Utitiri wa viwanda vya bati Tanzania na paa za nyumba zenye bati mijini kuwa na kutu ni Udhaifu mkubwa uliopo TBS

Utitiri wa viwanda vya bati Tanzania na paa za nyumba zenye bati mijini kuwa na kutu ni Udhaifu mkubwa uliopo TBS

Miji mingi Tanzania inakabiliwa na kupoteza ubora,nyumba nyingi zinaonekana kuchakaa hususani paa za nyumba nyingi kuonekana kuwa na kutu. Yawezekana ni bati kutokuwa na bati nyingi kukosa ubora licha ya hapa nchini Kuna taasisi ya umma inayoshughulika na ubora wa bidhaa.

Utitiri wa viwanda vya bati umeleta changamoto lukuki Kwa TBS kiasi Cha kushindwa kutambua uwezo wa bati kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa. Kiuhalisia mwanzo wa kufuatilia ubora wa bidhaa Kwa TBS huwa mwanzoni tu,ukishapata cheti Cha ubora, TBS huwa hawana muda wa kufuatilia,hapo ndipo viwanda huanza kuchakachua.

Tatizo lingine TBS wameshindwa kudhibiti ubora wa rangi kwenye mabati,bati zimekuwa zikipauka mapema tangu kupauliwa, siku hiz bati hupauka kuanzia mwezi mmoja Hadi sita tangu kupauliwa.

TBS inatakiwa kujitathimini, wengi wamejaa wafanyakazi wenye uwezo mdogo,connection zinaiharibu hii nchi.
Umesema sahihi kabisa, TBS wako mifukoni mwa watu fulani
 
Kabisa
Inazidi kwa mbali...pia hakuna bati la elfu kumi hata used.
Hiyo elfu kumi si bei ya bati, ni gharama ya kupaka rangi paa lote lililopata kutu, yaani ununue bati shs.400,000/= upake rangi shs.600,000/=! Hii ni biashara kichaa.
 
Back
Top Bottom