Utofauti kati ya mashabiki wa Simba na Yanga

Afisa Tabibu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2021
Posts
511
Reaction score
848
Mashabiki wa hizi timu kubwa mbili hapa Tanzania wanatofautiana katika maeneo haya;

1.Timu inapofanya vibaya iwe wachezaji hawajitumi au kocha anazingua, Mashabiki wa Simba huwa wakali hata kuwarushia chupa wachezaji wao, mashabiki wa Yanga huwa wanatafuta hata kitu kdg kizuri wanakikuza na kujifariji na hicho.

2.Mashabiki wa Simba wameshaona kama vile timu yao haishiriki ligi kuu ya NBC wanaumia zaid wakifungwa klabu bingwa kuliko kufungwa hata na Ihefu, tofauti na mashabiki wa Yanga.

3.Mashabiki wa Yanga wapo na timu yao wakat wowote kwa muda wote, mashabiki wa Simba sio wavumilivu sana kweny magumu

4.Mashabiki wa Yanga ni wabunifu sana kweny staili za kushangilia kuliko Mashabiki wa Simba na ndo maana mashabiki wa Yanga wana majina makubwa na kujulikana kuliko wale wa Simba

5.Ni rahis sana kuwadanganya na kuwapumbaza mashabiki wa Yanga, na ndo maana hata wakitolewa kweny mashindano au kufungwa, Viongozi wao hutumia propaganda rahis sana nao husahau mapema, hii ni tofaut na Simba, rejea mwaka Simba anatolewa na Ud songo.

6.Viongozi na wachezaji wa Simba wanawaogopa sana mashabiki wao kuliko Viongozi na wachezaji wa Yanga, Wachezaji wa Yanga wamerelax sana, hawana hofu ya mashabiki

7.Mashabiki wa Yanga wananunua na kuvaa sana Jersey zao kuliko mashabiki wa Simba

8.Mashabiki wengi vijana wa Yanga ni wapambanaji tu mtaani, Mashabiki wengi vijana wa Simba ni wa Kishua.
 
Huu uzi wako naona umeamua kuthibitisha kuwa mashabiki wa yanga ni manyani.. Hawana maamuzi yao binafsi.
 
9. Mashabiki wa simba wanaipenda sana timu yao ndio mana hujaa sana uwanjani pindi timu yao inapocheza kuliko mashabiki wa yanga ambao kwenda uwanjani ni kwa mbinde
Mbona yanga anaongoza kwa mapato overall?
 
Points zako kadhaa zinaonesha zahiri shahiri kuwa ndio sababu inayoipelekea Simba kufanya vizuri kudogo kimataifa kuliko sisi migongo wazi (Yeboyebo)
 
"Simba ni wa Kishua" hii siyo kweli kabisa wengi ni wa kiswazi ndiyo maana uswahili ni mwingi sana Simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…