Utitiri wa Festival za Makabila Nchini: Tumeanza Harakati za Kujitenga Kimakabila?

Utitiri wa Festival za Makabila Nchini: Tumeanza Harakati za Kujitenga Kimakabila?

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
1,033
Reaction score
723
Mara kadhaa hapa chini yamekuwa yakifanyika matamasha au shughuliza kijamii zinazolenga makabila fulani kama
WASUKUMA FESTIVAL.

WAHAYA FESTIVAL:
View: https://www.youtube.com/watch?v=qR_H1N7bWjo

WACHAGA FESTIVAL:
View: https://www.youtube.com/watch?v=DW0Qynrl7uE

NK.
Hizi festival mara nyingi huanzishwa kwa malengo mazuri, kama vile:
Festival hizi ulenga kuonesha mila, desturi, sanaa, na historia ya makabila husika. Hii husaidia kuhifadhi utamaduni ambao ungeweza kusahaulika pamoja kujenga mshikamano wa kijamii kupitia kusherehekea mila zao.

wakati mwingine utumia tamaduni hizo kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje, hivyo kuleta faida kiuchumi kwa eneo husika au kusaidia kukuza Lugha nyingi za asili ambazo ziko hatarini kupotea. Festival hizi hutoa nafasi ya kuzitumia na kuzifundisha vizazi vipya.

LAKINI KUNA HATARI YA KUENDELEZA UKABILA NA UBAGUZI.

Hata hivyo, kama festival hizi hazitasimamiwa vyema, zinaweza kuchangia ukabila kwa njia zifuatazo:

Kujitenga na jamii nyingine: mara nyingi hzii festival Ikiwa festival inalenga zaidi kutukuza kabila moja na kupuuza mengine, inaweza kuwatenganisha watu wa makabila tofauti.

Kujenga ubaguzi: Ikiwa hotuba au matendo katika festival hizo yanasisitiza "ubora" wa kabila moja juu ya mengine, hii inaweza kuibua chuki au hisia za kutoelewana.

Kuzorotesha umoja wa kitaifa: Tanzania imejengwa juu ya msingi wa umoja wa kitaifa. Mwalimu Julius Nyerere alisisitiza Azimio la Arusha na Siasa ya Ujamaa kwa lengo la kuondoa ukabila. Festival zinazojikita zaidi kwenye tofauti za kikabila zinaweza kudhoofisha maono haya.

KATIKA MJADALA mwandishi mkongwe Bw Phinias Bashaya nashauri njia za kuepusha nchi yetu kutumbukia katika lindi la ukabila kupitia haya matamasha

Moja ni vema matamasha haya yaahusisha makabila mengine: Badala ya kuwa sherehe ya kabila moja pekee, waandaaji wanaweza kualika makabila mengine kushiriki na kuonyesha utamaduni wao pia.
Kulenga mshikamano wa kitaifa: Badala ya kuangazia tofauti za kikabila, festival ziwe fursa ya kuonyesha jinsi makabila mbalimbali yanavyoweza kushirikiana na kuimarisha Tanzania.

Kuondoa hotuba za kibaguzi: Waandaaji wanapaswa kuhakikisha kwamba hotuba zote na maudhui ya festival hayana mwelekeo wa kubagua kabila lingine au kupandikiza hisia za chuki.

Pia nasema Serikali inaweza kuhamasisha festival za kitamaduni lakini kwa sharti kwamba zinachangia mshikamano wa kitaifa. Kufanya hivyo kunaweza kujumuisha:​

Udhibiti wa sera: Kuwa na mwongozo wa wazi juu ya jinsi festival za makabila zinavyopaswa kufanywa.
Kuhamasisha ushirikiano: Kupanga maadhimisho ya kitaifa ambapo makabila yote yanapata nafasi ya kuonesha utamaduni wao kwa pamoja, kama vile Siku ya Utamaduni.

Baadaye nitaweka hapa link ya mjadala huo.

Kwa kifupi, festival za makabila si lazima zionekane kama tishio kwa mshikamano wa kitaifa, lakini zinahitaji kusimamiwa kwa makini. Lengo kuu liwe kuenzi utamaduni wa Tanzania kwa ujumla badala ya kuimarisha tofauti za kikabila. Umoja na mshikamano vinapaswa kuwa misingi ya maadhimisho yoyote ya kitamaduni.
 
Back
Top Bottom