Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO visa vya utoaji mimba takribani milioni 25 hutokea kila mwaka kote duniani, huku nusu ya visa hivyo ambavyo hukadiriwa kama milioni 12 pekee hutolewa kwa njia salama na nusu yake hutolewa kwa njia isiyo salama.
Utoaji huo wa mimba usio salama kote duniani husababisha vifo vya wanawake takribani 39,000 duniani kote huku inakadiriwa takribani 60% ya vifo hivyo hutokea barani Afrika na 30% hutokea barani Asia na 10% iliyobaki hutokea kwenye Mabara yaliyobaki yaani Ulaya , Marekani ya kaskazini na Marekani ya kusini.
Kabla ya kuendelea tuangalie maana ya utoaji mimba usio salama ni kitendo kinachofanywa kwa mwanamke ambaye ni mjamzito kwa yeye mwenyewe au akafanyiwa na mtu yeyote kwa kujua huku lengo lake ni kuutoa ujauzito kinyume na taratibu zilizowekwa kwenye nchi au taifa husika.
Utoaji huo wa mimba usio salama na wa siri huhusisha njia za kiasili na njia za kisasa zinazofanywa na baadhi ya wahudumu wa afya kwenye baadhi ya vituo vya afya ambavyo vingine vimesajiliwa na vingine havijasajiliwa kote nchini.
Utoaji mimba kwa njia za asili huhusisha unywaji wa mizizi ,majani ambayo huaribu mimba na kwa njia za kisasa huhusisha vidoge na njia nyingine za kitabibu.
Kwa hapa kwetu nchini utafiti uliofanywa na taasisi ya Guttmacher Institute ambayo inashirikiana na taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu pamoja na chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi muhimbili(MUHAS) zilibainisha takwimu kadhaa kuhusu hali ya utoaji mimba usio salama kwa hapa nchini kwetu nazo ni
Tanzania ni kati ya nchi zenye uwiano wa juu wa vifo wajawazito duniani (410 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa wakiwa hai) na utoaji mimba usio salama ni moja kati ya sababu zinapolekea idadi ya vifo hivyo.
Pia utoaji huo wa mimba usio salama unachangia theluthi (1/3) ya mabinti na akina mama wenye umri kati ya miaka 15 - 49 wanaolazwa mahospitalini kote nchini kutokana na matatizo yanayohusiana na mimba.
Pia utoaji huo wa mimba usio salama husababisha robo( 1/4 ) ya vifo vinavyotokana na uzazi kote nchini.
Pia utoaji mimba usio salama kwa Tanzania ni 36 kwa kila wanawake 1000 walio kwenye umri wa uzazi.
Inakadiriwa takribani 405, 000 ya visa vya utoaji wa mimba kwa mwaka 2013 zilitolewa nchini huku nyingi zikitolewa kwa njia isiyo salama na kuhatarisha maisha ya wanawake kote nchini na 66,600 ya wanawake walipewa huduma kwenye vituo vya afya kote nchini kutokana na matatizo ya utoaji wa mimba kwa njia isiyo salama.
Kulingana na takwimu hizo hadi leo tatizo hilo linatuandama kwenye jamii zetu kuna haja ya kuangalia tulipojikwaa na si tulipoaangukia. Hivyo basi huenda kuna sababu sababishi ya hali hizi ambazo tukizirekebisha huenda tukapunguza tatizo hili.
Miongoni mwa njia hizo ni kuongeza ufanisi wa elimu inayotolewa kuhusu uzazi wa mpango , elimu kwa sasa inatolewa lakini itabidi tuongeze ufanisi wa elimu hiyo kwa mifano kadhaa tutakayoiona nayo ni kama ifuatayo:-
Moja ya mfano kwa sasa vijana wengi hutumia muda mwingi kwenye internet site (mitandaoni) tofauti tofauti hivyo ni vyema elimu tuipitishe kwenye njia hizo kwa kufanya hivyo nafikiri walengwa wengi itawafikia.
Mfano mwengine kuna matamasha makubwa yanayofanyika kwenye nchi yetu kwa sasa nafikiri tukiandaa vipeperushi vinavyotoa elimu katika matamasha hayo huenda wadau wengi wakafikiwa na elimu ambayo wataifikisha kwa wake zao, dada zao na jamii kwa ujumla , mfano wa matamasha hayo ni kama matamasha ya kimichezo simba day na kilele cha siku ya mwananchi pia kuna matamasha ya kiburudani kama fiesta ya clouds media na mengine yanayofanywa na media zingine kama azam media sinema zetu ambazo hutembea sehemu kubwa ya nchi . matamasha ya aina hii ambayo yapo mengi nafikiri tuandae vipeperushi vinavyotoa elimu juu ya uzazi wa mpango elimu itakayotolewa huenda watu wakaelimika na ikawa sababu ya kupunguza vifo vinavyopatikana na utoji wa mimba usio salama na na ukosefu wa elimu ya uzazi wa mpango.
Njia nyngine nafikiri elimu ya mahusiano ianze kutolewa kuanzia shule zetu za sekondari awepo mwalimu kabisa wa kutoa hii elimu sababu kuna wimbi kubwa la vijana ambao hawajui ni nini mahusiano na muda upi sahihi wa kuanza mahusiano utashangaa binti wa miaka 16 anakwambia mimi simuamini mwanaume yeyote kwa yaliyonikuta cha kushangaza ni binti wa miaka 16 lakini huenda kashatendwa au kusalitiwa kimahusiano si chini ya mara 5 na je mfano kwenye mahusiano hayo angepata ujauzito kwa vyovyote angetumia njia ambazo si salama kuutoa kwa lengo la kutopata aibu katika jamii au kumkomesha mwanaume aliyemsaliti na kwa hali kama hiyo mabinti zetu wengi tunawapoteza kwa sababu ya kutojua elimu ya mahusiano .
Serikali yetu inayoongozwa na Raisi mh Samia Suluhu inajitahidi kwenye kudhibiti athari ambazo zilikua zinawakuta mabinti zetu kwa matatizo yanayoikumba jamii yetu kama matatizo ya mimba za utotoni mfano wa jitihada hizo ni kuwarudisha shule wale mabinti waliojifungua au wale wenye ujauzito kuendelea na masomo ili wasiingie kwenye sekeseke la msongo wa mawazo ambalo upelekea utoaji wa mimba kwa njia isiyo salama , kwa serikali kufanya hivyo iliwafanya mabinti wajione bado hawajapoteza lolote kwenye jamii kwa kua wanaweza kuendelea tena na masomo na kutimiza malengo yao.
Lakini kama ilivyo kwa waswahili husema ukiona kosa linarudiwarudiwa huenda sheria ya jambo hilo bado watu hawaiogopi kwa maana adhabu inayotolewa ni ndogo au faini inayotolewa kwa vituo vya afya au matabibu wanaofanya shughuli hizi za utoaji mimba kwa siri kwa njia zisizo salama ni ya kawaida kiasi cha kusababisha tatizo hili kuendelea hivyo kuna haja ya wadau wa sheria kukaa tena na kuishauri serikali kipi kifanyike.
Viongozi wa dini, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla tuongeze elimu ya kiimani na ya kimaadili kwa mabinti zetu juu ya kuingia kwenye mahusiano ambayo si salama , elimu juu ya ukubwa wa dhambi hii ya kutoa mimba na elimu ya uzazi wa mpango kama imani zilivyofundisha.
Pia viongozi wa dini tuwape elimu waumini wetu haswa wanaume wanaosabibisha hizi mimba kwa mujibu wa imani zetu, sababu ukiliangalia jambo la ujauzito kisayansi lazima mwanaume na mwanamke wakutane na baada ya hapo kama sababu zote za kihali kimwili ziko sawa lazima ujauzito upatikane hivyo basi hawa wanaume tuwafikishie mawaidha na mahubiri mbali mbali juu ya kuwasababishia wanawake ujauzito kisha kuwakimbia au kuwasaliti ni dhambi juu ya dhambi .
Visa vingi vya utoaji mimba usio salama baadhi ya mabinti husema ni ugumu wa maisha au kusalitiwa, kukimbiwa na walio sababisha hizo mimba.
Hivyo elimu ya kiimani ikitolewa kwa wanaume juu ya kutowasiliti wanawake huenda ikapunguza tatizo hili.
Jamii pia kama ilivyo desturi yetu watanzania mtoto wa mwenzako ni wako na sisi tujikune pale tuwezapo juu ya kutatua hili kwa mawazo na mapendekezo mbalimbali kwa sekta zinazohisika kutatua hili.
Rejea
Guttmacher.(2016)."utoaji mimba usio salama ni jambo la kawaida nchini Tanzania".https://www.guttmacher.org

Upvote
1