Utofauti wa mishahara katika Utumishi wa umma, kunavunja moyo na kusababisha watu kubeza kusoma sana

Utofauti wa mishahara katika Utumishi wa umma, kunavunja moyo na kusababisha watu kubeza kusoma sana

Mkuu hawa wana leta hoja za kitoto sana.kama wamechoka kazi waache tu vijana wengi sana jobless mtaani.

Wanaongea vitu ambavyo sio practical kabisa. Mishahara haiwezi fanana tu kisa mna elimu sawa au fani sawa.

Tija, ugumu, unyeti na risk ziambatanazo Na kazi husika ndovina determine mshahara.

Dereva wa rais wanataka alipwe sawa Na dereva wa halmashauri serious kabisa!!!! MTU unamuendesha the most important person katika nchi ulipwe sawa Na MTU anaendesha milingoti kuipeleka site !!!
Mfano mzuri ni Air Traffic controllers wa TCAA ambao baada ya kuwa recruited wanachukua miaka 2 kuwa trained kwenye chuo cha usafiri wa anga kisha wanafanya mitihani ya leseni ya kimataifa ili wafuzu kufanya kazi rasmi.
Bado vipimo vya afya kila baada ya mwaka ili waendelee kuwa bora. Kazi yao ina tension ya kutosha imagine ndege zikigongana tu kwenye airspace ya TZ kesi yake sio ndogo.
Technically mishahara yao haiwezi kuwa sawa na wenzao waliosoma nao bachelors degree ya Physics, Mathematics au Geomatics.
 
Mkuu...hili swali la dereva wa rais vs dereva wa halmashauri/tanesko hamna aliyelijibu.
Nimejaribu kulirudia tena na tena lakini halijibiki.

Wote wamelikwepa kama hawajaliona vile.
Wanacho suggest sio kitu practical kabisa.

Hakuna equality ya namna hio. Dunia ndo IPO hivyo and they have to accept it.
 
Harmonisation of salaries sio kumpandisha aliechini na kumshusha alioko juu waje walingane sawa kwa sawa.
Maana halisi ya mleta mada ni kusiwe na gap kubwa la mishahara kwa watu wenye skills sawa, kisomo sawa na pengine majukumu sawa.
Mahali inji hii ilipofikia ambapo wafanyakazi wamekuwa wapole, waoga na wanyonge serikali ikisema HARMONISATION ianze hata kesho inaanza sema suuu uoneee.
Yy mwenyewe kashasema kashusha mshahara wake sasa nani mwingine ajikune akitaka inakuwa tuu.
 
Nilishangaa kuona salary slip ya ndugu yangu mmoja ambae ni police mwenye cheo cha ACP,ni RTO kwenye moja ya mikoa hapa nchini..mshahara wake kabla ya makato ni 2.1m..nikajisemea ndio maana police wanakula rushwa sana asee.yani cheo kikubwa afu mshahara kiduchu.
Kuwa serious aisee ACP wa polisi awe RTO? Au ulimaanisha ASP.
 
Wakati watu wanahimizwa kusoma tangu utotoni na kujiendeleza hata wakiwa makazini, ila ukweli ni kwamba, kusoma sana na kupata ma-degree mengi, sometimes huwa hakuna maana sana na hii ni kutokana na ulipaji wa mishahara serikalini kutegemea mtu anafanya kazi katika taasisi au shirika gani la umma.

Unaweza kuwa na masters ila kama uko wizarani au katika Halmshauri, unawezakuta unazidiwa mshahara na mtu mwenye Bachelor au hata Diploma anaefanya kazi katika taasisi (mara nyingi hizi Authority) za serikali. Hapo bado marupurupu.

Kwa mfano, dereva mwenye form iv anaeanza kazi pale BOT au TRA, sijui kama anazidiwa mshahara na mtumishi anaenza kazi akiwa na Diploma au Bachelor katika Halmshauri zetu.

Haya mambo ya kila taasisi kuwa na scale zake za mishahara, sometimes kunaondoa kabisa maana nzima ya kukaa darasa moja na kusotea degree ile ile wakati mkija kuajiriwa mmoja anakuwa yuko mawingumi na mwingine ardhini.

Kuna umuhimu wa serikali kutazama upya jambo hili na kufanya harmonisation ya mishahara serikalini ili kuondoa hali hii.Mambo ya kusema kuna taasisi zinazalisha au zinaingiza fedha serikalini hakutoia uhalali wa huu upendeleo kwani elimu waliyonayo wangeipata wapi bila mwalimu au wakiuguwa bila daktari au nesi watakuwa na afya ya kukusanya hizo hela na kuzipeleka serikalini au kutoa gawio kwa serikali?

Kama huu utofauti ni lazima uwepo (haukwepeki!), basi uwe reasonable na sio kuwa na ma- gape makubwa na ya kukatisha tamaa kwani ukweli wote tunategemeana. Wewe unaelipwa mshahara wa mamilioni, bila Polisi usalama wa mali zako ungetoka wapi?

Siku tukipata mtawala ataeamua kuweka wazi/hadharani scale za mishahara kwa watumishi wa umma, nadhani siku hiyo mitandao ya kijamii itashindwa kuhimili mijadala itayoibuka baada ya hapo, na huyo Raisi atajizolea sifa nyingi iwapo atahakikisha kunawakuwa na harmonisation ya mishahara serikalini.

Kama mnasema kila mtu na bahati yake, basi hata wakati wa ukoloni wazungu na wahindi ilikuwa sahihi kulipwa mishahara minono kutokana na bahati yao ya kuwa na ngozi nyeupe.
Na kubwa zaidi wote sisi ni watanzaniaaa
 
Sasa wewe nani anakuambia ukaombe kazi huko halmashauri..?
 
ASP awe RTO, Kuwa serious bwana, ASP unajua ni nyota tatu? RTO wengi ni SSP na ACP
Mhh kuna ma DTO wa nyota moja na ma RTO wa nyota tatu....

Nilifikiri ma ACP hupewa u RCO na RPC tuu sikujua siku hizi ma ACP hupewa u RTO...
Btw: ACP awe na 2.1M kabla ya makato?
 
mtoa mada anahoja nzuri ila watu humu wanatoa majibu sio mfano mm nina jamaa zangu nilisoma nao chuo fulani wanemalia degree ya elimu hesabu na wote gpa zao ni 4.2 mmoja aliajiriwa kufundisha shule ya secondary mshahsra TGTS D1 ni 716,000 apo hajakatwa makato mwingine aliajiriwa kama tutor udsm mshahara ni 1.6M

kumbuka wote elimu sawa kabisaaa

shida hapa serikali inatakiwa kuwavuta wale wenyemishahara midogo angalau wapande wafanane na wengne
Uko sahihi
 
mtoa mada anahoja nzuri ila watu humu wanatoa majibu sio mfano mm nina jamaa zangu nilisoma nao chuo fulani wanemalia degree ya elimu hesabu na wote gpa zao ni 4.2 mmoja aliajiriwa kufundisha shule ya secondary mshahsra TGTS D1 ni 716,000 apo hajakatwa makato mwingine aliajiriwa kama tutor udsm mshahara ni 1.6M

kumbuka wote elimu sawa kabisaaa

shida hapa serikali inatakiwa kuwavuta wale wenyemishahara midogo angalau wapande wafanane na wengne
Nadhani mnashindwa kutofatuisha tofauti ya elimu na kazi, unalipwa kwa kazi (yaani position ilunayokuwa selected, ulipwi kwa elimu). Kuna tofauti kubwa ya kuwa mwalimu wa chuo vs secondary
 
Back
Top Bottom