Utofauti wa viti kwa Waziri Mkuu, Mawaziri, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri una tija gani kwa taifa?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Hapa nchini viongozi wote wakubwa huwa wanawekwa viti vya kukalia vyenye utofauti na watendaji au washiriki wengine wanapokuwa katika matukio mbali mbali ya kikazi yanayohitaji vikao.

Ukiingalia kiti cha waziri mkuu au mawaziri wengine wanapokuwa kwenye vikao hivyo na watendaji wao utagundua mara zote vina utofauti na vingine.

Mantiki ya kuweka huu utofauti ni nini, ilianza lini na ina tija gani? Hivi kweli kwenye nchi yenye matatizo lukuki kama hii kuna watu wanalipiwa kufikiria na kufanya kazi kama hizo za kuchagua na kuweka viti vya kipekee kwa baadhi ya viongozi wa serikali?
 
Kuna kile kiti cha uvivu anakalia baba tu.
Ole wako akute umekifungua na umekalia.
 
Wababa washamba ndio huwa na vyeti vyao spesho.Hata kuku akichinjwa wanatafutiwa sehemu zao spesho.Viongozi wetu watakuwa wanaiga huu utamaduni kwenye kuongoza nchi.
... ha ha ah! Firigisi ni za baba! Hamruhusiwi kula hadi baba aanze! Mambo ya kale sana hayo!
 
Kuna kile kiti cha uvivu anakalia baba tu.
Ole wako akute umekifungua na umekalia.
... mambo ya kale sana! Radio haiguswi na mwingine zaidi ya baba ndiye ataamua msikilize stesheni gani na hata kubadilisha "mawe" ni yeye tu!
 
Hapa nchini viongozi wote wakubwa huwa wanawekwa viti vya kukalia vyenye utofauti na watendaji au washiriki wengine wanapokuwa katika matukio mbali mbali ya kikazi yanayohitaji vikao.

Ukiingalia kiti cha waziri mkuu au mawaziri wengine wanapokuwa kwenye vikao hivyo na watendaji wao utagundua mara zote vina utofauti na vingine.

Mantiki ya kuweka huu utofauti ni nini, ilianza lini na ina tija gani? Hivi kweli kwenye nchi yenye matatizo lukuki kama hii kuna watu wanalipiwa kufikiria na kufanya kazi kama hizo za kuchagua na kuweka viti vya kipekee kwa baadhi ya viongozi wa serikali?
Achana na viti anza na magari yao mkuu, hawa ni waporaji wa rasimali za nchi
 
Hizi mambo za maviti ni huku afrika tu ulishawahi kuona wazungu wanazunguka na maviti kama waganga wa kienyeji, akili ndogo tunashida sana hatuwazi mambo ya maana hata kidogo
 
Back
Top Bottom