Utoaji Majina ya Viongozi katika Miundombinu ya nchi kusiwe ni kwa Mihemko, Unafiki, Ushkaji na Kukurupuka

Utoaji Majina ya Viongozi katika Miundombinu ya nchi kusiwe ni kwa Mihemko, Unafiki, Ushkaji na Kukurupuka

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Na All - Rounder nawaombeni enyi Watoa Majina Siku zingine kabla ya kutoa Majina ya Watendaji wenu au Wanasiasa muwe mnatuambia Kwanza Watanzania ni nini au kipi cha maana na chenye Tija kwa nchi na Jamii hao (hawa) Wahusika wamekifanya na Kinaonekana.

Nami naomba Mradi wa Umeme Rufiji au ule wa Treni ya Mwendokasi Dar to Dodoma au Bomba la Mafuta la Hoima to Tanga kwa Heshima ya Michango yangu na Mawazo yangu mema hapa JF na Mitaani basi mmoja wapo uitwe kwa Jina langu la All - Rounder. Mtakuwa mmenitendea haki na wala mtakuwa hamjakosea.

Na vyema pia hawa mnaokurupuka kuwapa Heshima ya Majina yao katika Miundombinu yenu hii muwe mnawauliza Kwanza kama watapenda muwape hizo Heshima kwani kuna wengine kwa ninavyowajua japo sasa wapo Makaburini wasingekubali kutokana na Unafiki wetu tunaowapa na tuliopo hai duniani.
 
Imekuwa kama fashion hivi sasa kubatiza miundombinu ya umma majina ya viongozi, hii si sawa kabisa. Lazima kuwe na utaratibu maalum wa kutoa majina katika miundombinu ya umma.

Siyo mtu anaamka na kutamka kwa kadri anavyojisikia. Na bahati mbaya majina yanatolewa kwa hawa viongozi wa sasa ambao hakuna tathmini ya kutosha imefanyika kuhusu mchango wao kwa Taifa.
 
Na All - Rounder nawaombeni enyi Watoa Majina Siku zingine kabla ya kutoa Majina ya Watendaji wenu au Wanasiasa muwe mnatuambia Kwanza Watanzania ni nini au kipi cha maana na chenye Tija kwa nchi na Jamii hao ( hawa ) Wahusika wamekifanya na Kinaonekana...
Kazi tunayo. Alikuwepo Katibu Mkuu Kiongozi Martin Lumbanga sijui kapewa nini
 
... usiwe na wasiwasi ndugu! Waache wafanye wapendavyo; siku zaja; Bwana atamwinua mtawala mwingine hayo yote yatawekwa sawa tu kwa kuzingatia Katiba na sheria za nchi.
 
Mradi wa bomba la mafuta Hoima Tanga sio mradi wa Tanzania
 
Kijazi=Tanroads
Mfugale=Tanroads
Magufuli=Wizara ya ujenzi (enzi za JK)

Najaribu ku connect dots, wote walikuwa wizara moja enzi za JK.
Kwa hiyo unataka kuniambia kwamba KMK anaekuja bada ya marehemu John W. Kijazi R.I.P atatokea Tanroad au Wizara ya Ujenzi?????......hapana, sidhani kama itakuwa hivyo!!!
 
Na All - Rounder nawaombeni enyi Watoa Majina Siku zingine kabla ya kutoa Majina ya Watendaji wenu au Wanasiasa muwe mnatuambia Kwanza Watanzania ni nini au kipi cha maana na chenye Tija kwa nchi na Jamii hao (hawa) Wahusika wamekifanya na Kinaonekana...
Mkuu Kijazi anastahili heshima kubwa sana. Uadilifu wake ndiyo tunaona matunda ya network ya barabara za lami nchi nzima. Zile mbovu nyingi zilijengwa baada ya Mh. Kijazi kukataa rushwa na hatimaye kuhamishwa na kupewa ubalozi ili watu waibe. So kila kiongozi anayepewa jina la kitu ana kitu muhimu kafanya kwa taifa.
 
Kwa hiyo unataka kuniambia kwamba KMK anaekuja bada ya marehemu John W. Kijazi R.I.P atatokea Tanroad au Wizara ya Ujenzi?????......hapana, sidhani kama itakuwa hivyo!!!
Sijasema hivyo mkuu, ila sitashangaa. Means JPM anapenda kufanya kazi na watu anaowafahamu vyema.
 
Imekuwa kama fashion hivi sasa kubatiza miundombinu ya umma majina ya viongozi, hii si sawa kabisa. Lazima kuwe na utaratibu maalum wa kutoa majina katika miundombinu ya umma. Siyo mtu anaamka na kutamka kwa kadri anavyojisikia. Na bahati mbaya majina yanatolewa kwa hawa viongozi wa sasa ambao hakuna tathmini ya kutosha imefanyika kuhusu mchango wao kwa Taifa.
Huwa nafurahi mno Kueleweka na Watu Werevu wa aina yako Ndugu.
 
Kwa hiyo unataka kuniambia kwamba KMK anaekuja bada ya marehemu John W. Kijazi R.I.P atatokea Tanroad au Wizara ya Ujenzi?????......hapana, sidhani kama itakuwa hivyo!!!
Nafikiri atatokea jeshini,JPM taasisi anayoiamini kuwa na hazina ya viongozi.
 
... usiwe na wasiwasi ndugu! Waache wafanye wapendavyo; siku zaja; Bwana atamwinua mtawala mwingine hayo yote yatawekwa sawa tu kwa kuzingatia Katiba na sheria za nchi.
Aanze kwa kufuta majina yasiyotija kwa taifa.Aweke usawa kwenye ajira atimue ndugu,kabila,dini pendwa wakaajiriane kwao.Nchi sio kampuni ya familia,sisi tulipe Kodi wao wasaze
 
Back
Top Bottom