Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
kwa waliotembelea Kigali (though not the whole Rwanda), kuna kitu kikubwa sana nimejifunza toka kwao, ambacho muda unavyoendelea wanaweza kufikia level zile za nchi za ulaya kabisa kwenye suala la usafi.
1. Tanzania usafi wa mazingira tupo nyuma sana, wenzetu wameweka misingi iliyokwisha ingia kwenye tabia ya mtu binafsi, ila sisi ipo tu kwenye nadharia ila mioyoni watu ni wachafu sana wa mazingira.
2. Barabara kuanzia Kibamba hadi Ubungo kwa mfano, imejengwa vizuri sana kuliko hata barabara za Kigali, kuna gardens katikati na pembezoni mwa barabara, lakini hazijafyekwa vizuri na kusawazishwa. wenzetu ulaya na kigali kidogo, pembezoni mwa barabara na kwenye gardens hata kwenye nyua za nyumba za watu, wamesawazisha na kama maji yapo wamemwagilizia gardens. hapa unakutana na vichaka katikati ya barabara na pembezoni, mateja wanakunyya na wazinzi wamerusha condoms.
3. Pembezoni mwa barabara, kuna marundo ya uchafu watu wamemwaga usiku. zile takataka magari ya uchafu yanapita kukusanya, DSM huwa wanatoka usiku wanamwaga karibu na barabara. ni uchafu wa moyo kabisa.
4. Pembezoni mwa barabara kuna gereji bubu kibao. angalia kutoka kibamba hadi ufike fire, kuna gereji bubu ngapi.
5. Pembezoni mwa barabara kuna vituo vya bodaboda na bajaji ambavyo sio rasmi. barabara nzurii ila kwa uwepo wa hawa jamaa holelaholela haina tofauti sana na zamani.
6. Mama ntilie wamejazana pembezoni mwa barabara, wanapika vyakula, kwenye lami zilezile safi, wanaosha mabakuli ya ugali na kumwaga barabarani. wakimaliza hawasafishi.ndio maana nnzi zipo everywhere DSM.
7. Wamenya machungwa na maembe na wauza mahindi ya kuchoma wamepangana pembezoni mwa barabara. barabara safiii ila unakutana na mtu kaweka toroli lake pale anakata machunga, wengine wanadondosha takataka haokoti anaacha palepale.
Kuna mengi ya kuandika. kwa wale wasioelewa, sijashobokea Kigali kana kwamba mimi ni mshamba hapana, nimeishi ulaya miaka mingi tu, najua maisha ya hapa na mbele, ila kwa afrika nimeona kama kigali wamejitahidi kwasababu vitu vyoote hivyo nilivyoorodhesha hapo juu, hauwezi kuvikuta pale, na ndio maana kidogo kidogo inaenda kuipiku Arusha kama Geneva ya Africa, mashirika makubwa na mikutano imeanza kwenda kigali badala ya Arusha.
Arusha imeshindwa nini, au Tz imeshindwa nini kuweka sheria za mchuma ili mazingira yawe safi na watu watajiadjust wenyewe polepole itafika mahali wataona ni tabia kuwa msafi.
mbarikiwe.