Utofautishi Tafadhali

Utofautishi Tafadhali

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
haya maneno bado ni ntihano kwangu

Kuwa na kua

Huwa na hua
 
Mfano: Huyu mtoto anarefuka haraka Sana. Nahisi atakua mrefu Kama baba yk
Mfano: je, wewe unapendelea kinywaji gani. Mimi Mara nyingi uwa napendelea kunywa maji tu
 
haya maneno bado ni ntihano kwangu

Kuwa na kua

Huwa na hua

1. Kuwa mwanangu, kuwa uyaone ya dunia
English: Word pertaining to growth, grow
2. Hii michongoma iliyozunguka ndio mpaka wa hua Wa nyumba yetu
English: Courtyard
 
1. Kuwa mwanangu, kuwa uyaone ya dunia
English: Word pertaining to growth, grow
2. Hii michongoma iliyozunguka ndio mpaka wa hua Wa nyumba yetu
English: Courtyard

hapana mkuu umekosea mno
 
Mfano: Huyu mtoto anarefuka haraka Sana. Nahisi atakua mrefu Kama baba yk
Mfano: je, wewe unapendelea kinywaji gani. Mimi Mara nyingi uwa napendelea kunywa maji tu
uwa????????????napendelea maji ya kunywa? mhhhhhhhhhh kiswahili cha watoto nadhani
 
Mfano: Huyu mtoto anarefuka haraka Sana. Nahisi atakua mrefu Kama baba yk
Mfano: je, wewe unapendelea kinywaji gani. Mimi Mara nyingi uwa napendelea kunywa maji tu

Miimi mara nyingi huwa napendelea kunywa maji tu
 
1. Kuwa mwanangu, kuwa uyaone ya dunia
English: Word pertaining to growth, grow
2. Hii michongoma iliyozunguka ndio mpaka wa hua Wa nyumba yetu
English: Courtyard
1.Kua mwanangu,kua uyaone ya dunia.
2.Hii michongoma iliyozunguka ndio mpaka wa ua wa nyumba yetu
 
Kua -- kuongezeka kimo au urefu/ miaka
Kuwa -- uwepo / utokeaji wa kitu fulani
 
Kuwa=uwepo.... Alikuwa barabarani
Kua=ongezeka.... Biashara yetu inakua siku hadi siku

Hua=kiswahili hiki ni mara chache husikia kikitumika.... Kuna ndege anaitwa njiwa hujulikana pia kama hua.... Biblia imemtaja jana njiwa kama hua.... Roho wa bwana akamshukia toka mbinguni kama hua.... (nisamehewe kama sijanukuu vile Ipasavyo ila nadhani sijapotea)

Huwa=huwa siwafungi mafisadi.....
 
Hua ni ndege/njiwa,
huwa ni hali fulani mf, nyuba huwa na madirisha, milango n.k
 
Back
Top Bottom