Utitiri wa shule za chekechea na Tuition wilayani Arumeru

Utitiri wa shule za chekechea na Tuition wilayani Arumeru

Emaoi

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2013
Posts
307
Reaction score
235
Wakuu narudia tena kuirudisha hii mada mpaka tupate majibu kutoka wizara husika. Kumekuwa na utitiri wa shule nyingi za chekechea na zingine zikiitwa Tuition zinazochukua watoto chini ya miaka mitano ambao hawajaanza shule. Katika safari zangu nilizotembea katika mji wa Arusha nimeona mjini hakuna shida sana labda uongozi wao Upo makini .

Sasa twende upande wa wilaya hii ya Arumeru/ Arusha DC kuna watoto wengi wanazagaa barabarani hakuna usalama wanatembea wenyewe na ni wadogo ukiwauliza wanatoka wapi wanasema shule.

Nimejaribu kuwauliza wenyeji kuanzia mitaa ya sekei, Sanawari ya chini mpaka Sanawari ya juu nimekuta chekechea nyingi zinaendeshwa kwenye nyumba za kupanga na maeneo mengine yasiyokuwa na vigezo .

Kwanza ukizingatia mazingira sio Rafiki kwa watoto hakuna fence wala vyoo na pia ukizingatia kipindi hiki cha corona watoto wanarundikana kwenye chumba kimoja hakuna hata ndoo za kunawa mikono.

Tunaomba kujua hizi shule za chekechea ziko chini ya mamlaka zipi? Kwakuwa hazina usajili na serikali haijawahi kuja kuzikagua na zinazidi kuwa nyingi mitaani. Hizi Tuition kwa watoto wadogo ambao hawajaanza shule na hizo chekechea zina usajili?

Nani ameruhusu watoto kuzagaa mitaani? Wizara ya Elimu tunaomba watendaji wenu wafuatilie hili kwa haraka na kama Serikali inazitambua je wanalipa kodi?

Arusha DC watu wa elimu mpo? Au hamtoki maofisini kutembea mitaani mjue mambo yanavyokwenda? Wizara ya elimu tunaomba fuatilieni watendaji wenu upande wa elimu huku Arumeru kumeoza wakaguzi hawapo
 
Acha watu watafute rizki mkuu, na wengi wao hapo ni degree holders, hivo kutokana na uhaba wa ajira wameamua kujishikiza huko, mostly ni wadada zetu hata mitaji hawana so ukisema wafungiwe wataish vp sasa.
 
Mkuu hakuna mahali nimesema wafungiwe bali tunahoji vigezo kama una vigezo huwezi kufungiwa. Suala la watoto wadogo ni lazima tuwe makini. Kuna mtoto mdogo alibakwa akitoka huko kwenye shule za vichochoroni
 
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom