jo5
JF-Expert Member
- Dec 15, 2022
- 894
- 1,381
Kweli aseeHapo umesahau kua kule kijijini ukiondoka unafungishiwa furushi la mazaga.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli aseeHapo umesahau kua kule kijijini ukiondoka unafungishiwa furushi la mazaga.
Sasa huyu mwanamke,ukarimu,ucheshi na kujali inawezekana kweli,wakati ndani hakuna hela?maana vyote hivyo vinakuja kama kuna msosi ndani...Ndoa ikipata mwanamke mkarimu, mcheshi kwa wageni na mwenye kujali hufanya wageni wafurahie sana wanapotembelea familia hiyo. Watoto humuiga sana mama.
La pili malezi, wazazi hawawafundishi watoto wao jinsi ya kuwakarimu wageni.
Hata mimi nshausoma uzi wa aina hii hapa jukwaani. Mfano ulikuwa ni Dodoma-Dar, sio Dar-Njombe kama nakumbuka vizuri.Kwani hiki kisa watu wa mkoani mtakirudia mara ngapi?
Mzee pesa na ukarimu havihusiani. Mtu anaweza akawa na pesa na bado ni mchoyoSasa huyu mwanamke,ukarimu,ucheshi na kujali inawezekana kweli,wakati ndani hakuna hela?maana vyote hivyo vinakuja kama kuna msosi ndani...
Mimi sikuwahi kusoma hiki kisa,Kwani hiki kisa watu wa mkoani mtakirudia mara ngapi?
FactUmeenda semina Njombe, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Ramadhani shukia kwa Sanga. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".
Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.
Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo.." Unakula unashiba.
Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene. Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.
Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".
Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti" Housegirl anaenda kufungua. Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.
Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajashituka kuna mtu kaingia. Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!
Mnazungumza kigogo, unamuuliza habari ya Dodoma. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza kuchat, mke wako naye anachat! Sitting room imejaa watu, lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula"
Unamgeukia mdogo wako unamwambia "aisee we jitegemee, hapa kima mtu anakula kwa wakati wake.!". Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza peke yake. Maji ya kunawa hakuna! Bahati nzuri dada wa kazi anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye "Hw basin" maji yanatoka!
Anaenda kunawa kinyonge. Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting room. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unampa, unamwambia chukua hii utalipa hiyo bodaboda.
Boda inafika, ndugu yako anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka. Mama bado yupo busy na simu anachat. Watoto game limekolea, hawataki kutoa macho kwenye computer. Ndugu yako anawaaga hata hawamuangalii usoni. Wanatupia kwa mbaali "kwa heri ba mdogo" wanaendelea na game. Ndugu anakamata mchuma na kuondoka.
____
Wengi tunaoishi mijini tuna maisha ya aina hii, na tunaona ni sawa. Tunajifanya tupo busy kwenye mambo yasiyo na msingi na kupuuza utu wa wengine. Hata watoto wetu tunawalea ktk mazingira ya kuthamini zaidi vitu kuliko utu. Hii si sawa hata kidogo. Tuwatendee wengine kama tunavyotaka kutendewa.
Share na wengine
Daah ww jamaa ww umeongea ikweli mtupu..tena hiko kutokujali utu hasa kwa hapa dar kupo kwenye zile familia zilizojipata zinazoona zinaishi kizungu..inasikitisha sanaUmeenda semina Njombe, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Ramadhani shukia kwa Sanga. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".
Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.
Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo.." Unakula unashiba.
Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene. Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.
Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".
Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti" Housegirl anaenda kufungua. Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.
Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajashituka kuna mtu kaingia. Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!
Mnazungumza kigogo, unamuuliza habari ya Dodoma. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza kuchat, mke wako naye anachat! Sitting room imejaa watu, lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula"
Unamgeukia mdogo wako unamwambia "aisee we jitegemee, hapa kima mtu anakula kwa wakati wake.!". Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza peke yake. Maji ya kunawa hakuna! Bahati nzuri dada wa kazi anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye "Hw basin" maji yanatoka!
Anaenda kunawa kinyonge. Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting room. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unampa, unamwambia chukua hii utalipa hiyo bodaboda.
Boda inafika, ndugu yako anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka. Mama bado yupo busy na simu anachat. Watoto game limekolea, hawataki kutoa macho kwenye computer. Ndugu yako anawaaga hata hawamuangalii usoni. Wanatupia kwa mbaali "kwa heri ba mdogo" wanaendelea na game. Ndugu anakamata mchuma na kuondoka.
____
Wengi tunaoishi mijini tuna maisha ya aina hii, na tunaona ni sawa. Tunajifanya tupo busy kwenye mambo yasiyo na msingi na kupuuza utu wa wengine. Hata watoto wetu tunawalea ktk mazingira ya kuthamini zaidi vitu kuliko utu. Hii si sawa hata kidogo. Tuwatendee wengine kama tunavyotaka kutendewa.
Share na wengine
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Watu wa mikoani tuna lawama sana, na watu wa Dar baada ya kujua hilo siku hizi wanatuzimia simu kabisa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Na ata tukija msibani tunaanzaga kula sisi. Wakati kaburi hatujachimba, wala nn. Ila tumepiga full black na miwani kama Kanye West.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mkuu maisha ya town changamoto sana kuna siku nilikuwa napita flyover ya Kijazi pale ubungo imagine kuna jamaha alikuwa Anaongea na bi mkuwa wake. mama mwezi wa kumi na mbili wadogo zangu waje Tu ilihali yeye kalala chini ya flyover
Upendo unazidi kupotea, binadamu wengi tumekuwa wabinafsi, hata kwenye magroup ya ndugu ya Whatsapp watu wapo kinafki, usoni wanaongea vizuri, wakila Kona kila mmoja anamsema vibaya mwenzake, mara nyingi mtu akipata uhakika wa tsh 200 ndo anakua na tabia hizo za ndugu wa dar Half americanHuu ni ukweli kabisa, watu wengi hawathamini wageni kwa namna wanavyompokea mpaka mgeni anakosa amani, hii hali haipo tu dar, ipo mijini kwenye miji mingi iliyochangamka.
Mgeni unaweza kuwaza huenda labda hawajapenda niende kwao.
Waambie waambie, Mimi nakuaga mchoyo nikiwa Sina hela, ila nikiwa na hela nazigawa kama zoteMzee pesa na ukarimu havihusiani. Mtu anaweza akawa na pesa na bado ni mchoyo
Unafiki kwa ndugu ni kawaida sana naona imeshazoeleka ila inashusha sana upendo ambao ndio msingi wa familia na undugu.Upendo unazidi kupotea, binadamu wengi tumekuwa wabinafsi, hata kwenye magroup ya ndugu ya Whatsapp watu wapo kinafki, usoni wanaongea vizuri, wakila Kona kila mmoja anamsema vibaya mwenzake, mara nyingi mtu akipata uhakika wa tsh 200 ndo anakua na tabia hizo za ndugu wa dar Half american
Umesema vyema mzeiyaWaambie waambie, Mimi nakuaga mchoyo nikiwa Sina hela, ila nikiwa na hela nazigawa kama zote
Wenye uchoyo ilhali Wana hela, aisee Mzee wa kupambania