Utoaji wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT), leo September 28, 2024

Utoaji wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT), leo September 28, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

View: https://www.youtube.com/live/xHd53cbsmoA?si=Rm1YGprC9EkHdvry

Snapinsta.app_461509597_500974169594163_7711485901875162466_n_1080.jpg

Snapinsta.app_461260388_536844668755030_3761315146850983996_n_1080.jpg



Zoezi la Utoaji Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) linaendelea muda huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ndiye Mgeni Rasmi akimuwakilisha Spika Tulia Ackson.

ZUNGU: KALAMU YA MWANDISHI WA HABARI INA NGUVU KULIKO UPANGA
DAR: Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amewataka Wanahabari kutumia taaluma yao ya Uandishi kulinda amani na kusimamia misingi ya taaluma pamoja na maadili ya kazi yao

ZUNGU: TUJIELIMISHE KUHUSU MATUMIZI YA ‘AI’ ILI KUPUNGUZA UPOTOSHAJI
Akizungumza katia hafla ya Utoaji wa Tuzo za umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania, (#EJAT), Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ametoa wito kwa Jamii kuwa makini na matumizi ya Akini Mnembe (AI), ili kuondoa upotoshaji, uzushi na kusababisha taharuki



==================== ===================​

Majaji saba wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) wamehitimisha kazi ya kutathmini ubora na weledi wa kazi zipatazo 1,135 na kuwateua waandishi wa habari 72 watakaoingia katika kinyang’anyiro cha kumtambua mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu na mshindi wa jumla.

Kati ya waandishi wa habari 72, wanaume ni 45 (sawa na 62.5%) na wanawake 27 (sawa na 37.5%). Kati ya wateule hao, wateule 14 (19%) wanatoka katika runinga; 13 (18%) wanatoka vyombo vya mtandaoni, redio 20 (28%) na wateule 25 (35%) wanatoka kwenye magazeti.

Wateule wamepatikana kwa kukidhi vigezo vya ubora ambavyo ni pamoja na ukweli, usahihi, uanuai, haki, kina, utafiti, ubunifu, uvumbuzi, upekee, uchambuzi, uwajibikaji, ufichuaji maovu, uadilifu, uwasilishaji unaoeleweka na uchunguzi. Ifahamike pia kwamba vigezo maalum vilitumika kuzingatia aina tofauti ya vyombo vya habari kama vile redio, televisheni, magazeti na habari za mitandaoni.

Kabla ya kutaja majina ya wateule hao 72 ni muhimu ifahamike kwamba kinyang’anyiro cha kumtambua mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu na mshindi wa jumla kwa makundi 20 ya kushindaniwa kitakuwa siku ya jumamosi, tarehe 28 Septemba, 2024 ambapo mgeni rasmi katika siku ya kilele cha kinyang’anyiro atakuwa ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Mabunge Duniani, Dkt Tulia Akson.

Mgeni rasmi ndiye atakayemkabidhi tuzo mshindi wa jumla atakayewapiku kwa umahiri waandishi wengine 71 katika hafla itakayofanyika katika ukumbi wa Aga Khan Daimond Jubilee, Dar es Salaam. Hii itakuwa ni mara ya 15 kutoa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Tanzania.

Moja ya jambo la kipekee katika kilele cha kinyang’anyiro hicho ni pamoja na kusikia kutoka kwa jopo la majaji kuhusu viwango vya uandishi wa habari za magazeti, redio, televisheni na mitandaoni kwa habari zilizohusu uwekezaji wa kampuni ya DP world katika bandari za Tanzania, habari kuhusu Ngorongoro na wamasai na kuhusu maporomoko ya Hanang.

Jambo la pili la kipekee ni kumshuhudia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry Silaa akizindua Jarida la Tuzo na Tuzo magazine ambayo yanajikita kuhamasisha umahiri katika sekta mbalimbali Tanzania na nje ya Tanzania. Kwa kuanzia majarida hayo, moja la Kiswahili na lingine la Kiingereza yatabeba maudhui ya tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Tanzania (EJAT).

Moja ya maudhui katika majarida yote mawili ni simulizi ya maisha ya wateule wote. Kazi ya kuandika simulizi hizo inaanza leo, hivyo wateule wote wawe tayari kufikiwa na waandishi wa Jarida la Tuzo wakati wowote kuanzia sasa. Maudhui mengine ni ya wafadhili wa tuzo ambao simulizi zitahusu mchango wao katika kubadilisha maisha ya watu ikiwemo kukuza na kujenga tasnia ya habari.

Aidha ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza kazi za kihabari kwa EJAT 2023 zimeongezeka hadi 1,135 kutoka kazi 893 za EJAT 2022. EJAT 2020 kazi zilikuwa 396 na EJAT 2021 kazi zilikuwa 608.

Waandishi wa habari wa mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka huu waliongoza kwa kuwasilisha kazi 290, wakifuatiwa na mkoa wa Arusha uliokuwa na kazi 81, Mwanza kazi 74, Iringa ilishika nafasi ya nne kwa kuwa na kazi 72, wakati mkoa wa Mtwara ulishika nafasi ya tano kwa kuwa na kazi 49. Kwa upande wa Zanzibar, kazi zilizopokelewa ni kutoka Kaskazini Pemba (36) Pemba Kusini (43) na Mjini Magharibi (29).

Dirisha la kupokea kazi za waandishi wa habari lilifunguliwa tangu Novemba 15, mwaka jana na kufungwa Februari 28, mwaka huu. Kazi ya kuchambua na kutathmini ubora wa kazi za kihabari za mwaka 2023 ilianza tarehe 7 hadi 15 baada ya Naibu msajili wa mahakama kuu, Morogoro, Mheshimiwa Fadhil Mbelwa kuwaapisha majaji.

Jopo la Majaji liliongozwa na Halima Shariff, katibu wake Dkt Egbert Mkoko na majaji wengine wakiwa ni pamoja na Ndugu Mkumbwa Ally, Eshe Muhiddin, Jeniffer Sumi, Halima Msellemu na Absalom Kibanda.

Jopo lilichaguliwa na wakuu wa taasisi za kihabari zinazounda kamati ya maandalizi ya EJAT kwa kuzingatia uadilifu, ujuzi na uzoefu katika uandishi wa habari, uwezo wa kuchambua na kutoa tathmini sahihi, uelewa wa mabadiliko ya kidigitali, uzoefu wa kimataifa au wa kijamii.

Aidha, jopo la majaji lilizingatia uwiano wa kizazi kipya na cha zamani, waliopo kazini na waliostaafu, wabobezi wa maudhui mahsusi, usawa wa kijinsia, uwakilishi wa Zanzibar na Tanzania Bara na uwakilishi wa aina ya vyombo vya habari (magazeti, redio, luninga na mitandao).

Mbali na Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari, mchakato wa kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Maisha ya Mafanikio Katika Uandishi wa Habari (LAJA) 2024 unatarajiwa kuhitimishwa leo na wakuu wa kamati ya maandalizi. Tuzo hii humtambua mwandishi ambaye katika maisha yake ametoa mchango mkubwa katika kuiendeleza tasnia ya habari.

Taasisi zinaounda Kamati ya Maandalizi ni Wakfu wa Vyombo vya Habari (TMF), Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri (TEF), HakiElimu, Umoja wa Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Sikika, Misa – Tan na Twaweza.
 
Back
Top Bottom