu kama wako
Maneno yako ni sahihi kwamba uliposema Mshahara ni Huduma ulikuwa sahihi??
Wewe ndio mjuaji halafu haujui
Hahahaaaa
Wako sawa kivipi

Ni wapi nimesema kwamba physical appearance siyo nature hebu acha kukaza fuvu, mimi nimesema kuogopa kiumbe sababu ya physical appearance yake siyo nature, yani uoga wa aina hiyo siyo nature bali ni made
Unajua unachokiandika kweli??
Sasa inategemea wewe muonekano mzuri kwako ni upi maana uzuri upo machoni pa mtu, mimi kuna jamii ya mbwa ambao nawaona ni wazuri lakini ni hatari, hata hao nyoka unaosema kwamba wana muonekano wa kutisha kuna watu wanawaona ni wazuri
Kwamba wale pet dogs na puppies ni hatari??
That is logical non sequitur mtu kumtii rais barabarani haihusiani na mwanamke kumtii mwanaume katika mazingira kama hayo, sijui kwanini unalazimisha kuhusianisha vitu kwa kuangalia category moja badala ya kuangalia hivyo vitu kwa ujumla, kumbuka huyo rais kinachoangaliwa hapo ni cheo chake na siyo jinsia yake
Cheo kina nini kwanini unamtii??
Tatizo ni kwamba unaleta maandiko bila uthibitisho unatakiwa ufahamu kwamba maandiko mengi yanakizana baina ya dini, kwahiyo unapoleta maandiko unatakiwa ulete uthibitisho kwamba maandiko ya dini fulani ndio ya kweli na ya dini nyingine ni ya uongo, vinginevyo bora usilete kabisa ni heri ujenge hoja zako nje ya dini kuliko kulazimisha na kunilisha maneno kuwa nimekana dini kana kwamba uliambiwa ukiniambia hivyo ndio utanitisha
Maandiko katika Utii wa Mke kwa Mumewe hayana Tofauti.
 
Tangu katikati ya Karne ya 19 harakati za ukombozi wa mwanamke (feminism) zilianza.

Lakini sio Harakati zote zilikuwa na Malengo makuu yanayofanana au Kuhusisha Kundi moja la Wanawake baina ya vizazi.

Katika historia harakati za kudai haki za wanawake zilianza Ulaya wakati haki za binadamu zilipoanza kutangazwa, ambazo awali zilijadiliwa kwa wanaume pekee.

Kutokana Na Tofauti Zilizopo Baina ya Vizazi kwenye Harakati za Feminism kuanzia Karne ya 19(1848) hadi karne Hii. Zimegawanywa Harakati hizi katika sehemu Kuu Tatu (au nne) (Waves)

First Wave: 1848 - 1920
Katika Wimbi hili Lengo kuu lilikuwa ni Kupambania Haki Sawa ya Kupiga Kula kati ya Wanaume na Wanawake (Suffragettes)

Harakati ya kuwapa wanawake haki za kupiga kura kwenye uchaguzi wa kisiasa ilikuwa kampeni ya awali kuanzia karne ya 19, lakini hasa ya 20.

Katika jambo hili waliohusika Walikuwa ni Wanawake wakizungu wenye hadhi ya Juu ambapo Wanaume weusi wa hadhi ya kawaida waliruhusiwa kupiga kura lakini Wanawake wa kizungu wa Hadhi ya Juu Hawakuruhusiwa.

Mnamo mwaka 1920 Rasmi Wanawake wa kizungu waruhusiwa kupiga kura.

Haikuwa hivyo hadi ilipofika mwaka 1965 ndipo Wanawake wa Rangi nyengine nao waliporuhusiwa kupiga kura.

Second Wave: 1963 - 1980s.
Katika Wimbi Hili Wanaharakati Walienda mbele zaidi kutaka Majukumu ya kijamii yatazamwe upya. Kwamba Mwanamke kazi yake si tuu kuwa Mke au Mama. Wakidai Usawa kati ya Wanaume na Wanawake.

Bado Harakati hizi ziliwahusu Sana Wanawake wa Kizungu Hadi kupelekea kuanzishwa kwa Harakati za Wanaharakati wanawake weusi(National Black Feminist Organization (NBFO)).

Third wave 1990- (radical feminism).
Harakati zimezonga mbele zaidi Kudai Usawa kamili Wa Mwanamke na Mwanaume katika nafasi za uongozi na majukumu ya kijamii.

Kwa mfano, kulingana na itikadi hii, tabia kati ya jinsia siyo za kibiolojia bali ni ya mafunzo tu.

Wafuasi hao wanaamini tofauti hizi zipo ili wanaume waweze kudhulumu wanawake.

Kwamba Mwanamke anaweza kufanya Kila Kitu ambacho mwanaume anaweza fanya Na Hizi tofauti zilizopo katika Jamii Ni matokeo ya Wanaume kuiaminisha Jamii kuwa Ni wao pekee wanaoweza kufanya hayo Jambo ambalo sio kweli.

Wimbi hili Limekufanya makundi mengi ya Jinsia na Rangi (Marginalized groups) Pamoja na Trans genders.

KATIKA MAELEZO HAYA UNAWEZA UKAONA KUWA HILI JAMBO LA U FEMINISM HALIKUANZA KAMA LILIVYO HIZI SASA HIVYO BAADA YA KUPATA NGUVU KUBWA YA KIMADALAKA HUENDA HARAKATI HIZI ZIKAFIKA MBELE ZAIDI KUDAI MASUALA MENGINE ZAIDI AMBAYO HATA HATUWEZI KUYAFIKILIA HIVI LEO. NA HAPO HUENDA KIKATOKEA KITU AMBACHO HATUWEZI KUKIFIKILIA KWA SASA.
 
Acheni hizi porojo zenu msingi wa mwanamke kumtii mwanaume uko katika mwanaume kumhudumia mwanamke huwezi kukitawala kiumbe usichokihudumia, kinachofanya wanawake wengi wa dunia ya leo kutokuwatii wanaume wao ni kile kitendo cha wao nao kuanza kujitafutia pesa na mali zao bila kuwategemea wanaume, hata mimi huwa nasema humu kama mwanaume anamhudumia mwanamke basi shurti huyo mwanamke amtii hiyo siyo hiyari bali lazima, ila kama mwanaume hawajibiki kwa lolote kwa mwanamke wake halafu anataka utii basi mtaendelea kulalamika na kutukana hadi mwisho wa dahari, huku mkisubiri mwanamke awe 'reject' ndio awe na utii
we mwongo kaka
 
Back
Top Bottom