Utoto hutegemea hali ya uchumi, hali ya uchumi ikiwa ngumu utoto huisha mapema

Mimi wazazi wangu wote nilikuwanao lakini mmmmmh, mambo yalikuwa magumusana darasa la kwanza mbaka la saba bila viatu, wakati wakutoka shule mchana naungua sana na jipoza pembeni ya barabara kwenye majani then nikipoa safari inaendelea hayo ndio yalikuwa maisha yangu kilometa 4 kwa miguu bila viatu kwa miaka saba shuleni mbaka bro alipokuja kuni nunulia viatu.

Nikiwa na miaka 8 tayari najua maisha, nalima nafua namlea mdogowangu namkorogea uji wakati wazazi wapo shamba, nabeba kilo 15 za mahindi natembeanazo kilomeza 7 kwenda na kurudi, kila wiki kwenda kusaga unga.

Daaaaah, jamani MUNGU yupo siamini jinsinilivyo sasa hapanilipo, nawakumbuka sana wenzangu tuliokuwanao katika mazingira hayo huko waliko sijui maisha yao yakoje,
Namwomba MUNGU awape faraja.
 
View attachment 2054076
Hali ya uchumi ikiwa nzuri kunakuwa na mpishi wa kupika na mtoto huitwa chakula kikiwa tayari. Anakua na michezo ya kuchezea na nguo zinazohitajika kwa wakati, mfano za kukalia, za shule, za ibada nk.

Elimu ndiyo imetoa nafasi kwa watoto wengi kupata muda wa kufaidi utoto wao wawapo shuleni. Wengine wakirudi nyumbani wana majukumu ya kutunza wazazi wagonjwa na kujitafutia chakula.

Maisha kama haya yasikie tu kwa wenginge.

Ila Mungu ana maajabuyake katika wakati mgumu kama huu anafanya njia na jinsi unavyo ishi unaona kama nikawaida na unafurahiya unachofanya ila badae ukiishi maisha tofauti then uki recall hali ya zamani ndio utajua ulipitia magumu kiasigani.
 
kukatishwa utoto sio kitu ambacho ni kizuri, huwa kuna trauma na insecurities nyingi ambazo huwa zinatengenezwa ndani kwa ndani ambazo kuzifix inakuwa ni ngumu sababu mtu anakua nazo. Japo kwa nje wengi huonekana ni mashujaa lakini ukichimba ndani zaidi utawahurumia tu na binafsi sitamani mtu apitie hali hiyo
 
Hapo kabla tulikuwa tukiishi maisha ya raha sana kwenye familia yetu, nakumbuka nilipokuwa darasa la kwanza mwaka 1995 nilikuwa naingia saa nne darasani au saa moja tunatoka saa 5 asubuhi, kila siku pesa ya shule nilipewa sh 100 ile ya noti huku kaka yangu akipewa sh 200 ya kula shule.

Hali ilikuja kubadilika mwaka 1996 mwishoni ambapo mzee alipoteza kazi na kimbembe kikaanza mwaka 1997 ambapo mzee alishtuka tukawa tumehamia kwenye nyumba yetu tukatoka upangajini, ile mwanzoni haikuwa tabu saaana ila kadri miaka ilivyozidi kusonga ndipo mambo yakazidi kuwa tabu. Tukawa tunakwenda shule bila pesa ya kula, chakula cha nyumbani kikawa cha tabu, kila kitu kikawa ni cha shida.

Mama alianza kutufundisha kupika na kazi zote za ndani tukiwa wadogo mnooo! Kwa namna alivyotufunza yule mama leo hii naelewa alichokuwa akikifanya. Ugumu ule wa maisha hakuna aliyeulalamikia kwetu sisi watoto sababu ndiyo iliyokuwa hali halisi. Ilitujenga kutoka akili za kitoto tukawa watu wazima katika umri mdogo.
 
View attachment 2054076
Hali ya uchumi ikiwa nzuri kunakuwa na mpishi wa kupika na mtoto huitwa chakula kikiwa tayari. Anakua na michezo ya kuchezea na nguo zinazohitajika kwa wakati, mfano za kukalia, za shule, za ibada nk.

Elimu ndiyo imetoa nafasi kwa watoto wengi kupata muda wa kufaidi utoto wao wawapo shuleni. Wengine wakirudi nyumbani wana majukumu ya kutunza wazazi wagonjwa na kujitafutia chakula.
I miss you Madam Sky Eclat
Be blessed.
Thank you.
 
Na watoto wa aina hii ndiyo wanaokomaa kiakili na kimtazamo mapema. Hata nidhamu ya pesa ya wanakuwa nayo katika umri mdogo kabisa. Na huwa ukubwani mafanikio hayawakwepi kabisa kwa sababu wamejifunza upambanaji na heshima ya pesa tangu wadogo.
Hapa umeteleza mkuu
 
Cycle of poverty everyday.

Hana mazingira ya kutoboa huyo.

Rahisi sana kuongea.
Mbona wengine tumetoboa zamani tu,hela ya mboga haiishi ipo.
Tunalisha mtu kibao bila uchoyo.
We mtoto wa kishua kaa na hela yako mbwiga wewe naweza kukulisha mwaka mzima kama mtoto tu.
Hela hiyo ipo na sijawai kumwonyesha mtu,hustle ndo zimenifikisha hapa unaongea poverty!
Kwetu sisi poverty hakuna ntakula magimbi ,matembele,ugali,dagaa life linaenda.
We uliekulia ushuani una nini? Hujawai pata mitihani kaa kimya wakubwa wanapoongea pumbavu sana.
Naongea miaka ya 80 sijui hata km ulikua umezaliwa.
Uwe na adabu.
 
Na watoto wa aina hii ndiyo wanaokomaa kiakili na kimtazamo mapema. Hata nidhamu ya pesa ya wanakuwa nayo katika umri mdogo kabisa. Na huwa ukubwani mafanikio hayawakwepi kabisa kwa sababu wamejifunza upambanaji na heshima ya pesa tangu wadogo.
Ujinga mtupu,wakina JPM,Mwigulu polepole wote hutokea huko
 
Lakini hata kama watoto watapitia utoto wenye utulivu, hawawezi kujua mpaka watakapokuwa wanaanza maisha ya kujitegemea ndiyo watajua kwamba walikua wakiishi vizuri, kikubwa maisha hayaachi kutufundisha hata kama unmezaliwa familia za kifalme yatakufundisha tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kukatishwa utoto sio kitu ambacho ni kizuri, huwa kuna trauma na insecurities nyingi ambazo huwa zinatengenezwa ndani kwa ndani ambazo kuzifix inakuwa ni ngumu sababu mtu anakua nazo. Japo kwa nje wengi huonekana ni mashujaa lakini ukichimba ndani zaidi utawahurumia tu na binafsi sitamani mtu apitie hali hiyo
Watoto wanaokatishwa utoto wao ni wengi sana, fikiria wale watoto wa mtaani hawajawahi kuamka na kuwa na uhakika wa chai huku mzazi akikuhimiza kunawa.
 
Lakini hata kama watoto watapitia utoto wenye utulivu, hawawezi kujua mpaka watakapokuwa wanaanza maisha ya kujitegemea ndiyo watajua kwamba walikua wakiishi vizuri, kikubwa maisha hayaachi kutufundisha hata kama unmezaliwa familia za kifalme yatakufundisha tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Point kubwa ni kuelewa kuwa watoto wanahitaji kuwa watoto na ukiweza kumsaidia mtoto anaeishi mazingira magumu hata kwa sare za shule ni msaada mkubwa.
 
Na watoto wa aina hii ndiyo wanaokomaa kiakili na kimtazamo mapema. Hata nidhamu ya pesa ya wanakuwa nayo katika umri mdogo kabisa. Na huwa ukubwani mafanikio hayawakwepi kabisa kwa sababu wamejifunza upambanaji na heshima ya pesa tangu wadogo.
kuna katoto ka ndugu yake mother kalimtembelea mwezi uliopita kale katoto kapo darasa la saba lakini mimi nilidhani kamemaliza form 4,kwa kifupi kanawazidi akili wasichana wengi wa umri wake na wakubwa kwake
kamekulia maisha magumu,kwao kanamyosha mdogo wake,kanapika na ndio kasimamizi ka nyumba
 
Mimi wazazi wangu wote nilikuwanao lakini mmmmmh, mambo yalikuwa magumusana darasa la kwanza mbaka la saba bila viatu, wakati wakutoka shule mchana naungua sana na jipoza pembeni ya barabara kwenye majani then nikipoa safari inaendelea hayo ndio yalikuwa maisha yangu kilometa 4 kwa miguu bila viatu kwa miaka saba shuleni mbaka bro alipokuja kuni nunulia viatu.

Nikiwa na miaka 8 tayari najua maisha, nalima nafua namlea mdogowangu namkorogea uji wakati wazazi wapo shamba, nabeba kilo 15 za mahindi natembeanazo kilomeza 7 kwenda na kurudi, kila wiki kwenda kusaga unga.

Daaaaah, jamani MUNGU yupo siamini jinsinilivyo sasa hapanilipo, nawakumbuka sana wenzangu tuliokuwanao katika mazingira hayo huko waliko sijui maisha yao yakoje,
Namwomba MUNGU awape faraja.
Pole mkuu, mi enzi baba yupo ilikua mboga saba ,na maza alikua kaajiriwa serikalini alipopiga mzinga dingi akajifia pale ndo life span yote ikafa.
Yaani ilikua km tumepoteza kilakitu.
Maza nae alikua na majonzi sana ikabidi tuhame.
Nilimuhamisha mwenyewe badae aje Dar kabla hajastaafu.
Kaja Dar si haba tuko vizuri
 
Kaja Dar si haba tuko vizur

Hongera mkuu mshukuru Mungu kwa kukuinua.
 
Back
Top Bottom